Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi Mabosi wa Polisi Mtwara na Kilindi kupisha uchunguzi wa mauaji

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,562
Waziri Mkuu mh Majaliwa amemuagiza IGP Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO wa Mtwara na OCD na OCID wa Kilindi Tanga ili kupisha uchunguzi wa Tume aliyoiunda.

Pia, Waziri Mkuu Mkuu Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu 9 yenye watu kutoka ofisi mbalimbali za serikali ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, mkoani Tanga. Ameipa siku siku 14 kukamilisha kazi hiyo kuanzia kesho.

Pia soma:

Kuhusu mauaji ya mfanyabiashara Mtwara
, soma Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7 (Januari 25, 2022)

Mauji ya wafugaji na wakulima wilaya ya Kilindi, soma Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji (Januari 30, 2022)

====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameunda timu maalum ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

“Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,” amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa leo (Ijumaa, Februari 4, 2022) mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Mheshimiwa Rais amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati hiyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na askari polisi. Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 05, 2022 na mauaji ya Kilindi yaliyotokea Januari 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Kamati hiyo ina maafisa wenye dhamana kutoka mamlaka tofauti za Serikali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Ofisi ya Mwanansheria Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro awasimamishe kazi maafisa wa Polisi wa Mtwara na Kilindi ili kupisha uchunguzi wakati timu aliyoiunda ikifanya kazi yake.

“Viongozi hawa wanapaswa wakae pembeni, watahojiwa na hii timu wakiwa nje ya ofisi,” amesema Waziri Mkuu na kuwataja maafisa hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara (RPC), Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mtwara (RCO) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara cha eneo alilofia mfanyabiashara Mussa Hamisi Hamisi na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Greyson Mahenge anayedaiwa kujinyonga.

Aidha, Waziri Mkuu ameagiza Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kilindi na Afisa Upelelezi wa Wilaya nao pia wakae pembeni kupisha uchunguzi



Kassim.jpg
 
Matokeo ya huo uchunguzi tuambiwe umma baada ya hizo siku 14, wasije kuendelea na tabia yao ya kukaa kimya.
 
Nashindwa kuelewa Uwajibikaji wa WAZIRI wa Mambo ya NDANI na IGP SIRRO kwenye SAKATA la KUUWAWA Mfanya Biashara wa MADINI na Kuporwa Fedha zake na POLISI.
Leo Mh.RAIS SAMIA Ameshangazwa kuundwa kwa TUME ya Kuchunguza hilo SAKATA na POLISI wenyewe WANAOTUHUMIWA na Kumwagiza WAZIRI MKUU Kuunda KAMATI HURU ya KUCHUNGUZA TUKIO HIYO bila KUWAHUSISHA POLISI
Baadae WAZIRI MKUU Akamwagiza IGP SIRRO Awasimamishe kazi RPC na RCO na Maofisa Wengine.
Najiuliza
1.Kwanini WAZIRI mwenye Dhamani Hakumwagiza IGP SIRRO kuwasimamisha KAZI hao WAHUSIKA hao Mpaka WAZIRI MKUU Atoe AGIZO?
2.Kwanini IGP SIRRO binafsi hakuwasimamisha kazi hao Wahusika au ndio KUWALINDA hao WAKUBWA?
1643988747857.jpg


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom