Hivi kwa nini TUTUMIE cards zenye microchip? Mimi nafikiri kwa nchi masikini kama Tanzania laminate cards inatosha. Bei yake ni karibu na bure. Ila tu ni kukomputerise huo utambulisho wa wahusika NA HAPO ITACHUKUA BILLION KIDOGO SANA.Sidhani wakati wote unahitaji local professionals kufanya kazi.Kuna suala la security na ufichaji teknolojia watu wasiibe wakaanza kuvitengeneza ovyo.
Swali ni je Mpiga chapa wa serikali anayo credibility ya kuficha siri ya tecknolojia yake ya kuchapisha document za siri? Wafayakazi wake waweza aminika na wana historia ya uaminifu wa kuficha siri na kutochapisha vya ziada na kuwapa wageni mamluki?
Documents nyingi zenye features za siri zikiwemo passport,fedha,cheki na kadhalika za nchi nyingi tu duniani huchapishwa na nchi nyingine si kuwa wataalamu wanakuwa hawapo katika nchi hizo nadhani hata marekani hawachapi passport na pesa zao huchapishwa kwingine pamoja na uwezo mkubwa wa teknolojia walionao.India pekee ndio nasikia wanachapa pesa zao wenyewe nchini mwao.Nadhani inawezekana kwao sababu culture ya wahindi ni wasiri mno wao labda wwanaweza mambo haya.Ila kwa watanzania sijui.Mtu akipewa hiyo kazi kusema akilewa hataropoka kwenye baa sijui.
Labda kama mpiganaji nitoe siri ndogo ya kivita kwa wanaojenga nyumba.Unapojenga nyumba unapoweka dari usimchukue fundi wa kupiga dari wa karibu na eneo unaloishi.Mtafute fundi toka mbali hata kama wapo mafundi wengi tu kwenye eneo unaloishi.Sababu ni kuwa kwenye dari kuna lile tundu unalomalizia kufunga dari ambalo mtu aweza kupanda akitaka kuingia darini.Lile tundu unalomalizia kufunika dari ni eneo la vita hatakiwi mtu ajue liko wapi asijue liko sebureni,chumbani,jikoni,au wapi.Wakija majambazi waweza panda kwa spidi ya mwewe darini ukawasubiria kwenye eneo la tundu ya dari na bastola au bunduki yako au jiwe lako la fatuma.Sasa majambazi yakikaribia hilo eneo unalifungua kwa spidi ya mwewe na kuwamiminia risasi na kurukia mbali eneo lingine ambako hata warushe risasi hawakupati au ukishawamiminia risasi kwa spidi unafumua bati au kigae na kuruka nje na kukimbia kwa spidi ya kenge aliyejeruhiwa kusalimisha maisha yako au kuitia msaada au kuhamishia vita nje kweupe kwenye uwanja mnapoweza kuonana vizuri.
Sasa kama kazi ya kumalizia dari ukimpa fundi wa maeneo jirani aweza mwaga siri kwa majambazi wakajua eneo lako la kujidai kivita liko wapi.Ina maana unampa fundi wa mbali si kwa sababu mafundi hawapo bali una vitu hutaki vijulikane hovyo kwa usalama wako.
Sipingi wazawa kuchapisha lakini kuna vitu vingine kinachoangaliwa si uwezo tu wa kufanya kazi lakini pia usiri,usalama n.k Kama waweza na wana historia ya usiri na usalama wapewe si kuchapa vitambulisho tu bali hata pasipoti na kazi za kuchapa pesa wawape tu.
Vituo vya Police pamoja na uongozi wa kata/tarafa/WILAYA wangehusika kuhakikisha uraia wa mtu.
Kama lazima kutumia makampuni, basi ya nje yasihusishwe. Anyway ni sisi nchi wachovu tunaopenda kuchapisha pesa, passports, etc, nchi zingine. Nchi imara km China, Korea, US, Japan, etc, hawafanyi hivyo