Zanzibar kufuta mitihani ya Taifa na kuwa na Mfumo Mpya wa Elimu

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,890
109,227
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya mageuzi makubwa ya mfumo wa elimu kuanzia sasa hivi. Watakuwa na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Katika mipango hiyo kuna mitihani ya Taifa ambayo itafutwa kabisa. Hawaoni sababu ya kuwepo kwa mfumo wao mpya wa elimu.

Jinsi nilivyolisikiliza tamko hili (video chini) la awali, inaonesha kama ni mipango mizuri. Watakuwa na mafunzo ya amali kuanzia mapema, yaani wanafunzi watafundishwa fani mbali mbali za kazi wakati wanaendelea na masomo yao mengine, na si kama ilivyo sasa kwa Zanzibar, kuwa mwanafunzi mpaka amalize kwanza form four ndiyo aweze kwenda vyuo vya kazi. Jisikilizie ufafanuzi zaidi:

Hii mbona ilishatangazwa na waziri wa Elimu Wa JMT alisema pia Kwa sasa Shule za Msingi watasoma mpaka Darasa la sita na Kuingia moja kwa moja Form one.

Pia alisema kuwa kutakuwa na mafunzo ya amali kama muziki na elimu ya kazi secondary na hakuna haja ya mtu kusma ma Physics wala ma Chemistry wala ma history.

Kama huu mtaala utafanikiwa nitakuwa wa kwanza kuipongeza Serikali ya CCM rasmi
 
Hii mbona ilishatangazwa na waziri wa Elimu Wa JMT alisema pia Kwa sasa Shule za Msingi watasoma mpaka Darasa la sita na Kuimgia moja kwa moja Form one..

Pia alisema kuwa kutakuwa na mafunzo ya amali kama muziki na elimu ya kazi secondary na hakuna haja ya mtu kusma ma Physics wala ma Chemistry wala ma history..

Kama huu mtaala utafanikiwa Nitakuwa wa kwanza kuipongeza Serikali ya CCM rasmi
Hiyo ya JMT sijaiona.
 
Katika mambo yatayofanyiwa marekebisho ni kuundwa tume ya walimu itakayosimamia majukumu na maadili ya Walimu.

Wanataka kuhakikisha Mwalimu anajuwa anachokifanya na ana maadili mema atayoyahamishia kwa wanafunzi.

Pia kitaanzishwa chuo mahsuzi cha "kuwachinga" waalimu kitaaluma na maadili. Hiki kitakuwa chuo cha Ualimu tu "Walimu watakuwa wanapikwa huko".
 
Mitaala na ufundaji pia itabadilika, hakutakuwa na mitihani ya taifa ya darasa la nne wala 12.
Mtihani utakuwepo kwenye darasa la 10 au form four au elimu ya chini ya secondary pitia wizara ya elimu kuna huo mtaala since may na mapendekzo yake yote aliyotoa adolf mkenda.
 
Mtihani utakuwepo kwenye darasa la 10 au form four au elimu ya chini ya secondary pitia wizara ya elimu kuna huo mtaala since may na mapendekzo yake yote aliyotoa adolf mkenda
Huo wa JMT ntautafuta niuone. Sijauona.

Niliouona ni huu na nimeupenda ikiwa utatekelezwa kama ninavyofikiria.

Nilipousikiliza huu, hawakusema kuwa ni wa Taifa, wamesema huu ni mpango wa SMZ, kuna uwezekano ipo tofauti kiasi.
 
Shule za Zanzibar kwa miaka nenda rudi zimekuwa za mwisho kwenye mitihani ya taifa, suluhisho si kukimbia na kutafuta namna ya kuwalegezea watoto wao bali wazazi waweke mkazo kwenye elimu dunia pia wajifunze kuumia pindi watoto wao wanapofeli.
Waangalie kilicho bora kwao, mimi nadhani kwa udogo wao wa kijiografia, idadi ya watu na harakati zao za kiuchumi wala hawahitaji wasomi wengi ki vile watasababisha tatizo la ajira bure! watafika tu, hata sisi wenyewe pamoja na makelele yote haya hatujafika mbali!... eti nchi ya watu milioni 65 tunajilinganisha na Zanzibar kielimu badala ya KENYA au UGANDA, GHANA SOUTH AFRICA etc. Utamsikia msomi 'shule za Zanzibar ni za mwisho kimatokeo sisi tunafanya vizuri' what a shame!
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya mageuzi makubwa ya mfumo wa elimu kuanzia sasa hivi. Watakuwa na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Katika mipango hiyo kuna mitihani ya Taifa ambayo itafutwa kabisa. Hawaoni sababu ya kuwepo kwa mfumo wao mpya wa elimu.

Jinsi nilivyolisikiliza tamko hili (video chini) la awali, inaonesha kama ni mipango mizuri. Watakuwa na mafunzo ya amali kuanzia mapema, yaani wanafunzi watafundishwa fani mbali mbali za kazi wakati wanaendelea na masomo yao mengine, na si kama ilivyo sasa kwa Zanzibar, kuwa mwanafunzi mpaka amalize kwanza form four ndiyo aweze kwenda vyuo vya kazi. Jisikilizie ufafanuzi zaidi:

safi sanaaa, ili wasiajirike kabisa huku bara. wakae huko huko wakivua samani.
 
Back
Top Bottom