Hilo unalodai 'waislamu wamefelishwa', NECTA walishalitolea ufafanunuzi na sina sababu ya kurudia huo mjadala. Hata hivyo, mimi na wewe si wasemaje wa NECTA.
Lakini, hoja ya msingi ni kuwa ni vizuri tukajifunza kuweka pembeni tofauti zetu za kidini, kiitikadi, kikabila, kijinsia n.k. ili tujadili mambo yanayotuhusu mustakabali wa nchi yetu kama watanzania na sio 'sisi' au 'wao'. Kuna tatizo kubwa katika mfumo wetu wa elimu na tunayaona na kuyasikia kuptia matokeo ya mitihani ni sehemu ndogo tu ya tatizo. Badala ya kutibu chanzo cha tatizo, tuko busy tunajadili 'dini' ya mtu anayeongoza taasisi fulani. Nikuhakikishie tu kuwa hata kama atapewa 'muislam' hiyo nafasi ya ukurugenzi NECTA kama unavyotaka, bado hawezi kufanya chochote kama matatizo ya kimfumo hayatashughulikiwa.
Mifano tunayo mingi, ingawa wakati mwingine hatupendi kujifunza kutokana na makosa ya nyuma. Kuna wakati uwaziri wa fedha uligawiwa kwa 'mwanamke' si kwa sababu ya weledi, uzoefu na ujuzi wake katika masuala ya fedha na uchumi lakini kwa sababu ni 'mwanamke'. Leo hii nani anaweza kusimama na kusema huyo waziri wa fedha mwanamke alifanya nini kuimarisha uchumi na hali ya maisha ya watanzania? Vivyo hivyo, wazee wa CC ya sisiemu wakaona sasa ni zamu ya mwanamke kuongoza bunge. Yanayoendelea sasa kila mtu ni shahidi yameturudisha nyuma nafikiri miaka kama 50 hivi au zaidi iliyopita.