Safari ya Sudani Kusini

Oct 14, 2020
5
44
Safari Yangu Nchini Sudani Kusini
------------------------

Nchini Sudan Kusini, Mifugo Ni Mingi Kuliko Wanandamu.
------------------------

FB_IMG_1602698258767.jpg

Nchi ya Sudani Kusini ni moja ya nchi inayopatikana hapa barani Afrika. Ukiwa hapa barani Afrika nchi ya Sudan Kusini inapatikana upande wa Afrika mashariki. Ni miongoni mwa Taifa changa hapa barani Afrika, kwani lilianzishwa mnamo mwaka 2011. Ambapo hapo awali ilikuwa nchi moja ya Sudan. Ni baada ya 2011, tifa hili likajitenga na kuwa Sudan Kusini. Mji mkuu wake unaitwa Juba, Ni m oja ya mji WA Afrika, unaoendelea kukua siku hadi siku.

Twende sasa………..

Ukisikiliza redio au ukiangalia kwenye Tv, au saa zingine akasoma habari mbalimbali kwneye mitandao ya kijamii, ukasikia au kuliona neno “Sudan Kusini” akili mwako itakuja picha ya machafuko , mauaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Yaani unapotaja habari za Sudan Kusini, unataja masuala ya vita. Yaani watu watakushangaa kusikia unaenda Sudan Kusini Kutembea.

Ni kweli Sudan Kusini kuna vita lakini nataka nikwambie ya kwmaba, pamoja na kwamba, Sudan Kusini kuna vita, bado kuna maisha nje ya vita. Makala hii naiandika nikiwa na ushahidi wa kuona na sio wa kusikiliza wala kusoma kwenye kitabu.

Hivyo kabla sijakusimulia habari za Mifugo kuwa mingi kuzidi wanadamau nchini Sudan Kusini, ngoja nikusimulie Safari yangu ya Kwenda Sudan Kusini.

Kwa majina yangu naitwa Joseph Mayuni , mimi ni kijana wa kiafrika niliyejitolea kuandika masuala mbalimbali ya kihistoria kuhusu bara la Afrika. Mnamo mwaka 2018, nikiwa mkoani Tabora wakati nafanya tafiti juu ya orodha ya Chifu za Kinyamwezi, ghafla nilipata ujumbe kwenye “Facebook Massager” ambapo kulikuwa na mtu alitaka kujua historia ya Wamasai. Na ndipo nilipoamua kusoma vitabu takribani 24, vyenye kuhusu historia ya Wamasai ambavyo vingi havikuandikwa kwa lugha ya Kiswahili, hivyo kusoma kwangu nilikuwa na kazi mbili, kuelewa na kisha kuandika kwa lugha ya Kiswahili.

Katika vitabu vyote hivyo niligundua ya kwamba, vinataja sana maeneo ya Sudan Kusini kama moja ya maeneo muhimu sana yenye kubeba historia ya Wamasai. Basi kuanzia hapo nikaanza kutamani sana kujua mengi zaidi kuhusu Sudan Kusini hususani masuala ya historia. Ndipo nilipoamua kutafuta marafiki na habari kuhusu nchi hiyo.

Wakati nikitafuta habari kuhusu nchi ya Sudan Kusini. Ghafla nikasikia tangazo la kwamba, huko nchini Sudan Kusini wanahitajika walimu wa lugha ya Kiswahili kutoka Tanzania kwenda kufundisha huko. Na hii ni kutokana na Sudan kusini kuwa miongoni mwa nchi zilizopo kwenye Jumuhiya ya Afrika Mashariki inayohitaji kutumia lugha ya Kiswahili.

Kwa upande wa marafiki nilipata watatu. Mmoja akiwa afisa wa jeshi bwana Gabriel Bor Anuer, mwengine ni mwakilishi wa Jumuhiya yan Afrika mashariki wa Sudan Kusini Mh. Kim Gai Ruot Duop na watatu ni msichana aliyefahamika kwa jina la Anifa. Wote hawa walifanya safari yangu ya kwenda huko kuwa nyepesi kiasi Fulani.

Ndipo nilipogundua kuwa, kuna uwezekano wa mimi kufika huko. Na wakati huo huo nikasoma kwenye mtandao wa serikali ya Sudan Kusini, kupitia wizara ya mambo ya ndani, kwamba, watanzania hawahitajiki kulipia VISA (50$=115000/=) kuingia Sudan kusini. Na hii ikiwa na maana ya kwamba, fursa zilizopo huko Sudan Kusini , watanzania zinatuhitaji Zaidi. Kuanzaia hapo nikawa na tamaa kubwa sana ya kuingia nchini Sudan Kusini, kwa malengo mawili, moja kujua historia ya Sudan Kusini na kupata fursa za ajira huko. Ndipo nilipoamua kufungasha virago vyangu na kusonga mbele bila kujali vita na mapigano yaliopo huko.

Safari Ikaanza…………………..

Safari yangu ilianzia mkoani Tabora, ambapo nilitoka Tabora mjini kuelekea jiji la Mwanza, nilitumia usafiri wa basi la kampuni ya NBS, na nilitumia gharama ya 15000/= kutoka Tabora kwenda Mwanza. Nilifika Mwanza mchana na hapo hapo nikaulizia mabasi ya kwenda Kampala na kuambiwa kuwa, mabasi ya kwenda Uganda yaani Kamapala yameshajaa na kampuni ni moja tu ya FRIENDS. Ndipo nilipoamua kutafuta sehemu ya kupumzika yaani Lodge. Nilikaa hapo kwa siku mbili ili nipate muda wa kuvuta hewa safi kutoka katika ziwa Victoria, huku nikitafakari safari yangu. Kwa mbali nilikuwa nikisikia makele kutoka uwanja wa CCM Kilumba, ambapo kulikuwa na sherehe za Sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuri.

Wakati huo tiketi yangu ya basi ikiwa mfukoni na kwa mwaka 2019, gharama ya kutoka Mwanza kwenda Uganda Kampala ilikuwa ni 40000/= kwa kweli usiku ule kabla ya safari sikulala mawazo yangu yote yalikuwa juu ya kufika kampala na kisha kufika huko nchini Sudan Kusini. Basi asubuhi na mapema niliamka na kuwahi stendi ya mabasi hapo Nyegezi, na safari ya kutoka Mwanza ilianzia mida ya saa 12,alfajiri. Mwanzoni nilijawa na furaha kwa maana nilipata nafasi ya kuijua nchi yangu kwa maana njiani nilibahataika kuona mambo kibao ya kuvutia. Kikubwa nilipenda pale kwenye kivuko cha Busisi kuelekea kivuko cha Kikongo,maana ghafla niliona watu wanashuka na kukimbia, kuuliza wakaniambia hapa tunashuka na kwenda kuwahi kivuko.

