Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Tatizo la mawaziri wa kikwete wamewekwa kishikaji hivyo wakichemsha hakuna wa kuwachukulia hatua.wote ni watoto wa mjini.fikiria mkulo alivyotemwa nssf kwa kashfa leo ndo waziri wa fedha,mataka na kashfa ya ppf sasa ndo mkurugenzi mkuu atc na wengine.hebu watanzania tumuulize kikwete hawa watu anawatoa wapi?

Anawatoa CCM.
 
Habari zinazotiririka sasa hivi ni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha amekanusha madai kukutana na watu wa SAGEM jinsi ilivyoripotiwa na gazeti moja nchini wiki iliyopita. Hata hivyo Bw. Masha amekiri kuwa katika tarehe iliyotajwa ni kweli alikuwa Uswisi. Habari zaidi zaja.
 
Last edited:
Eeh Mzee,

sasa ina maana magazeti ya Mengi yaliandika habari za uzushi?makanjanja bwana...watu hawana ushahidi..

tusubiri kuona watu wakilipa Fidia.Madhara ya siasa za Kuchafuana
 
Mkuu Gembe, nadhani it is too late kuanza kujudge kwani lilichofanya gazeti ni kutoa tuhuma (kwa maneno) na alichofanya masha ni kujibu tuhuma (kwa maneno vilevile). katika mazingira kama hayo, ndipo tuwatake kila mmoja athibitishe, tukianza na gazeti. Waje na ushahidi unaoonmyesha kuwa kikao hicho kilikuwepo. Wakifanya hivyo Masha atawajibika na yeye kutoa ushahidi kuonyesha kuwa kikao hicho hakikuwepo. iwapo gazeti litashindwa kuthibitisha, basi Masha atakuwa ameshinda, tena kwa kock out
 
Wengi wana tabia ya kukanusha lakini baadaye mambo huwabadilikia na kuamua ku mute.
 
ni rahisi zaidi sana kukana kuliko kuthibitisha! Ni watu wachache sana ambao wanaweza kukubali kufanya kosa wanapotuhumiwa mara ya kwanza. Mmojawapo wa mifano ya namna hiyo ni ule wa Rais wa zamani wa Marekani aliyeiangalia Kamera na kuzungumza na wananchi wapi na kudai kuwa "I did not have sexual relationship with that woman, Ms. Lewinski".

Baada ya kusikia kuna "bluu dressi" alibakia kubishana juu ya maana ya neno "is" ni nini.

Kwa hiyo tusipoangalia tusije kujikuta tunauliza "kukutana" maana yake nini? Je kula chakula cha jioni ni sawa na "kukutana"? Je kupishana kwenye hoteli moja na kusalimiana kijuujuu tunaweza kusema ni "kukutana".. at the end.. maneno ni fani ya watu wachache na Masha sidhani kama anaimudu.
 
Eeh Mzee,

sasa ina maana magazeti ya Mengi yaliandika habari za uzushi?makanjanja bwana...watu hawana ushahidi..

tusubiri kuona watu wakilipa Fidia.Madhara ya siasa za Kuchafuana

yale yale! ngowi atolewe huku fisadi mwingine unamtetea -Askari wa kukodi wewe!
 
yale yale! ngowi atolewe huku fisadi mwingine unamtetea -Askari wa kukodi wewe!

Shalom,

wee kazi yako ni kusoma nachoandika na kutoa Comment kuhusu mimi badala ya kuangalia Hoja yenyewe?achana na tabia ya kipaka !

Mpaka sas asijaona kosa la Masha na nitaendelea kumeteta mpaka atakapopatikana na Hatia.Ya ngowi yanafahamika wazi na hayafichiki kwa kuwa yameandikwa kila pahala

Next time don't attack me personally.
 
Habari zinazotiririka sasa hivi ni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha amekanusha madai kukutana na watu wa SAGEM jinsi ilivyoripotiwa na gazeti moja nchini wiki iliyopita. Hata hivyo Bw. Masha amekiri kuwa katika tarehe iliyotajwa ni kweli alikuwa Uswisi. Habari zaidi zaja.

Haya mkuu, tunazisubiri hizo habari,
asiishie kukanusha bila uthibitisho. Nakumbuka nipashe walitaja hoteli na chumba alichokutana nao, sasa atueleze kinagaubaga ukweli wa mambo maana isije ikawa ile bifu ya waziri kijana ndo inamtafuna!!!!Na kama ikithibitika kwamba hakukutana na SAGEM na kama hana mawasiliano yoyote ya siri ili kuunufaisha upande mmoja basi achukue tahadhari siku nyingine asijaribu kumtunishia misuli mfanyabiashara mwanasiasa!!!
 
