Yericko: Makonda Aitwe Bungeni,Tuhuma za Kesi ya Uhaini ya mawaziri, Na Generali Mobeyo Aitwe kueleza Bunge ukweli wa Kesi ya uhaini Uliofanyika 2021

Nchi hii baada ya Mwinyi, Mkapa na Magufuli kuondoka mtu “mkubwa” wakuheshimika anayeijua nchi nje ndani ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Sasa alieleze taifa kama ni huyu kiongozi wetu mstaafu anawatuma hao mawaziri au ni porojo zake tu zinazohatarisha taifa.

Makonda, huyu ana kublackmail hadharani na sirini. Alifanikiwa kwa Hayati Magufuli akamtia hofu sana, Magufuli akawa Rais Dikteta asiye na mfano, akaumiza watu wengi sana, Baada alikuja kustuka lakini akiwa ameshachelewa jini likiwa lishatoka katika chupa

Hizi nguvu mbili ndiyo hatari kwa nchi hivi sasa

 
Nadhani inahitajika tume ya kuchunguza chanzo cha kifo cha Rais John Pombe Magufuli akiwa madarakani. Ifahamike tu kama tulichagua Rais mgonjwa mgonjwa bila kujua kuwa asingevuka kipindi chake cha pili wakati mengine wakijua kuwa hatavuka. 🧐 🧐
 
Huoni kwamba Hapo ndipo ulipo ufanano wa Mange na Makonda, tofauti ni mmoja ni hadharani wakati mwingine ni mafichoni?

Haiwezekani kwenye awamu ya tano mchezesha kete pia aliwachezesha kwa namna ile ile wanayochezeshwa sasa hivi?

Na master wa awamu ile ndio wa awamu hii?

Mmoja yuko upande wa Rais mwingine yuko dhidi ya Rais, ni Kama marudio ya awamu ya tano?!

Je hakuna pattern hapo ya mchezesha kete?

Anaendelea sasa kwasababu lengo lake halijatimia? Ama ndilo lengo tangu awamu hiyo ila sasa anaendelea na mchezo wake?

Unataka kusema ni vita ya Rais na Rais?

Kwa muono wangu, sina hakika kama kuna kitu kama hicho
 
watanzania tumeshasahau mambo ya CAG tumerukia mambo ya kibaka wa koromije hii nchi raha sana na aslay akitoa pilau part 2 tutasahau ya bashite. muhudumu tuongezee tano watu tulewe huku. cheers wanangu
 
Sijasema chochote, nimeuliza maswali kupata maoni yako kutokana na maoni yako ya mwanzo kuhusu Makonda kuwa kete.

Hakuna mchezo wenye Kete moja. Mchezeshaji anatambua hili.

Ni kweli Michezo mingi inakete nyingi.
Labda mchezeshaji anatumia mchezo wa Golf.

Sioni kama Mange awe kipaza sauti cha mtu aliyenyuma aliyejificha.
Yule ni kama mercenary
 
Unataka kusema Rais hawajui wateule wake
Hell No anawajua vizuri sana
Rais hajaingia siasa leo wala jana na anawajua wote kwa tabia zao
Kuna watu unaweza kumuona ana biashara zake ila kuna mmoja ni mwizi sana na anamuibia tajiri na kila wakishtaki tajiri anamuacha tu
Kumbe kuna maslahi makubwa au siri kubwa nyuma yake

Tuwaache wao ndio wanajuana
Mama kakataa aitwe mama ila jamaa anamuita tena mara mbili
Siasa za nchi masikini zinaenda kwa matukio lakini maendeleo hakuna zaidi kumalizana tu na majungu
Watu wanatafuta mali nothing else
 
Anaandika Yericko Nyerere

Wengi mmeomba nitoe maoni yangu kuhusu kauli za mtu anayejiita Paulo Makonda kwamba kuna mawazi wanawalipa watu ili kumtuna Rais na kwamba mawaziri hao wana wawatu nyuma ambao ni watu wa kuheshimika katika nchi.

Kabla sijazungumzia kauli hiyo naomba niwarejeshe kwenye kauli ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu General Mabeyo kwamba kuna watu walitaka Makamu Rais asiapishwe, Kauli hii hadi leo haijajibiwa ni akina nani hao walioleta mabishano ya kikatiba hadi Jeshi likasimamia Katiba? Kimantiki na ushahidi wa mazingira ni wale waliokuwa mdarakani baada ya Hayati Magufuli kufariki, sasa ukimtoa makamu Rais, anayefuatia ni Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Jaji Mkuu, hawa ndio viongozi waliokuwa katika madaraka kikatiba na kisheria baada ya Rais kufariki.

Swali halijajibiwa nani alipinga Katiba kutekelezwa ili makamu rais asiapishwe? Lakini swali lingine muhimu linaibuka, Nani alikuwa nyuma ya Mabeyo akaamrisha katiba ifuatwe na kwamba Makamu Rais aapishwe amalizie muhula wake wa 5? Tukimjua huyu basi tuhoji muhula wa 5 upo au Samia amebadilisha na sasa anajiita wa muhula wa 6 ambapo anataka akaumalize 2030 kama nyimbo zinavyoimbwa? Tukijua hapa huu ndio mzizi wa ugomvi mkubwa wa kisiasa ndani ya CCM. Ifahamike huu ni ugomvi wa ccm sasa wanaoshindwa vita wanauleta nje uwe ugomvi wa Taifa. Tukatae! Kwanza Binafsi sioni logic ya Rais kutukanwa ikawa agenda ya kitaifa ikaandaliwa jukwaa lililosahaulika 40yrs, Waseme vizuri kuna makubwa zaidi ya hilo.

Majibu ya hapo juu ndio yanatupa fursa ya kujua mengi zaidi baada ya kauli ya Makonda, Swali moja tu jiulize kwa miaka 40 hatujawahi kuwa na siku ya maadhimisho ya kifo cha Sokoine, lakini ghafla bin vuu, Serikali nzima na vyombo vya ulinzi wamebuni tukio hili ambalo msingi wake umekuwa kujibu mapigo na kuwatishia wanaotishia nafasi zao. Rejea taarifa ya ikulu iliyotolewa mapema yaani saa moja kabla hata shughuli ya maadhimisho hayo haijaanza. Hii inatafsiri kwamba Maadhimisho ya kifo cha Sokoine ilikuwa kusaka jukwaa tu la kujibu vita vikali ndani ya ccm kuelekea 2025 ambayo kikatiba ndani yw ccm watu watu wote wanaruhusiwa kugombea, yaani hakuna kitu kinaitwa awamu, Awamu ya Tano ya Rais hayati Magufuli, Rais Samia anaimaliza October 2025.

Sasa turudi kwenye uhalisia ingekuwa kweli ni ugomvi wa kiinch kama Makonda anavyotaka umma ujue, Basi Makonda leo angekuwa kizuizini kwa kesi ya UHAINI, yes unaweza usinielewe, lakini Kauli ya Makonda inaangukia kwenye kuunda kosa la uhaini kwamjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 54 (3). Ibara hii inatamka wazi kwamba chombo KIKUU cha Kumshauri rais ni Baraza la Mawaziri, Sasa Baraza la Mawaziri linatuhumiwa kumtukana Rais na anayewatuhumu ni mteule wa Rais mbele ya Rais, Huo ni Uhaini. IGP yupo, DGIS yupo, CDF yupo, wanataka hadi rais wetu adhuriwe ndio wanze kuunda tume za uchunguzi?

Kwanini Vyombo hivi havijamuita CDF mstaafu aseme watu waliokuwa wakigoma Makamu Rais asiapishwe kuwa Rais baada ya Rais kufariki Dunia? Hawa tukiwapata ndio mzizi wa haya yote. Kwanini hata Bunge liko Kimya halijamwita CDF Mstaafu limhoji ikiwa Bunge ndio chombo kikuu cha kuisimamia Serikali? Tutegemee Bunge litamwita Makonda limhoji? Lakini swali lingine kwa Rais Samia, wewe si mgeni kwa Makonda, amekuwa ni mtu wa kutuhumu na kuchafua viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wakubwa tangu akiwa mtoto huko UVCCM, na tuhuma zake hazijawahi kuthibitishwa popote, kitendo cha kumrejesha katika mfumo mtu ambae ana rekodi mbaya ya kidunia haya ndio matunda unayovuna, Atakugombanisha na Wanaccm wenzako hadi utajikuta 2025 unaenda jumba la wastasfu kule Kizimkazi bila kuamini.

Rais Samia, una mtihani mgumu sana mbele yako ambao wewe ndio umeutengeneza bila kujua au kwakujua, Umejizibia njia kwakumletw Makonda ambae 98% ya Wenye CCM hawamtaki kuanzia Kizimkazi hadi Chamwino, Makonda amefanikiwa kukuaminisha kuwa yeye ni turufu kwako ukaondoa ccm nzuri uliyoisuka baada ya kushika urais na sasa unakwenda na ccm ya kimakondamakonda ambayo ushindi wake unategemea zaidi Bunduki, Swali kwako Rais Samia, Uko tayari kuupata ushindi wa damu 2025 chini ya Makonda?

Mwambie Makonda aseme hao watu wanaoheshimika nchini ambao wapo nyuma ya mawaziri ni akina nani? Nchi hii baada ya Mwinyi, Mkapa na Magufuli kuondoka mtu “mkubwa” wakuheshimika anayeijua nchi nje ndani ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Sasa alieleze taifa kama ni huyu kiongozi wetu mstaafu anawatuma hao mawaziri au ni porojo zake tu zinazohatarisha taifa.

Mimi nakutahadharisha Mheshimiwa Rais dhidi ya Makonda, huyu ana kublackmail hadharani na sirini. Alifanikiwa kwa Hayati Magufuli akamtia hofu sana, Magufuli akawa Rais Dikteta asiye na mfano, akaumiza watu wengi sana, Baada alikuja kustuka lakini akiwa ameshachelewa jini likiwa lishatoka katika chupa likizagaa Kigamboni likitaka ubunge ndipo akambwaga mazima! Leo umemuokota umemrudisha kwenye mfumo, Tabia haibadili ni kama ngozi! Watch it! narudia Watch it!
Andiko lote refu namna hii kumbe mlengwa ni Makonda tu?

Tukisema Rc Makonda kawashika kunako ndururu zenu na hamna pa kupumulia, mnakimbilia humu kuja kupata afueni tutakuwa tumekosea!
 
Mtu aliyefukuzwa uenezi? Ana nini cha kushika watu lbd nyie chawa wake
Siwezi kuwa mice wa kihivyo miye.

Isipokuwa tunawapiga madongo wanaomwandika kila page kutwa nzima kwa namna na sababu tofauti tofauti.

Yaani mtu mmoja tu kawa kama wimbo wa Taifa, tumechoka!

Baadaye hali ikiendelea hivi watu kujitoa ufahamu na kuandikq pumba, tutaanza kuwatukana matusi ya nguoni ya wazi yasiyo na staha.
 
Makonda ndiye mtu pekee anayeweza msaidia Samia , ambaye amezungukwa na genge la Msoga ambalo halimtaki kwa Sasa

Samia awarudie kundi la Magufuli na kuachana na Msoga hili kundi la Magufuli ndilo la kumvusha
kwa hiyo ccm kwa sasa ina mapande mawili tu, la msoga na la magufuli?
 
Ushauri wa chadema.kwa cccm. Ushauri wako umefika,wataufanyia kaz kwa ajili ya manufaa yao
 
huyu sijui labda ana hoja lakini uandishi wake hauna taste nzuri,kuna jamaa yangu alinunua kitabu chake niligusa page moja tu nikaishia hapo hapo,hili andiko nimesoma mpaka kati,hoja unaiona,ila taste ya uandishi kukuvutia uendelee kusoma hamna.
Ukiona hivyo wewe ni mjinga/bwege.hakuna kitabu unachoweza kusoma ukaelewa page Moja tuu.
 
Back
Top Bottom