Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

Waziri Mkuu mh Majaliwa amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO wa Mtwara na OCD na OCID wa Kilindi Tanga ili kupisha uchunguzi wa Tume aliyoiunda.

Pia, Waziri Mkuu Mkuu Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu 9 yenye watu kutoka ofisi mbalimbali za serikali ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, mkoani Tanga. Ameipa siku siku 14 kukamilisha kazi hiyo kuanzia kesho.

====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

“Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,” amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Mheshimiwa Rais amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati hiyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na askari polisi. Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 05, 2022 na mauaji ya Kilindi yaliyotokea Januari 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kamati hiyo ina maafisa wenye dhamana kutoka mamlaka tofauti za Serikali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Ofisi ya Mwanansheria Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mtwara na Kilindi ili kupisha uchunguzi wakati timu aliyoiunda ikifanya kazi yake.

“Viongozi hawa wanapaswa wakae pembeni, watahojiwa na hii timu wakiwa nje ya ofisi,” amesema Waziri Mkuu na kuwataja maafisa hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara (RPC), Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mtwara (RCO) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara cha eneo alilofia mfanyabiashara Mussa Hamisi Hamisi na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Greyson Mahenge anayedaiwa kujinyonga.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kilindi na Afisa Upelelezi wa Wilaya nao pia wakae pembeni kupisha uchunguzi

Pia soma

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Mtwara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

Mauji ya wafugaji na wakulima wilaya ya Kilindi, soma Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji (Januari 30, 2022)

Mjomba wa marehemu alie ambatana na mfanya biashara alie uawa na polisi ajihadhari, anaweza mfuata polisi aliejinyonga.
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
Siro kuondoka bila waziri wa mambo ya ndani kujiuzuru
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
Nyboma, ajiuzulu ale wapi?
 
Cha ajabu Waziri wa Mambo ya Ndani yupo halafu anakuwa hana nguvu ya kuwasimamisha hao mpaka Rais aongee

Hivi hawa watu majukumu na kazi zao na maamuzi yao hawajui?

Nguvu na uwezo wao wa kuamua kitu hawana au huwa wana uoga fulani kwa kukosa confidence?

Hata PM alichelewa sana hili shauri sio lazima Rais aingilie
Hawa watu wanabebana sana mpaka kinyaa

PM hawezi kumuwajibisha Mkuu wa Polisi wanajuana
Hii ndio inafanya watu wengi wakose haki zao hata kama wameuwawa

Rais anaingilia really?
 
Mjinga anangoja hadi aaibishwe
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
 
Nchi ya mauza uza hii. Waziri mkuu mwenyewe pamoja waziri wa mambo ya ndani walipaswa kujiuzulu ama kufukuzwa kazi.

Cha ajabu hata Nyakoro Siro bado IGP wa jeshi la polisi.

Only in Tanzania
Polisi wakifanya ujambazi ajiuzuru waziri mkuu?
Sabaya kafanya ujambazi kala 30, Cha msingi ni kutenda haki kwa Hawa wauwaji wanyongwe ila kama wauwaji wataachiwa Basi inabidi viongozi wawajibishwe.
 
Nchi ya mauza uza hii. Waziri mkuu mwenyewe pamoja waziri wa mambo ya ndani walipaswa kujiuzulu ama kufukuzwa kazi.

Cha ajabu hata Nyakoro Siro bado IGP wa jeshi la polisi.

Only in Tanzania
Kwanini asijiuzulu hangaya mwenyewe?
 
Nashindwa kuelewa Uwajibikaji wa WAZIRI wa Mambo ya NDANI na IGP SIRRO kwenye SAKATA la KUUWAWA Mfanya Biashara wa MADINI na Kuporwa Fedha zake na POLISI.
Leo Mh.RAIS SAMIA Ameshangazwa kuundwa kwa TUME ya Kuchunguza hilo SAKATA na POLISI wenyewe WANAOTUHUMIWA na Kumwagiza WAZIRI MKUU Kuunda KAMATI HURU ya KUCHUNGUZA TUKIO HIYO bila KUWAHUSISHA POLISI
Baadae WAZIRI MKUU Akamwagiza IGP SIRRO Awasimamishe kazi RPC na RCO na Maofisa Wengine.
Najiuliza
1.Kwanini WAZIRI mwenye Dhamani Hakumwagiza IGP SIRRO kuwasimamisha KAZI hao WAHUSIKA hao Mpaka WAZIRI MKUU Atoe AGIZO?
2.Kwanini IGP SIRRO binafsi hakuwasimamisha kazi hao Wahusika au ndio KUWALINDA hao WAKUBWA?
View attachment 2107931

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Samia mwenyewe aliwapiga mkwala watendaji Wake live,kuwa hiki sio kipindi cha kuwajibisha watendaji hata wakikutwa wamekosea inabidi waitwe pembeni,ndipo ahambiwe makosa yake, sasa kwa mwendo huko ninani atasubutu kumsimamisha kazi mtumishi kabla tamko la rais?
 
Safi sana👏👏

Hivi inawezekanaje Polisi wakiwa watuhumiwa, wajichunguze wenyewe??

Hilo ndilo tatizo la matukio mengi ya Mauaji yanayotokea nchi hii, kutojulikana wahusika

Kwa kuunda Tume huru namuunga mkono kwa asilimia 100 Waziri Mkuu, kuwa amefanya uamuzi wa busara Sana.

Kilichokuwa kikifanyika hapa nchini ni Kesi ya nyani kumpa ngedere aamue!

Hakika Haki isingeweza kupatikana
Unataka yamkute ya Ndungai?
 
Waziri Mkuu mh Majaliwa amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO wa Mtwara na OCD na OCID wa Kilindi Tanga ili kupisha uchunguzi wa Tume aliyoiunda.

Pia, Waziri Mkuu Mkuu Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu 9 yenye watu kutoka ofisi mbalimbali za serikali ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, mkoani Tanga. Ameipa siku siku 14 kukamilisha kazi hiyo kuanzia kesho.

====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

“Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,” amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Mheshimiwa Rais amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati hiyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na askari polisi. Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 05, 2022 na mauaji ya Kilindi yaliyotokea Januari 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kamati hiyo ina maafisa wenye dhamana kutoka mamlaka tofauti za Serikali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Ofisi ya Mwanansheria Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mtwara na Kilindi ili kupisha uchunguzi wakati timu aliyoiunda ikifanya kazi yake.

“Viongozi hawa wanapaswa wakae pembeni, watahojiwa na hii timu wakiwa nje ya ofisi,” amesema Waziri Mkuu na kuwataja maafisa hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara (RPC), Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mtwara (RCO) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara cha eneo alilofia mfanyabiashara Mussa Hamisi Hamisi na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Greyson Mahenge anayedaiwa kujinyonga.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kilindi na Afisa Upelelezi wa Wilaya nao pia wakae pembeni kupisha uchunguzi

Pia soma

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Mtwara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

Mauji ya wafugaji na wakulima wilaya ya Kilindi, soma Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji (Januari 30, 2022)

Nilitegemea Waziri Mkuu atakuwa na Ujasiri wa kuteua Wajumbe wawili kutoka kwenye Kamati ya Haki na Amani ya Viongozi wa Dini. Awemo Sheikh mmoja na Askofu mmoja ili Ripoti ya hiyo Tume ikubalike, iwe 'credible'.
Kuweka Watumishi wa Serikali pekee kunatia shaka.
 
Ndugu yangu na rafiki yangu IGP Sirro Nyakoro kwanini anakuwa mgumu kujiuzulu, ajifunze kusoma alama za nyakati Mama hamuhitaji tena kwenye serikali yake anayoiongoza maana anaitia doa.
labda akijiuzuru kuna baadhi ya haki za kimafao anapoteza kuliko akisubiri asataafishwe. umri wake nao umeenda. au wenye uelewa watuambie, manake ukiona hadi maza kasema polisi wajitathimini, ndio lugha yenyewe hiyo kwamba kama usipojitathimini unaweza kufurushwa kinguvu na kwa aibu, sema kwasababu polisi huwa na roho ngumu hilo sio la kuogopa kwao.
 
Nilitegemea Waziri Mkuu atakuwa na Ujasiri wa kuteua Wajumbe wawili kutoka kwenye Kamati ya Samani ya Viongozi wa Dini. Awemo Sheikh mmoja na Askofu mmoja ili Ripoti ya hiyo Tume ikubalike, iwe 'credible'.
Kuweka Watumishi wa Serikali pekee kunatia shaka.
hakuna kupeleka watu wa dini hapo, kwasababu ukigusa kwenye dini tu itabidi uweke kila dhehebu, hao wawakilishi wa dini usifikiri huwa wanawakilisha kila mtu, mfano , padre akienda pale usije fikiri ananiwakilisha mimi, anawakilisha wakatoliki, bado kuna waprotestanti,wasabato n.k, futa hayo mambo. weka watu wa serikali. ambacho najua huwa kinatokea hapo wataweka mtu wa tiss, jeshi, polisi, mwanasheria,pccb, na wengine kadhaa. na kwenye timu kama hizo hakika huwa wanafanya kazi ya kueleweka kwasababu wao kwa wapo pia huwa wanakaa kwa machale ya kuchunguzana wao kwa wao na kila mtu ana report kwa boss wake hivyo ni ngumu kuconspire kudanganya. hapo najua kuna moto utawawakia hao wakubwa aliowasema baba wa marehemu polisi na hao waliosababisha kifo cha mfanyabiashara. hata hao walioko gerezani kwa tuhuma wakahojiwe vizuri. patachimbika, na waongezewe ulinzi huko gerezani.
 
Nchi ya mauza uza hii. Waziri mkuu mwenyewe pamoja waziri wa mambo ya ndani walipaswa kujiuzulu ama kufukuzwa kazi.

Cha ajabu hata Nyakoro Siro bado IGP wa jeshi la polisi.

Only in Tanzania
Kwa kweli, hili ndilo lilitakiwa kufanyika tena bila aibu.

Ila naye Siro mpaka anaagizwa na kuonyeshwa watu wa kusimamishwa kazi, yeye yuko wapi? Unajua kweli ukisha pigwa upofu wa maono, unakuwa kituko tu.....tujitahidi tusifike huko Wajameni. Tuanzage mapema tu ktk maeneo yetu.
 
Waziri Mkuu mh Majaliwa amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO wa Mtwara na OCD na OCID wa Kilindi Tanga ili kupisha uchunguzi wa Tume aliyoiunda.

Pia, Waziri Mkuu Mkuu Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu 9 yenye watu kutoka ofisi mbalimbali za serikali ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, mkoani Tanga. Ameipa siku siku 14 kukamilisha kazi hiyo kuanzia kesho.

====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

“Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,” amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Mheshimiwa Rais amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati hiyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na askari polisi. Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 05, 2022 na mauaji ya Kilindi yaliyotokea Januari 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kamati hiyo ina maafisa wenye dhamana kutoka mamlaka tofauti za Serikali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Ofisi ya Mwanansheria Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mtwara na Kilindi ili kupisha uchunguzi wakati timu aliyoiunda ikifanya kazi yake.

“Viongozi hawa wanapaswa wakae pembeni, watahojiwa na hii timu wakiwa nje ya ofisi,” amesema Waziri Mkuu na kuwataja maafisa hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara (RPC), Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mtwara (RCO) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara cha eneo alilofia mfanyabiashara Mussa Hamisi Hamisi na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Greyson Mahenge anayedaiwa kujinyonga.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kilindi na Afisa Upelelezi wa Wilaya nao pia wakae pembeni kupisha uchunguzi

Pia soma

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Mtwara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

Mauji ya wafugaji na wakulima wilaya ya Kilindi, soma Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji (Januari 30, 2022)

Sema mara nyingi hizo tume za PM huwaga haziletagi majibu.Huwa zinaishiaga moja kwa moja.Bora hata zile tume za Amos makala zinaletaga majibu hata kama dhaifu lakini huwa tunajulishwaga
 
Back
Top Bottom