Ushuhuda wa breakthrough!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,402
19,070
Naomba niweke hapa ushuhuda huu, hata akiusoma mtu mmoja tu kwangu inatosha, unaweza kubadilisha maisha yake kwa namna moja au nyingine. ni juu ya yale Mungu amenitendea leo hii, siwezi kunyamaza.

kwa muda wa miezi kadhaa nimekuwa nikipitia kwenye kipindi fulani cha jangwani, na januari hii ikaja kuongeza makali yake. hii inatokana na kuyumba fulani kwenye biashara yangu fulani, na ilitokana na makosa niliyoyafanya ya kupeleka pesa nyingi kwenye ujenzi wa nyumba Dodoma na viwanja viwili besides ya hiyo nyumba (namshukuru Mungu kwa hilo pia). na niwe muwazi, nilishaachaga kutoa fungu la kumi (zaka) zamani tu pamoja na kwamba nilikuwa nasali.

kutokana na ujenzi na manunuzi ya viwanja, niliyumba sana kipesa na nikapitia wakati mgumu sana. Mimi nimeokoka, ninasali kanisa la kilokole lakini sio hayo ya mafuta na manabii wa kisasa.

nilipita kwenye mitandao nikakutana na mchungaji mmoja anahubiri kwamba fungu la kumi ni lazima kutoa na kwa kutoa fungu hil (Malaki 3:10-12) ni njia ya kumjaribu Mungu, Mungu ametangaza agano ambalo hawezi kutengua kwasababu yeye sio mwanadamu hata aseme uongo, kwamba kwa mtu anayetaka kumjaribu ili amwone kama hatafungua madirisha ya mbinguni, atoe fungu la kumi (hata kama kuna sadaka zingine) ili kiwemo chakula katika nyumba yake.

as soon as nilipoamua moyoni kuwa mtoaji, nikapita sehemu tena mchungaji mwingine akawa anafundisha kwamba fungu la kumi lilikuwa kwa ajili ya agano la kale tu, wakati wa agano jipya hatulazimiki kutoa, lakini nilishasoma pia Mathayo 23:23 na Luka 11:42, Yesu aliwaambia mafarisayo kuwa besides wanayotakiwa kuyafanya, hawatakiwi kuneglect fungu la kumi. hivyo nilikuwa kwenye njiapanda, na nilivyo mdadisi, mchungaji mmoja anasema fungu la kumi ni agizo la Mungu, mwingine anasema sio lazima kwa sasa. ila nikaazimia moyoni lazima nipate ukweli kwa kufanya practical. Mungu alinijalia fedha fulani kufikia kam 4m ambayo iliisha hata sikujua iliishaje ni kama ilipitia kwenye mfuko uliotoboka, lakini ikatakiwa nitoe fungu la kumi lake sasa mwishoni mwa mwezi wa kwanza huu kwasababu nilidhamiria kujaribu kurudi kule awali ambako nilikuwa natoaga fungu. actually, zamani nilipokua natoa fungu la kumi nilikuwa sijawahi kuishiwa pesa sasa nafikiri sikuwa najua kama ndio zilikuwa baraka za Mungu nikaachana nalo na ukiacha kuja kuanza tena ni mbinde kwasababu shetani hataki uanze kwasababu anajua ukianza kutoa tu utabarikiwa.

kupunguza maneno mengi, nilichodhamiria kufanya ni kuanza kutoa fungu la kumi sambamba na Neno la Mungu linavyosema ili nimjaribu Mungu kama alivyosema tumjaribu, sio kwasababu Mungu ananidai, bali kwasababu Mungu amesema tufanye hivyo kama namna ya kumjaribu ili tuone kama hatafungua madirisha ya mbinguni na kutumwagia baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha. nikatoa fungu la kumi kwenye 4m hiyo, tena nilikuwa nahitaji sana hiyo potion na tayari nilishaitumia hivyo nikahisi mwisho wa mwezi nipate pesa nitoe, nikapata ile inayotosha fungu la kumi tu, ikabidi nitoe kwa imani ili mimi nibaki na Mungu tukiangaliana usoni.....

baada ya kutoa fungu linalouma na ambalo wakati huo nilikuwa nalihitaji mno, nikaanza kuangalia Mungu atafanyaje, I was like testing to see whether Mungu bado anahitaji sisi katika agano jipya tutoe au la, manake kama Mungu angereact in accordance with his word ni uthibitisho kwamba anataka tutoe, kama singereact nisingefuata. hivyo nilimjaribu Mungu kama yeye alivyosema tumjaribu.

wandugu, baada tu ya kufanya hivyo, ndio kipindi kigumu kilizidi, nilipita kwenye jangwa moja hatari ambalo nilishawahi pitaga miaka 12 iliyopita, na nilikuwa sioni njia kabisa, akili yangu yote ilishindwa kupata suluhisho, elimu, marafiki, career, ndugu n.k vilishindwa. nikaingia kwenye maombi na kuanza kumuuliza Mungu mbona sasa huonekani kama ulivyoahidi kwenye Neno lako wakati mimi nimekujaribu? au hukuwa unamaanisha nilivyofanya? nilivyomaliza tu maombi, nikakutana na clip moja ya mchungaji anatoa ushuhuda kwamba, UKIWA UMEOMBA UKAONA MUNGU KAMA HATOKEI, Jua kuna mambo mawili. aidha, haupo kwenye njia sahihi hivyo Mungu hajasikia, au kama wewe unaona upo kwenye njia sahihi, jua Mungu ameshajibu, hivyo relax subiri kuona matokeo. gafla moyoni nikashuhudiwa kuwa Mungu ameshajibu na atakushangaza muda si mrefu, kuna sauti ya Roho Mtakatifu yenye uhakikisho huwa inaongea, wale waliookoka wanajua ninachosema. nikaamua kurelax.

SASA LEO majira tarehe 04/02/2022 majira ya saa kumi na moja jioni, Mungu ameamua kunishangaza, amefungua mlango wa pesa mahali ambapo sikutegemea kabisa kwamba pangetoa pesa, sikustahili kuzipata, amenipa tu na wala sikuzitolea jasho, kama huwa unasikia kuwa Mungu alishawahi kutoa maji kwenye mwamba wana wa Israel wakanywa jangwani, ndio imekuwa kwangu, sikutegemea kupata ile pesa, sikustahili kuipata, na sikuitolea jasho, imekuja tu, na kwasababu imekuja siwezi kunyamaza kama haijaja, Mungu ameamua iwe hivyo, naona shetani alikuwa amepafunga tu nilango na madirisha ya mbinguni ya baraka zangu kwa hila zake, Mungu kafumua lango hilo na nimepata millions of money ndugu zangu. sisemi uongo. Mungu amenifanyia sapraizi jamani.

sasa, nina uhakika wa kurevive biashara yangu yote kwasababu hela niliyopewa na Mungu (ambayo hata sikustahili ni neema yake tu na nilikuwa sitegemei kwasabbu sikuifanyia kazi), millions, inatosha kufufua biashara yangu, inatosha kujenga nyumba zingine kwenye viwanja viwili besides ile niliyokuwa najenga, inatosha kuongeza mtaji mkubwa tu kwenye biashara ya mke wangu.

na zaidi ya yote, hata kwa hiyo nayo, nitamtolea Mungu fungu la kumi. Mungu anisaidie nisiache kwasababu hapo ndio nimethibitishiwa na Mungu kwamba ndiko eneo la kumjaribu Mungu. Malaki 3:10-12) anasema leteni zaka kamili ghalani mwangu ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo muone kama sitafungua madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha, namni nitamkemea yeye alaye na kuharibu mazao yenu..., hivyo kumbe Mungu amemkemea shetani aliyekuwa amefunga milango ya baraka, sasaivi ninaye mkemeaji kwenye biashara yangu, kwenye career yangu etc. Jina la Bwana litukuzwe.

ushauri wangu kwako msomaji, uanze kutoa fungu la kumi, ila toa kwenye udongo mzuri, kwa maana kwamba utoe sehemu ambayo watu wanamwabudu Mungu katika roho na kweli, kwa upande wangu mimi huko huwa naamini ni sehemu ambayo watu wameokoka wanaenda mbinguni (nikiwa muwazi tu) sio sehemu watu wanaabudu dini na Mungu hayupo, utapoteza pesa yako kwasababu haitaenda kwenye kazi/ghala la Mungu. kwa aliyeelewa, usiache fungu la kumbi, usiache fungu la kumi, usiache fungu la kumi ! utakuja kunishukuru.

Sifa na utukufu kwa Mungu. ushuhuda huu ni wa kweli kabisa na umenitokea leo hii, kwa atakayeamini aamini, kwa atakaye neglect aneglect ila mimi nimeshautoa.
 
Imani ikizidi hichi ndicho kinachotokea na kuwa played na your own mind.
Elon musk, bill gate, jeff bezos, mo, bakheressa hawa jamaa bila shaka hawajawahi hata kutoa fungu la 3 lakini angalia gape walilokupiga.

Una point kuback that up?
 
Imani ikizidi hichi ndicho kinachotokea na kuwa played na your own mind.
Elon musk, bill gate, jeff bezos, mo, bakheressa hawa jamaa bila shaka hawajawahi hata kutoa fungu la 3 lakini angalia gape walilokupiga.

Una point kuback that up?
Hao jamaa uliwataja fedha wanazorudisha kwa jamii. Unajua idadi yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endelea kutajirisha wachungaji tu huku wakikuita kondoo
amini usiamini, fungu la kumi ni agizo la Mungu, hasa kama utatoa mahali ambapo Mungu yupo, hautakuja kujuta.nimethibitisha kwenye maisha yangu leo, though miaka kadhaa pia nilikuwa natoa na nilikuwa natembea kwenye baraka sasa sikuwa najua baraka zinakotoa,nilijua zinakuja tu. pamoja na kwamba kwa watoaji, usitoe kama unadaiwa na Mungu, toa kwa moyo wa kupenda kwa Mungu wako na kwa kufuata Neno lake yeye amesema nini?amesema mkanijaribu kwa njia hii muone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwawamwagieni barakak hata isiwepo nafasi ya kutosha, nami nitamkemea yeye alaye na kuharibu....., mimi naishi nikijua sihitaji mganga, sihitaji hirizi kwenye ulinzi wangu na biashara yangu, Mungu atawakemea na kuwafyekelea mbali kwa ajili yangu. huu ndio ukweli, ukitaka chukua, usipotaka acha.
 
Imani ikizidi hichi ndicho kinachotokea na kuwa played na your own mind.
Elon musk, bill gate, jeff bezos, mo, bakheressa hawa jamaa bila shaka hawajawahi hata kutoa fungu la 3 lakini angalia gape walilokupiga.

Una point kuback that up?
Mkuu umejuajee kuwa hawa hawatoei mkuu,bill gates daily anatoa misaada all the word ndio ashindwe kutoaa fungu la kumi,kwan kutoaa fungu la kumi n dhambi mkuu ??iman yake yy mwandishi ndio ameani hvyo kuwa akitoa fungu la kumi atafanikiwa nayo n dhambi yy kusema???
 
Imani ikizidi hichi ndicho kinachotokea na kuwa played na your own mind.
Elon musk, bill gate, jeff bezos, mo, bakheressa hawa jamaa bila shaka hawajawahi hata kutoa fungu la 3 lakini angalia gape walilokupiga.

