Tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.

Lakini sio rahisi kwa raisi wa Tanzania atokaye bara kufanya kazi kwa maslahi ya bara zaidi kuliko visiwani, kwa kuwa Zanzibar ina serikali yake tayari ambayo inasimamia maslahi ya visiwani, na inajumuishwa katika serikali ya muungano.

Kuna mambo kadhaa yamekuwa yakijadiliwa ambayo nitayaainisha hapa chini. Haya ni maoni toka wadau mbalimbali na nayaweka hapa ili kutoa wigo wa kuyajadili, sio kama shutuma.

Maoni mojawapo ni kwamba udhaifu wa kutoa maslahi upande wa visiwani raisi akitoka visiwani unajitokeza hasa ukizingatia kwamba katiba ya Tanzania inampa raisi mamlaka makubwa ya kuamua mambo bila hata kujadiliana na viongozi wengine au kuwa na kikao rasmi kitakachowakilisha maoni ya upande wa bara. Rais kutoka visiwani ana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri kimkakati ili kuinufaisha Zanzibar, na hakuna namna ya kuweza kumzuia. Labda mfano mzuri katika suala hili ni suala la DP World na bandari, ambapo Zanzibar waliikataa DP World kwa sababu wana uwakilishi wao wa kiserikali, tofauti na bara. Sasa inakuwa kama raisi wa kutoka visiwani aliiamulia Tanzania bara kuwa na DP World. Je kungekuwa na serikali ya Tanzania bara, hili lingekubalika?

Na pia kuna maoni kwamba kila inapotokea raisi akitokea Zanzibar, ule msukumo wa kutoka Zanzibar kutaka muungano urekebishwe au uvunjwe unakwisha. Swali ni kwa nini? Je, ni kwa sababu katika hivyo vipindi upande wa visiwani unaona kuwa unafaidika zaidi na uwepo wa raisi kutoka visiwani? Wengine wamedokeza kwamba wakati wa raisi Magufuli uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua zaidi ya uchumi wa Zanzibar, lakini kwa sasa uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi zaidi ya ule wa Tanzania, kuonyesha kwamba upande wa bara kuna kushuka kwa kasi ya kukua kwa uchumi. Na wengi wanaona hili linaweza kuwa linachochewa na maslahi mengi ya kitaifa kuelekezwa upande wa visiwani kwa kuwa kuna raisi toka visiwani.

Labda lililo kubwa zaidi ni maoni kwamba ikiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hatari ya kuvunjika, au kwamba watu wa upande wa visiwani hawautaki japo hawasemi hivyo hadharani, hatuoni kwamba tunaweza kumpata raisi kutoka visiwani ambae hana imani na muungano, japo anadai kuutetea, na akafanya mambo kwa namna ambayo kama muungano ukivunjika basi awe amewanufaisha upande wa visiwani kwa namna ya kutosha, yaani akatumia fursa ya uraisi wake kuimarisha upande wa visiwani akijua muungano unaweza kuvunjika wakati wowote?

Mfano umetolewa kwamba wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikaribia kuvunjia miaka ya 1977, Wakenya wakijua hili kwamba walitaka kuivunja jumuia, walifanya mkakati wa mali za jumuiya ya mashariki kuhodhiwa upande wa Kenya. Siku jumuiya ya mashariki ilipovunjika Tanzania na Uganda walikuja kugundua kwamba Kenya walikuwa na mkakati huu siku nyingi na walitenda mambo wakijua hilo linakuja! Je philosophy hii inawezekana pia katika suala la muungano, kwa kuwa upande wa bara hakuna serikali itakayokuwa macho kusimamia maslahi ya bara?

Sasa haya ni mambo yanajadilika na ni muhimuhimu kuyatafakari katika suala la muungano. Ndio maana basi, tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana kabisa raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi ya uraisi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano. Kujifanya kama hilo haliwezekani ni kujidanganya, na haya mambo yasipojadiliwa, yanaweza kuleta madhara na chuki zisizostahili. Na lazima pia tukiri ni mambo kama haya ambayo yamekuwa yakichochea madai ya kuwapo na serikali ya kusimamia maslahi ya upande wa bara, kama ilivyo kwa upande wa visiwani.

Nini maoni yako?
 
Hiyo ni wazi kabisa kwa kuwa anakuwa hana maslahi na cho chote cha Tanganyika. Suluhisho hapa ni kuwa na serikali tatu.

Serikali ya Muungano itashughulikia masuala ya ulinzi wa Taifa na ya kimataifa tu wakati kila nchi itashughulikia masuala yake ya ndani.
 
Ni kweli ila Kuna kitu mfano huko nyuma kulikuwa na Tuhuma kuwa Tanganyika inaimeza Zanzibar akishika mzaznzibar uraisi wa muungano ndie huongoza kuhakikisha Zanzibar inamezwa na utamaduni wa mzaznzibar unaharibiwa Kwa sera kama za Ajira.Mfano Sasa hivi wako wazanzibari kibao wamepewa ajira bara matokeo Sasa muda mfupi tu wameshaharibika walikuja na hijabu Toka Zanzibar Sasa hivi kutembea vifua wazi na kuvaa vimini Wala hawaoni shida sababu wamekuja kwenye Jamii huru isiyowadhibiti uvaaji au tabia sababu huku Kuna utamaduni wa mtanganyika sio mzaznzibari ajira vyeo nk wanapewa lakini at the expense ya maadili ya kizanzibari na hawana mpango wa kurudi Zanzibar

Huku wanajisikia huru sana wakilewa hakuna wa kuwafokea,Wakifanya umalaya hayuko wa kuwafokea kama kwao Zanzibar

Nafikiri kuua uzanzibari wazanzibari waendelee kupewa nafasi zaidi kwenye muungano waje Tanzania bara kiwanda Cha kuua maadili na utamaduni wa mzaznzibari Wapewe na nafasi ndio namna Bora ya kuimeza Zanzibar.Kupitia kuua maadili na utamaduni wa mzanzibar mlipe vizuri afanye kazi ofisi moja na Wala kitimoto na walevi na wavaa wapendavyo na wajirusha viwannja halafu uone baada ya miaka mitano huyo mzànzibari Aliyekuja kufanya kazi kwenye taasisi za muungano kama ndie yule yule uashangaa ajira aliyopewa imezalisha shetani ambaye Zanzibar hatakiwi na yeye hataki Hana mpango wa kurudi Zanzibar
 
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.

Lakini sio rahisi kwa raisi wa Tanzania atokaye bara kufanya kazi kwa maslahi ya bara zaidi kuliko visiwani, kwa kuwa Zanzibar ina serikali yake tayari ambayo inasimamia maslahi ya visiwani, na inajumuishwa katika serikali ya muungano.

Kuna mambo kadhaa yamekuwa yakijadiliwa ambayo nitayaainisha hapa chini. Haya ni maoni toka wadau mbalimbali na nayaweka hapa ili kutoa wigo wa kuyajadili, sio kama shutuma.

Maoni mojawapo ni kwamba udhaifu wa kutoa maslahi upande wa visiwani raisi akitoka visiwani unajitokeza hasa ukizingatia kwamba katiba ya Tanzania inampa raisi mamlaka makubwa ya kuamua mambo bila hata kujadiliana na viongozi wengine au kuwa na kikao rasmi kitakachowakilisha maoni ya upande wa bara. Rais kutoka visiwani ana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri kimkakati ili kuinufaisha Zanzibar, na hakuna namna ya kuweza kumzuia. Labda mfano mzuri katika suala hili ni suala la DP World na bandari, ambapo Zanzibar waliikataa DP World kwa sababu wana uwakilishi wao wa kiserikali, tofauti na bara. Sasa inakuwa kama raisi wa kutoka visiwani aliiamulia Tanzania bara kuwa na DP World. Je kungekuwa na serikali ya Tanzania bara, hili lingekubalika?

