Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
Kama Zitto ni mtu makini, hawezi kupingana na viongozi wake/wenzake inje ya chama kwa kusema bayana, hadharani bila aibu na kwa mbembwe mambo ya ndani ya chama chake. Kijana hana adabu analewa sifa na anapotea ajirekebishe.

Zidumu fikira za Chama cha Mapinduzi, Zidumu fikira za Mwenyekiti Mbowe....
 
amani iwe kwenu ma-great thinkers!
hivi leo gazeti la mwanahalisi limetoa ripoti ya kina kuhusiana na maongezi ya simu ya mara kwa mara kati ya Rostam Aziz na zitto kabwe. Hata hivyo gazeti halikuweza kupata mada waliyokuwa wanaongea akina zitto hivyo limetoa tu muda wa maongezi kati ya watu hao. Mfano zitto akitumia simu no. +255756809535 na rostam no. +255754555555 walifanya mawasiliano tarehe 11/08/2010 saa 7:08, saa 22:09, saa22:28, saa 22:49, saa 22:44 na saa 22:45. Wakati mawasiliano hayo ya simu yanafanyika simu ya zitto ilisomeka kuwa yuko uzunguni, dodoma huku simu ya rostam ikisomeka kuwa yuko area d, dodoma. Pia mawasiliano mengine yalifanyika siku mbili kabla ya kikao cha wabunge wa chadema kule bagamoyo huku simu ya zitto ikisomeka yuko ohio, dar. Huu ni mendelezo wa machapisho ya wiki iliyopita kuhusiana na maongezi ya mara kwa mara kati ya zitto na jack zoka (bosi wa tiss).

Hebu tujiulize hivi kweli zitto achukuliwe hatua gani za kinidhamu? Kwa sababu gazeti limemnukuu mama mzazi wa zitto akisema mwanawe ni mkorofi na sii msikivu. Karibu great thinker tujadili.

Wewe na huyu mwandishi wa hii Habari mna tofauti gani na yule Mwandishi wa Habari Leo anaelisakama Kanisa Katoliki kule Sumbawanga? Unpotoa habari kama hii ni vizuri ukawa Objective, ungetuambia walikua wanaongea kitu gani ingekuwa rahisi kumhukumu na hayo waliyokuwa wanazungumza.Tuondoe prejudice katika kujadili mambo kisomi. Hata huyo Mwandishi amekosa weledi ktk hili.
Mbona hakuandika wakati Mh. Wenje anaahidi kumuomba huyohuyo Rostam Azizi asaidiane nae kuchangia katika ile shule kule Mwanza? usiwe na bad impression kwa Zitto ktk kila jambo. Halafu tuepuke double std katika kujadili mambo. Alichofanya Wenje na Zitto inawezekana ni sawa tu, mbona tunamsakama Zitto tu?
 
Hapa sioni issue ya kujiuma uma!ZITO ni Fisadi mdogo.
Rostam unaongea nae nini tena Usiku?Zitto amewasaliti watz long time.
Njaa nyingine hazina maana,halafu CDM kwanini msi mtimue huyu bwana mdogo?hana maana tena
 
Kipi kisichobebeka, Kuwa alipokea milioni 100 mwaka 2005 na nginginezo wakati wa by elections za Tarime? Ama kuwa alikuwa akilobby kwa JK ili ateuliwe Ubunge? Ama kumpa fedha mgombea wa CUF Kigoma Kasakazini....yapo mengi ya kusema with facts available lakini inategemea wewe upo tayari kusikia yapi........
bwana JINIAS mbona husemi zitto aliongea nin na MTATIRO JULIUS(cuf) wakat wa kampeni?
mbona hutaki kuweka wazi kwamba zitto alimwambia MTATIRO kuwa yuko tayari kumpa FINANCIAL SUPPORT kuhakikisha anachukua jimbo la ubungo?
 
Hili ndio tatizo la OVERCOMPLICATIONS.... kwahiyo kusoma na kuhoji validity ya habari kuhusu Zitto kuongea na RA unahitaji kujua the workings of media with politics???? !!!!!!!! Thats why hatutafika popote baadhi yetu hawasomi na hawataki kujua kinachoendelea wale wanaosoma they are busy complicating and looking for a story behind the story while doing so they are leaving the story infront of them......

Well maybe kwenye fani yako ndio hivyo, katika fani yangu hayo ni muhimu kuyajua kuliko kuswallow kila kinachosemwa ama kuandikwa.....
 
Well maybe kwenye fani yako ndio hivyo, katika fani yangu hayo ni muhimu kuyajua kuliko kuswallow kila kinachosemwa ama kuandikwa.....
........Then do us all a favour and tell us what is really happening with some concrete evidence and facts... bila ya hayo itakuwa ni udaku tu....
 
big up mkuu waberoya umeweka sawa mambo bila kuwa bias,upo juu mkuu ua a greet thinker
 
bwana JINIAS mbona husemi zitto aliongea nin na MTATIRO JULIUS(cuf) wakat wa kampeni?
mbona hutaki kuweka wazi kwamba zitto alimwambia MTATIRO kuwa yuko tayari kumpa FINANCIAL SUPPORT kuhakikisha anachukua jimbo la ubungo?


Huo ndi unafiki mwengine. Zitto hajawahi kumuamini Mtatiro hata siku moja. Ni Zitto huyo huyo ndiye aliyekuja kutoka Kigoma na kumpigia kampeni Mnyika. Na tafadhalini msimuingize Mnyika jamani.......Please msichokonowe zaidi ya hapa mlipofika....Mnyika bado ni asset ya mapambano huko mbeleni....Huu ujinga wa kumgombanisha na Zitto ingawa naye anaonekana kuuvaa hautamsaidia na wala kusaidia prospects za Chadema na Taifa kwa ujumla..............Tafadhalini jamani
 
This is ridiculous; hivi kila mtu afuatilie nani anazungumza na nani? Mbona sisi wengine basi tungekuwa na hatia by phone records!

This is a very simple rick.
Kila phone company inaweka records kwa computer kwa kila phone connection na kuzistore kwenye data base for future use.
Mkuu this is technical
 
labda walikuwa wakichuana kiitikadi; sio lazima iwe usaliti. hata hivyo, kama nukuu zote kuhusu mh kabwe ni kweli, basi kuna sehemu atakuwa ameegemea!
 
Huo ndi unafiki mwengine. Zitto hajawahi kumuamini Mtatiro hata siku moja. Ni Zitto huyo huyo ndiye aliyekuja kutoka Kigoma na kumpigia kampeni Mnyika. Na tafadhalini msimuingize Mnyika jamani.......Please msichokonowe zaidi ya hapa mlipofika....Mnyika bado ni asset ya mapambano huko mbeleni....Huu ujinga wa kumgombanisha na Zitto ingawa naye anaonekana kuuvaa hautamsaidia na wala kusaidia prospects za Chadema na Taifa kwa ujumla..............Tafadhalini jamani
itafahamika tu!
we endelea kutokwa na povu
mfa maji
 
kuna haja ya kuyaangalia haya mambo kwa makini! kuna usemi wa kingereza unasema "Show me your friend, i will tell who are you" wahenga wetu nao wakasema rafiki wa mwizi ni mwizi mwenzie! Rafiki wa muungwana ni muugwana mwenzie, Ndege wafananao huruka pamoja, kule Zanzibar kuna usemi usemao waarabu wa pemba wanajuana kwa vilemba, Tunaujua pia kwenye msafara wa mamba kenge pia hakosekani.... Tuendelea kufuatilia kwa umakini tutaona wanako elekea maana hata marafiki wa Rostam pia wanajulikana ni kina nani...

Naomba kuwasilisha.
 
Dr. Slaa,

Umemsikia Omar? tunaomba neno lako usikimbie bila kutamka lolote.
 
Tusubirii matokeo ya Tume ya wazee, hapo tutajua mengi, ila kifupi bwa mdogo zitto kajitwisha mzigo ambao hawezi kuubeba. Kuongea na mtu yeyete hatukatai ila tuangalie mazingira na ulazima wa maongezi hayo - Leo mnasema mwanahalisi amekuja na udaku udaku tu na je akitoa ushahidi wa VOICE mtasemaje? Jamani kumbukeni UTANDAWAZI una faida na athari zake.