Safari iliendelea tulipita maeneo mengi sana ya mkoa wa Mwanza, Geita na Kagera. Mkoa wa Geita tulipita maeneo kama Chato, mkoa wa Kagera tulipita maeneo kama Bukoba mjini na Biharamulo. Kwa hakika nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa na jiografia nzuri sana hasa hasa mpangilio wa milima. Safari iliendelea mpaka kufika mpakani hapo Mutukula, yaani boda ya Tanzania na Uganda. Abiria wote tulishuka na kufanyiwa ukaguzi na mwisho kugonga hati ya kusafiria, kubadilisha fedha na kisha kusonga mbele.

Tulifika mjini Kampala mida ya saa 2:34usiku wakati tunaingia mjini Kampala tulishuhudia foleni kubwa sana. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba, foleni huko mjini Kampala zinasababishwa na bodaboda, kwa maana huko nchini Uganda hususani kampala boda boda ni nyingi sana.

Basi tulifika hapo stendi ambapo huko Uganda wanapaita “Tax Park” nilishuka na kutafuta sehemu ya kupumzika. Ndipo nilipopelekwa katika hotel moja ya bei rahisi iliyopo kati kati ya mji iliyofahamika kwa jina la Hotel Havana. Hotel hii alikuwa inamikiwa na Waithiopia, kwa maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya watu kutoka taifa la Ethiopia. Hapa nilikaa kwa siku 4 ili kupata taarifa zaidi kuhusu safari ya kwenda mjini Juba nchini Sudan Kusini.

Na kutokana na muonekano wangu waithiopia wengi walitokea kunipenda sana na nilipata nafasi ya kuwaambia mengi kuhusu nchi yangu ya Tanzania. Cha kushangaza kwa siku hizo 4, sikuwahi kukutana na mtanzania kwenye hotel ile. Na ndani ya siku hizo nne nilizitumia katika kufanya matembezi, hasa nilipotembea makumbusho ya Taifa na chuo kikuu cha Makerere na sehemu zingine nyingi za kihistoria. Bila kusahau kuwa siku hizo nne nilikuwa nakwenda “Tax Park” kupata taarifa za usafiri wa kwenda mjini Juba. Watu wengi niliokutana nao hapo hotelini, walishauri kuwa, nitumie ndege kufika huko kwa usalama zaidi. Lakini gharama ni kubwa kulingana na hali yangu ya Uchumi. Kwani kwa ndege iligharibu $192 sawa na 441600/= tanznaia ambapo kwa Shilingi ya Uganda ni sawa na 794,880. Ni pesa nyingi sana hiyo.

Ndipo siku ilipowadia asubuhi na mapema, nilipoamka na kwenda stendi ya basi kukata tiketi nah ii ni baada ya kupata taarifa za kutosha. Nilifika hapo na kukata tiketi ya Basi la kampuni ya ECO. Maana hapo mjini Kampala kampuni za mabasi zipo nyingi sana zaidi ya 14. Lakini yaliokuwa ya uhakika ni Kampuni ya ECO na Trinity. Gharama ya usafiri ni 110000, kwa kampuni ya ECO lakini mabasi mengine kuanzia 70000 pesa ya Uganda. Tofauti na huku Tanzania, huko Uganda mabasi ya kwenda Juba na sehemu zingine kama Nairobi, safari inaanzia muda wa saa 4 usiku. Nikiwa kama mtanzania kwa kweli nilishangaa sana na nilipouliza niliambiwa kuwa, ni kutokana na masuala ya usalama huko sudan kusini. Ndipo niliposhtuka na kuuliza kwa kushangaa….Usalama?

Ndipo kijana mmoja mwenye asili ya Sudan Kusini aliponijibu kuwa, tukitoka hapa saa 4 usiku, tutafika mpaka ya Uganda na Sudan Kusini asubuhi na mapema sana. Na hivyo tutasafiri nchini Sudan Kusini nyakati za asubuhi na mchana, kwani ni hatari sana kwa mabasi kusafiri usiku. Ndipo nikajiuliza kimoyomoyo, itakuwa kama gari likapata kuharibika? Basi nikapiga moyo konde na kuendelea na safari yangu. Na kwa kuwa safari ya kutoka Kampala ilikuwa ni usiku, basi muda mwingi nilikuwa nimelala tu. Tulipita miji mingi sana usiku, lakini mji wa Gulu niliupenda sana na ulikuwa na mpangilio mzuri sana wa majengo na barabara

Basi nyakati za alfajiri tulifika mpakani mwa Uganda na Sudan Kusini. Kama kawaida tukashuka kwa kazi kubwa mbili, kugonga hati ya kusafiria na kubadilisha fedha kutoka shilingi ya Uganda kwenda Paundi ya Sudan Kusini. Ili kupata mahesabu vizuri, nilibadilisha ( 100$ =UgSh.414,000/=) na kupata Paundi ya Sudan Kusini 18000. Nilipewa noti nyingi sana kiasi kwamba hazikutosha kukaa kwenye wallet na kuamua kuziweka kwenye begi. Yaani kama ningeamua kuweka kwenye ndoo, basi zingejaa nusu. Kwani huko wana noti ya shilingi kumi, shilingi 5 n.k.

Baada ya hapo tuliingia Sudan Kusini maeneo ya Nimule kwenye ofisi ya Uhamiaji, hapo ndipo kasheshe ikaanza.

Kwanza afisa mmoja wa uhamiaji alikuwa mrefu sana na mweusi tii, aliniomba hati ya kusafiria na 50$ ya kulipia, na ndipo nilipoamwambia mbona nimeona watanzania ni “free entry” inakuwaje nilipe $50, nilijibu hivyo huku nikiwa na woga kweli. Maana watu wenyewe hawaeleweki wale. Abilia wote walipita salama isipokuwa mimi tu mtanzania. Lakini baadae nikaruhusiwa kupita na wala sikulipa hiyo $50 na tuliendelea na safari yetu. Mara kidogo tukaingia sehemu ya kukaguliwa.

Hapo napo balaa tupu, maana ni mwendo wa wewe kaa huku na wewe kaa huku. Yaani wale raia wa Sudan Kusini wanakaa kulia, wale wenzangu na mie tulikaa kushoto kuulizwa maswali na kama majibu hayaeleweki basi safari inaishia hapo. Hapo nilikuwa na woga sana maana wale wakaguzi walikuwa na silaha nzito sana na ninazokumbuka ni RPG na Machin Gun. Kumbe kwenye lile basi kulikuwa na idadi kubwa sana ya Wasomali, na miongoni mwa wa watu ambapo wanakaguliwa sana ni Wasomali na Waganda. Basi wengi walikaguliwa na kuulizwa maswali kibao, lakini nilipofika mimi nilipojitambulisha kuwa natoka Tanzania, kwanza walicheka sana na kuniuliza kuwa, “Magufuri na Harmonize Hawajambo” nikajibu hawajambo, basi nikapita na kuendelea na safari.

Lakini kufika mbele kidogo niliona mabasi yote yamepanga mstari, nilipouliza nikaambiwa mabasi haya hayawezi kwenda bila kuwepo wanajeshi wa kutulinda yaani “Convoy) na hivyo hapo mabasi yalisubiriana na mwisho nilishuhidia wanajeshi wakiwa na silaha nzito ambazo nikiwa kama mtanzania ninayetoka kwenye nchi yenye amani, nilishangaa na kushikwa na woga. Kwanza nikiwa hapo nilitoa simu yangu na kutaka kupiga picha, ghafla nikashangaa jamaa anatoka kwenye vichaka na kunipokonya simu, kisha kuniambia “ Hey No Photo” na nilipomambia, mimi ni mgeni natokea Tanznaia, akanitupia simu ile. Abilia wengi walishangaa sana mimi kurudishiwa simu na kuachwa bila kucharazwa viboko.

Basi safari iliendelea, Na kwa bahati mbaya zaidi nilikaa siti ya mbele, na basi letu lilikuwa la kwanza. Hivyo safari nzima macho yangu yalikuwa yanashuhudia silaha nzito zilizokuwa zimeshikwa na vijana wadogo sana wenye mitindo ya kila aina ya nywele, wengine wakiwa na heleni masikioni, huku wakiwa na sura za kutisha sana.

Na kwa bahati mbaya, nilikaa siti moja na mtu ambaye kwa kweli alikuwa hana ukarimu kwa mgeni. Maana alikuwa ananisimulia habari za kutisha sana. Kwa maana njiani tulikuwa tunaona majengo yaliolipuliwa na mabomu. Mara tukawa tunakutana na magari madogo yakiwa yametelekezwa njiani, huku yakiwa na matundu ya risasi. Na kila nilipokuwa nauliza , yule jirani alikuwa anatoa majibu ambayo kwa kwlei yalikuwa yananitisha na kunipa hofu. Hapo hapo nilichukua dawa aina ya Pilitoni na kisha kulala usingizi, kwa maana ningekufa na presha kutokana na niliyokuwanayaona kule njiani na jinsi msimuliaji alivyokuwa anasimulia.

Kwa kweli nilishuhudia mengi sana nikiwa njiani kutoka maeneo ya Nimule kuelekea mjini Juba. Tulitoka mpakani mwa Sudan Kusini na Uganda mida ya S 2: 13asubuhi na tulifika mjini Juba mida saa 6:38mchana. Kwa kweli niliinama chini na kusali sala zaidi ya 4, kumshukuru mwenyezi Mungu kunifikisha salama. Maana nikishika ramani ya Afrika nikiangalia nilipotea, nilikuwa na kila sababu ya kumshukuru mungu. Basi nilipofika hapo nilitafuta sehemu ya kulala na nikapelekwa hotelini na kupumzika. Kwenye hotel ile nililipia paund 1500, kwa siku moja, na baada ya siku mbili nilienda kukaa kwa rafiki yangu ambaye alikuwa afisa wa jeshi la Sudan kusini, alikuwa akiitwa Gabriel Bol Anuer.

Kwa wakati wote ule nilikuwa nikitembea kwa miguu ili kuweza kuufahamu kwa kina mji wa Juba. Kwa kweli nilikuwa nafurahi kuwaona watu wakiwa warefu na weusi, asilimia kubwa watu wa Sudan Kusini wamevaa heleni masikioni wake kwa waume. Na pia wengi wao hupenda kuvaa urembo wa shingoni. Kitu cha kushangaza ni kwamba, watu wa Sudan Kusini, hawapendi masuala ya picha, na hii ilinipelekea kukaa Sudan Kusini bila kuwa na picha nzuri, kwani picha nyingi nilikuwa napiga kwa woga, kwa maana mitaa mingi ilikuwa imezunguukwa na wanajeshi wenye sura za kutisha wakiwa na silaha nzito sana.

Nilipata kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba, ambapo nilishuhudia uwanja ukiwa busy sana, kwani ndege zinapaa na kutua kila dakika. Nikiwa pale uwanja wa ndege nilikutana na raia wa kila nchi na wengi wao walikuwa watumishi wa UN. Mitaa mingi ya Sudan Kusini imetulia sana huku magari ya thamani yakiwa yamepaki na mengine yakipita barabarani. Binafsi nilipenda sana kunywa chai nyakati za asubuhi, na chai zao zilikuwa tamu sana kutokana na aina ya viungo vilivyokuwa vinawekwa. Na kwenye kila mgahawa kwa nje ni lazima kunakuwa na watu wanavuta Shisha. Kule mjini Juba kuvuta shisha ni jambo la kawaida sana.

Kitu ambacho sitokuja kusahau ni siku ya jumatano tarehe 19/12/2019, nilipokuwa hotelini nikipata kinywaji, nilimuona mtoto wa baba wa taifa wa Sudan Kusini John Mobior Garang. Nilikuwa na furaha kwa maana nilikumbuka huko nyumbani Tanzania, kulikuwa na mada mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ikimzungumzia Mobior De Garang Mobior ambaye awali alikuwa waziri wa maji nchini Sudan Kusini. Nilitamani sana kumsogelea lakini kutokana na ulinzi wake ambao du, ulikuwa na watu warefu na wenye kutisha sana, lakini moyoni nilifurahi sana.

Kitu kingine nilichofurahia ni kugusa na kunawa usoni maji yam to Nile ambao unakatiza pale mjini Juba, na ukiwa hapo utakutana na daraja kubwa sana. Nilifurahi sana kugusa maji yam to Nile, kwa maana toka nikiwa elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, nilikuwa nasoma habari za mto huu. Kwani huwezi kusoma historia ya watu wa kale wa Misri bila kutaja mto Nile.

Kitu kingine kilichonishangaza sana nilipokuwa nchini Sudani Kusini, ni suala la madereva ya magari makubwa ya mizigo. Ukiwa huko utaona malori makubwa ya kubeba mizigo yakiwa yanaendeshwa na Wasomali. Yaani madereva wengi wa maroli huko yanaendeshwa na Wasomali. Na nilipouliza kwa nini asilimia kubwa madereva ni wasomali, nikaambiwa kuwa, watu wa Somalia wana roho ngumu, hawana uwoga na ni majasili sana. Ni kweli kwa maana nimekuwa nishuhudia maroli yakitembea usiku na mchana. Na bora mchana maana kunakuwa na ulinzi lakini usiku ni shida sana. Kutokana na sababu ya kuwepo kwa vikundi vya waasi vya msituni. Na kutoka Juba hadi Nimule ni misitu tu!

Nilikaa nchini Sudan Kusini kwa siku 28, ambapo huko nilijufunza mambo mengi sana hususani masuala ya historia ya wamasai na mambo mengine mengi sana mazuri na mabaya. Na nilipokuwa huko niliu]kutana na balaa zaidi ya mara tatu. Nikiwa huko mjini Juba niliporwa vitu zaidi ya mbili. Nilipoteza kamera, nilipoteza simu aina ya Iphone 4s, nilipoteza pesa zaidi ya $230.

Lakini kwa bahati nzuri walichukua tu vitu na kuachiwa uhai wangu. Kwa hakika sitokuja kusahau safari yangu ya kwenda nchini Sudan Kusini kufahamu historia ya Wamasai na kuangalia fursa za ajira za ualimu wa Kiswahili. Naamini siku moja ntarudi tena Juba nchini Sudan Kusini kwa maana hali ya sasa ni amani tofauti na miaka 10 iliyopita huko.

Hivyo katika makala hii ntaeleza suala la Mifugo kuwa mingi zaidi kuliko Wanadamu

Ni kwamba, Kulingana na ripoti kutoka shirika la chakula na kilimoa yaani Food and Agriculture Administration (FAO), zinasema kuwa, huko nchini Sudan Kusini kuna makadirio ya mifugo mingi kuzidi binadamu wanaoishi nchini humo. Kwani kuna ng’ombe milioni 12, kuna kondoo milioni 20 na kuna mbuzi milioni 25. Kwa namna hiyo nchi ya Sudani Kusini ni moja ya nchi yenye kuwa na idadi kubwa ya wanyama wanaofungwa hapa ulimwenguni.

Wakati mifugo ikiwa na idadi hiyo, mpaka kufikia mnamo mwaka 2018, idadi ya watu wa Sudan Kusini ni Milioni 10.98. Na kulingana na takwimu hizi, ina maana kuwa nchini Sudan Kusini wanyama wanaofungwa ni wengi kuliko binadamu wanaoishi nchini humo. Cha kushangaza sasa, pamoja na Sudan Kusini kuwa na wanyama wanaofungwa kwa idadi hiyo, bado nchi hiyo inategemea nyama kutoka nchi jirani. Kwani kwenye mfumo mzima wa maisha ya watu wa Sudan Kusini, kwao wanyama ni ishara ya utajiri. Na matumizi ya wanyama hao ni sifa na maali kwa ajili ya ndoa. Ambapo ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa, utamaduni huu bado upo hata hapa Tanzania kwa makabila kama Wamasai na Wasukuma. Na idadi kubwa ya watu wanaofunga ng’ombe ni wale wanaoishi vijijini.

Kwa namna hiyo mifugo nchini Sudan Kusini inaongezeka sana kwa maana mifugo hiyo haitumiki sana kwa masuala ya chakula. Na hata kama watatumika kwa masuala ya chakula basi ni kwa familia tu na sio kwa biashara. Na ukiwa nchini Sudan Kusini, vyakula vingi vinatoka nchi jirani, kwani asilimia kubwa watu wa Sudan Kusini hawana muda wa kulima kutokana na mtindo wa maisha yao. Na hivyo mifugo kwao ni suala la kujipatia sifa na ni sehemu ya utamaduni hasa kwenye masuala ya uchumba na ndoa.

Kwa hakika kuna mengi sana ya kusimulia juu ya nchi ya Sudan Kusini. Na kunahitajika karatasi zaidi ya 3000 kuweza kusimulia habari za Sudan Kusini. Na kutokana na mimi kufahamu habari za Sudan Kusini kuna idadi kubwa sana ya watu nimewasaidia kufika huko Sudan Kusini kwa kuwapatia taarifa zenye ukweli na zenye uhakika. Kwa kweli Sudani Kusini ni nchi ambayo kwa namna Fulani ipo salama kuishi hasa kwa sisi watanzania. Japo bado kuna changamoto kubwa sana ya masuala wa ajira kule. Lakini kuna baadhi ya taaruma zinahitajika sana, hasa hasa, masuala ya biashara, teknolojia na afya.

Nadhani kuna machache umeyapata kupitia makala hii. Na kama kuna mengi zaidi unahitaji kujua, unaweza kuwasiliana nami na kuweza kukufahamisha unayohitaji kujua, kulingana na uzoefu wangu, kwa maana kamwe siwezi kujua yote lakini naamini yapo ya kujifunza.
 
Mkuu nimeipenda hyo safari yako. Nilitaman isiishe mapema lakin nimeshangaa kuisha mapema.

Nashauri ungeandika kitabu ingesaidia, au uandike makala kma hizo zenye mwendelezo na sura kadhaa. Itasaidia sana watu tunaopenda kujua historia.

Nilipenda sana kujua suala la matumizi ya Lugha katika maeneo yote uliyopita Uganda na Sudan kusini. Lakini haswa matumiz ya lugha ya Kiswahili yakoje Sudan Kusin hivi sasa.
 
Mkuu nimeipenda hyo safari yako. Nilitaman isiishe mapema lakin nimeshangaa kuisha mapema.

Nashauri ungeandika kitabu ingesaidia, au uandike makala kma hizo zenye mwendelezo na sura kadhaa. Itasaidia sana watu tunaopenda kujua historia.

Nilipenda sana kujua suala la matumizi ya Lugha katika maeneo yote uliyopita Uganda na Sudan kusini. Lakin haswa matumiz ya lugha ya kiswahili yakoje Sudan Kusin hivi sasa.
Mkuu Nakuomba uendelee kufuatilia kwani nina uzi za kutosha kuhusu makala za safari za ndani na nje ya Tz na zote zitaletwa hapa hapa JF... Zina sisimua na kukufanya ujifunze mengi kana kwamba upo live... #Makala
 
Safari Yangu Nchini Sudani Kusini
------------------------------

Nchini Sudan Kusini , Mifugo Ni Mingi Kuliko Wanandamu.
-------------------------------
View attachment 1600312
Nchi ya Sudani Kusini ni moja ya nchi inayopatikana hapa barani Afrika. Ukiwa hapa barani Afrika nchi ya Sudan Kusini inapatikana upande wa Afrika mashariki. Ni miongoni mwa taifa changa hapa barani Afrika, kwani lilianzishwa mnamo mwaka 2011. Ambapo hapo awali ilikuwa nchi moja ya Sudan. N baada ya 2011, tifa hili likajitenga na kuwa Sudan Kusini. Mji mkuu wake unaitwa Juba, Ni m oja ya mji WA Afrika, unaoendelea kukua siku hadi siku.

Twende sasa………..

Ukisikiliza redio au ukiangalia kwenye Tv, au saa zingine akasoma habari mbalimbali kwneye mitandao ya kijamii, ukasikia au kuliona neno “Sudan Kusini” akili mwako itakuja picha ya machafuko , mauaji na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Yaani unapotaja habari za Sudan Kusini, unataja masuala ya vita. Yaani watu watakushangaa kusikia unaenda Sudan Kusini Kutembea. Ni kweli Sudan Kusini kuna vita lakini nataka nikwambie ya kwmaba, pamoja na kwamba, Sudan Kusini kuna vita, bado kuna maisha nje ya vita. Makala hii naiandika nikiwa na ushahidi wa kuona na sio wa kusikiliza wala kusoma kwenye kitabu.

Hivyo kabla sijakusimulia habari za Mifugo kuwa mingi kuzidi wanadamau nchini Sudan Kusini, ngoja nikusimulie Safari yangu ya Kwenda Sudan Kusini.

Kwa majina yangu naitwa Joseph Mayuni , mimi ni kijana wa kiafrika niliyejitolea kuandika masuala mbalimbali ya kihistoria kuhusu bara la Afrika. Mnamo mwaka 2018, nikiwa mkoani Tabora wakati nafanya tafiti juu ya orodha ya Chifu za Kinyamwezi, ghafla nilipata ujumbe kwenye “Facebook Massager” ambapo kulikuwa na mtu alitaka kujua historia ya Wamasai. Na ndipo nilipoamua kusoma vitabu takribani 24, vyenye kuhusu historia ya Wamasai ambavyo vingi havikuandikwa kwa lugha ya Kiswahili, hivyo kusoma kwangu nilikuwa na kazi mbili, kuelewa na kisha kuandika kwa lugha ya Kiswahili.

Katika vitabu vyote hivyo niligundua ya kwamba, vinataja sana maeneo ya Sudan Kusini kama moja ya maeneo muhimu sana yenye kubeba historia ya Wamasai. Basi kuanzia hapo nikaanza kutamani sana kujua mengi zaidi kuhusu Sudan Kusini hususani masuala ya historia. Ndipo nilipoamua kutafuta marafiki na habari kuhusu nchi hiyo. Wakati nikitafuta habari kuhusu nchi ya Sudan Kusini. Ghafla nikasikia tangazo la kwamba, huko nchini Sudan Kusini wanahitajika walimu wa lugha ya Kiswahili kutoka Tanzania kwenda kufundisha huko. Na hii ni kutokana na Sudan kusini kuwa miongoni mwa nchi zilizopo kwenye Jumuhiya ya Afrika Mashariki inayohitaji kutumia lugha ya Kiswahili. Kwa upande wa marafiki nilipata watatu. Mmoja akiwa afisa wa jeshi bwana Gabriel Bor Anuer, mwengine ni mwakilishi wa Jumuhiya yan Afrika mashariki wa Sudan Kusini Mh. Kim Gai Ruot Duop na watatu ni msichana aliyefahamika kwa jina la Anifa. Wote hawa walifanya safari yangu ya kwenda huko kuwa nyepesi kiasi Fulani.

Ndipo nilipogundua kuwa, kuna uwezekano wa mimi kufika huko. Na wakati huo huo nikasoma kwenye mtandao wa serikali ya Sudan Kusini, kupitia wizara ya mambo ya ndani, kwamba, watanzania hawahitajiki kulipia VISA (50$=115000/=) kuingia Sudan kusini. Na hii ikiwa na maana ya kwamba, fursa zilizopo huko Sudan Kusini , watanzania zinatuhitaji Zaidi. Kuanzaia hapo nikawa na tamaa kubwa sana ya kuingia nchini Sudan Kusini, kwa malengo mawili, moja kujua historia ya Sudan Kusini na kupata fursa za ajira huko. Ndipo nilipoamua kufungasha virago vyangu na kusonga mbele bila kujali vita na mapigano yaliopo huko.

Safari Ikaanza…………………..

Safari yangu ilianzia mkoani Tabora, ambapo nilitoka Tabora mjini kuelekea jiji la Mwanza, nilitumia usafiri wa basi la kampuni ya NBS, na nilitumia gharama ya 15000/= kutoka Tabora kwenda Mwanza. Nilifika Mwanza mchana na hapo hapo nikaulizia mabasi ya kwenda Kampala na kuambiwa kuwa, mabasi ya kwenda Uganda yaani Kamapala yameshajaa na kampuni ni moja tu ya FRIENDS. Ndipo nilipoamua kutafuta sehemu ya kupumzika yaani Lodge. Nilikaa hapo kwa siku mbili ili nipate muda wa kuvuta hewa safi kutoka katika ziwa Victoria, huku nikitafakari safari yangu. Kwa mbali nilikuwa nikisikia makele kutoka uwanja wa CCM Kilumba, ambapo kulikuwa na sherehe za Sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika zilizoongozwa na Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuri.

Wakati huo tiketi yangu ya basi ikiwa mfukoni na kwa mwaka 2019, gharama ya kutoka Mwanza kwenda Uganda Kampala ilikuwa ni 40000/= kwa kweli usiku ule kabla ya safari sikulala mawazo yangu yote yalikuwa juu ya kufika kampala na kisha kufika huko nchini Sudan Kusini. Basi asubuhi na mapema niliamka na kuwahi stendi ya mabasi hapo Nyegezi, na safari ya kutoka Mwanza ilianzia mida ya saa 12,alfajiri. Mwanzoni nilijawa na furaha kwa maana nilipata nafasi ya kuijua nchi yangu kwa maana njiani nilibahataika kuona mambo kibao ya kuvutia. Kikubwa nilipenda pale kwenye kivuko cha Busisi kuelekea kivuko cha Kikongo,maana ghafla niliona watu wanashuka na kukimbia, kuuliza wakaniambia hapa tunashuka na kwenda kuwahi kivuko.

Safari iliendelea tulipita maeneo mengi sana ya mkoa wa Mwanza, Geita na Kagera. Mkoa wa Geita tulipita maeneo kama Chato, mkoa wa Kagera tulipita maeneo kama Bukoba mjini na Biharamulo. Kwa hakika nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa na jiografia nzuri sana hasa hasa mpangilio wa milima. Safari iliendelea mpaka kufika mpakani hapo Mutukula, yaani boda ya Tanzania na Uganda. Abiria wote tulishuka na kufanyiwa ukaguzi na mwisho kugonga hati ya kusafiria, kubadilisha fedha na kisha kusonga mbele.

Tulifika mjini Kampala mida ya saa 2:34usiku wakati tunaingia mjini Kampala tulishuhudia foleni kubwa sana. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba, foleni huko mjini Kampala zinasababishwa na bodaboda, kwa maana huko nchini Uganda hususani kampala boda boda ni nyingi sana.

Basi tulifika hapo stendi ambapo huko Uganda wanapaita “Tax Park” nilishuka na kutafuta sehemu ya kupumzika. Ndipo nilipopelekwa katika hotel moja ya bei rahisi iliyopo kati kati ya mji iliyofahamika kwa jina la Hotel Havana. Hotel hii alikuwa inamikiwa na Waithiopia, kwa maana kulikuwa na idadi kubwa sana ya watu kutoka taifa la Ethiopia. Hapa nilikaa kwa siku 4 ili kupata taarifa zaidi kuhusu safari ya kwenda mjini Juba nchini Sudan Kusini.

Na kutokana na muonekano wangu waithiopia wengi walitokea kunipenda sana na nilipata nafasi ya kuwaambia mengi kuhusu nchi yangu ya Tanzania. Cha kushangaza kwa siku hizo 4, sikuwahi kukutana na mtanzania kwenye hotel ile. Na ndani ya siku hizo nne nilizitumia katika kufanya matembezi, hasa nilipotembea makumbusho ya Taifa na chuo kikuu cha Makerere na sehemu zingine nyingi za kihistoria. Bila kusahau kuwa siku hizo nne nilikuwa nakwenda “Tax Park” kupata taarifa za usafiri wa kwenda mjini Juba. Watu wengi niliokutana nao hapo hotelini, walishauri kuwa, nitumie ndege kufika huko kwa usalama zaidi. Lakini gharama ni kubwa kulingana na hali yangu ya Uchumi. Kwani kwa ndege iligharibu $192 sawa na 441600/= tanznaia ambapo kwa Shilingi ya Uganda ni sawa na 794,880. Ni pesa nyingi sana hiyo.

Ndipo siku ilipowadia asubuhi na mapema, nilipoamka na kwenda stendi ya basi kukata tiketi nah ii ni baada ya kupata taarifa za kutosha. Nilifika hapo na kukata tiketi ya Basi la kampuni ya ECO. Maana hapo mjini Kampala kampuni za mabasi zipo nyingi sana zaidi ya 14. Lakini yaliokuwa ya uhakika ni Kampuni ya ECO na Trinity. Gharama ya usafiri ni 110000, kwa kampuni ya ECO lakini mabasi mengine kuanzia 70000 pesa ya Uganda. Tofauti na huku Tanzania, huko Uganda mabasi ya kwenda Juba na sehemu zingine kama Nairobi, safari inaanzia muda wa saa 4 usiku. Nikiwa kama mtanzania kwa kweli nilishangaa sana na nilipouliza niliambiwa kuwa, ni kutokana na masuala ya usalama huko sudan kusini. Ndipo niliposhtuka na kuuliza kwa kushangaa….Usalama?

Ndipo kijana mmoja mwenye asili ya Sudan Kusini aliponijibu kuwa, tukitoka hapa saa 4 usiku, tutafika mpaka ya Uganda na Sudan Kusini asubuhi na mapema sana. Na hivyo tutasafiri nchini Sudan Kusini nyakati za asubuhi na mchana, kwani ni hatari sana kwa mabasi kusafiri usiku. Ndipo nikajiuliza kimoyomoyo, itakuwa kama gari likapata kuharibika? Basi nikapiga moyo konde na kuendelea na safari yangu. Na kwa kuwa safari ya kutoka Kampala ilikuwa ni usiku, basi muda mwingi nilikuwa nimelala tu. Tulipita miji mingi sana usiku, lakini mji wa Gulu niliupenda sana na ulikuwa na mpangilio mzuri sana wa majengo na barabara

Basi nyakati za alfajiri tulifika mpakani mwa Uganda na Sudan Kusini. Kama kawaida tukashuka kwa kazi kubwa mbili, kugonga hati ya kusafiria na kubadilisha fedha kutoka shilingi ya Uganda kwenda Paundi ya Sudan Kusini. Ili kupata mahesabu vizuri, nilibadilisha ( 100$ =UgSh.414,000/=) na kupata Paundi ya Sudan Kusini 18000. Nilipewa noti nyingi sana kiasi kwamba hazikutosha kukaa kwenye wallet na kuamua kuziweka kwenye begi. Yaani kama ningeamua kuweka kwenye ndoo, basi zingejaa nusu. Kwani huko wana noti ya shilingi kumi, shilingi 5 n.k.

Baada ya hapo tuliingia Sudan Kusini maeneo ya Nimule kwenye ofisi ya Uhamiaji, hapo ndipo kasheshe ikaanza.

Kwanza afisa mmoja wa uhamiaji alikuwa mrefu sana na mweusi tii, aliniomba hati ya kusafiria na 50$ ya kulipia, na ndipo nilipoamwambia mbona nimeona watanzania ni “free entry” inakuwaje nilipe $50, nilijibu hivyo huku nikiwa na woga kweli. Maana watu wenyewe hawaeleweki wale. Abilia wote walipita salama isipokuwa mimi tu mtanzania. Lakini baadae nikaruhusiwa kupita na wala sikulipa hiyo $50 na tuliendelea na safari yetu. Mara kidogo tukaingia sehemu ya kukaguliwa. Hapo napo balaa tupu, maana ni mwendo wa wewe kaa huku na wewe kaa huku. Yaani wale raia wa Sudan Kusini wanakaa kulia, wale wenzangu na mie tulikaa kushoto kuulizwa maswali na kama majibu hayaeleweki basi safari inaishia hapo. Hapo nilikuwa na woga sana maana wale wakaguzi walikuwa na silaha nzito sana na ninazokumbuka ni RPG na Machin Gun. Kumbe kwenye lile basi kulikuwa na idadi kubwa sana ya Wasomali, na miongoni mwa wa watu ambapo wanakaguliwa sana ni Wasomali na Waganda. Basi wengi walikaguliwa na kuulizwa maswali kibao, lakini nilipofika mimi nilipojitambulisha kuwa natoka Tanzania, kwanza walicheka sana na kuniuliza kuwa, “Magufuri na Harmonize Hawajambo” nikajibu hawajambo, basi nikapita na kuendelea na safari.

Lakini kufika mbele kidogo niliona mabasi yote yamepanga mstari, nilipouliza nikaambiwa mabasi haya hayawezi kwenda bila kuwepo wanajeshi wa kutulinda yaani “Convoy) na hivyo hapo mabasi yalisubiriana na mwisho nilishuhidia wanajeshi wakiwa na silaha nzito ambazo nikiwa kama mtanzania ninayetoka kwenye nchi yenye amani, nilishangaa na kushikwa na woga. Kwanza nikiwa hapo nilitoa simu yangu na kutaka kupiga picha, ghafla nikashangaa jamaa anatoka kwenye vichaka na kunipokonya simu, kisha kuniambia “ Hey No Photo” na nilipomambia, mimi ni mgeni natokea Tanznaia, akanitupia simu ile. Abilia wengi walishangaa sana mimi kurudishiwa simu na kuachwa bila kucharazwa viboko.

Basi safari iliendelea, Na kwa bahati mbaya zaidi nilikaa siti ya mbele, na basi letu lilikuwa la kwanza. Hivyo safari nzima macho yangu yalikuwa yanashuhudia silaha nzito zilizokuwa zimeshikwa na vijana wadogo sana wenye mitindo ya kila aina ya nywele, wengine wakiwa na heleni masikioni, huku wakiwa na sura za kutisha sana.

Na kwa bahati mbaya, nilikaa siti moja na mtu ambaye kwa kweli alikuwa hana ukarimu kwa mgeni. Maana alikuwa ananisimulia habari za kutisha sana. Kwa maana njiani tulikuwa tunaona majengo yaliolipuliwa na mabomu. Mara tukawa tunakutana na magari madogo yakiwa yametelekezwa njiani, huku yakiwa na matundu ya risasi. Na kila nilipokuwa nauliza , yule jirani alikuwa anatoa majibu ambayo kwa kwlei yalikuwa yananitisha na kunipa hofu. Hapo hapo nilichukua dawa aina ya Pilitoni na kisha kulala usingizi, kwa maana ningekufa na presha kutokana na niliyokuwanayaona kule njiani na jinsi msimuliaji alivyokuwa anasimulia.

Kwa kweli nilishuhudia mengi sana nikiwa njiani kutoka maeneo ya Nimule kuelekea mjini Juba. Tulitoka mpakani mwa Sudan Kusini na Uganda mida ya S 2: 13asubuhi na tulifika mjini Juba mida saa 6:38mchana. Kwa kweli niliinama chini na kusali sala zaidi ya 4, kumshukuru mwenyezi Mungu kunifikisha salama. Maana nikishika ramani ya Afrika nikiangalia nilipotea, nilikuwa na kila sababu ya kumshukuru mungu. Basi nilipofika hapo nilitafuta sehemu ya kulala na nikapelekwa hotelini na kupumzika. Kwenye hotel ile nililipia paund 1500, kwa siku moja, na baada ya siku mbili nilienda kukaa kwa rafiki yangu ambaye alikuwa afisa wa jeshi la Sudan kusini, alikuwa akiitwa Gabriel Bol Anuer.

Kwa wakati wote ule nilikuwa nikitembea kwa miguu ili kuweza kuufahamu kwa kina mji wa Juba. Kwa kweli nilikuwa nafurahi kuwaona watu wakiwa warefu na weusi, asilimia kubwa watu wa Sudan Kusini wamevaa heleni masikioni wake kwa waume. Na pia wengi wao hupenda kuvaa urembo wa shingoni. Kitu cha kushangaza ni kwamba, watu wa Sudan Kusini, hawapendi masuala ya picha, na hii ilinipelekea kukaa Sudan Kusini bila kuwa na picha nzuri, kwani picha nyingi nilikuwa napiga kwa woga, kwa maana mitaa mingi ilikuwa imezunguukwa na wanajeshi wenye sura za kutisha wakiwa na silaha nzito sana.

Nilipata kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba, ambapo nilishuhudia uwanja ukiwa busy sana, kwani ndege zinapaa na kutua kila dakika. Nikiwa pale uwanja wa ndege nilikutana na raia wa kila nchi na wengi wao walikuwa watumishi wa UN. Mitaa mingi ya Sudan Kusini imetulia sana huku magari ya thamani yakiwa yamepaki na mengine yakipita barabarani. Binafsi nilipenda sana kunywa chai nyakati za asubuhi, na chai zao zilikuwa tamu sana kutokana na aina ya viungo vilivyokuwa vinawekwa. Na kwenye kila mgahawa kwa nje ni lazima kunakuwa na watu wanavuta Shisha. Kule mjini Juba kuvuta shisha ni jambo la kawaida sana.

Kitu ambacho sitokuja kusahau ni siku ya jumatano tarehe 19/12/2019, nilipokuwa hotelini nikipata kinywaji, nilimuona mtoto wa baba wa taifa wa Sudan Kusini John Mobior Garang. Nilikuwa na furaha kwa maana nilikumbuka huko nyumbani Tanzania, kulikuwa na mada mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ikimzungumzia Mobior De Garang Mobior ambaye awali alikuwa waziri wa maji nchini Sudan Kusini. Nilitamani sana kumsogelea lakini kutokana na ulinzi wake ambao duuu…ulikuwa na watu warefu na wenye kutisha sana, lakini moyoni nilifurahi sana.

Kitu kingine nilichofurahia ni kugusa na kunawa usoni maji yam to Nile ambao unakatiza pale mjini Juba, na ukiwa hapo utakutana na daraja kubwa sana. Nilifurahi sana kugusa maji yam to Nile, kwa maana toka nikiwa elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, nilikuwa nasoma habari za mto huu. Kwani huwezi kusoma historia ya watu wa kale wa Misri bila kutaja mto Nile.

Kitu kingine kilichonishangaza sana nilipokuwa nchini Sudani Kusini, ni suala la madereva ya magari makubwa ya mizigo. Ukiwa huko utaona malori makubwa ya kubeba mizigo yakiwa yanaendeshwa na Wasomali. Yaani madereva wengi wa maroli huko yanaendeshwa na Wasomali. Na nilipouliza kwa nini asilimia kubwa madereva ni wasomali, nikaambiwa kuwa, watu wa Somalia wana roho ngumu, hawana uwoga na ni majasili sana. Ni kweli kwa maana nimekuwa nishuhudia maroli yakitembea usiku na mchana. Na bora mchana maana kunakuwa na ulinzi lakini usiku ni shida sana. Kutokana na sababu ya kuwepo kwa vikundi vya waasi vya msituni. Na kutoka Juba hadi Nimule ni misitu tu!

Nilikaa nchini Sudan Kusini kwa siku 28, ambapo huko nilijufunza mambo mengi sana hususani masuala ya historia ya wamasai na mambo mengine mengi sana mazuri na mabaya. Na nilipokuwa huko niliu]kutana na balaa zaidi ya mara tatu. Nikiwa huko mjini Juba niliporwa vitu zaidi ya mbili. Nilipoteza kamera, nilipoteza simu aina ya Iphone 4s, nilipoteza pesa zaidi ya $230.

Lakini kwa bahati nzuri walichukua tu vitu na kuachiwa uhai wangu. Kwa hakika sitokuja kusahau safari yangu ya kwenda nchini Sudan Kusini kufahamu historia ya Wamasai na kuangalia fursa za ajira za ualimu wa Kiswahili. Naamini siku moja ntarudi tena Juba nchini Sudan Kusini kwa maana hali ya sasa ni amani tofauti na miaka 10 iliyopita huko.

Hivyo katika makala hii ntaeleza suala la Mifugo kuwa mingi zaidi kuliko Wanadamu

Ni kwamba, Kulingana na ripoti kutoka shirika la chakula na kilimoa yaani Food and Agriculture Administration (FAO), zinasema kuwa, huko nchini Sudan Kusini kuna makadirio ya mifugo mingi kuzidi binadamu wanaoishi nchini humo. Kwani kuna ng’ombe milioni 12, kuna kondoo milioni 20 na kuna mbuzi milioni 25. Kwa namna hiyo nchi ya Sudani Kusini ni moja ya nchi yenye kuwa na idadi kubwa ya wanyama wanaofungwa hapa ulimwenguni.

Wakati mifugo ikiwa na idadi hiyo, mpaka kufikia mnamo mwaka 2018, idadi ya watu wa Sudan Kusini ni Milioni 10.98. Na kulingana na takwimu hizi, ina maana kuwa nchini Sudan Kusini wanyama wanaofungwa ni wengi kuliko binadamu wanaoishi nchini humo. Cha kushangaza sasa, pamoja na Sudan Kusini kuwa na wanyama wanaofungwa kwa idadi hiyo, bado nchi hiyo inategemea nyama kutoka nchi jirani. Kwani kwenye mfumo mzima wa maisha ya watu wa Sudan Kusini, kwao wanyama ni ishara ya utajiri. Na matumizi ya wanyama hao ni sifa na maali kwa ajili ya ndoa. Ambapo ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa, utamaduni huu bado upo hata hapa Tanzania kwa makabila kama Wamasai na Wasukuma. Na idadi kubwa ya watu wanaofunga ng’ombe ni wale wanaoishi vijijini.

Kwa namna hiyo mifugo nchini Sudan Kusini inaongezeka sana kwa maana mifugo hiyo haitumiki sana kwa masuala ya chakula. Na hata kama watatumika kwa masuala ya chakula basi ni kwa familia tu na sio kwa biashara. Na ukiwa nchini Sudan Kusini, vyakula vingi vinatoka nchi jirani, kwani asilimia kubwa watu wa Sudan Kusini hawana muda wa kulima kutokana na mtindo wa maisha yao. Na hivyo mifugo kwao ni suala la kujipatia sifa na ni sehemu ya utamaduni hasa kwenye masuala ya uchumba na ndoa.

Kwa hakika kuna mengi sana ya kusimulia juu ya nchi ya Sudan Kusini. Na kunahitajika karatasi zaidi ya 3000 kuweza kusimulia habari za Sudan Kusini. Na kutokana na mimi kufahamu habari za Sudan Kusini kuna idadi kubwa sana ya watu nimewasaidia kufika huko Sudan Kusini kwa kuwapatia taarifa zenye ukweli na zenye uhakika. Kwa kweli Sudani Kusini ni nchi ambayo kwa namna Fulani ipo salama kuishi hasa kwa sisi watanzania. Japo bado kuna changamoto kubwa sana ya masuala wa ajira kule. Lakini kuna baadhi ya taaruma zinahitajika sana, hasa hasa, masuala ya biashara, teknolojia na afya.

Nadhani kuna machache umeyapata kupitia makala hii. Na kama kuna mengi zaidi unahitaji kujua, unaweza kuwasiliana nami na kuweza kukufahamisha unayohitaji kujua, kulingana na uzoefu wangu, kwa maana kamwe siwezi kujua yote lakini naamini yapo ya kujifunza.

-------------------
Ahsante sana kwa mara ya kwanza nimesoma article ndefu kama hii. Wewe ni noma
 
Mkuu Nakuomba uendelee kufuatilia kwani nina uzi za kutosha kuhusu makala za safari za ndani na nje ya Tz na zote zitaletwa hapa hapa JF... Zina sisimua na kukufanya ujifunze mengi kana kwamba upo live... #Makala
Inaonekana wazi wazi kuwa hii ni safari yako ya mwanzo kutoka nchini Tanzania.Afadhali umekuwa mkweli katika uandishi na kuonesha sura yako halisi. Pale ulipoambiwa watanzania kuingia kule hakuna shida ulitafsiri hakuna visa wala masuala yoyote.Hivyo ulipodaiwa dola 50 ukaanza ubishi.Una bahati sana wale watu walikupenda na kukuwachia uingie bure.

Ujuwe kila nchi mpakani ina masuala ya uhamiaja na aina ya visa ya kituo unachoingia bila kupata mwaliko ni aina moja ya viza rahisi lakini sio bure.

Umeanza kutoka nje ya nchi kwa kutumia mabasi uliyoyazoea kule Tabora.Ungesafiri kwa kutumia ndege za kimataifa na ikawa safari yako ni ya kubadilisha ndege kwenye miwanja mikubwa ya kimataifa na sio kama ule wa Dar es salaam au ule wa Juba basi nadhani ungeaachwa uwanjani na ndege ukajitafutia balaa jengine. Ungekuwa unashangaa shangaa na usipate hata wa kumuuliza kwani kule huwa wanatumia mifumo ya kielektronic tu hata spika hawazitumii tena isipokuwa kwa dharura kubwa itakapokuwa kuna mtu kapotea hajaingia kwenye ndege.

Halafu tangu mwanzo umeshaambiwa ile nchi haina usalama, wewe umeshikilia kupiga piga picha na kutembea na kamera kwapani.Hiyo kamera kuporwa ni adhabu ndogo.Ungepigwa kabisa sijui ungmlaumu nani.

Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu urudi tena huko na siku moja ufike angalau London.Ukiniona utanishtua nitakuwa pamoja nawe lakini mambo ya kuingia mabaa kupata kinywaji itakuwa ndio mwisho wa urafiki wetu.
 
Mkuu asante sana mimi naomba kujuzwa jamaa salam zao natamani kujua wanasalimianeje asubuhi mchana na jioni asante
 
1602779994138.png

Uwanja fulani wa ndege niliowahi kutua. Hapo dereva wako wa teksi lazima awe ni mzoefu.Akiwa mshamba akafuata hiyo ya kulia au ya katikati ndiyo keshakupotezea safari kwa sababu zote zinafika uwanjani lakini hakuna njia ya kupinda kurudi wala kukatisha kuelekea kule Arrivals na departure na masafa yake huko ndani kwa ndani ni kilomita kadhaa.Kuna vitreni vidogo vya glasi lakini hata ukifika lango ulilokusudia muda umekwenda sana.Utakuwa umesubiriwa sana na ndege imepitisha muda wa kusubiri abiria aliyepotea na kuondoka zake.
Nakupa picha tu siku utakayotua kwenye mchi yenye viwanja kama hivyo
 
Back
Top Bottom