Jongwe bwana anazeeka vibaya sasa! Kura zilipoanza kumwendea vibaya alijaribu kuchonga mbinu za kuleta utaratibu wa muafaka kama ule wa Kibaki na Odinga, lakini yeye akitaka upatikane kabla ya fujo ili aonekane bingwa! Alipotuma "feelers" ikamrudia feedback kuwa kuna uwezekano wa kuzungukwa na kina Tsvangirai. Na hii suala la muafaka fulani wala si siri, Askofu Tutu ndiye aliye-broker hii dili, lakini yeye alitaka Mugabe aachie madaraka kwa "heshima", kwamba Mbeki akaongee naye kama "kaka" kumshawishi hivyo, kwa hiyo angetoa tangazo kuwa anajiuzulu, hatashiriki re-run. Kisha hiyo re-run ingekuwa kati ya Tsvangirai na Makoni, halafu iundwe serikali ya umoja. Lakini watu wa usalama, wakikumbuka kiapo walichosema kuwa hawatakubali mshindi zaidi ya Mugabe, na wanasiasa wa ZANU-PF wanaohofia nafasi zao, kwa pamoja wakamletea Mugabe kitisho kipya. Wakamtishia kuwa hata wakifanya vipi, Makoni hawezi kumshinda wala kumkaribia kwa kura Tsvangirai. Pia wakamtisha kuwa kina Tsvangirai wakiingia madarakani watamgeuzia Mugabe kibao, na hapo hata walio marafiki zake watashindwa kumtetea kwa kuwa then itakuwa kila mtu na lwake. Politburo ya ZANU-PF ikaamua kwa pamoja itasimama na Mugabe hadi mwisho, watafanya hiyo re-run! Mazingira yanawekwa ya kubakisha ushindi kwa Mugabe!
Kuna madai kuwa Mugabe aliwahi kusema licha ya degree saba alizo nazo (zote kasomea, hakuna honorary wala usanii), ati pia anayo degree ya violence!
Jongwe bwana!