Move ya wabunge wa CDM kutokuwa na imani naye inamsumbua sana kichwa, nafikiri ni challenge yake ya kwanza ngumu tangu aanze movement ya kisiasa - utawaongozaje watu bungeni ambao wameshatangaza kutokuwa na imani na wewe? na je utakiongozaje chama ambacho hadharani umetamka kukiuka misimamo yake?

Kuna points za baadhi ya wana JF kutetea lakini mi naona kijana ana hoja za msingi za kujibu kwa tume ya wazee.
 
Nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa JF inachokihusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), lakini mijadala hii mara nyingi imekuwa ikiishia kwenye Malumbano, watu kuitana Majina ya Ajabu ambayo naamini kabisa kama tungekuwa tunatumia majina yetu halisi basi ni wazi wakati mwingine huwa tunawatukana hata Baba zetu.
Nimejaribu kuwa mfwatiliaji (Kuliko Mchangiaji) katika hizi mada na nimefanikiwa kugundua ni kwa nini basi hii mijadala haina Manufaa kwa CHADEMA wala kwa Taifa


1: Mijadala mingi ya JF Imejenga makundi makuu mawili na sasa hata hiyo mijadala imekuwa na Mabishano na Matukanano kati ya hayo makundi Mawili ( Mimi nawaita Watu wazima Hovyo)


2: Kuweko kwa makundi hayo Mawili kumesababisha baadhi ya Member Makini wa JF kutochangia hiyo Mijadala kwa kuogopa kuwekwa katika moja ya hayo makundi na kwa sababu watu wengi wamekuwa wakichangia kimajungu na kivisa.


3: Makundi hayo ni

1: Zitto Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Zitto ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa hata Mwanachama wa CHADEMA. Kundi hili limekosa support ya Member wa JF ambao kwa michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM ( Chama ambacho kwao ustawi wa CHADEMA ni tishio la Maisha na Ulaji wao)

2: Mbowe Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Mbowe ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Kundi hili ( Sijui ni Bahati Mbaya au Nzuri) linaungwa mkono na Member wengi kama si wote ambao kutokana na Michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM damu (Chama ambacho Maslahi na Ustawi wake unategemea zaidi na namna gani uongozi wa CHADEMA uko, eidha weak au strong)mfano Dar Es Salaam, Malaria Sugu, JayKey na wengine wengi tu.



Lengo la kuweka hii topic ni kuwafanya Wana CHADEMA wote makini ( Namaanisha wale wanaoamini kwamba Chama hakijengwi na Mtu Mmoja) kupima na kuangalia juu ya ama kuchangia ama kuipuuza mijadala yeyote inayolenga kuvunja umoja na Mshikamano ulioko ndani ya Chama

Asanteni
 
Take your time to read this and connect the dots.....

Mimi nimekuwa nikimfuatilia mheshimiwa Zitto, tangu alipoongoza mapinduzi ya kupindua serikali ya DARUSO mwaka 2002/2003 wakisaidiana na Ridhwan Kikwete na Omar Ilyas. Kipindi hicho nikiwa mmoja wa mawaziri wa serikali, ambayo ilipona kupinduliwa. Na tumekuwa wote ndani ya bunge la UDSM-USRC

Mimi personally nimekuwa muwazi sana na mkweli katika kila kitu kinacholigusa taifa hili na hasa uhuru wa mawazo na maoni ambao umedhihirika kuwa watanzania wengi sio kuwa hawana, bali huwa wepesi sana kuamini mambo na ni waoga kuonekana wanapingana na hali iliyopo.

Mtazamo huu umenifanya nimpende Zitto na JF members wowote wale ambo huwa wanapenda kufikiria nje ya box, au another direction/angle. Zitto amekuwa akinifurahisha kwa kuleta changamoto za kuleta mawazo tofauti na kile ambacho wengi huwa wanafikiria.

Zitto ni kweli anapenda sifa, kama binadamu mwingine yeyote yule, ila unapotaka sifa kwa kusimamia haki na ukweli na hasa unapopigania haki basi sifa hii ni sifa timilifu na inapendeza. Omar Ilyas naye alikuwa mmoja wao wa wanaopenda sifa ila kwa sasa naona amekua kidogo, nadhani Salim A Salim amemkuza.

Si nia yangu niwaharibie hawa jamaa , ila ni hali yangu kueleza ninachowaza baada ya kuwafuatilia hawa watu tangu enzi hizo. Sijajua status ya Omar Ilyas kwenye issue nzima za udini, siwezi kumtuhumu, personally nimemuona ni mtu mzuri tu na anayependa wote pasi kujali udini ila bado ni rafiki wa Zitto!

Tuendelee: Role model wa Zitto ni Salim A. Salim, rais bora kwake yeye ni Kikwete, MD bora aliyewahi kumsema yeye ni Rashid Idrisa yule wa TANESCO.

Tie, cord, umoja, Urafiki wa Zitto, Ridhwan, Omar Ilyas ni mkubwa sana kuliko maelezo, hili group lililotaka kuipindua serikali ya Kayombo-DARUSO, ili wao wapate madaraka si tu ni la hatari bali la kuangaliwa sana. Ridhwan amekuwa akijitetea sana yeye anataka ku-practise sheria hili hali kutaka uongozi amekuwa akitamani tangu siku nyingi sana.

Ukiwa rafiki na Ridhwan umekuwa rafiki wa Kikwete!!! Huwezi kuwa adui wa JK ukawa rafiki wa Ridhwan, JK si tu anampenda Ridhwan kama motto, bali kama mwanaCCM mwenzie aliye tayari kulinda interest zao.

Si ajabu Zitto kuwa alikuwa mmoja wa wanakamati ya bunge ya kuchunguza madini, maana JK anampenda Zitto, ambaye ni rafiki wa Ridhwan!

Alichotamka Juzi ni mwendelezo wa kumuonyesha JK kuwa yuko ‘NAYE' na yuko mbali na chadema na kuwa yeye hakuwa na mawazo kama wanachadema wengine!!!. Hakuishia hapo tu bali alisema JK amefanya mengi Kigoma! Hivyo hakuona sababu ya kutoka nje ya bunge, kwa hiyo hakwenda kabisa, Huu ujumbe haukuwa kwa wananchi, ulikuwa unaenda kwa JK rafiki yake! Hata kama JK kafanya mambo mengi huko jimboni kwake Kigoma ni wajibu wake kama rais na haikuwa zawadi.

Kilichonifanya nijiulize je what makes Zitto na JK kuwa marafiki? Je Zitto na JK walikuwa wanajuana kabla ya JK kuwa rais? Definitely Yes!

Je swali gumu na baya ambalo halina ushahidi ni je Zitto kuwa inclined kwa JK, Salim na kuwapenda baadhi ya viongozi wa kiislam je ni mdini?..........I mean chunguzeni hili. May be not! Kindly don't conclude! What Salim teaches Zito?? Salim is CCM, is Salim and JK close friends? Cause Ommy and Zitto are close friends, Ooh! Ommy ni personal assistant wa Salim, Nauliza Kama Ridh, Zitto, Ommy ni marafiki then Salim and JK ni maadui? Find out please. However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieni

Nani anayejua Zitto ana mtambo wa kusaga kokoto na alipata tender ya barabara ku-supply kokoto? Is he defending his interest indirectly?

Au ni kuwa ni great thinker ambaye anaishi kwa falsafa zake ambazo hatuzijui! Je mnafikiri Zitto kuwaambia waandishi wa habari yaliyojiri ndani ya chadema alikuwa hajui watu watamrudi? Who is greater to him? JK, wananchi wake Kigoma, mali au?

I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence. But we should examine him carefully and not judge him. Nimegusia tu swala la uislam maana mpaka leo kuna baadhi ya waislamu wanaofikiri kuwa wanaiweza kuigawa nchi hii kidini, na kuna wakristo wanaofikiri wanaweza kuigawa nchi hii kidini.

That's bringing another bitter question how far do we believe these opposition leaders? I mean all!

That said, I am just thinking
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom