Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aruhusu ghorofa lijengwe, wawili wasimamishwa, mmoja arudishwa Wizarani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Elikana Balandya awasimamishe kazi watumishi wawili wa Jiji la Mwanza huku akiagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa huo arudishwe wizarani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Ameagiza ujenzi wa ghorofa uliositishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Amos Makalla uendelee kwenye viwanja namba 194 & 195 kitalu ‘U’ Rwagasore, jijini Mwanza na wamiliki wa viwanja hivyo wakabidhiwe hati zao kama alivyokuwa ameelekeza awali.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Oktoba 3, 2023) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma cha viongozi wa majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga na Dodoma ili kujadili migogoro ya ardhi iliyokithiri kwenye majiji hayo.

“Ninaagiza Katibu Tawala wa Mkoa wasimamishe kazi Mkuu wa Idara ya MipangoMiji, Bw. Robert Phares na Afisa Mteule na Mkuu wa Kitengo cha Ardhi katika Jiji la Mwanza, Bi. Halima Iddi Nasoro. Na Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi (Mwanza), Bw. Elia Kamihanda arudishwe makao makuu na achukuliwe hatua za kinidhamu.’’

Chanzo: Ofisi ya Waziri Mkuu
 
Upigaji tu.

Watu hawashibi.

Kila kitu mle mtu kujenga mnamfanyia nongwa.

Kasim, liwalo na liwe, songa mbele, kwanza washakuvuruga
 
Kuujua UKWELI wakati mwingine ni Hadi wadau wa mgogoro pande zote mbili wawe nje ya mfumo.

Tofauti na hapo!!
 
... la muhimu asije naye akawa na maslahi kwenye hilo ghorofa! Ninaogopa kweli kweli!
 
Ameagiza ujenzi wa ghorofa uliositishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Amos Makalla uendelee kwenye viwanja namba 194 & 195 kitalu ‘U’ Rwagasore, jijini Mwanza na wamiliki wa viwanja hivyo wakabidhiwe hati zao kama alivyokuwa ameelekeza awali.
Huyu Mkuu wa Mkoa si ndiyo yule aliyekuwepo Dar es Salaam kipindi cha mgomo wa wafanyabiashara?
Midimay
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Elikana Balandya awasimamishe kazi watumishi wawili wa Jiji la Mwanza huku akiagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa huo arudishwe wizarani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Ameagiza ujenzi wa ghorofa uliositishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Amos Makalla uendelee kwenye viwanja namba 194 & 195 kitalu ‘U’ Rwagasore, jijini Mwanza na wamiliki wa viwanja hivyo wakabidhiwe hati zao kama alivyokuwa ameelekeza awali.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Oktoba 3, 2023) kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma cha viongozi wa majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga na Dodoma ili kujadili migogoro ya ardhi iliyokithiri kwenye majiji hayo.

“Ninaagiza Katibu Tawala wa Mkoa wasimamishe kazi Mkuu wa Idara ya MipangoMiji, Bw. Robert Phares na Afisa Mteule na Mkuu wa Kitengo cha Ardhi katika Jiji la Mwanza, Bi. Halima Iddi Nasoro. Na Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidizi (Mwanza), Bw. Elia Kamihanda arudishwe makao makuu na achukuliwe hatua za kinidhamu.’’

Chanzo: Ofisi ya Waziri Mkuu
Kusimamishwa pekee hakutoshi jamani
 
Makala kaukuta msala, hapo Kuni mikono ya wakubwa.

Si Rahisi kuujua UKWELI.
Vyovyote vile lakini kauli ya PM inamuweka pabaya sana ,kitendo Cha PM kutoa maelekezo Kwa RAS ambaye ni msaidizi wa RC kufanya kile alichozuia bosi wake ni jambo dogo?

Ni kama Leo Rais ampe Waziri mamlaka ya kutenda kinyume na agizo la Waziri mkuu hapo inaonesha waziri mkuu kuna kitu kakosea pakubwa sana
 
Huyu Mkuu wa Mkoa si ndiyo yule aliyekuwepo Dar es Salaam kipindi cha mgomo wa wafanyabiashara?
Midimay
Huyu Amos Makalla alishafukuzwa kazi ya kuwa RC na Magufuli lakini Kikwete akamshinikiza Samia amrudishe kulinda maslahi yake baada ya kifo cha Jiwe!! Hafai.
 
Shida huyu hatakuwa waziri mkuu wa milele , akitoka haki za huyo mtu zitakuaje, inabidi haki itendeke na c matamko
 
Huyu Amos Makalla alishafukuzwa kazi ya kuwa RC na Magufuli lakini Kikwete akamshinikiza Samia amrudishe kulinda maslahi yake baada ya kifo cha Jiwe!! Hafai.
Huelewi chochote, angalia kwa jicho pana. Rudi tena kwenye mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo
 
Back
Top Bottom