Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,506
Rais Jakaya Kikwete leo ametangaza rasmi kumtema Dr Joyce Ndalichako kutoka baraza la mitihani la taifa na kumteua Dr Charles Msonde kuwa Katibu mtendaji.
Ikulu imesema Dr Ndalichako anarudi kufundisha UDSM mara baada ya kumaliza Sabbatical leave yake aliyokuwa akiifanya.
Maamuzi haya yametangazwa leo na kuhitimisha safari ya Dr Ndalichako kuiongoza NECTA
Ikumbukwe Ndalichako aliamua kuchukua likizo ya masomo baada ya kukataa mpango wa serikali kurekebisha matokeo ya kidato cha nne ya mwaka juzi ambapo kiwango cha kufeli kilikuwa kikubwa. Serikali iliilazimisha NECTA ku standardize ili ufaulu upande kiasi kufuta aibu ya maelfu kufeli
CHANZO: Habari Leo

MSONDE BOSI MPYA NECTA
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Dk Charles Msonde kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA).
Uteuzi wa Dk Msonde, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam juzi jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ulianza Agosti 13 mwaka huu.
Kabla ya uteuzi wake, Dk Msonde alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo la mitihani.
Dk Msonde anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Joyce Ndalichako ambaye amerudi kuendelea na kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo yake ya kujinoa (Sabbatical Leave) aliyoianza Oktoba mwaka jana.
Ndalichako alikuwa katika nafasi hiyo kwa miaka minane kuanzia mwaka 2005 alipochukua nafasi ya Dk Emmanuel Nkumbi aliyeshika wadhifa huo kwa miaka saba kuanzia mwaka 1998.
Kabla ya kuanza likizo ya kujinoa, Ndalichako alikumbana na changamoto kadhaa katika majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kushinikizwa kujiuzulu kutokana na kile kilichotajwa kuporomoka kwa ufaulu na pia baadhi ya madhehebu ya dini kudai anayabana na kuyafelisha kwa sababu tu ya udini.
CHANZO: Habari Leo