Ritz na
FaizaFoxy
===>Nawaomba sana fanyeni haya ili mlisaidie taifa hili:
a---Watafuteni walimu wanaotoka kwenye shule za kiislamu ambao walishawahi kwenda kusahihisha mitihani ya darasa la saba,kidato cha nne,kidato cha sita,grade A ualimu na Diploma ualimu halafu muwaulize kama kuna chochote ambacho mnahisi kina walakini kuhusu usahihishaji wa mitihani hiyo
b---Waulizeni baada ya kutoka kusahihisha hiyo mitihani uzoefu wanaokutana nao huko unawasidiaje wao katika kuboresha au kuongeza mbinu za ufundishaji ili kuongeza ufaulu katika shule wanazotoka?
c---Fanyeni uchunguzi wa kawaida tu wa kiutawala,miundombinu ikijumuisha majengo,walimu pamoja na mazingira ya kusomea kati ya shule za kikristo na shule za kiislamu
d---Tembelea uwekezaji uliofanyika katika shule ya FEZA (ambayo ni ya waislamu) halafu linganisha mambo yafuatayo
i.Mazingira ya shule ya kiusomaji, Ubora wa walimu
ii.Uongozi wa shule
e---Fanya uchunguzi wa idadi ya shule kama FEZA ambazo waislamu wanazo,
f---Fanya uchunguzi wa idadi ya shule kama FEZA ambazo ziko chini ya makanisa
g---Fanya uchunguzi wa idadi ya shule (nursery,secondary) zilizopo kwenye makanisa na misikitini ukizingatia ubora wa miundombinu (madarasa,maabara,sehemu za michezo) na ubora wa walimu.
h---Fanya uchunguzi wa idadi ya vyuo vikuu kila mkoa vya kiislamu na kikristo ukizingatia ubora wa miundombinu (madarasa) na ubora wa walimu.
i---Kama ukiweza na si vibaya siku moja ingieni kwenye makanisa mkasikilize jinsi wanavyochangishana kuweza kutoa pesa mifukoni kwa ajili ya kuendeleza hizo shule na vyuo vikuu
j---Fanya uchunguzi wa kiwango cha ufaulu kati ya shule hizi (za makanisa na za waislamu)
===>Fanya uchunguzi kuhusu ufaulu katika shule za serikali kuanzia mwaka 1996 hadi 2012
a---Ubora wa shule hizo kuanzia mwaka 1996 kurudi nyuma na 1996 kuja 2012
b---Maslahi na moyo wa kujituma kwa walimu kuanzia 1996 kurudi nyuma na 1996 hadi 2012
c---Uwekezaji uliofanywa na serikali kwenye zile shule zilizokuwepo ie 1996 kurudi nyuma na 1996 hadi 2012
d---Ubora wa maatokeo ya wanafunzi,ubora wa uelewa wa wanafunzi hao hao na kiwango cha ufaulu katika shule za serikali zilizokuwepo kuanzia mwaka 1996 kurudi nyuma na 1996 hadi 2012
===>Unaweza ukaongeza vigezo vyako hapo ambavyo unahisi vinaweza vikaja na majibu ambayo yataweza kutupa picha ya wapi tumepotoka,na wapi tuko sawa.
===>Adui yetu tunamkimbia na anatumia huu udini kutugawa na kututawala kwa kutuchonganisha katika mambo yafuatayo:
a---Kutufanya tugombane sisi wananchi kwa chuki za udini,kwa kuwaaminisha waislamu kuwa wanaonewa wakati wao watawala hwathubutu hata kidogo kutimiza majukumu yao
b---Kuwafanya waislamu wasitimize majukumu yao ya kuwekeza kwenye elimu,huduma za afya na maeneo mengine kwa kuwaaminisha kuwa wananyonywa na kuonenewa na wakristo
c---Kuwafanya wakristo kuchukua tahadhari na kuongeza umakini katika kuwekeza kwenye elimu,huduma za afya na mambo mengine maana wanaona kabisa kuwa kama wasipofanya hivyo hali yao itakuwa mbaya sana.
Tuwe makinsana,tusaidiane jamani,nchi hii ni yetu sote,ukimuacha mtoto wa ndugu hajasoma au hana shughuli ya kufanya unatengeneza jambazi au gaidi wa kesho,lazima twende wote kwa pamoja.