Na pia kuna maoni kwamba kila inapotokea raisi akitokea Zanzibar, ule msukumo wa kutoka Zanzibar kutaka muungano urekebishwe au uvunjwe unakwisha. Swali ni kwa nini? Je, ni kwa sababu katika hivyo vipindi upande wa visiwani unaona kuwa unafaidika zaidi na uwepo wa raisi kutoka visiwani? Wengine wamedokeza kwamba wakati wa raisi Magufuli uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua zaidi ya uchumi wa Zanzibar, lakini kwa sasa uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi zaidi ya ule wa Tanzania, kuonyesha kwamba upande wa bara kuna kushuka kwa kasi ya kukua kwa uchumi. Na wengi wanaona hili linaweza kuwa linachochewa na maslahi mengi ya kitaifa kuelekezwa upande wa visiwani kwa kuwa kuna raisi toka visiwani.

Labda lililo kubwa zaidi ni maoni kwamba ikiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hatari ya kuvunjika, au kwamba watu wa upande wa visiwani hawautaki japo hawasemi hivyo hadharani, hatuoni kwamba tunaweza kumpata raisi kutoka visiwani ambae hana imani na muungano, japo anadai kuutetea, na akafanya mambo kwa namna ambayo kama muungano ukivunjika basi awe amewanufaisha upande wa visiwani kwa namna ya kutosha, yaani akatumia fursa ya uraisi wake kuimarisha upande wa visiwani akijua muungano unaweza kuvunjika wakati wowote?

Mfano umetolewa kwamba wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikaribia kuvunjia miaka ya 1977, Wakenya wakijua hili kwamba walitaka kuivunja jumuia, walifanya mkakati wa mali za jumuiya ya mashariki kuhodhiwa upande wa Kenya. Siku jumuiya ya mashariki ilipovunjika Tanzania na Uganda walikuja kugundua kwamba Kenya walikuwa na mkakati huu siku nyingi na walitenda mambo wakijua hilo linakuja! Je philosophy hii inawezekana pia katika suala la muungano, kwa kuwa upande wa bara hakuna serikali itakayokuwa macho kusimamia maslahi ya bara?

Sasa haya ni mambo yanajadilika na ni muhimuhimu kuyatafakari katika suala la muungano. Ndio maana basi, tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana kabisa raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi ya uraisi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano. Kujifanya kama hilo haliwezekani ni kujidanganya, na haya mambo yasipojadiliwa, yanaweza kuleta madhara na chuki zisizostahili. Na lazima pia tukiri ni mambo kama haya ambayo yamekuwa yakichochea madai ya kuwapo na serikali ya kusimamia maslahi ya upande wa bara, kama ilivyo kwa upande wa visiwani.

Nini maoni yako?
Kwanza nikusahihishe kidogo:

1. Nchi zilizoungana ni mbili TANGANYIKA na ZANZIBAR. Hakuna wala hakujawahi kuwa na nchi au taifa linaitwa "Bara" au "Tanzania Bara" lililoungana na nchi ya pili iitwayo Zanzibar!

2. Kwa hiyo haina mantiki kabisa na ni makosa kutumia sentensi kama "tukipata Rais toka Bara/Tanzania Bara" ktk ku - refer chochote/lolote..

Back to the topic;

👉Ni kweli usio na ubishi kuwa, wa nature ya union yenyewe ni kuwa, ikitokea Rais anatoka upande mmoja wa Muungano lazima atazingatia na kuelekeza nguvu za utumishi wa u - Rais wake ktk nchi atokako.

👉Mfano wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli (2015 - 2021) sikuwahi kuona akiijali wala kuitilia maanani Zanzibar. Vivyo hivyo kaingia huyu mama Mzanzibari tunaona macho na nguvu ameelekeza kujenga Zanzibar. Anashindwa tu kujitoa mazima kwa sbb ya ukubwa na nguvu iliyonayo Tanganyika

👉Moreover, laiti Magufuli angeendeleaga kuwepo hai, kwa hakika kabisa huyu ndiye ambaye angeutupilia mbali Muungano huu. Infact he (Magufuli) never considered Zanzibar as part of Tanzania. Huyu aliichukulia Zanzibar nchi nyingine kabisa inayojitegemea....!

👉Muungano huu hauna maisha marefu kuanzia sasa Kwa sababu ni Muungano wa kilaghai usiobebwa na utashi wa wananchi wote wa nchi hizi mbili..!

👉Uhakika mwingine ni kuwa Tanganyika itarudi na historia itaandikwa upya
 
👉Ni kweli usio na ubishi kuwa, wa nature ya union yenyewe ni kuwa, ikitokea Rais anatoka upande mmoja wa Muungano lazima atazingatia na kuelekeza nguvu za utumishi wa u - Rais wake ktk nchi atokako.

👉Mfano wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli (2015 - 2021) sikuwahi kuona akiijali wala kuitilia maanani Zanzibar. Vivyo hivyo kaingia huyu mama Mzanzibari tunaona macho na nguvu ameelekeza kujenga Zanzibar. Anashindwa tu kujitoa mazima kwa sbb ya ukubwa na nguvu iliyonayo Tanganyika
Katika mfumo uliopo, ukiwa raisi wa muungano huhitaji kufanya chochote juu ya Zanzibar, kwa kuwa tayari imejitosheleza kiutawala. Na ukijaribu kufanya chochote inaonekana unaingilia mamlaka za Zanzibar, inaleta mgogoro. Hivyo Magufuli was right. Sio kwamba aliwapuuza, bali hakuna ambalo angefanya
 
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.

Lakini sio rahisi kwa raisi wa Tanzania atokaye bara kufanya kazi kwa maslahi ya bara zaidi kuliko visiwani, kwa kuwa Zanzibar ina serikali yake tayari ambayo inasimamia maslahi ya visiwani, na inajumuishwa katika serikali ya muungano.

Kuna mambo kadhaa yamekuwa yakijadiliwa ambayo nitayaainisha hapa chini. Haya ni maoni toka wadau mbalimbali na nayaweka hapa ili kutoa wigo wa kuyajadili, sio kama shutuma.

Maoni mojawapo ni kwamba udhaifu wa kutoa maslahi upande wa visiwani raisi akitoka visiwani unajitokeza hasa ukizingatia kwamba katiba ya Tanzania inampa raisi mamlaka makubwa ya kuamua mambo bila hata kujadiliana na viongozi wengine au kuwa na kikao rasmi kitakachowakilisha maoni ya upande wa bara. Rais kutoka visiwani ana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri kimkakati ili kuinufaisha Zanzibar, na hakuna namna ya kuweza kumzuia. Labda mfano mzuri katika suala hili ni suala la DP World na bandari, ambapo Zanzibar waliikataa DP World kwa sababu wana uwakilishi wao wa kiserikali, tofauti na bara. Sasa inakuwa kama raisi wa kutoka visiwani aliiamulia Tanzania bara kuwa na DP World. Je kungekuwa na serikali ya Tanzania bara, hili lingekubalika?

Na pia kuna maoni kwamba kila inapotokea raisi akitokea Zanzibar, ule msukumo wa kutoka Zanzibar kutaka muungano urekebishwe au uvunjwe unakwisha. Swali ni kwa nini? Je, ni kwa sababu katika hivyo vipindi upande wa visiwani unaona kuwa unafaidika zaidi na uwepo wa raisi kutoka visiwani? Wengine wamedokeza kwamba wakati wa raisi Magufuli uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua zaidi ya uchumi wa Zanzibar, lakini kwa sasa uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi zaidi ya ule wa Tanzania, kuonyesha kwamba upande wa bara kuna kushuka kwa kasi ya kukua kwa uchumi. Na wengi wanaona hili linaweza kuwa linachochewa na maslahi mengi ya kitaifa kuelekezwa upande wa visiwani kwa kuwa kuna raisi toka visiwani.

Labda lililo kubwa zaidi ni maoni kwamba ikiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hatari ya kuvunjika, au kwamba watu wa upande wa visiwani hawautaki japo hawasemi hivyo hadharani, hatuoni kwamba tunaweza kumpata raisi kutoka visiwani ambae hana imani na muungano, japo anadai kuutetea, na akafanya mambo kwa namna ambayo kama muungano ukivunjika basi awe amewanufaisha upande wa visiwani kwa namna ya kutosha, yaani akatumia fursa ya uraisi wake kuimarisha upande wa visiwani akijua muungano unaweza kuvunjika wakati wowote?

Mfano umetolewa kwamba wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikaribia kuvunjia miaka ya 1977, Wakenya wakijua hili kwamba walitaka kuivunja jumuia, walifanya mkakati wa mali za jumuiya ya mashariki kuhodhiwa upande wa Kenya. Siku jumuiya ya mashariki ilipovunjika Tanzania na Uganda walikuja kugundua kwamba Kenya walikuwa na mkakati huu siku nyingi na walitenda mambo wakijua hilo linakuja! Je philosophy hii inawezekana pia katika suala la muungano, kwa kuwa upande wa bara hakuna serikali itakayokuwa macho kusimamia maslahi ya bara?

Sasa haya ni mambo yanajadilika na ni muhimuhimu kuyatafakari katika suala la muungano. Ndio maana basi, tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana kabisa raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi ya uraisi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano. Kujifanya kama hilo haliwezekani ni kujidanganya, na haya mambo yasipojadiliwa, yanaweza kuleta madhara na chuki zisizostahili. Na lazima pia tukiri ni mambo kama haya ambayo yamekuwa yakichochea madai ya kuwapo na serikali ya kusimamia maslahi ya upande wa bara, kama ilivyo kwa upande wa visiwani.

Nini maoni yako?
Mtu kwao!
 
Katika mfumo uliopo, ukiwa raisi wa muungano huhitaji kufanya chochote juu ya Zanzibar, kwa kuwa tayari imejitosheleza kiutawala. Na ukijaribu kufanya chochote inaonekana unaingilia mamlaka za Zanzibar, inaleta mgogoro. Hivyo Magufuli was right. Sio kwamba alwapuuza, bali hakuna ambalo angefanya
Mbona huyu mama macho na nguvu ameelekeza huko?
 
tatizo kubwa ni umaskini na low IQ ambapo vyote vinategemeana kwa upande wa bara.

I mean kwa nini mko soooo obsessed na zanzibar? Its a mere 2500 square km wakati bara ni more than 900 000 sqkm, sasa iweje bado mnalia lia?

Muungano wa Uingereza UK ni copy & paste ya muungano wetu lkn huwezi sikia mtu wa englanda anali lia kutawaliwa na scotlanda, unajua kwa nini ? ila kwetu watu milioni 50 wanaliloa hakia ya kwenda kuishi kwenye kisiwa cha sqkm 2 000 , shida ni IQ ndogo ya wabara …
 
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.

Lakini sio rahisi kwa raisi wa Tanzania atokaye bara kufanya kazi kwa maslahi ya bara zaidi kuliko visiwani, kwa kuwa Zanzibar ina serikali yake tayari ambayo inasimamia maslahi ya visiwani, na inajumuishwa katika serikali ya muungano.

Kuna mambo kadhaa yamekuwa yakijadiliwa ambayo nitayaainisha hapa chini. Haya ni maoni toka wadau mbalimbali na nayaweka hapa ili kutoa wigo wa kuyajadili, sio kama shutuma.

Maoni mojawapo ni kwamba udhaifu wa kutoa maslahi upande wa visiwani raisi akitoka visiwani unajitokeza hasa ukizingatia kwamba katiba ya Tanzania inampa raisi mamlaka makubwa ya kuamua mambo bila hata kujadiliana na viongozi wengine au kuwa na kikao rasmi kitakachowakilisha maoni ya upande wa bara. Rais kutoka visiwani ana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri kimkakati ili kuinufaisha Zanzibar, na hakuna namna ya kuweza kumzuia. Labda mfano mzuri katika suala hili ni suala la DP World na bandari, ambapo Zanzibar waliikataa DP World kwa sababu wana uwakilishi wao wa kiserikali, tofauti na bara. Sasa inakuwa kama raisi wa kutoka visiwani aliiamulia Tanzania bara kuwa na DP World. Je kungekuwa na serikali ya Tanzania bara, hili lingekubalika?

Na pia kuna maoni kwamba kila inapotokea raisi akitokea Zanzibar, ule msukumo wa kutoka Zanzibar kutaka muungano urekebishwe au uvunjwe unakwisha. Swali ni kwa nini? Je, ni kwa sababu katika hivyo vipindi upande wa visiwani unaona kuwa unafaidika zaidi na uwepo wa raisi kutoka visiwani? Wengine wamedokeza kwamba wakati wa raisi Magufuli uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua zaidi ya uchumi wa Zanzibar, lakini kwa sasa uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi zaidi ya ule wa Tanzania, kuonyesha kwamba upande wa bara kuna kushuka kwa kasi ya kukua kwa uchumi. Na wengi wanaona hili linaweza kuwa linachochewa na maslahi mengi ya kitaifa kuelekezwa upande wa visiwani kwa kuwa kuna raisi toka visiwani.

Labda lililo kubwa zaidi ni maoni kwamba ikiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hatari ya kuvunjika, au kwamba watu wa upande wa visiwani hawautaki japo hawasemi hivyo hadharani, hatuoni kwamba tunaweza kumpata raisi kutoka visiwani ambae hana imani na muungano, japo anadai kuutetea, na akafanya mambo kwa namna ambayo kama muungano ukivunjika basi awe amewanufaisha upande wa visiwani kwa namna ya kutosha, yaani akatumia fursa ya uraisi wake kuimarisha upande wa visiwani akijua muungano unaweza kuvunjika wakati wowote?

Mfano umetolewa kwamba wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikaribia kuvunjia miaka ya 1977, Wakenya wakijua hili kwamba walitaka kuivunja jumuia, walifanya mkakati wa mali za jumuiya ya mashariki kuhodhiwa upande wa Kenya. Siku jumuiya ya mashariki ilipovunjika Tanzania na Uganda walikuja kugundua kwamba Kenya walikuwa na mkakati huu siku nyingi na walitenda mambo wakijua hilo linakuja! Je philosophy hii inawezekana pia katika suala la muungano, kwa kuwa upande wa bara hakuna serikali itakayokuwa macho kusimamia maslahi ya bara?

Sasa haya ni mambo yanajadilika na ni muhimuhimu kuyatafakari katika suala la muungano. Ndio maana basi, tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana kabisa raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi ya uraisi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano. Kujifanya kama hilo haliwezekani ni kujidanganya, na haya mambo yasipojadiliwa, yanaweza kuleta madhara na chuki zisizostahili. Na lazima pia tukiri ni mambo kama haya ambayo yamekuwa yakichochea madai ya kuwapo na serikali ya kusimamia maslahi ya upande wa bara, kama ilivyo kwa upande wa visiwani.

Nini maoni yako?
Kwanza hawezi maana Urais ni taasisi

Pili Tanzania Bara Tanganyika wanachukua pesa ya Zanzibar zaidi ya bil.400 Kila mwaka.
 
Mmmh, ni kawaida mito kupeleka maji kwenye maziwa, lakini Nile huchukua maji kuyatoa kwenye ziwa. Ni kitu cha ajabu lakini kipo kinatokea!
 
Back
Top Bottom