Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu, Coplo Hafidh Abdallah Mohamed atoa ushahidi wake, kesi kuendelea Jumatatu 01 November 2021

Hivi jamani mbona kama mimi sijaelewa au nyie mmelewa vipi shahidi namba 3 anasema kaanza kazi 2013 na uko elfu 2004,2006 sijui kasoma kozi za mambo ya bunduki zanzibar na mambo mengine mara sijui 2010 kasomaje hayo mambo wakati kazi kaanza 2013?
Sasa hapo huelewi nn, kwani kozi na kazi inaanza nini
 
Barua iliyoambatanishwa na vithibitisho hailandani na report ya afande....

Barua inasema ufanyie uchunguzi hivyo vitu, yeye report yake inasema conspiracy to commit terrorism.
IGP alisema kuna ushahidi wa kutisha katika kesi hii. Nadhani tunaanza kuamini sasa.
 
Tatizo katumia muda mwingi kusema kasoma mpaka Botswana kwenye mambo ya vilipuzi ni mtaalamu mbobezi ina maana huko Gaborone alikua anaongea kizigua chetu asijue hata maana ya utalii kwa kimalkia..
Kutokujua kiingereza haikufanyi ukawa mjinga mkuu. Mbona Wachina, Warusi, Wakorea n.k. hawajui kiingereza lakini ni wagunduzi wa mambo mengi tu hapa duniani.
 
Kutokujua kiingereza haikufanyi ukawa mjinga mkuu. Mbona Wachina, Warusi, Wakorea n.k. hawajui kiingereza lakini ni wagunduzi wa mambo mengi tu hapa duniani.
Kama hujui kitu kwanini ukitumie, angeandika tu kwa kiswahili, lakini kuandika kitu ambacho hujui maanake huo ni uzuzu.
 
Kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea leo katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo upande wa mashitaka utaleta shahidi mwingine.

Fuatilia hapa kujua kitakachojiri katika mchakato mzima wa kesi hiyo kwa siku ya leo 29/10/2021


UPDATES

Mpaka sasa mawakili upande wa utetezi tayari wamewasili mahakamani.

Mpaka sasa ni saa nne kasoro, kesi bado haijaanza.

Jaji anaingia 3:50

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe dhidi ya Jamhuri inatajwa.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anasimama kutambulisha

1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majige
6. Jenitreza Kitali
7. Abdallah Chavula

Wote ni Mawakili wa Serikali Waandamizi isipokuwa Jenitreza Kitali ni Wakili wa Serikali.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja, tupo tayari Kuendelea

Jaji: Utetezi

Wakili Peter Kibatala: na sisi tupo tayari Kuendelea

Jaji anaandika

JAJI: Anakuwa Shahidi namba ngapi?

Wakili wa Serikali: Namba 03

Jaji: Majina

Shahidi: namba F 5914 D Coplo Hafidh Abdallah Mohamed

JAJI: umri

Shahidi: 38yrs

Jaji: Kazi S

hahidi: Askari Polisi

Jaji: Dini

Shahidi: Muislam

Shahidi: Mimi namba F5914 Coplo Hafidh naapa kuwa kwa ushahidi huu nitakaotoa utakuwa wa kweli, Eeeh Mwezi Mungu nisaidie

JAJI: KIAPO KIPO SAWA?

Jaji: asaidiwe

Shahidi: Mimi Coplo Hafidh nathibitisha kuwa Ushahidi nitaka toa utakuwa wa kweli, kweli mtupu, Eeh Mwenye Mungu nisaidie

Wakili wa Serikali: nitakuuliza Maswali utajibu kwa Sauti

Wakili wa Serikali: Kazi yako

Shahidi: Askari Polisi, nafanya Makao Makuu DSM

Wakili wa Serikali: Askari polisi tangu lini

Shahidi: 2013

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama tukufu Kituo chako cha kazi ni wapi

Shahidi: Forensic Beaural Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Forensic Beaureau ni kitu gani

Shahidi: ni Maabara ya Uchunguzi wa Kisayansi

Wakili wa Serikali: Upo Kitengo gani

Shahidi: Silaha na Milipuko

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kitengo chako kinahusika na Nini (Ballistic and Explosions)

Shahidi: Uchunguzi wa silaha na Milipuko

Wakili wa Serikali: Upo tangu lini?

Shahidi: Tangu 2014

Wakili wa Serikali: umesema Kitengo Chako Kinahusika Kuchunguza silaha, eleza Majukumu yako ya Msingi ni yapi

Shahidi: Kuchunguza Kitako cha Risasi(cartridges)

Wakili wa Serikali: Jingine

Shahidi: Kwenda Eneo la tukio kwa Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Jingine

Shahidi: Kuandaa Riport baada ya Kuchunguza Ballistic and Explosion Report

Wakili wa Serikali: Jingine

Shahidi: Kutoa Ushahidi Mahakamani

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama kama unajukumu lingine

Shahidi: Hakuna

Wakili wa Serikali: Mnafanya Mambo yapi

Shahidi: Kupokea Silaha mbalimbali zinazofanya Uhalifu, Je hii silaha Inafanya kazi..? Hii silaha ni Mzima..? Hii sasa ni Physical Examination.

Wakili wa Serikali: sasa Mnafanya nini

Shahidi: Tunafanya Visual Examination

Shahidi: hii Bunduki ni Mzima, Ina Koki,.? Ina Magazini.? Je Magazini ni Nzima..? Kama inagonga Vizuri kama Nyundo inanguvu..? NitaIkoki katika Upande wa Mitambo Inafanya Vizuri Je Fine pin Inafanya Kazi?

JAJI: fine pin ni nini?

Shahidi: Kiwashio cha Risasi

Shahidi: Nitaangalia Ndani ya Bao (Mtutu) internal Ballistic Ni Safi..? Nitaikoki kama Inafanya Vizuri, Ni hayo tu

Wakili wa Serikali: sasa Uchunguzi wa aina ya pili ni upi

Shahidi: Nimepokea Pistol au SMG

Wakili wa Serikali: Unaitwaje huu Uchunguzi wa Pili

Shahidi: Comparison Examination

Wakili wa Serikali: Kitu gani kinafanyika

Shahidi: Nachukua Ganda nililoletwa na Mteja Kisha napeka kwenye Mitambo Maalum

Wakili wa Serikali: Unafanya hii Comparison Kubaini nini

Shahidi: Je hii Risasi inasifa hii

Wakili wa Serikali: Mnatumia Mitambo Maalum

Shahidi: Unaitwa Computer Microscope and digital Camera Forensic Machine LAECA 2004

Wakili wa Serikali: Umeeleza Vyema, Kuhusu Uchunguzi wa Silaha Kwenye Risasi unafanya kitu gani

Shahidi: Kitaalamu inaitwa Life ammunition...Risasi itaangalia Kiwashio, Je imegongwa..!

Wakili wa Serikali: na hiyo Miss fired ieleze Mahakama, Je live ammunition ikiwa Miss fired Maana yake ni nini

Shahidi: Ni mbovu sababu ulipiga haikulipuka

Wakili wa Serikali: fafanua sasa Mahakamani endapo haijagongwa ni vipi

Shahidi: kama haijagongwa ni Nzima

Wakili wa Serikali: Tofauti na Kugomgwa na kutokugongwa Mnafanya kitu gani

Shahidi: tunaangalia Gun Powder Resolutions

Shahidi: kwemye Risasi Kuna Powder tunaangalia Je powder yako imeganda au Nzima

Yani Bullets Catridge tuna angalia Michuruzi yani Internal Ballistic

Hizo alama za Kipekee tunasema Proved, Shahidi Tuna angalia kitu kinaitwa Twist, Twist silaha/Risasi Kuna Twist Right na Twist Left, Na angalia Counts inasema Twist Right na Left Nyingine unapopiga Kuna Counts Mbili unapopiga Mpaka Kumdhuru Mtu. Inatusaidie Silaha mbalimbali zinazoweza Kufanya uhalifu

Wakili wa Serikali: Tumalizie kwenye Mlipuko, unachunguza nini

Shahidi: Inapotokea Mlipuko wowote sisi tunakwenda Kwenye Eneo la Tukio (SCENE), Wanaenda Askari wa awali. Alafu tunaenda sisi wataalamu Kuangalia kama Kilichotokea ni Local Explosive au Industrial Explosive

Wakili wa Serikali: Wewe unautalamu gani sasa,

Shahidi: Kuchunguza Silaha Mbalimbali ambazo zinatumika kwenye Uhalifu

Wakili wa Serikali: Kozi ya kwanza

Shahidi: Kuchunguza Maganda ya Risasi Mbalimbali

Wakili wa Serikali: Ulifanya kwa Muda gani

Shahidi: kwa Miaka 2

Wakili wa Serikali: kingine tofauti ya kuchunguza

Shahidi: Kuandaa Riport za Kitaalamu

Wakili wa Serikali: Kozi gani Nyingine umefanya

Shahidi: Kozi ya Uchunguzi wa awali ya Upelelezi, Basic CID course

Wakili wa Serikali: Ulifanya Mwaka gani na wapi

Shahidi: Mwaka 2004 kwenye Polisi College Zanzibar

Wakili wa Serikali: Ulijifunza nini huko Zanzibar

Shahidi: Nilijifunza Mambo mbalimbali ya Kiupelelezi, Nilijfunza Bunduki Kupiga, Kuchukua alama za Vidole, kutafuta Finger Prints. Kulift Finger Prints, baada ya Kuchunguza Finger prints na Kuhamisha

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Kufungua na Kuirudishia Bunduki

Wakili wa Serikali: Kingine

SHAHIDI: Nilipata Elimu ya awali Juu ya ku Collect Ushahidi Katika Crime scenes

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama kama ulioata Kozi Nyingine

Shahidi: Baada ya Kurudi Ofisni nilihitajika kwenda Kozi Nyingine Moshi Mwaka 2006

Wakili wa Serikali: Ulijifunza kitu gani

Shahidi: Techniques, protocol in Fire arms Evidence

Wakili wa Serikali: fafanua

Shahidi: Kufungua silaha, Vifaa vyake Kuirudishia, na Kutengeneza kama inawezekana NikAfanya Polisi College Dar es Salaam ambayo inaitwa Ballist tools, fire arms, tools and Ballistic Materials testing Mwaka 2007.

Wakili wa Serikali: Kozi Nyingine

Jaji: Jina Kozi rudia

Shahidi: To determine and Examination of fire arms

Wakili wa Serikali: Wapi

Sahidi: Botswana police College Mwaka 2010

Wakili wa Serikali: NYINGINE

Shahidi: 2015 inaitwa Forensic in General

Ballistic Woundage, Vidonda, Mtu amepigwa Bastola amekufa naangalia Shooter alikuwa Upande gani

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Utaratibu wa Kupokelewa Vitu Vya kufanyia kazi ukoje

Shahidi: Kwanza Mteja awe na Barua

Wakili wa Serikali: kwenye Barua kuna kuwa na nini

Shahidi: Barua ionyeshe kosa

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: aeleze nini anaomba tumfanyie

Wakili wa Serikali: Tofauti na Barua anakuwa na Nini

Shahidi: aje na hivyo Vielelezo husika sasa

Wakili wa Serikali: Barua pamoja na Vielelezo hupokelewa eneo gani na nani anapokea

Shahidi: anakuwa Afisa wa zamu anayetupangia Leo utakuwa zamu na Kupokea Vielelezo Tunakuwa wawili

Wakili wa Serikali: Makishapokea kama Afisa wa zamu anafanya nini

Shahidi: Tunapokea Barua na Kielelezo nafungua Kujiridhisha Alivyovileta yupo sahihi

Wakili wa Serikali: Ofisini Kwako Unapofanyia kazi, ifahamishe Mahakama Silaha au Mlipuko I natokea wapi

Shahidi: Vituo Vya Polisi na hata TANAPA kuja Kufanya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Utaratibu wa Kupokelewa Vitu Vya kufanyia kazi ukoje

Shahidi: Kwanza Mteja awe na Barua

Alivyovileta yupo sahihi

Wakili wa Serikali: Ukishajiridhisha

Shahidi: Lazima niangalie Safety kabla haijaingia Laboratory

Wakili wa Serikali: Umeshajikizisha Vielelezo na Usalama sasa, Unatakiwa Ufanye kitu gani

Shahidi: Natakiwa Kuingia Laboratory nitai Register

Wakili wa Serikali: Barua pamoja na Vielelezo hupokelewa eneo gani na nani a napokea

Shahidi: anakuwa Afisa wa zamu anayetupangia Leo utakuwa zamu na Kupokea Vielelezo, Tunakuwa 2

Wakili wa Serikali: Mkipokea kama Afisa wa zamu anafanya nini

Shahidi: Tunapokea Barua na Kielelezo nafungua Kujiridhisha

Wakili wa Serikali: inapelekwa kwa Afisa incharge kwa Madhumuni gani

Shahidi: Lazima atambue ni silaha gani, Na nitampa Mtu Kuchunguza hii Kesi

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Mnamo tarehe 25 November Unakumbuka ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Ofisini Kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Kwa Kufanya nini

Shahidi: Nita andika Exibit K1 nitaweka FStroke ya Mwaka gani

Wakili wa Serikali: inapelekwa kwa Afisa incharge kwa Madhumuni gani

Shahidi: Lazima atambue ni silaha gani Na atampa Mtu Kuchunguza hii Kesi

WS: baada ya Kusajili Vielelezo Upelekwa wapi

Shahidi: Nitapeleka Sehemu ya Kuhifadhi silaha WS Barua utaipekeleka wapi

Shahidi: Kwa Afisa Incharge

Wakili wa Serikali: inapelekwa kwa Afisa incharge kwa Madhumuni gani

Shahidi: Lazima atambue ni silaha gani Na atampa Mtu Kuchunguza hii Kesi

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Mnamo tarehe 25 November Unakumbuka ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Ofisini Kwangu Makao Makuu madogo Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi

Shahidi: Kwenye Dawati la Kupokea Vielelezo Mbalimbali

Wakili wa Serikalil Ulipokea Vielelezo Vipi Siku hiyo

Shahidi: nikipokea Vielelezo Kutoka Ofisi ya DCI, Ambavyo ni Pistol yenye namba A5340 callibre 9mm, Ikiwa na Magazine Yenye Rangi Nyeusi Na Nikapokea Risasi 03 WS: za Silaha gani

Shahidi: za Pistol Caliber 9mm

Wakili wa Serikali: Vielelezo hivyo viliambatana na nini

Shahidi: kwanza alivileta PC Goodluck kutoka Ofisi ya DCI

Wakili wa Serikali: Goodluck aliwasilisha nini

Shahidi: Barua

Wakili wa Serikali: baada ya Kupokea Vielelezo hivi na Barua ieleze Mahakama Ulifanya nini

Shahidi: Nilivi-Lebel kama nilivyosema awalI Pistol niliioa alama Exhibit K1, Nikosa ili kwa FB /BALL/LAB 158/2020

Wakili wa Serikali: na hizi Risasi 03

Shahidi: nilizipa alama ya K2 K3 na K4 Wakili wa Serikali: Risasi hizi ulizipa Usajili upi

Shahidi: 158 Kama Pistol

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Usajili wa Vielelezo Ulichukua hatua gani

Shahidi: Kufanya Uchunguzi wa Kuutambua Hiyo Bunduki na Risasi ni Nzima K2, K3 na K4

Wakili wa Serikali: na Kuhusu Vielelezo Pistol na Risasi ukafanya nini

Shahidi: Kwanza ile Pistol niliipima

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kupima, Tupo kwenye hatua ya Upokeaji

Shahidi: Nika-Minutes Kumpelekea Boss

Wakili wa Serikali: Vielelezo Ukapeleka wapi

Shahidi: Nilipeleka Chumba cha Kuhifadhia Silaha

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Nani aliteuliwa kufanya Uchunguzi

Shahidi: Mimi Mmoja wapo

Wakili wa Serikali: Uchunguzi huo ulifanya lini

Shahidi: nilianza Kufanya Tarehe 25 Uchunguzi wa Awali

Wakili wa Serikali: Katika Uchunguzi wako Ulifanya nini Kulingana na Mahitaji

Shahidi: Hatua ya kwanza

Wakili wa Serikali: Mteja alikuwa anataka nini

Shahidi: Mteja alikuwa anataka Kujua ile Pistol na Risasi zilifanya kazi

Wakili wa Serikali: sasa wewe Ulifanya nini

Shahidi: Kwanza Ile Bastola nilipima na Kifaa kinaitwa GUN BARROW GAUGE

Hapo nilikuwa napima Kwenye Barrow yani Mtutu kwamba ile Callibre ni kweli 9mm

Nikaona ni kweli ipo sahihi ni 9mm

Wakili wa Serikali: KingiNe

Shahidi: nikatoa Magazine kumbuka ilikuwa na Magazine inaitwa MAGAZINE RELEASE, Naangalia Magazine yake ile Bastola ni ya kwake, Nikaona Okey Magazine ni ya Kwake

Wakili wa Serikali: Jingine

Shahidi: Ndani ya Magazine Kuna Spring ambayo Ukiweka Risasi inashuka Chini, yenyewe inapandisha Risasi juu, Nikaona Nzima Nikaangalia Nyundo Hummer Kama Nzima sometime inakuwa loose nimabaini, Nzima Nikaangalia Triger kwa kutumia Triger Pull ....kama inafika kwenye 100 nimEbaini ni Nzima

Shahidi: Nikaenda ndani ya Barrow nikatumia Mdeki Kuangalia kama Ilikuwa Safi au Chafu Kupoteza Ubora wake, Nimabaini Barrow lipo Vizuri halina Vumbi hakuna Mchanga Maana yake Barrow lipo safi, Lolote linaweza Kufanya Baada ya hapo nikaikoki kungalia Firing Pin Mechanism kama ..Nilibaini Ipo

Kwa hatua hiyo niliishia hapo

Wakili wa Serikali: Kwa Aina za Uchunguzi ulizotutajia huu ni Uchunguzi wa aina gani

Shahidi: ni Visual Examination

Wakili wa Serikali: kwenye zile Risasi 3 ulichunguza nini

Shahidi: pale niliingia Sana kwenye Pin Impresion kwa Maana Primer au Kiswahili Chake ni Kiwashio au Kitako cha Risasi

Wakili wa Serikali: Hatu gani ikafuata Shahidi: Hatua ya Pili ya Uchunguzi wa Pili

Shahidi: Nilichukua Risasi Mbili ya zile nilizoletewa callibre yake 9mm, Nikaenda kwenye Chumba Maalum Kwenye Chumba Kuna sehemu ya kupigia Silaha Mbalimbali.

Wakili wa Serikali: Ulienda na Kitu gani

Shahidi: Nilikuwa na Pistol na Risasi 03

Wakili wa Serikali: Ulienda Kufanya akitu gani hasa

Shahidi: Kuna Kifaa kinaitwa Tank Water Recovered Bullets

Wakili wa Serikali: Kiswahili ni nini

Shahidi: Ni tanki la Maji tunalotumia kupata risasi

Wakili wa Serikali: Kwanini sasa Mnapiga Risasi Kwenye Tanki la Maji

Shahidi: ili Kupata Maganda ya Risasi na Vichwa vyake

Wakili wa Serikali: Kwanini sasa Mnapiga Vile Vielelezo

Shahidi: Najiridhisha sasa, Je Ni kweli zile Risasi ni Nzima.? Na kwenda Kupiga sasa

Wakili wa Serikali: Nini Matokea ya Uchunguzi wa Kina

Shahidi: Nikichukua Risasi Mbili nikaweka Kwenye Magazine Nikaweka kwenye ile Bastola nikapiga sasa, nikapata Maganda na Vichwa Vya risasi. Nikafanya hivyo tena kwa Risasi ya pili, nikapiga

Wakili wa Serikali: Risasi zako zilikuwa na alama, Je Risasi zina alama zipi ambazo ulipiga

Shahidi: K2 na K4

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini sasa kuhusiana na Yake maganda

Shahidi: Nilienda kuyalebo yale Maganda yangu mawili

Wakili wa Serikali: Kwa kuyapa alama gani

Shahidi: T1 na T2, T1 ilikuwa K2 na T2 iliyokuwa K4

Wakili wa Serikali: baada ya Labeling Kitu gani sasa Kingine kilifuata

Shahidi: Nikaenda Kuandaa Report yangu (Ballistic Examination Report)

Wakili wa Serikali: baada ya Kuandaa Ulifanya nini

Shahidi: Nilisaini

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Nilipiga Muhuri

Wakili wa Serikali: Muhuri gani

Shahidi: Forensic Beaural Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Kuhusiana sasa na Silaha Yenyewe

Shahidi: Baada ya hatua zote zote hizo nikafunga kwenye Mfuko na Nikafunga seal, nikasaini na Kuandika Tarehe

Wakili wa Serikali: Baada ya Kusaini Ukapeleka wapi

Shahidi: Chumba cha Kutunzia Silaha Wakili wa Serikali: Na Report yako sasa

Shahidi: Niliweka kwenye Bahasha na Nikairudisha kwenye File Book. Baada ya hapo nikiwa nasubiri wenyewe Waje Kuchukua Vielelezo vyao

Wakili wa Serikali: Vielelezo Vyao Vilikuwa Kuchuliwa Siku gani

Shahidi: Tarehe 27 November 2020

Wakili wa Serikali: Nani alikuja Kuchukua Vielelezo hivyo

Shahidi: Afande Swila Kutoka Ofisi ya DCI

Wakili wa Serikali: Nani aliyemkabidhi afande Swila hivyo Vielelezo

Shahidi: Mimi Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Swila Vitu gani

Shahidi: Riport yangu ya Kiuchunguzi Ballistic Examination Report, nikamkabidhi Pistol Moja ambayo ni Exibit K1 Callibre A5340 9mm Model yake CZ 41 Rangi Nyeusi Ikiwa na magazine yake. Pia nikamkabidhi Risasi Moja Nzima iliyobaki Ambayo nili nililebel K3. Nikamkabidhi Maganda Mawili na Bullets zake Yale Maganda niliyalebel kama T1 na T2

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba tangu ulivyomkabidhi Swila ni Lini tena ulipata Kuviona tena Vielelezo

Shahidi: Jana

Wakili wa Serikali: Kwa Jambo lipi

Shahidi: ili aniletee Vielelezo Kwa ajili ya Ushaidi Mahakamani hii Leo.

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama hii Report yako ya Kiuchunguzi uliyoiandaa ni kitu gani kitakutambulisha

Shahidi: Kwanza Kwa Nembo ya Ofisi, Nembo ya Polisi Force a namba zangu F5914 Majina yangu ya Copo Hafidh Abdallah

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Na Signature Na Muhuri wa Ofisi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha anaweza akatambua Nyaraka aliyofanyia Kazi kwa Ruhusa ya Mahakama Tunaomba Kumuonyesha Shahidi anakabidhiwa

Wakili wa Serikali: Shahidi itizame hiyo Kabrasha Ndogo sasa Uimbie Mahakama nilichokupatia ni Kitu gani

Shahidi: Ni report Yangu niliyoindaa kuhusiana na Uchunguzi wa Silaha na Risasi

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Vitu gani vinaonyesha wewe Ndiyo uliandaa

Shahidi: Kuna Nembo ya polisi, Force Namba, Signature yangu, Kuna Muhuri wa Ofisi kwa hiyo Riport hii ni ya kwangu

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama hii

Shahidi: Naomba Mahakama hii Ipokee Riport yangu kama Sehemu ya Ushahidi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba Ipokelewa Ballistic Examination Report Wakili wa Serikali Wanaipeleka Upande wa Mawakili wa Utetezi

Nashon Nkungu: kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza sina Pingamizi

John Mallya: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili Pia sina Pingamizi

Dickson Matata: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa tatu pia hatuna Pingamizi

Peter Kibatala: Kwa niaba Ya Mashitakiwa wa Nne pia hatuna Pingamizi

Jaji anapelekewa Nyaraka Mahakama bado Ipo Kimya Kidogo, Jaji anaendelea kuandika

JAJI: Mahakama Imepokea Nyaraka Hii yenye Kichwa cha Habari Ballistic Report Ambayo iliandaliwa tarehe 26 November 2020, Napokea na Kama Kielelezo namba 02

Jaji: Nakuomba Shahidi usaidie Kuisoma

Shahidi anapewa

Shahidi: Forensic Beaural Ballistic Laboratory DSM/F Ya Tarehe 26, Nov 2020 Shahidi anaisoma upya yote

Shahidi amemaliza Kusoma Riport yote ambayo Ndiyo yale aliyokuwa anayaeleza, lakini Sheria inataka asome Upya Mahakamani.

Wakili wa Serikali: Kwa mujibu wa a Taarifa hiyo ulikuwa unachunguza silaha ya aina gani

Shahidi: Pistol A5340 ya Callibre 9mm

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Uchunguzi wako Ulibaini nini Kuhusu Bastola

Shahidi: Ni Nzima

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Nzima

Shahidi: Ukiweka Risasi inalipua

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Taarifa yako uliyofanyia Uchunguzi Risasi tatu, Je za Silaha gani

Shahidi: za Pistol caliber 9mm

Wakili wa Serikali: Uhusiano wake Risasi na Bunduki ukoje

Shahidi: Ni za Kwake, kwa Maana zimeingia na Ikapiga (Fire)

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Taarifa yako umesema Unaambatanisha K1, K2, K3 na K4, was attached, sasa Elezea kwanini Kwenye Taarifa Yako Umeandika tena K4 Wakati unasema Ulishailipua

Shahidi: Nimekosea Mheshimiwa Jaji, Ni Typing Error Kwa sababu Nilishailipua.

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo attachments zitakuwa ni nini

Shahidi: K1 ambayo ni Bastola na K3 Wakili wa Serikali: Ukionyeshwa utavitambuaje

Shahidi: Nimeweka Kwenye bahasha, nimesaini nikaandika na tarehe

Wakili wa Serikali: Mbali na hivyo, silaha ina vitu gani Vingine vitakavyokufanya uitambue

Shahidi: kwanza ni serial Namba, Lebbeling ya Forensic ambayo ni K1 FB /BALL /LAB 158 of 2020 Maganda niliya-Lebel kwa T1 na T2 Na vile vile Nika-Lebel FB /BALL /LAB 158 of 2020

Na Bullets nili-Lebel kwa Maganda yake

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameonyesha Uwezo wa Kuvitambua, Kwa Ruhusa ya Mahakama naomba Kumuonyesha anaruhusiwa na mahakama Shahidi Tizama Mfuko Mmoja baada ya Mwingime Shahidi anatizama Mifuko ya Nailon ambayo ni Transparent

Wakili wa Serikali: Huo Mfuko ni nini

Shahidi: Mfuko wa Kuwekea Vielelezo Mbalimbali

Wakili wa Serikali: Una uhusiano gani na wewe Shahidi

Shahidi: Ndiyo nilitumia kuweka Bastola

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kinachotambulisha kuwa wewe ndiye Ukiweka silaha

Shahidi: Nilisaini nikaweka na Tarehe 26 November 2020

Wakili wa Serikali: Unasema Kwenye Mfuko huo kuna Kitu gani

Shahidi: Bastola yenye serial Namba A5340 Callibre 9mm CZ 100 nyeusi

Wakili wa Serikali: Mfuko wa Kwanza

Shahidi: Una Risasi, na Nika Lebel na Nikafunga Kwa Seal

Wakili wa Serikali: Kinachokutambulisha kuwa wewe Ndiye Uliweka

Shahidi: Nilisaini na Nikaweka Tarehe, ina alama Exibit K3

Wakili wa Serikali: Tumalizie Mfuko wa Mwisho

Shahidi: Niliweka Maganda T1 na T3 na Bullets zake

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama

Shahidi: Naomba Mahakama hii Ipokee Vielelezo hivi kwenye kesi husika Wakili wa Serikali: Ipokee nini

Shahidi: Bastola yenye serial Namba A5340 Callibre 9mm ikiwa na Magazine Nyeusi kwa Rangi yake, Model ni CZ 100.

Wakili wa Serikali: Kwenye hiyo Mifuko Mingine

Shahidi: Naomba Mahakama Ipokee Risasi ya Pistol ya Callibre 9mm

Wakili wa Serikali: Uliipa alama gani

Shahidi: K3

Wakili wa Serikali: Mfuko wa Mwisho Mahakama Ipokee

Shahidi: Maganda Mawili ya risasi na Bullets Mbili (Vichwa Vya Risasi)

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameomba Vielelezo ambavyo amevitaja Vipokelewe na Mahakama

Wakili wa Serikali Wanaipeleka Mifuko 3 kwa Mawakili Wa Utetezi Mawakili Wa Utetezi Wamezingira Vielelezo wanavikagua Kimoja baada ya Kingine vikiwa bado ndani ya Mifuko.

Nashon Nkungu: Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza hatuna Pingamizi dhidi ya Vielelezo hivi vyote kwa Pomoja

John Malya: hatuna Pingamizi kwa niaba ya Mshitakiwa wa Pili

Dickson Matata: Hatuna Pingamizi kwa Vielelezo Vyote

Peter Kibatala: Mhe. Jaji nasi pia hatuna Pingamizi

Jaji anainama anaandika Kidogo Jaji anawakumbusha kuwa Mahakama Ya Rufani imesema Kuwa Vielelezo havipaswi kupokelewa kwa pamoja Kwa hiyo kwa namba nitavipokea Kwa tofauti tofauti.

Jaji: Basi Mahakama Inapokea Silaha Moja ya Moto aina ya Pistol aina ya A5340 kama Kielelezo Mahakama Inapokea Maganda Mawili ya Risasi ambayo yametumika kama T1 na T3

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Sasa Shahidi akate Mifuko ili aweze Kutuelezea anaruhusiwa Shahidi anachana Mifuko MAHAKAMA ipo Kimyaaaaa

Wakili wa Serikali: Shahidi hiyo unasema ni silaha ya aina gani

Shahidi: Ya Pistol

Wakili wa Serikali: anaishika na yeye

JAJI: Wakili wa Serikali nakutaadharisha ulivyoibeba naona Unamuelekezea Jaji MAHAKAMA KICHEKO Kidogo

Wakili wa Serikali: hii ni Pistol ya aina gani

Shahidi: Luger ya 2005

Wakili wa Serikali: elezea mahakama ulivyokuwa unaelezea hii Pistol

Shahidi: Hiki ni Kifunguo cha Magazine Ukiminya Unaruhusu Magazine Itoke Magazine hii inauwezo wa Kuchukua Risasi nane

Wakili wa Serikali: Unasema Ulitest Magazine

Shahidi: Ukibonyeza hii spiring, nilipima Kama Inanguvu ya kusukuma Risasi Na hiii ni Box Magazine, Na Magazine hii ni Nzima

Wakili wa Serikali: na Ulisema Barrow ndiyo ipi

Shahidi: Ndiyo hii kwa Kiswahili ni Mtutu. Nilipima kwa Kuchukua Barrow Gauge nikatoa kwenye Barrow, Je hii ni 9mm, Ikaniambia ni Yenyewe

Wakili wa Serikali: Ulisema Triger, Triger eleze Triger ipo wapi

Shahidi: nilipima Triger kwa Kuminya hivi, Nikaona Ikafika kwenye 100

Wakili wa Serikali: Kwenye 100 Ikafika hapa

Wakili wa Serikali: Hebu onyesha Mahakamani Firing yake na Uwezo wake

Shahidi: Hapa naikoki, hii ni Pini na hapa Nikikoki pana kuwa na Risasi inaenda Chemba nikaikoki nika-fire nikaona Nyundo Inagonga Vizuri.

Wakili wa Serikali: Kitu gani Nyingine Ulifanya

Shahidi: Nilipima Barrow Kupima Kama ni safi, Nikaona Barrow ipo Safi hii ina serial Namba hawa Luger wanaweka Serial Namba hapa na hapa

Wakili wa Serikali: Ni ipi

Shahidi: Imesajiliwa A5340 Kama haijagongwa serial Namba sijajua imeingia Vipi Nchini hii pia ni Risasi niliipa K3

Wakili wa Serikali: Ulichunguza nini kwenye hii Risasi

Shahidi: Nilichunguza Kiwashio, hapa ikiwa na Chuma Ukigonga inalipuka

Wakili wa Serikali: Kiwashio cha hiyo Risasi kikoje

Shahidi: Kizima

Wakili wa Serikali: Twende Kielelezo Cha Mwisho

Shahidi: Haya ni Maganda Kama Ulienda Marekani wanakuandika 9mm Pass 50 Kwamba Kutoka kwenye Base hadi kwenye Kichwa ni Pass 50 Hizi mbili ni Bullets nimezipata baada ya Kupiga kwenye tenki la Maji Kwa Maana hazikudhuru Mtu. Wanaita Terminal Firing Shahidi anarudishia Vielelezo kwenye mifuko yake

Wakili wa Serikali: Mwisho, kwa ufupi nini Ugunduzi wako

Shahidi: Kwamba Vyote Kuanzia Bastola na Hizo Risasi 3 ni Vizima na Vinafanya kazi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu

Jaji: upande wa Utetezi

Wakili Peter Kibatala: Naomba kwa Ruhusa yako nimtambulishe Jeremiah Mtobesya ambaye alichelewa kwa sababu alikuwa Mahakama ya Rufaa Na ninamatambulisha kwa sababu Yeye Ndiye ataanza Maswali Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza

Jaji anaandika Kidogo

Jaji: naliingiza Jina lako kwenye Orodha ya Mawakili

Jaji: Nitaruhusu watu wapumzike Kidogo kunyoosha Miguu na Kupata maji Mpaka Saa saba Na nusu

Naomba tujitahidi Kutunza Muda

Jaji anatoka

Mpaka sasa mahakama haijarejea

Jaji anaingia

Wakili Jeremiah Mtobesya anauliza maswali Kwa niaba ya Mshitakiwa wa kwanza

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji Kama Unajua Fomu Polisi Fomu Namba 145

Shahidi: Siijui

Mtobesya: shahidi Unafahamu kitu kinaitwa Exibit Lebel

Shahidi: sifahamu

MTOBESYA: wewe Kama Polisi nitakuwa sahihi Nikisema Exibit Lebel ni fomu namba Ngapi

Shahidi: siyo fomu ni Lebel, Siyo Fomu, sisi Ballistic Tunayakwetu, siyo fomu

Mtobesya: unaelewa Kwamba ni Matakwa ya Kisheria Kuhusu Movements za Exibit Kwamba Polisi yoyote anaye Hamisha Kielelezo, hasa Polisi Kuweka Kumbukumbu ya Jina lake na Cheo Chake anatakiwa Kufanyia nini.

Shahidi: Hakuna kitu kama Hicho, Sisi tunasaini uweji Jina wala Cheo

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi nikisema Kwenye Mdomo wa Silaha huwa Kuna Vitu ambavyo Risasi ikitoka inaacha, inaacha Groove ambayo ni Unique kwa Kila silaha

Shahidi: Hapana wewe Unazungumzia Gun powder

MTOBESYA: sasa ndiyo nasema Bullets Ikitoka inaacha Groove?

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Hizo impression za Grooves zinatoka wapi

Shahidi: Hapana, wewe Unasema Gun Powder

MTOBESYA: sasa tuokea Muda wa Mahakama, wewe Unajua Grooves ni nini

Shahidi: Ni Michirizi baada ya Kutoka Risasi

Mtobesya: Kwa hiyo Grooves inapatikana kwenye nini

Shahidi: Baada ya Risasi Kutoka Kwenye Silaha

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi sasa Nikisema kila Bullets inapotoka inaacha Grooves ambayo ni Unique kwa Kila silaha

Shahidi: Sahihi

MTOBESYA: Nitakuwa sahihi, ili utambue Kuwa Risasi hii imetoka kwenye Silaha gani ni lazima nifafanishe Barrow na Grooves Kujua imetoka kwenye silaha gani

Shahidi: Hapana

Mtobesya: Ni kwanini nikitaka Kujua Kuwa Risasi Imetoka kwenye silaha hii, Imetoka kwenye silaha fulani ni lazima nipigie (Fire) na Kwenda Kulazimisha

Shahidi: Lazima uwe na Specimen ambayo ina Standard fulani ili kuweza Ku-Compare Kwahiyo mimi ni lazima nitapiga Kwenye Bullets water Tank kufanya Mlinganisho

Mtobesya: Kwa hiyo ili Ujue ni lazima Kulinganisha grooves?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Kwa hiyo Wakati Unaonyesha Vielelezo ulituonyesha hizi Grooves ndiyo zilizofanana?

Shahidi: Nilionyesha Bullets

Mtobesya: Ulionyesha Grooves

Shahidi: Nilionyesha Pin Impresion

MTOBESYA: Ulionyesha Grooves hukuonyesha shahidi: nilionyesha Pin Impresion

Mtobesya: Kuna tofauti gani kati ya 9mm na 9mm Luger

Shahidi: 9mm ni aina ya Risasi na Luger ni aina ya Bunduki

Mtobesya: Ni Ushahidi wako kwamba Luger siyo aina fulani ya Bastola

Shahidi: Luger ni aina ya Bastola

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Maana ya CZ 100

Shahidi: Maana yake ni ZCheck republic ni Majina yake

Mtobesya: Kwa hiyo Unakumbuka wakati Goodluck anakupatia Silaha alikwambia ni silaha ya aina gani

Shahidi; Ile ni Ofisi tunaenda kwa Documents Siyo Lala lalala lala tunaenda Kwa Documents Bwanaaaaa

Mtobesya: Wakati anakukabidhi alikukabidhi nini

Shahidi: Pistol yenye Serial Namba A 5340 Callibre 9mm black in Colour

Mtobesya: Unaweza Kuiambia Mahakama Kama kuna sehemu Yoyote Mliandikishana wakati mnakabidhishana

Shahidi: Niliandika Kwenye PF113 Mtobesya aliweka Model Namba

Shahidi: Ndiyo aliweka CZ 100

Mtobesya: Baada ya wewe Kumalizia ulimrudishia nani

Shahidi: Afande Swila

Mtobesya: Mliandikishana pia

Shahidi: Ndiyo nilimkabidhi kwa Documents

Mtobesya: Na Kwenye Makabidhiano uliandika Model Namba

Shahidi: Ndiyo Niliandika Model namba, aina ya silaha, Callibre yake na namba za Risasi

Mtobesya: Wakati wewe umeletewa Silaha Kwa ajili ya kungalia kama ni Nzima Je Mlifanya Finger Prints Kuangalia hiyo silaha

Shahidi: Sikufanya

Mtobesya: Kwa Upande wa Shitakiwa namba 1 naomba Kuishia hapo


Wakili Mallya anauliza maswali

Mallya: shahidi nitakuuliza mambo machache Malya: ni sahihi nikisema ni Maabara iliyosheeni Vifaa Vya Kisasa

Shahidi: Of course

Mallya: Ni sahihi inauwezo wa Kufanya Uchunguzi wa maswala yote unayoyafanya

Shahidi: Inafanya Yote

Mallya: Ni sahihi Kwamba Mnafanya Uchunguzi Kwa Mujibu wa Barua

Shahidi: Ni sahihi kwamba nafuata Maelekezo ya Barua

Mallya: Naomba Kielelezo Mheshimiwa Jaji

Mallya: Soma Paragraph ya Kwanza hapa

Shahidi: I F5914 Hafidh Abdallah Mohamed Coplo wa Police Force States Thats have been engaged in Examination of Fire Arms, Catridge, suspected.... "

Mallya: Kwa Maelezo Yako Ulitumwa na Barua kufanya Nini

Shahidi: nilitumia Kuchunguza Bunduki, Risasi na Maganda ya Risasi

Mallya: We uliletewa Vitu gani Uchunguze

Shahidi: Risasi 03 na Bunduki

Mallya: Maganda yalikwepo

Shahidi: Sikuletewe

Mallya: Vichwa Vya Risasi Uliletewa

Shahidi: Sikuletewa

Mallya: I have been Engaged Maana yake nini

Shahidi: Maana yake "Nimefanya Uchunguzi

MAHAKAMA kicheko

MALYA: uliletewa Maganda ya Risasi?

Shahidi: Nililetewa Risasi

Mallya: uliletewa

Shahidi: Sikuletewa

Mallya: Kwenye Maandishi yako Umeandika "and tools" Vifaa ambavyo hapa hujatuletea

Shahidi: Sikuletewa Vifaaa

Mallya: Soma hapa

Shahidi: And tools, Vifaa Mbalimbali

Malya: eenheee alafu wewe hujatuletea hivyo Vifaa

Jaji: asome sentence Yote tuelewe

Malya: Kwa hiyo Mwambie Jaji Riport yako siyo ya Kesi hii tu

Shahidi: Mimi Sikuletewa Vifaa kwa kesi hii

Malya: Riport hiyo kwa Ushahidi wako inahusiana na Kesi hii na Inazungumzia Uzoefu wako wa kazi

Shahidi: Ndiyo, ndiyo Maana Nimeweka hapa

Shahidi: anasoma... Mwisho and tools Malya Kwa hiyo hizo tools ziko wapi

Shahidi: tools siyo kwa kesi hii tu

Malya: Mwambie Mheshimiwa Jaji

Mallya: Ulisema Umeanza Kazi Mwaka 2013 ni sahihi

Shahidi: Sahihi, Kutoka Mwaka 2013 Mpaka sasa Ni Miaka Mingapi

Shahidi Miaka 18

Malya: haya Katika Riport Yako unasema Unauzoefu wa Miaka 18 Je Umetoa wapi Miaka 18

Shahidi: Siyo kwamba tangu nianze kazi yangu, nikiwa nasoma.

MALYA: Kwenye Riport yako umesema hapa Kuna Errors, Je kuna Erros Ngapi

Shahidi: Hiyo hiyo moja.

Mallya: Shahidi Maana ya Terrorist Maana yake nini?

SHAHIDI: ni ugaidi

Mallya: Terrorism Maana yake nini

Shahidi: Ni Maswala ya Utalii

MAHAKAMA KICHEKO

Malya: narudia tena, Terrorist umesema ni Ugaidi na Terrorism Maana yake nini

Shahidi: Ni Maswala ya UTALII

Mallya: Msomee Mheshimiwa Jaji hapo Ulipoandika Kuhusu "Conspiracy" na Terrorist

Shahidi: anasoma Spelling zake C. o. n. s. I. p. a. r. a. n. C. y

Mallya: Ulikuwa unajua Kuwa Unafanyia Uchunguzi Silaha Zimetoka wapi

Shahid:i Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo Ulikuja Kujua Muda gani kuwa Silaha zinahusika na Ugaidi

Shahidi: nilijua baada ya Kufungua Barua

Mallya: Je, kati ya Barua na Silaha Ulianza Kupokea nini

Shahidi: Nilipokea Vyote kwa Pamoja

Mallya: Kabla ya Kesi hii Ulishawahi Kufanya Uchunguzi Juu ya mabomu Au Bunduki

Shahidi: Ndiyo, Niliwahi Kufanya

Mallya: Kwa hiyo unafahamu kwamba Makosa ya Ugaidi ni Makosa Serious au Ni Makosa Mepesi

Shahidi: Mimi niulizie kuhusu Bunduki na Risasi tu mambo ya Ugaidi siyajui. Nita eleza facts Kuhusu Risasi na Bunduki

Malya: Mheshimiwa Jaji aambiwe ajibu swali langu

Shahidi: Sijui Kama ni Makosa Serious au Mepesi

Mallya: Wakati unaelezea Ushahidi wako ulitueleza kwamba wakati unapokea, ulivaa Gloves na Vifaa vingine

Shahidi: Hayo ni Mambo ya Kawaida sana siwezi Kueleza Kila Kitu hapa kwamba Nilivaa Miwani, Gloves na Hijab

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba ajibu swali langu

Shahidi: Sikueleza

Mallya: Je Mtu akiwa na Bunduki haijasajiliwa na haimiliki kihalali Je imaanisha amefanyia uhalifu

Shahidi: Jibu linategemea

Mheshimiwa Jaji naomba Nipewe risasi, MALYA anapewa anamkabidhi Shahidi

Mallya: Je Shahidi Kuna uwezekano hii ambayo hujaipiga, hatujui kama Inafanya kazi

Shahidi: Hii nimeiacha

Mallya: Si Kuna uwezekano wa kapiga Risasi halafu isilipuke

Shahidi: Ndiyo kama Kumefanyika Mishandling.

Mallya: Kwa hiyo hata Hii inawezekana iwe Nzima

Shahidi: Ndiyo lakini Nilipiga Mbili nikabakisha moja

Mallya: Katika Maabara yenu kuna Vifaa Vya Kupima Finger Prints

Shahidi: Kwa Ofisi yetu?

Mallya: Ndiyo

Shahidi: Ipo lakini Ni Upande wa Mtu Mwingine

Malya: na wewe hukujisumbua kutaka Kujua Kama hii Bunduki Imetoka Kwa binadamu au Kwa Ng'ombe hukujisumbua Kufanya hivyo

Shahidi: Miye nacheza na Barua kwa sababu inataka nifanye nini, nafanya hicho tu.

Mallya: Soma tena hapa

Shahidi: I have been engaged in identification Malya: Mnapo Identify Silaha, Mnafanya Nini

Shahidi: Kungalia Serial Namba Kuangalia Magazine, Tuna angalia Silaha Kwa Ujumla, Tuna angalia Fire arms, Firing Pin, pin Impresion, Hammer, Barrow ..aina ya silaha, Serial Namba yake, Model yake.

Mallya: hapo hapo Kuna Mahali umeandika Examination Report Page Number 02 Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Orodha Ya Vitu Vyote kama Umevionyesha ama Ku-Identify Katika hiyo Report Yako

Shahidi: Sikuvionyesha

Malya: Mheshimiwa Jaji ya kwangu ni hayo tu

Dickson Matata: Kwa ajili ya Mashitaka Wa tatu Sitofanya Cross Examination

jaji: Wakili wa Mshitakiwa namba 04

Wakili Kibatala anauliza maswali

Kibatala: Naomba Nipatiwe Kielelezo P3 P4 na P5 halafu nipewe Dakika 01

JAJI: umevaa Gloves MAHAKAMA kichekoooooo

Kibatala: Sijavaa Gloves

Kibatala; nipo tayari Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Nimeomba Kielelezo Namba 04 Live Amution

Kibatala: umesema hizi Risasi Zina Uhusiano na Luger..?

Kibatala: na Kuonyesha Usome kwenye Kitako

Shahidi: 9mm

Kibatala: Kuna Sehemu imeandikwa Luger

Kibatala: Kuna Sehemu yoyote Umefafanua kwa Jaji kwamba Ktk Kielelezo namba 04 utaona 9mm lakini hakuna Maneno Luger

Shahidi: Sikufanya hivyo

Shahidi: Hapana

Kibatala: nakuonyesha Risasi Nyingine Soma Kwenye Kitako Iwapo Maneno 75 kama Ilivyokuwa kwenye kielelezo namba 04

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Je, ulifafanua kwa Mheshimiwa Jaji kwamba Kuna Utofauti wa namna hiyo

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Ushahidi wako Katika Mahakama Kwamba hakuna Neno Luger kwenye Risasi na Mheshimiwa Jaji atumie Kupima Ukweli na Uongo wako.

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji hii ni Bunduki au Risasi

Shahidi: Risasi, Ganda la Risasi

Kibatala: Hakuna Neno Luger Chini ya Kitako?

Shahidi: Sioni naona tu 9mm

Kibatala: naomba Mheshimiwa Jaji upatiwe uone

Kibatala: Nakuuliza tena Chini ya Kiapo Usichezee Mahakama

Shahidi: Maneno Luger yapo

Kibatala: Bado unataka Mahakama Ukichukulie wewe ni shahidi Serious kabisa na ni Afisa wa Polisi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Kielelezo hicho kina Maneno 75

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: umesema, wewe Moja ya kazi yako ni Kufanya Comparison Analysis

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kuna tofauti au Hakuna

Shahidi: Upo

Kibatala: Kwa hiyo wewe Unasisitiza, wewe ni Shahidi wa Ukweli Kabisa

Shahidi: Ni sahihi pamoja na haya uliyoyasema

Kibatala: Kazi yangu Kuuliza Maswali tu analysis watafanya watu wengine

Kibatala: Uwepo wa Utofauti wa Maneno Luger na hii 75, hukufafanua kwa Jaji

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Na Kwenye report hiyo tofauti haipo

Shahidi: Haipo ndiyo

Kibatala: KWENYE report umesema wewe Ni Mtaalamu wa Miaka Mingapi

Shahidi: 11

Kibatala: umesema Kilichokufanya Ufanye Uchunguzi ilikuwa ni Barua kutoka KWA NANI

Shahidi: DCI

Kibatala: na Barua hii ni Nyenzo Muhimu sana

Shahidi: Ndiyo, sababu inasema Nini nifanye

Kibatala: na Kwamba Riport yako haiwezi kuwepo bila Barua

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Kwamba wewe ndiyo ulipokea Barua kutoka kwa DCI

Shahidi: Ndiyo Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Iwapo hiyo Barua Umetoa kama Kielelezo

Shahidi: sikuitoa

Kibatala: Sema kwa Mheshimiwa Jaji Iwapo Uliitambua kuwa Barua hiyo ni Hii Hapa hata Kama hujatoa kama Kielelezo

Shahidi: Haipo hapa

Kibatala: Kwa hiyo hujaitambua

Shahidi: Niliitambua Ofisni

Kibatala: Kwani hapa ni Ofisini

Shahidi: Hapa Mahakamani

Kibatala: Uliitambua

Shahidi: Hapana

Kibatala: Barua inaonyesha Bunduki na Risasi Zimetoka kwa nani

Shahidi: Haupo sahihi inaonyesha makosa tu

Kibatala: Kwa hiyo wewe yale Makosa Kwenye Riport yako yametoka kwenye ile Barua

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ambapo hiyo Barua hapa Mahakamani Haipo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Hapana hatuwapi watuletee Ombi Kwa Mujibu wa Sheria.

Jaji: Kwa nini sasa

Wakili wa Serikali: Ndiyo Msimamo wetu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji ili Kuokoa Muda Wakili Mtobesya ataendelea Kunitafutia

Kibatala: Naomba Mahakama Inisaidie Kielelezo p2

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi Ulisema Uliletewa Vielelezo Vya Bunduki na inatoka Ofisi ya DCI

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Katika Maelezo yako Hukusema D. COPLO Goodluck anatoka Ofisi ya Upelelezi Dar es Salaam

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi Ulisema Uliletewa Vielelezo Vya Bunduki na inatoka Ofisi ya DCI

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Katika Maelezo yako Hukusema D. COPLO Goodluck anatoka Ofisi ya Upelelezi Dar es Salaam

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Hukusema D. COPLO Goodluck anatoka CID Arusha..?

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Barua inasema D. COPLO Goodluck Anatoka wapi

Shahidi: Ofisi ya DCI

Kibatala: Shahidi Una uhakika na hilo nakukumbusha Upo chini ya Kiapo

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Katika Report yako hii hakuna a Mahala popote Hakuna Mahala umezungumzia Bunduki aina ya luger

Shahidi: Sikuweka, Nimeweka Model na Namba

Kibatala: Shahidi CZ100 Ulitoa wapi

Shahidi: Kwenye Bunduki

Kibatala: Hukutoa Katika Nyaraka za Makabidhiano wala Katika Barua iliyotoka kwa DCI

Shahidi: Ilikwepo

Kibatala: Je katika Hati ya Makabidhiano hii MODEL CZ 100 Ilikwepo au haikuwepo

Shahidi: Ilikwepo

Kibatala: Kupitia Kielelezo P2 unasema Ulipokea K2 Mpaka K4 Mwambie Mheshimiwa jaji Kama Maelezo hayo yapo au hayapo

Shahidi: Sikuweka

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji pia Kuwa Maelezo ya ufafanuzi tuliyoyaona katika Live Catridge hapa, hayapo

Shahidi: Sikuweka

Kibatala: Unafahamu Kwamba Riport Kama hii haiongezewi Nyama Kutoka kwenye kizimba inatakiwa ijiongelee Yenyewe, Unafahamu au hfahamu

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Ni sahihi Nikisema wewe Kingereza Unakifahamu Ndiyo Maana Taarifa umeandika kwa Kiingereza

Shahidi: Ndiyo

KIBATALA: Nini Maana ya DCI

Shahidi: Director Criminal of Investigation

Kibatala: na ukasema Goodluck ametokea Ofisi gani DCI

Kibatala: Soma hapa shahidi: D/C Goodluck from Criminal Investigation Office

Kibatala: Nilipokuuliza Ulisema hivyo

Shahidi: Sikusema hivyo

Kibatala: kwa hiyo Kuna Utofauti Ulichoandika na Ulichosema Kwenye kizimba

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Shahidi Kwa Mujibu wa Kielelezo namba P2 ulipewa Risasi 03 ambazo ni Live, ambazo sisi ndiyo Vidhibiti vyetu, Umeviona hapa Mahakamani

Shahidi: Havipo, Nilivipiga

Kibatala: Sijakuuiza Kuhusu Kuvipiga

Kibatala: Ulicholeta Wewe ni Risasi Moja na Maganda Mawili ambayo hata hivyo vinatofautiana

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji ilikulazimu Kutimiza Vidhibiti, Kwamba Katika Ofisi ile palikuwa hakuna Risasi Nyingine Mbadala ililazimu Nitumie hivyo

Shahidi: Sikusema hivyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Iwapo Kuna Mahala yoyote ulipata Idhini ya kutumia Vithibiti kutoka kwa incharge wako kwa Kesi ya Ugaidi Kubwa kama hii

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwani Barua upo Mstari unasema Unaweza Kutumia Risasi Kupiga kwenye Water Tanki

Shahidi: Upo Kibatala: ikija tutaona

Kibatala: lakini Mahakamani pia hukusema

Shahidi: Ndiyo sikusema

Kibatala: Rangi ni Kitu ambacho unaweza Kujua Kwa Visual Examination au Ballistic Examination?

Shahidi: Kwa Visual Examination

Kibatala: Na Kuonyesha Kidhibiti kama Uliweka Rangi wakati unapokea

Shahidi: Sikuweka Rangi, Kwenye Visual Niliweka Rangi

Kibatala: Wakati unapokea

Shahidi: Sikuweka Rangi

Kibatala: Pamoja na Rangi unaona kwa Kuangalia tu, ila wewe hukuweka Rangi baada ya Kupokea

Shahidi: Siku weka Rangi

Kibatala: Kwa kuwa hukuweka Rangi huku ukaweka Rangi, Kuna Utofauti au Hakuna Utofauti

Shahidi: Kuna Utofauti

Kibatala: Barua iliyokuja hilo Kosa ambalo limeandikwa huko liliandikwa hivyo Conspiracy to Commit Terrorist

Shahidi: Iliandika kwa Kiswahili Kujihusisha na Ugaidi

Kibatala: Wewe sasa KINGEREZA chake ndiyo Ukatafsiri kuwa "Conspiracy to Commit Terrorist"

Shahidi: Ndiyo Nimetafsiri hivyo

Kibatala: Kuna Mahala Popote Umemwambia Jaji Kuwa wewe ni Gazzeted Officer?

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Umetaja Serial Namba, Je umemwambia jaji Kuwa ile Serial Namba ya Bunduki Kielelezo P3, inapatikana Kwenye Bunduki Moja tu Hapa Duniani, Ulimwambia hivyo

Shahidi: Si kumwambia Hivyo

Kibatala: Wakati wa Ushahidi Wako nilisikia Umesema Mwaka wa Kutengeneza Bunduki ilikuwa Mwaka gani

Shahidi: Mwaka 1995

Kibatala: Ulielezea hivyo

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Nimesikia Ulisema Bunduki hiyo Inauwezo wa Kubeba Risasi 08 ila wewe ulipewa Risasi 03

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mhe. Jaji Iwapo Ulisema Lolote la Kiuchunguzi Iwapo Risasi Nyingine 05 katika Bunduki hiyo Ilipiga Kwa Muda Mfupi uliopita

Shahidi: Sikuzungumzia

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwamba ni Utaratibu wa Kawaida Kila Bunduki inapokuja Kwenye kwenye Uchunguzi lazima Nitumie Vielelezo Vilevile Kupiga katika water Tank

Shahidi: Nilimwambia

Kibatala: Shahidi Katika Ushahidi wako wote kuna Mahala popote umesema Kuna Nyaraka Ilikuonyesha kwamba Kuna Uhusiano na Mtu anayeitwa Adam Kasekwa

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Katika Barua iliyoletwa Majina hayo yalikwepo au hayakwepo

Shahidi: Hayakwepo

Kibatala: katika Hati ya Makabidhiano Majina hayo yalikwepo au hayakwepo

Shahidi: hayakuwepo

Kibatala: katika Hati ya Makabidhiano Goodluck alikukabidhi wewe Vidhibiti, Je 9mm iliandikwa?

Shahidi: Haikuandikwa

Kibatala: Ulishawahi Kumwambia Mheshimiwa Jaji kwamba Hiyo Calliber 9mm

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Pamoja na Hati ya Makabidhiano na Barua kutokutaja Callibre 9mm, Katika Kidhibiti K1 Bastola ametaja Callibre 9mm kabla Ya Uchunguzi

Shahidi: Ndiyo Nilijaza Kabla Ya Uchunguzi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji kuhusiana Zoezi nililositisha kuhusiana tulichozungumza Asubuhi, Nasubiria sasa

JAJI: nawaomba Mawakili wa Pande zote mbili Ofisini Kwangu

JAJI: nahairisha Kwa Dakika 10

Jaji anatoka

Dakika 10 zimekwisha, bado jaji na mawakili hawajarejea

Jaji amerejea

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire na Wenzie inatajwa

Jaji: Muda uliopita Wakili aliomba Jambo Mahakama, Sasa tunaweza Kuendelea

Kibatala: Unakumbuka Kila kitu D/Coplo Goodluck alikutambulisha anatoka Ofisi ya DCI?

Shahidi: Sikusema anatoka Arusha

Kibatala: Ni Ushahidi Wako Katika Makabidhiano Kwamba D/Coplo Goodluck anatoka KWA DCI au CID Arusha

Shahidi: CID Arusha

Na Nyaraka hii ni Nyaraka ya Kisheria

Kibatala: Unafahamu Madhara ya Utofauti wa Ushahidi Wako na Yaliyopo kwenye Nyaraka?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni sahihi Katika Hati hii Ya a Makabidhiano Inasema Vitu Fulani, Kutoka Sehemu fulani na Inasehemu ya kutaja Majina

Shahidi: Haina sehemu hiyo

Wakili wa Serikali: OBJECTION wakili Kibatala ananyanyuka Nyaraka Juu Maana yake nink

JAJI: kwahiyo tatizo Kunyanyua

Kibatala: Nitaweka Chini basi

Kibatala: Kwa hiyo shahidi Nyaraka hii haina sehemu ya Kujaza Majina

Shahid:i HAKUNA

Kibatala: Hakuna Sehemu Unayotakiwa Kujaza aina Ya Vifaa unavyokabidhiwa?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nyaraka hii pia Inasehemu ya a nafasi ya Kuweka Majina ipo au Haipo

Shahidi: HAIPO

Kibatala: na Sehemu Ya Kujaza Aina ya Mashitaka Kwamba anatuhumiwa kwa Makosa........... IPO HAIPO..?

Shahidi: Haipo

Kibatala: Je katika Hii Hati ya Makabidhiano kuna Mahali inasema Jina la Fulani na mkabidhi Mtu fulani katika Fomu hii

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Inasehemu ya Kuweka Saini

Shahidi: Ipo Nimeweka Force Namba na Saini yangu

Kibatala: Ndiyo Ushahidi Wako huo?

Kibatala nilikusikia sahihi Ujuzi una utalamu wa Kutosha kuhusu Maswala ya Bunduki Nchini Tanzania

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika Ushahidi wako wote Uliwahi Kumwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa aina ya Bunduki CZ100 Luger ni Moja wapo ya Bunduki kutoka Jeshi la Wanachi Tanzania

Kibatala: Swali la Mwisho Kwako Kuna Mahala Popote ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusu Ulinganifu Kati ya Ofisi ya CO ARUSH na DCI..?

Shahidi: Sikumwambia

Jaji: Re examination

Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuuliza Kwa ajili ya ufafanuzi kwa Yale uliyoulizwa Mahakama uweze Kuelewa Ushahidi wako

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kwenye Riport Yako Paragraph ya Kwanza inapoanza I have been engaged...Tools na Maganda

Shahidi: Paragraph ya Kwanza Inajielezea Na Inajielezea Uchunguzi Nilikuwa nafanya pale Forensic kwa Miaka 10 nikaweka Bunduki, Risasi(ammunition), Maganda (spent Catridge) Na nikarejea Nimefanya Uchunguzi huu kwa Muda wa Miaka 10

Wakili wa Serikali: Sasa Tools ambayo havikuletwa kwako Vifafanue hapo

Shahidi: Sasa hao hawakuleta Tools, Wakili wa Serikali: sasa Kwanini hukivikufika hapa

Shahidi: Sababu, Ndiyo navichunguza pale Forensic Beaural

Wakili wa Serikali: Kuna Maswali Umeulizwa hapa ukasema Ni Maswala ya Utalii Unakumbuka

Shahidi: Ndiyo, Nilisema Terrorist, spelling nikatamka, Nikasikia Tourism, Tourism ni Maswala ya Kitalii.

Wakili wa Serikali: Lakini kilichopo kwenye Riport yako ni Kitu gani

Shahidi: ni Terrorist

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Ukasema Hapa Firing Pin, Barrow na Ukaulizwa ulionyesha Mahakama Jinsi hivyo Vitu vinavyofanya kazi

Shahidi: Nilionyesha

Wakili Mallya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Sikuuliza Swali la namna hiyo

Wakili wa Serikali: Nauliza na wenzangu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Nimeulizana na Wenzangu Jibu ni kuwa Sikuonyesha, ipo katika Riport Yangu

Wakili wa Serikali: Shahidi Kwanini sasa Hukuweka

Shahidi: Nilichoweka nilichoombwa na Mteja tu

Wakili wa Serikali: Sasa Ulichoombwa ni nini

Shahidi: Kuchunguza Pistol, Risasi na Maganda ya Risasi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Ukasema Kwenye Riport Yako hakuna Neno Luger, Ieleze Mahakama Kwanini hukuweka

Shahidi: Bunduki ni Serial Namba

Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema Bunduki ni Serial Namba

Shahidi: Serial Namba ni Unique

Wakili Malya: OBJECTION Hiyo ni New Fact Kwa sababu Hakueleza Kuwa Serial Namba ni Unique

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tukumbushwe

JAJI: Ndiyo, Kibatala alimuuliza Kwamba Je serial Namba haiwezi Kuonekana kwenye Bunduki Nyingine yoyote

Wakili wa Serikali: Hukueleza Mahakama Kwanini Luger hukuweka Kwenye Riport

Kibatala: OBJECTION tuliuliza Luger ipo au Haipo, Jibu likasema Haipo, akijibu Lolote ni New Fact labda turuhusiwe tena Kumuhoji wakimaliza.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi tunataka atoe Sababu Kwanini Haipo

JAJI: hiyo itatupeleka kwenye New facts na Sababu watatakiwa warudi pia Kumuhoji upya

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tunashukru

Wakili wa Serikali: ulimaanisha Nini Kusema Vielelezo Haipo Mahakamani

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kuwa havipo Kwa sababu Nimevitumia Kupiga Katika Ile Bastola

Wakili wa Serikali: Ilifuatiwa na Swali Hukumwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusu Kutoleta hivyo Vielelezo

Shahidi: Mimi nilifuata Maelekezo ya Barua, Kwamba Natakiwa Kupiga, nikapiga

Jaji: Swali lilikuwa linahusu nini na Alichokujibu ndiyo ulichouliza

Wakili wa Serikali: Kajibu Tofauti

Wakili wa Serikali: Nilikuwa nataka Kujua Shahidi Ulikuwa unamaanisha Nini Kusema Hukuwa na Idhini

Shahidi: Kimyaaaaaaaaa

Wakili wa Serikali: Naomba Nitoke hapo Mheshimiwa Kuokoa Muda wa Mahakama

Wakili wa Serikali: Katika Ushahidi wako Unasema ulipokea Kielelezo Cha kumpokea 9mm lakini kwenye Barua Hakuna

Shahidi: Kwa sababu Wale ni Layman hawawezi Kujua ni Silaha ya namna gani, Mimi Ndiyo Mtaalamu nikajua ni Pistol Calliber 9mm

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Mwenzangu aendelee

Wakili wa Serikali Katuga: Shahidi Uliulizwa Kama Uliomba Idhini Kwa Kiongozi wako ili utumie Risasi hizo hizo, Hebu eleza Ni kwanini Hukuomba Idhini Wakili Peter

Kibatala: OBJECTION tunarudi Kulekule kama alitoa Sababu itakuwa Mpya, Anaalika Shahidi atoe Sababu

Jaji: Swali linasema

Wakili wa Serikali: Kwanini hakuomba Idhini

Wakili Peter Kibatala: Itakuwa New Fact akijibu

Wakili wa Serikali: Tunaomba tupewe Nafasi wao Ndiyo walifanya Cross Examination

JAJI: Ngoja aendelee

Shahidi: Kwanza ni Mambo ya Kiofisi siwezi Kueleza Hapa Mahakamani, miye naangalia Barua siwezi Kuuliza Afande.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali ni kwanini hukutumia Risasi zilizokwepo Maabara kwa Uchunguzi wako badala yake Ukatumia zilezile zilizoletwa na wao

Shahidi: Kutokana na Barua Yao walitaka Kujua ni Nzima.? ndiyo Maana nikatoa nikapiga kwenye Bunduki

Wakili wa Serikali: Uliletewa Kielelezo Ukatakiwa Usome Nyuma ya maganda, Ukasema ni Tofauti Elezea Maana yake ni nini Wakili

Peter Kibatala: OBJECTION Huko wanakoenda Kupya

Jaji: Naona Kuna problem

Wakili wa Serikali: Sawa Mheshimiwa Jaji Nita rephrase

Shahidi: Hakuna nipoombwa Kufafanua Kwenye Barua

Wakili wa Serikali: Kwani wewe Uliomba Kufanya nini

Shahidi: Waliniomba Kufanya Uchunguzi wa Pistol na Risasi, ni Nzima?

Wakili wa Serikali: Katika Uchunguzi wako hakuna Sehemu Umetumia Neno Luger Ukasema ni Kweli Hakuna ulipo tumia, Sasa Uliandika kwa utambulisho Upi

Shahidi: Kwa Serial Namba yake A5340 callibre 9mm, Cz100.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana na Tarehe 21 November 2020 Vielelezo Kwa ajili ya uchunguzi, Swali Lilikuwa Hukumtaja Ofisa aliyekuwa Hammery ni Ofisa yupi, kwanini hukusema

Shahidi: Sikusema Kwa sababu hayo Mambo ni ya Kiofisi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kwamba Katika Ushahidi wako wote hujataja Jina la Silaha aliyekamatwa nazo, Kwanini hukutaja

Shahidi: Kwanza sijui Adamoo

JAJI: mmeleta Kitu Kipya

Wakili wa Serikali: Asante

Wakili wa Serikali: Endelea na Kitu cha Pili

Shahidi: Barua hakutaja Majina

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusu D/C Goodluck kwamba anatoka Ofisi ya DCI na Baadae CID Ofisi Arusha

Wakili Peter Kibatala: we Musta OBJECT sisi tulifika Mbali tukamuuliza kama alifafanua Utofauti wa DCI na CID Arusha, Anachotaka ni Maelezo Mapya

Wakili wa Serikali: Basi Naondoa Swali Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kwamba Barua haikuwa na Maelezo ya silaha

Shahidi: Mimi Ndiyo Nitaeleza Kitaalamu wala siyo wewe Mteja

Wakili wa Serikali: Hafidhi Uliulizwa kuhusu Bastola ambayo Kibatala alitaja CZ 100 kama Ulisema ni Standard ya JWTZ, kwanini sasa Hukusema

Shahidi: Sijui, Miye sijui

Wakili wa Serikali: Hafidh Uliulizwa swali Moja kuwa kwenye Ushahidi wako Hakuna Mahala Popote ulipozungumzia kama Silaha ilikuwa imepigwa kabla ya Kuleta Forensic Beaural

Shahidi: Hawakuomba Kufanya Uchunguzi wa Gun Powder Resolution

Wakili wa Serikali: ambayo ni Kitu gani

Shahidi: Gun Powder Ni Baruti

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali na Wakili Msomi Malya kama Bastola ile iliwahi Kuwa Mbovu na Baadae Ikatengenezwa

Shahidi: Sikuweza Kujua Kama Ingekuwa Mbovu na Vilevile Sikuombwa nifanye

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali pia kuhusiana na Grooves zinazotoka kwenye Bullets kama Zinalinganishwa kutoka kwenye Mtutu Ukasema Hapana, kwanini Hakuwezi kulinganisha

Shahidi: Grooves unaweza kulinganisha endapo Zinakuja Mbili Unachua Specimen Side A na Side B Kufanya Mlinganisho

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu, Hatuna Maswali Mengine

Jaji: Shahidi Tunashukuru kwa Ushahidi wako na Unaweza kwenda

Jaji: upande wa Jamhuri

Wakili wa Serikali: Robert Kidando Tunaomba ahirisho la Shauri hili Mpaka Jumatatu Tarehe 01 November 2021 Tuweze kuendelea na Usikilizwaji

Wakili Peter Kibatala: Hatuna Objection Mheshimiwa

Jaji: Ombi la Kuhairishwa limekubaliwa Mpka Jumatatu Tarehe 01 November 2021

Jaji: Washitakiwa wataendelea Kuwa chini ya Magereza Mpaka tarehe Hiyo

Jaji anatoka
Mawakili wa utetezi mbona maswali yenu butu
 
Kutokujua kiingereza haikufanyi ukawa mjinga mkuu. Mbona Wachina, Warusi, Wakorea n.k. hawajui kiingereza lakini ni wagunduzi wa mambo mengi tu hapa duniani.
kumbuka yuko mahakaman akitoa ushahidi wa kile alichokiandika, sasa kama hujui ulichokiandika unaenda kutoa ushahidi wa kitu gan? mahakaman sio bar ujue
 
Polisi wanasema wamemkuta nayo, yeye anasema wamemuwekea. Sasa hapo Nani anasema ukweri?? Na kwanini polisi hawakuchukua finger print ili wapati kidhibiti kisichokua na Shaka?
Wanapima sijui kitako,mara mm...sijui Bore nini nini huko..Inakera.. Kesi ya Kipuuzi kama Polisi wenyewe walivyo wapuuzi..
 
Ndo maana wanajitoa... Huyu Jaji wa sa hivi naye atajitoa very soon!
Mtu timamu hawezi kusikiliza na kusimamia maagizo toka juu ya kipuuzi kiasi kile!
Ushiriki wa jina la Sabaya na uwepo wa mashahidi waongo kwenye hii kesi ni uthibitisho kuwa:
✓Tuhuma zote ni haramu!
✓Mbowe na wenzake si magaidi!
✓Shahidi namba 2 ni mhujumu uchumi aende aliko Sabaya!
✓Mashahidi toka PT ni zero brainers!
Refa kuibeba timu yenye uwezo duni ni kazi kubwa Sana, aidha ajitoe au akubali kupopolewa.
 
Hii nchi hakika viongozi wala wasimamizi wa mahakama huwa hawapati akili, kama hawa ma Judge wa hii kesi (Aliejitoa na Huyu Alikuwepo Sasa).

1) Wanasahau kwamba maisha hubadilika. Leo unaemkandamiza pengine kesho mungu anaweza akampa mamlaka juu yako.

2) Kuna maisha baada ya vyeo.

3) Kuna kudharaulika na kuharibu sifa zao za kazi waliozifanyia juhudi kwa miaka mingi, pengine maisha yao yote.

4) Mungu yupo, anaona na anajua kila kinachofanyika.
Askari polisi anaejiita mtaalamu wa sikaha hajui kutofautisha kati ya tourist na terrorist
 
Back
Top Bottom