YESU amenipa kazi UN

YESU amenipa kazi UN

nafikiri mnatofautiana viwango vya kuamini....lkn ana hai ya kuamini kwamba KING OF KINGS,LION OF JUDAH ndo amempa kazi...jamani huyu YESU mtamu sana!
Kila mtu ana chaguo la imani katika maisha yake lakini haimaanishi kuwa kila mmoja lazima ukubaliane na imani hiyo.
 
Ninasema kwa sauti ya juu kuwa YESU amenipa kazi umoja wa mataifa, maana katika ile interview kulikuwa na wasomi waliobobea na experienced sana! mimi peke yangu tuu ndio nilikuwa sina utitiri wa experience! mda wote wa Interview nilikuwa nikimuomba yesu anisaidie nipate kazi, leo nimepata skype call kuwa nimeshinda ile nafasi, my working station will be in Nairobi Kenya then after 3 months nitahamia JUba Sudan. Asante sana Yesu

Ebeneza, naam nami nasema Amina katika Jina la Yesu Kristo. Mtukuze Mungu sasa na hata milele kwa matendo yake makuu.
 
na ikiwa kila mtu aana haki ya kuamini atakavyo basi hata huyu ana haki ya kumshukuru YESU wake kwa kumpa kazi UN

Kila mtu ana chaguo la imani katika maisha yake lakini haimaanishi kuwa kila mmoja lazima ukubaliane na imani hiyo.
 
na ikiwa kila mtu aana haki ya kuamini atakavyo basi hata huyu ana haki ya kumshukuru YESU wake kwa kumpa kazi UN
Ni kweli, haki anayo sana. Lakini kama ukisoma vizuri bandiko lake utagundua maana yangu kusema hivyo. may be, she was just incautious.
 
Ulijuaje wewe peke yako ndo huna utitiri wa experience? au tuseme ulijuaje wengine wana utitiri wa experience? Ukipata kazi usijikweze kwa kujificha nyuma ya jina la Yesu, hukutakiwa kuwabeza wenzako, mtu asie jua maandiko anaweza kuona kama unantukuza Yesu lakini sivyo. unajikweza. hata yesu laifanya interview sio kwamba wale waliochaguliwa walijisifu juu ya wale wengine. kwani maandiko yanasema yesu alichagua mitume kumi na wawili miongoni mwa wanafunzi wake. Sasa sidhani kama kuna sehemu hawa wanafunzi walijisifu. pia jitahidi kuwa spiritual sio kila kazi anatoa Yesu hata shetani anaweza kukupa kazi kwa sababu zake mwenyewe usipokua na macho ya roho. kuna watu huwa hata hawasomi wanabaki kushuhudia tu kwa kusema Yesu atanifanyia mtihani matokeo yake huwa ni kufeli. Pia Interview ina vigezo vingi inategemea wanataka mtu wa aina ipi. kazi zingine wanataka fresh Graduate hasa UN.
 
Muombe sana yesu akusaidie kwenye safari yako ya UN! Nasikia waliomo ndani wanafahamu zaidi matatizo yaliyopo!

Hongera

Ninasema kwa sauti ya juu kuwa YESU amenipa kazi umoja wa mataifa, maana katika ile interview kulikuwa na wasomi waliobobea na experienced sana! mimi peke yangu tuu ndio nilikuwa sina utitiri wa experience! mda wote wa Interview nilikuwa nikimuomba yesu anisaidie nipate kazi, leo nimepata skype call kuwa nimeshinda ile nafasi, my working station will be in Nairobi Kenya then after 3 months nitahamia JUba Sudan. Asante sana Yesu
 
========
Wale wagonjwa kumi wa ukoma waliomwendea YESU awaponye, wote waliponywa,kwa hiyo hata hao wengine wenye experienceskama wangeingia kwa hiyo interview kwa kuliitia jina la YESU wote wangepata kazi,huwa anafanya mambo juu ya kawaida.

unachojaribu kutuambia ni kwamba hao wengine wote hawakumuomba Yesu?
 
Ishu sio fungu la kumi tu, Yesu hayupo kwa ajili ya pesa za fungu lako la kumi, mtolee maisha yako sasa, ni vyema sana umeamini ni yeye ndio amekupa kazi na si nguvu zako binafsi, mtumikie sasa!

Kuna namna nyigi sana za kutoa fungu la kumi, sio lazima uchukue kalkuleta ukokotoe asilimia kumi ya mshahara wako mpya wa UN!

Hongera. Fungu la kumi ni lazima hata tusijipe moyo. Na kumtumikia ni lazima pia ukitaka kutumika. No shortcuts.
 
Ukiwa na imani hakuna kinachoshindikana, muombe Mungu akudumishe katika imani hasa utakapokuwa Juba ili usijekutana ana kwa ana na LRA. Juba kuzuri japo jua duh na kuna wabongo wa kutosha kwenye mashirika ya UN. Babu kanisimulia
 
Yesu apewe sifa. Hongera sana kwa kupata kazi. Shika sana imani yako.
 
UN wanajua kuwa mtu mwenye experience hatokubali kuishi Juba na ndiyo maana wanatafuta watu wanaoanza maisha ili wasijekimbia mapema. Hata hivyo hongera sana tena sana. Hapo nairobi utakaa huo muda kwa kuwa ni lazima ufanye security awareness courses na zingine kwa kuwa ni mandatory then ndo wakupeleke huko kwa Kir. All the best.
 
Ninasema kwa sauti ya juu kuwa YESU amenipa kazi umoja wa mataifa, maana katika ile interview kulikuwa na wasomi waliobobea na experienced sana! mimi peke yangu tuu ndio nilikuwa sina utitiri wa experience! mda wote wa Interview nilikuwa nikimuomba yesu anisaidie nipate kazi, leo nimepata skype call kuwa nimeshinda ile nafasi, my working station will be in Nairobi Kenya then after 3 months nitahamia JUba Sudan. Asante sana Yesu

Praise the Living GOD,sasa kwani wee mkuu ulikuwa tomaso?je kuna jambo gumu lolote asiloliweza?check marko11:23-24,i love that verse
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom