Yericko: Makonda Aitwe Bungeni,Tuhuma za Kesi ya Uhaini ya mawaziri, Na Generali Mobeyo Aitwe kueleza Bunge ukweli wa Kesi ya uhaini Uliofanyika 2021

Makonda ndiye mtu pekee anayeweza msaidia Samia , ambaye amezungukwa na genge la Msoga ambalo halimtaki kwa Sasa

Samia awarudie kundi la Magufuli na kuachana na Msoga hili kundi la Magufuli ndilo la kumvusha
Lakini kwa Mujibu wa Katiba Mkuu wa Mkoa Sio Mshauri wa Rais..
Au inakuaje ??
 
Nisahihi kusema Baraza la mawaziri limefitinika??
Kwamba lina wasaliti wanaoshiriki kutukana taasisi iliyowateua!!
Waziri mkuu anayajua haya? Ameyakalia kimya? Kama sio part of solution je yeye ni part of the problem?
Kama baraza la mawaziri Likifitinika Kisheria na Kikatiba maana yake ni kwamba hakuna Serikali tena Rais anaongoza nchi bila muongozo au bila serkali
 
Makonda ndiye mtu pekee anayeweza msaidia Samia , ambaye amezungukwa na genge la Msoga ambalo halimtaki kwa Sasa

Samia awarudie kundi la Magufuli na kuachana na Msoga hili kundi la Magufuli ndilo la kumvusha
Unataka nchi irudi gizani tena?? Au nawewe ni miongoni mwa lile kundi la wasiojulikana?? Hatuhitaji kuona tena watu wakishambuliwa kwa risasi mchana kweupee bila wahusika kuchukuliwa hatua wala kuhojiwa.
 
W

Wewe Chadema huwezi kumtakia Mh Samia ashinde 2025, eti unamtahadharisha kabisa kuwa akiendelea kumuacha Makonda katika uongozi atashindwa uchaguzi. Kwani nyinyi Chadema mnataka Rais ashinde 2025?
Unatumia fursa ya alichosema
Mskonda kutaka kulipa kisasi kwa Rais kunfukuza kazi Makonda?
Jambo la heri kwa Rais Samia haliwezi kutoka mdomoni mwa kada kindakindaki wa Chade.a.
Baada ya kusema hayo rudi kwenye hoja
 
Ccm wana namna yao wanavyoendesha mambo yao,ukitaka kuwaelewa au ukitaka wafanye jambo kama ambavyo utaratibu unaeleweka kwa kila mtu utapoteza muda bure.

Ndani ya CCM unaweza kurupuka tu kama mwehu asubuhi,ukadai rais anataka kupinduliwa na mambo yakaisha hivyo hivyo😁😁,hata police bawawezi kuomba muongozo zaidi wa madai yako,achia mbali kukuhoji.
Katiba ya nchi hata ikikanyagwa na ccm kama jpm alivyokuwa anaichezea vyovyote anavyojisikia poa tu. Ndivyo unavyotaka kusema?
 
Makonda ndiye mtu pekee anayeweza msaidia Samia , ambaye amezungukwa na genge la Msoga ambalo halimtaki kwa Sasa

Samia awarudie kundi la Magufuli na kuachana na Msoga hili kundi la Magufuli ndilo la kumvusha
Kundi la Magufuli litamvusha kwenda wapi? kwani si anamalizia awamu ya tano ya Magufuli kikatiba? au ameigeuza awamu ya 5 kuwa ya awamu 6 muhula wa kwanza. Mshaurini mama aridhike na alichopewa bure na M/Mungu na asiwe na tamaa ya uraisi.
 
Hao " wenye CCM Yao", wasiomtaka RC ni akina nani?

Nijuavyo Mimi, chama ni Cha wanachama wote, wanaingia na Kutoka daily, hao "wenye chama" ni akina nani Hasa?

Yeriko akiulizwa hapo " CHADEMA wenye chama" ni akina nani, atajibuje?
 
Watawala wamemweka Makonda makusudi ili wawape kazi Watu kama Yericko Nyerere kukosa muda wa kupanga ya kwao.

Makonda yupo kwaajili Political Drama,
Kwa jamii ya kitanzania na nature ya siasa za upinzani hapa nchini, Makonda ni kete muhimu kuitumia ili kuwapoteza maboya mahasimu wa CCM

Nakubali Makonda ni kete inachezeshwa, lakini je…kete hii inaenda sambamba na ile ya Mange wa New York kumvua nguo Madame President?

Kuna mipaka ikivukwa ujue bendera nyekundu imepeperushwa tayari na wahusika tu ndio wanaiona, kwa sasa.
 
Mimi simfuatilii Mañge.
Sijajua nini kapost ambacho Watu wanakipigia kelele.

Kwamba Mange kuna mtu amemlipa?
 
Huyu mdau, Anahoja, Tunahitaji majibu ya kina.
Hivi ni kweli General Mobeyo alitamka kwa kinywa chake kwamba kuna watu /kundi halikutaka Madame Samia aapishwe? Hadharani msibani?

Ama kumwambia Rais Samia kwamba anamazungumzo nae, wao wawili tu, ndio ina maana hiyo?

Hoja ya Yericko hapa ni kwamba anamtahadharisha Rais Samia kuhusu Makonda na kwamba Yericko leo hii anasema Makonda alifanikiwa kumtia uoga marehemu Rais Magufuli? Kwamba blackmail za Makonda kwa marehemu Magufuli ndio ziliuzaa “udikteta wa marehemu Magufuli? Hii ndio hoja?

It’s either Makonda is too overrated ama tunatishwa na kinyago tulichokichonga wenyewe. Na Kama ni hofu, hii hofu inatokana na nini haswa?

What do these humans have in their closets?!
 
Mimi simfuatilii Mañge.
Sijajua nini kapost ambacho Watu wanakipigia kelele.

Kwamba Mange kuna mtu amemlipa?
Sifahamu Kama analipwa.

Umesema kuhusu Makonda kuwa kete muhimu for dramatic reasons, nikahoji kuhusu Mange na kashfa zake chafu juu ya Rais Samia nayo ni kete?

Na Kama sio kete ni nini ama nani mwenye maslahi na anayoyafanya Mange Kama ilivyo kwa Makonda?
 
Mange hayupo serikalini Mkuu.
Ila Makonda ni mserikali na mccm yupo kwenye majukumu yake ya kila siku
 
Katiba ya nchi hata ikikanyagwa na ccm kama jpm alivyokuwa anaichezea vyovyote anavyojisikia poa tu. Ndivyo unavyotaka kusema?
kuna rais halafu katiba inafuata,kama huamini utaendelea kusema rais anachezea katiba.

Rais ni mwenyekiti wa chama tawala.
Rais ni amiri jeshi,wa jeshi linalolinda katiba.
Rais ni mteuzi wa wakuu wote wa taasisi serikali kuu.

Unaweza ukaona ni kwa namna gani katiba inapata nguvu kwa hisani tu za rais sio kwa kujisimamia yenyews.
 
Back
Top Bottom