Una point kuback that up?
kuna baraka na pesa za aina nyingi. kuna pesa zinatokana na mashetani, freemason, majini n.k, pia kuna pesa zinatoka kwa Mungu kabisa. sisi tunaomwamini Mungu tunaamini kwamba, "baraka za Mungu hazina majuto". yani Mungu akikubariki hutajuta, hutatoa kafara, ni furaha. unaweza usiwe na pesa kama za hao matajiri wa dunia lakini ukawa tajiri kwa kuwa na Mungu anayekupa provisions, na pia anayekupa uzima. Mungu ndiye ameshikilia pumzi za wote, na Biblia inasema Mungu ndiye atupaye utajiri. namshukuru Mungu kwasababu ananipa baraka na ninaye yeye kwenye maisha yangu, kuliko mabilioni ningekuwa nayo lakini sina Mungu...sihitaji hilo.
 
Atajuliaa wap amejuropokeaa tu ,angejuaa hao hawaishii kutoaa fungu la kumi na makanisa na misikiti wanajengaaa
 
Asante kwa ushuhuda, Mwenyezi Mungu akubariki kwa kushuhudia matendo makuu aliyokutendea, kushukuru ni kuomba tena, watakaobadilika kupitia uzi huu utapata baraka nyingi mno. Nami naungana nawe, atakayekubali akubali, atakaye neglect aneglect, mwenye masikio na asikie na mwenye macho na aone. Ubarikiwe sana
 
Mkuu umejuajee kuwa hawa hawatoei mkuu,bill gates daily anatoa misaada all the word ndio ashindwe kutoaa fungu la kumi,kwan kutoaa fungu la kumi n dhambi mkuu ??iman yake yy mwandishi ndio ameani hvyo kuwa akitoa fungu la kumi atafanikiwa nayo n dhambi yy kusema???
Mungu ndiye anajua. ila cha muhimu nimekwambia, uwe tajiri kama wao au uweje, jua kuwa Mungu ndiye atupaye utajiri wa kudumu na wa furaha, utajiri mwingine unaotoka huko kwingine hauna faida kwetu kwasababu haujatoka kwa Mungu na hauna Mungu maishani. Mungu amesema kwenye Neno lake kwamba ÿeye Mungu ndiye atupaye utajiri na kwamba baraka za Mungu hazina majuto, ukibarikiwa na Mungu hutajuta....na tunaamini alichokisema Mungu ndicho cha kweli. na utajiri wa Kimungu sio tu wa fedha ambazo pia atakupatia kama atakavyonipatia mimi, bali ni utajiri wa uhakika wa maisha kwasababu upo mikononi mwa Mungu aliyeshika uhai wa wanadamu wote. umeona korona ilivyochekecha matajiri, watu wana pesa lakini hazikuwasaidia? pesa bila Mungu sio utajiri wa kutosha.
 
Umepata sh ngapi? Imetoka kwenye investment gani? Au ni mtu kakuletea?
Wana wa Israel walipokuwa jangwani, ilifika mahali hakuna maji kabisa, wakalia kwa Mungu, Mungu akamwambia Musa apige mwamba, alipopiga mwamba kwa fimbo, maji yakaanza kutoka kwenye mwamba (jiwe). sehemu ambayo sio kawaida maji kutoka. waliposema wanataka kula nyama, Mungu akaleta kware, hawakujua zilikotoka, wakala nyama ya kware hadi ikakinai. Mungu kamwelekeza mtu aniletee tu pesa ndefu, free of charge. kabisa kabisa.
 
fungu la kumi ni ten percent ya kipato chako (kama ni mfanya biashara ni faida unayoipata, kama mfanyakazi ni 10% ya mshahara wako). unautoa kwa Mungu, hautoi kwa watu. charities hizo ni kitu kingine na haimaanishi ukishatoa fungu la kumi usitoe charities. cha Mungu mpe Mungu, cha wanadamu wape wanadamu, cha kaisari mpe kaisari.
 
Back
Top Bottom