Makonda awaweka matumbo joto Mawaziri

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Rukwa. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amewaambia viongozi wa Serikali, wakiwamo mawaziri kuwa si lazima wampende.

Amesema akihitimisha ziara katika mikoa 20 ataanika udhaifu uliopo katika kila sekta.

Makonda ameeleza hayo leo Jumanne Februari 6, 2024 alipozungumza na wananchi wa Laela wilayani Sumbawanga, mkoani Rukwa akiwa njiani kuelekea Mkoa wa Songwe.

Makonda ameshafanya ziara katika mikoa 13 na leo ameingia wa 14 ambao ni Songwe. Mingine aliyotembelea ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tabora, Shinyanga, Singida, Simiyu, Kigoma, Katavi na Rukwa.

"Tutaweka bayana udhaifu wa kila sekta, ili mtu ajitathamini, anafanya kazi yake kama inavyotakiwa? Hatuwezi kuwa tunalipwa mshahara halafu wengine hamfanyi kazi.

"Bahati mbaya wengine wamepewa wizara, badala ya kuhangaika kufanya kazi ya wizara ili kujenga heshima ya Rais (Samia Suluhu Hassan) aliyewaamini wanahangaika kutafuta vyeo na kutengeneza mitandao yao, kucha kutwa kuwalipa watu kuwasifia, wakati kwenye mamlaka yao mambo hayaendi," amesema.

Makonda aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema: "Mimi mnichukie sijaja ili mnipende, nimepewa kazi ya kuwasemea wananchi na CCM, nitasema ukweli daima fitina kwangu mwiko, bahati mbaya mimi si muoga."

Januari 28, 2024 akiwa mkoani Shinyanga, Makonda alisema baada ya kuhitimisha ziara atawasilisha orodha ya watendaji wazembe kwa Rais Samia, ili kuchukuliwa hatua.

"Baada ya ziara hii nitakabidhi ripoti na hatua mtaziona, nimekula kiapo nitawapigania wanyonge wa Taifa hili, niwaambie watumishi wote wa Serikali ngazi zote, ukiboronga au kuharibu Makonda hatakutetea utabeba mzigo wako," amesema.

Kabla ya kuanza safari ya kuenda Songwe, Makonda na msafara wake walizuru kaburi la mwanasiasa mkongwe, Dk Chrisant Mzindakaya aliyefariki dunia Juni, 2021 kwa maradhi ya moyo.

Dk Mzindakaya alijizolea sifa na umaarufu katika miaka 1990 kutokana na umahiri wake wa kuibua hoja na tuhuma zilizotikisa kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na hayati Benjamin Mkapa na kupachikwa jina la 'mzee wa mabomu'.

Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM ikiwemo ubunge wa Kwela aliohudumu kwa miaka 45 kabla ya kustaafu mwaka 2010.

"Tuwaenzi wajane hawa tuwaheshimu na tuwape heshima ileile tuliyokuwa tukiwapa wakati waume zao wapo hai, wazee wakishaondoka na vyeo basi tunawaacha," amesema Makonda.
 
"Bahati mbaya wengine wamepewa wizara, badala ya kuhangaika kufanya kazi ya wizara ili kujenga heshima ya Rais (Samia Suluhu Hassan) aliyewaamini wanahangaika kutafuta vyeo na kutengeneza mitandao yao, kucha kutwa kuwalipa watu kuwasifia, wakati kwenye mamlaka yao mambo hayaendi" - Makonda
Rukwa. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amewaambia viongozi wa Serikali, wakiwamo mawaziri kuwa si lazima wampende.

Amesema akihitimisha ziara katika mikoa 20 ataanika udhaifu uliopo katika kila sekta.

Makonda ameeleza hayo leo Jumanne Februari 6, 2024 alipozungumza na wananchi wa Laela wilayani Sumbawanga, mkoani Rukwa akiwa njiani kuelekea Mkoa wa Songwe.

Makonda ameshafanya ziara katika mikoa 13 na leo ameingia wa 14 ambao ni Songwe. Mingine aliyotembelea ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tabora, Shinyanga, Singida, Simiyu, Kigoma, Katavi na Rukwa.

"Tutaweka bayana udhaifu wa kila sekta, ili mtu ajitathamini, anafanya kazi yake kama inavyotakiwa? Hatuwezi kuwa tunalipwa mshahara halafu wengine hamfanyi kazi.

"Bahati mbaya wengine wamepewa wizara, badala ya kuhangaika kufanya kazi ya wizara ili kujenga heshima ya Rais (Samia Suluhu Hassan) aliyewaamini wanahangaika kutafuta vyeo na kutengeneza mitandao yao, kucha kutwa kuwalipa watu kuwasifia, wakati kwenye mamlaka yao mambo hayaendi," amesema.

Makonda aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema: "Mimi mnichukie sijaja ili mnipende, nimepewa kazi ya kuwasemea wananchi na CCM, nitasema ukweli daima fitina kwangu mwiko, bahati mbaya mimi si muoga."

Januari 28, 2024 akiwa mkoani Shinyanga, Makonda alisema baada ya kuhitimisha ziara atawasilisha orodha ya watendaji wazembe kwa Rais Samia, ili kuchukuliwa hatua.

"Baada ya ziara hii nitakabidhi ripoti na hatua mtaziona, nimekula kiapo nitawapigania wanyonge wa Taifa hili, niwaambie watumishi wote wa Serikali ngazi zote, ukiboronga au kuharibu Makonda hatakutetea utabeba mzigo wako," amesema.

Kabla ya kuanza safari ya kuenda Songwe, Makonda na msafara wake walizuru kaburi la mwanasiasa mkongwe, Dk Chrisant Mzindakaya aliyefariki dunia Juni, 2021 kwa maradhi ya moyo.

Dk Mzindakaya alijizolea sifa na umaarufu katika miaka 1990 kutokana na umahiri wake wa kuibua hoja na tuhuma zilizotikisa kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na hayati Benjamin Mkapa na kupachikwa jina la 'mzee wa mabomu'.

Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM ikiwemo ubunge wa Kwela aliohudumu kwa miaka 45 kabla ya kustaafu mwaka 2010.

"Tuwaenzi wajane hawa tuwaheshimu na tuwape heshima ileile tuliyokuwa tukiwapa wakati waume zao wapo hai, wazee wakishaondoka na vyeo basi tunawaacha," amesema Makonda.
Mmh! Jiwe limetupwa gizani, atakaye piga kelele tu ya maumivu ujue limempata. Acha wafu wazike wafu wao, mchimba kaburi yupo kazini.
 
Huwezi kumfukuzisha kazi mtu ambaye hukushiriki kumuajiri. Itakuwa ni upumbavu wa kiwango cha makonda
 
Sasa hivi yupo chini ya Waziri wa TAMISEMI, anatakiwa kila siku atoe ripoti ya mkoa.
 
Back
Top Bottom