Hivi Tume za Uchunguzi zinazoundwa na Mamlaka lengo lake ni kutuliza upepo au kuzima matukio?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Kwa miaka ya hivi karibuni kuna Ripoti nyingi zimewasilishwa za uchunguzi kuhusu matukio mbalimbali iwe ya vurugu, mauaji au tuhuma mbalimbali lakini changamoto kubwa ni kukosekana mwendelezo wa ripoti hizo ambazo huwa zinaundiwa Tume.

Ninavyoona kuna matukio mengi ambayo yamezimwa kisiasa au kupotezewa kwa kigezo cha kuwa mamlaka zimeunda Tume kuchunguza, wakati mwingine wakaiona upepo bado upo wa tukio husika wanajibu kuwa imewasilishwa lakini baada ya hapo kimyaa

Hoja yangu ni kuwa hizi ripoti zipo kwa ajili ya kuzima matukio au kutuliza upepo?

Hivi hapa chini ni baadhi ya ipoti za miaka ya hivi karibuni ambazo Serikali iliingilia na kusema Tume zimeundwa lakini kilichofuata baada ya hapo ni...... unaweza kukumbushia Tume nyingine unazozikumbuka"

=====

Februari 4, 2022
Maafisa wa Polisi kupisha uchunguzi kuhusu mauaji ya Mtwara, Kilindi Tanzania, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameunda timu maalumu ya watu tisa ambayo imepewa jukumu la kuchuguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi Tanga.

''Kamati hiyo inapaswa kuanza kazi yake kesho na inatakiwa iwe imekamilisha ripoti yake ndani ya siku 14,'' amesema Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alilolitoa akiwa mjini Magu, Mwanza.

Rais Samia amesema anatambua Jeshi la Polisi limeunda kamati ya uchunguzi lakini ameagiza iundwe kamati iliyo huru ili ikafanye uchunguzi wa mauaji ya Mtwara yaliyofanywa na polisi.

Mauaji ya Mtwara yalitokea Januari 5 na mauaji ya Kilindi yalitokea Januari 30 mwaka huu.

Februari 26, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya kamati maalum aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza mauaji katika mkoa wa Mtwara na wilaya ya Kilindi, mkoani Tanga. Na kusema kwamba baada ya kuipitia taarifa hiyo ataiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye aliyetoa maagizo ya kuundwa kwa kamati hiyo ya kuchunguza mauaji kwenye Mikoa ya Mtwara na Tanga.

Oktoba 3, 2022
Tume ya kuchunguza mauaji ya mfanyabiashara wa madini Mtwara iliishia wapi? Moja ya nchi zinazoongoza kwa Kuunda Tume mbalimbali za Uchunguzi kwenye Majanga na Matukio kadhaa ni Tanzania.

Miezi kadhaa kulitokea mauaji ya mfanyabiashara wa madini huko Mtwara na Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi waliunda Tume lakini ikaonekana kuwa ndugu wa Marehemu wanalilalamikia Jeshi la Polisi kuhusika katika hayo mauji basi Serikali ikaunda Tume yake.

Sasa ni miezi kadhaa imepitia hatujasikia majibu ya hiyo Tume, je, kulikoni?

Tume ya kuchunguza mauaji ya mfanyabiashara wa madini Mtwara iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom