Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.

Paulo

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
350
66
amani iwe kwenu ma-great thinkers!

Hii leo gazeti la Mwana Halisi limetoa ripoti ya kina kuhusiana na maongezi ya simu ya mara kwa mara kati ya Rostam Aziz na zitto kabwe. Hata hivyo gazeti halikuweza kupata mada waliyokuwa wanaongea akina zitto hivyo limetoa tu muda wa maongezi kati ya watu hao. Mfano zitto akitumia simu no. +25575...535 na rostam no. +2557545....5 walifanya mawasiliano tarehe 11/08/2010 saa 7:08, saa 22:09, saa 22:28, saa 22:49, saa 22:44 na saa 22:45.

Wakati mawasiliano hayo ya simu yanafanyika simu ya zitto ilisomeka kuwa yuko uzunguni, dodoma huku simu ya rostam ikisomeka kuwa yuko area d, dodoma. Pia mawasiliano mengine yalifanyika siku mbili kabla ya kikao cha wabunge wa chadema kule bagamoyo huku simu ya zitto ikisomeka yuko ohio, dar.

Hebu tujiulize hivi kweli zitto achukuliwe hatua gani za kinidhamu? Kwa sababu gazeti limemnukuu mama mzazi wa zitto akisema mwanawe ni mkorofi na sii msikivu. Karibu great thinker tujadili.
 
This is ridiculous; hivi kila mtu afuatilie nani anazungumza na nani? Mbona sisi wengine basi tungekuwa na hatia by phone records!
sio redikulas bana wee!

''something is not rught somewhere''

TUTAJUA TU SIKU MOJA!nawaamini sana mwanahalisi,HAWAKURUPUKI HAO
 
Not ridiculous...there is public interest in this! Utakumbuka kuna Dowans na mengine mengi yanayohusiana na Rostam na utakumbuka Rostam anavyotumia vyombo vyake vya habari kuua demokrasia. Watu kama nyie ndiyo mnasupport wikileaks lakini inapokuja issue ya Zitto mnakuwa mbogo. Lazima tumjue Zitto inside out! Freedom of expression!
 
Mkuu mwanakijiji, let us not take this issue so lightly! Haya sii maongezi ya kawaida! Zitto has changed nowadays. Take it from me, these are the people who are behind his recent attitude. Sasa wanayoyaongea lazima yanahusu CDM ndiyo maana wabunge wenzake hawamuelewi tena hadi wakafikia kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Sijui Katiba ya CHADEMA au waraka/kanunu yoyote ya nidhamu inasemaje kuhusiana na makosa gani na nidhamu gani zichukuliwe dhidi ya mwanachama husika. But mengi tulishasema humu, CHADEMA si mtu hivyo kwa trend ya ZK inabidi aachie ngazi mwenyewe kulinda heshima yake (ambayo ameishaichakachua mbele ya macho ya Watanzania) au kanuni za CHADEMA zifuatwe na kama ni kufukuzwa, AFUKUZWE.
 
ZITTO safari hii analo!.....
atajuta ''kuingia kwenye mtego'' wa ccm
na atarudisha vihela hela vyote na hiyo hummer atarudisha alikoitoa
 
Paulo mjadala mzuri ni kujua walikuwa wanaongea nini! wasije kuwa walikuwa wanaongea mechi za hispania au UK! Paulo nikisema ulimpigia simu mke wa jirani , mara kumi ndani ya mwezi mmoja, bila kujua na kuweka mazungumzo walikuwa wanaongea nini tutakuwa tunakosea sana hupo? si kila wanachoandika mwanahalisi ukimeze kama kilivyo watu huwa wanameza kasa!

Rostam huyu ni mfanya biashara, majirani zetu, ndugu zetu wamejiriwa na huyu mtu, EL hali kadhalika, nyumba za kupanga hata daladala you never know pengine zao!!

Nilisema miaka mingi , dawa ya mafisadi ni JELA! WAKIWAMO MTAANI NI WASAFI!! , tukisema hatuna uwezo wa kuwapeleka jela kama alivyosema Pinda basi hakuna serikali! we need strategic move ya kuondokana na dhana hizi za kumtafuta mchawi, ni sawa na ukihudhiwa kazini unarudi nyumbani kufokea mke na watoto! unatafuta sehemu za KUPUNGUZIA stress na kinachoonekana ndio hiki! we have failed to do great things, tunakazania kupigana na watu wadogo!

Take time, breath deeply! relax, READ...Kama RA ni fisadi angekuwa jela Zito angepata wapi muda wa kuongea naye?? maana kwa akili ndogo ya wafuata mkumbo itakuwa kuwa Zito anaongea na fisadi! who principally siyo fisadi maana sehemu yake ni JELA!!

Tunakuwa kama mbwa tunabweka watu wakija na kutisha wanachukua mawe tunakimbia na kwenda kubwekea uani.Watanzania tumewashindwa mafisadi, tumefikia muda kila mtu tutamuita fisadi, maskini!!!! hata wale wasio.... kisa yuko tofauti na sisi!!

Kazi iliyo mbele yetu na Kubenea analijua hilo ni kuwapeleka jela hawa mafisadi, tukishindwa hapo tukae kimya, kutupa mawe na kuitana mafisadi pasipo ushahidi ni uonevu mbaya sana , hasa pale tunapowasema watu wazuri.

Unamfahamu PA wa Rostam? unawafahamu waliojiriwa naye? unafahamu kampuni yake ya Caspian imeajiri watu wangapi? then who is Zito?

Zito ni nani hata atuzibe mdomo wa kutokuwaza makubwa ya nchi hii ya kuwaweka mafisadi jela? Zito ni nani? nani aliyewaroga kuwa hoja za Zito zitatufikisha pazuri, why you guys dont think globally? kesho Kubenea atatoa Zito alimpigia simu Pengo! keshokutwa watasema alimpigia simu girlfriend wake! who is Zito is he president?? why you guys feeling inferiority towards Zito??-Slaa chukua hiyo! kama kuongea na wenye tuhuma za mafisadi ni Zito pekee?? makanisa mangapi akina Rostam wanaalikwa na kutoa michango, misikiti mingapo kaijenga?? hivi huu ujinga UTATUONDOKA LINI KUWA TUWEZE KUWAZA YA JUU NA MBALI SANA NA SIO AKINA ZITO!!!!

Kubenea hagawi gazeti kama pipi! anauza!!! note this anauza! na wakati mwingine pengine anaowasema wanahusika kugawana fedha ,....who knows?? umeliwa bongo hii!

Ngau magazeti ya UDAKU yenye picha na waliofumaniwa live!! magazeti ya udaku nchi hii yanafanya vizuri sana kuliko Kubena na mwanahalisi!

Kesho baba yako wakati yuko kazini akimpigia simu housegirl mara 3 kwa siku kwa siku 5 za kazi huwezi ukajua wanaongea nini, the same case kama mama yako akiongea na houseboy!!! why conclude by surmising?

Mwambie lengo la kubenea na hizo article ni nini? anataka tumuite Zito fisadi au tumntenge?? muulize yeye aliyechukua fomu za kutaka kugombea ubunge mafia kwa kutumia CCM, si angekuwa anaishi na kukaa vikao na akina Rostam?? Muulize yule matanzania wa kawaida anayetembea kwa mguu toka ubungo mpaka posta hii habari inamsaidia vipi? Tumezoea majungu na wanasiasa wanakula kwa akili na tabia zetu za kusema ''asulubiwe asulubiwe'

Slaa alikiri kuwa nusu ya usalama wa taifa wanareport kwake! kwa njia gani? maana kama simu basi ili la Zito lina ugeni gani na linataka attention gani? au kusema huyu aliongelea kinampanda na huyu aliongelea Rufiji??
 
Zitto ni kuwadi wa mafisadi na wakala wa TISS. Kwa hapa alipofika hana ujanja. hawa TISS wameshamtumia vya kutosha sasa wameamua kumu expose ili sehemu iliyobakia wamalizie Chadema kisha aende zake NCCR. Alishasema siku nyingi kuwa anataka kuacha siasa ndiyo maana hajali matokeo ya matendo yake kwani anajichimbia kaburi la kisiasa.
 
Sijui Katiba ya CHADEMA au waraka/kanunu yoyote ya nidhamu inasemaje kuhusiana na makosa gani na nidhamu gani zichukuliwe dhidi ya mwanachama husika. But mengi tulishasema humu, CHADEMA si mtu hivyo kwa trend ya ZK inabidi aachie ngazi mwenyewe kulinda heshima yake (ambayo ameishaichakachua mbele ya macho ya Watanzania) au kanuni za CHADEMA zifuatwe na kama ni kufukuzwa, AFUKUZWE.

Sasa mkuu itakuwaje kama Zitto atakataa kujiuzulu nyadhifa zake ndani ya chama na bunge? Nasema haya kwsbabu kuna siku ZT mwenyewe alisema hakuomba uongozi ndani ya chama ila ni wao wenyewe walimpa baada ya kujiridhisha kuwa anafaa. Akaongeza, kawa wanaona sifai basi waniondoe lkn sii mimi nijiondoe kwani sikuomba kupewa cheo.
 
Mkuu mwanakijiji, let us not take this issue so lightly! Haya sii maongezi ya kawaida! Zitto has changed nowadays. Take it from me, these are the people who are behind his recent attitude. Sasa wanayoyaongea lazima yanahusu CDM ndiyo maana wabunge wenzake hawamuelewi tena hadi wakafikia kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Paulo nakubaliana na wewe mtu wangu, question is; say right here right now walizungumza nini?? kama haujui hauoni unajidhalilisha?
watu wangapi mafisadi huwa unaongea nao?
 
ZITTO safari hii analo!.....
atajuta ''kuingia kwenye mtego'' wa ccm
na atarudisha vihela hela vyote na hiyo hummer atarudisha alikoitoa

Hivi huyu bwana mdogo ana Hummer cku hizi? Kaipateje na wakati tunajua mshahara wake wa miaka 5 hautoshi kumiliki na kuservice haya madude ya kijeshi?
 
Mkuu mwanakijiji, let us not take this issue so lightly! Haya sii maongezi ya kawaida! Zitto has changed nowadays. Take it from me, these are the people who are behind his recent attitude. Sasa wanayoyaongea lazima yanahusu CDM ndiyo maana wabunge wenzake hawamuelewi tena hadi wakafikia kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Mkuu hiyo ni kweli kabisa maana nasikia huyu Dogo ametoa gari tatu kwa Kafulila zimsaidie kampaini. Tena nasikia anaendesha Hummer (h---). Habari kama hizo ni muhimu ili tujue tanadeal na mtu wa aina gani. Tusije fanya makosa kumpa dhamana mtu fisadi.

Hivi huyu bwana mdogo ana Hummer cku hizi? Kaipateje na wakati tunajua mshahara wake wa miaka 5 hautoshi kumiliki na kuservice haya madude ya kijeshi?
ndugu yangu haya mambo ni mazito sana.....!

mtu anaposema ''REDIKULAS'' sijui anakuwa ameangalia parameters gani.......!

lakin yule kijana nadhani 40 zake zimewadia
 
Pumba zingine asubuhi.....mmezidi ujinga nyie
Sio pumba hizi..kuna substance hapa...RA ni mtu wa kumwogopa kama ukoma...Ni maongezi gani marefu na frequent namna hiyo??..Network searching~~~~~~~!
Kuwa na urafiki wa pembeni na mtu mwenye rekodi mbaya mbele ya macho ya Watanzania wote ni namna ya usaliti...Urafiki gani huukati ya Simba na sungura...Urafiki gani huu kati ya mwanambuzi na Chui!..
Somewhere, sometime...........
 
This is ridiculous; hivi kila mtu afuatilie nani anazungumza na nani? Mbona sisi wengine basi tungekuwa na hatia by phone records!

MMJJ,
Tatizo ni mazingira ya maongezi na nyakati zenyewe na waongeaji wenyewe ni controversy tupu....hata wewe tukiambiwa umeongea na Rostam mara kadhaa na misimamo yako tutakujadili hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom