Rais Mwinyi amefanya mabadiliko ya Wakurugenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Uteuzi

IMG-20240314-WA0040.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Wakurugenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kama ifuatavyo;
  • Ndugu Othman Omar Othman ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Ualimu. Kabla ya Uteuzi, Ndugu Othman alikuwa Mkuruenzi wa Braza la Mitihani la Zanzibar.
  • Dkt. Rashid Abdulazizi Mukki ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar. Kabla ya Uteuzi Dkt. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Ualimu.
  • Ndugu Hafsa Talib Aboud ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni. Kabla ya Uteuzi Ndugu Hafsa alikuwa Marajis wa Elimu Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 14 Machi, 20224.
 
Mauteuzi uteuzi

Ila kuteuliwa raha sana ingawa Pascal Mayalla hajawahi kuionja raha hii yeye ni kupanda magari ya thamani

Haya na nyie mlioteuliwa tuwatakie kazi njema
 
Hivi Zanzibar kuna shida ya wanasheria kuwa hawapo? Cheo cha katibu baraza kinatakiwa kushikwa na Mwanasheria.

Inakuwaje katibu wa baraza kuwa Mhandisi huyo mhandisi Zena Said aliyetoa hilo tangazo la uteuxi.
Wazanzobar vipi nyie yakhe
 
Kwanini taarifa kwa vyombo vya habari na sio kwa umma?
 
Back
Top Bottom