Kwa kuwa Masha ni ADVOCATE, sishangai ninapoambiwa anajihusisha na madili machafu haya. Ndio zao ma-Advocate wa nchi hii. Mtaje yeyote utaambiwa madudu kibao kwenye fani yao hiyo. Wamewafanya MAHAKIMU na MAJAJI wa nchi hii wawe wala rushwa wakubwa nchi hii.
 
Shalom,

wee kazi yako ni kusoma nachoandika na kutoa Comment kuhusu mimi badala ya kuangalia Hoja yenyewe?achana na tabia ya kipaka !

Mpaka sas asijaona kosa la Masha na nitaendelea kumeteta mpaka atakapopatikana na Hatia.Ya ngowi yanafahamika wazi na hayafichiki kwa kuwa yameandikwa kila pahala

Next time don't attack me personally.

Umh! Mbona Gembe na Shalom mnaanza ngumi kabla ya hata filimbi kupigwa? Nafikiri hapa ni kuchambua hoja na sio kucharurana. Gembe hujakatazwa kumtetea Masha mpaka mwisho, hata akipelekwa mahakamani wewe nenda kamtetee tu, ni hiari yako! Ila inaelekea unawenza kumtwanga ngumi hakimu asipokubaliana na wewe. Tupunguze munkari kidodgo.
 
Sasa wanaanza kuwa wawazi katika mchakato baada ya kelele.

Sita zapita zabuni ya vitambulisho
Geofrey Nyang'oro

HATIMAYE Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza kampuni sita zilizopita kwenye mchujo wa zabuni iliyogubikwa na utata ya kutengeneza vitambulisho vya taifa, ambavyo vitawekwa teknolojia ya kisasa, huku kampuni mbili kati ya hizo sita zikitokea nchini India.

Zabuni hiyo ilikumbwa na utata mkubwa kwa karibu mwezi mmoja uliopita baada ya mbunge wa Karatu, Dk. Wilibrod Slaa kudai kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha aliingilia mchakato huo kwa kuandika barua ya malalamiko kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipinga kuondolewa kwa baadhi ya wazabuni.

Hata hivyo, suala hilo lilizimwa na Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ambayo baada ya kusikiliza hoja za Dk. Slaa, iliamua kutomruhusu Masha kujitetea kwa madai kuwa mchakato ulikuwa bado unaendelea na sheria ya Manunuzi ya Umma hairuhusu jambo kujadiliwa wakati zabuni ikiwa kwenye mchakato.

Hata spika wa Bunge, Samuel Sitta alizuia suala hilo kujadiliwa hadi hapo mchakato utakapokamilika.

Kampuni za India zilizopita kwenye mchakato huo ni TATA Consultancy Services inayoshirikiana na Ontrack Innovations LTD, na Madras Security Printers.

Kampuni nyingine zilizopita katika mchujo huo wa tenda iliyotengewa kiasi cha Sh222 bilioni, zinatoka Afrika Kusini, Dubai, Malaysia na Japan.

kampuni hizo ni Unisys ya Afrika ya Kusini, Giesecke $ Devrient Fze (Dubai), Iris Corporation Berhad (Malyasia) na Maruben Corporation inayoshirikiana na Zetez na NEC ya Japan.

Kampuni hizo zimefanikiwa kuingia awamu ya pili baada ya kupita katika mchujo wa kwanza uliozihusisha kampuni 54 kutoka mataifa mbalimbali duniani zilizotuma maombi ya kufanya kazi hiyo, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyosainiwa na msemaji wake, Issa Natanga.

"Baada ya kukamilika kwa mchujo huu, mchujo wa pili utaanza mara moja na kukamilika haraka iwezekanavyo," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Masha anadaiwa kuipigia debe kampuni moja ya Uswisi ya Segam Security, ambayo ilikuwa moja ya kampuni zilizolalamika baada ya kuenguliwa kwenye hatua za awali za zabuni hiyo, zikidai kuwa hazikutendewa haki.

Imeripotiwa kuwa katika mchujo wa kwanza, kampuni 33 zilienguliwa na baadaye 13 zikatemwa na kubakia kampuni nane.

Masha pia ameripotiwa kuwa alikerwa na kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kumuagiza katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kuwasilisha kwenye kikao cha baraza la mawaziri ripoti ya utekelezaji wa tenda hiyo, akidai kuwa hakuhusishwa kwenye mchakato huo.
Source: Mwananchi Read News
 
Masha hana hatia kama wengi wanavyofikiri,leo asubuhi kwenye kipindi cha jambo Tanzania kinachorushwa na TBC1,Masha ameeleza ukweli wa mambo,kwanza ameonyesha passport yake ambayo inaonyesha tarehe 1 oct alikuwa anawasili nchini kutoka dubai,hivyo si kweli kwamba tarehe 1oct alikuwa Geneva kama ambavyo magazeti yaliandika.Mara nyingi magazeti yamekuwa yakipotosha umma wa watanzania kwa kuandika uongo na kuendeleza chuki zao binafsi dhidi ya baadhi wa viongozi au watu maarufu.na la msingi hapa tujiulize kwa nii ni magazeti ya makampuni ya IPP tu????????kama wameweza kuandika uongo kuwa alikuwa Geneva tar 1oct,that means the whole issue ni UZUSHI mtupu!!!!tena walivyo wanafiki wanadai wa ushahidi,upi tena kama passport ya Masha inaonyesha that day alikuwa anawasili kutoka dubai,na tarehe aliyokwenda Geneva still magazeti yamandika uongo,na amekanusha hata htl aliyofikia na hao watu wa SAGEM hakuonana nao kwasababu sicho kilichompeleka huko,alikwenda kwenye mkutano wa UNHCR!!!SIKU ZOTE KWENYE UKWELI UONGO HUJITENGA!
 
Kwa kuwa Masha ni ADVOCATE, sishangai ninapoambiwa anajihusisha na madili machafu haya. Ndio zao ma-Advocate wa nchi hii. Mtaje yeyote utaambiwa madudu kibao kwenye fani yao hiyo. Wamewafanya MAHAKIMU na MAJAJI wa nchi hii wawe wala rushwa wakubwa nchi hii.

Mkuu Wildcard, sijapenda jinsi ulivyowarundika advocates kwenye chungu kimoja na kuwahukumu kwa pampja namna hii. Siamini kuwa wote wanaweza kuwa ghivyo, lazima watakuwepo angalau wachache wenye tabia tofaut na hizo
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitatumia Operesheni Sangara kuwashtaki kwa wananchi, waliohusika na utoaji wa zabuni ya vitambulisho vya utaifa na kwamba pia kitabainisha ufisadi uliotendeka.

Chama hicho pia kimemshutumu Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kucheza na maisha ya Watanzania kwa kuzuia kujadiliwa bungeni kwa hoja kuhusu vitambulisho, ambayo imekuwa ikimkabili Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha.

Mkurugenzi wa Bunge wa Chadema, John Mrema, aliwaambia wananchi kuwa kunzia leo, chama hicho kitawashitaki kwa wananchi wait wote waliohusika na upotevu wa fedha kupitia utoaji wa zabuni ya vitambulisho vya utaifa.

"Tunaipeleka hoja hii katika mahakama ya wananchi kama tulivyoipeleka hoja ya kashfa ya upotevu wa mabilioni katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania," alisema Mrema.

"Kesho (leo) tupo Kawe na tutawaeleza wananchi ufisadi wote ulIofanyika na ikibidi tutaweka hadharani nyaraka zote kwa sababu tumefanya utafiti na kujiridhisha kuwa Waziri Masha, alikiuka sheria za manunuzi.

"Tunamtaka Rais Jakaya Kikwete, amfukuze kazi waziri huyo kwa kuwa yeye mwenyewe ameshindwa kuwa muungwana kwa kuamua kutojiwajibisha."

Waziri Masha alikuwa anatuhumiwa kuingilia kati mchakato wa zabuni na alimwandikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kumlalamikia kwa kile alichokielezea kuwa ni, kutotendewa haki kwa baadhi ya wazabuni.

Habari zilisema waziri huyo alifanya hivyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa makampuni yaliyoenguliwa katika mchujo wa awali, ikiwemo kampuni ya Sagem Securite ya Uswisi.

Hata hivyo, Mrema alisema wana habari kuwa hadi leo kampuni hiyo haijawasilisha malalamiko dhidi ya kuenguliwa kwake.

Mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo alisisitiza kuhusu umuhimu wa kujiuzulu kwa waziri huyo.

"Tangu mwaka 2004 kamati ya zabuni imekuwa ikikaa vikao mbalimbali kujadili suala hilo, unadhani ni kiasi gani cha fedha kimetumikka tangu mwaka huo. Vikao vile haviendeshwi bure," alisema Tumbo.

Alisema uamuzi wa spika kusitisha mjadala kuhusu hoja ya vitambulisho,si sahihi kwa kuwa unapingana na maslahi ya umma.

"Spika alitumia mgongo wa kamati ya Masilingi kuzima mjadala wa hoja ya vitambulisho bungeni, wakati sisi kutokana na taarifa tulizonazo, kamati haijawahi kumshauri spika kitu hicho. Spika anacheza na maisha ya Watanzania," alisema Tumbo.

Tayari kampuni sita zimetangazwa kupita kwenye mchujo huo na sasa zinasubiri mchujo wa mwisho ili zishinde tenda hiyo yenye thamani ya Sh 222 bilioni
 
What about Mpiga Chapa wa Serikali?😕😕😕


A statement released yesterday by the Ministry of Home Affairs said that the six companies were short-listed from 54 companies.

The six companies were identified as Unisys (South Africa), Giesecke & Devrient FZE (Dubai), Iris Corporation Berhad (Malaysia), Madra Security Printers (India), Marubeni Corporation in collaboration with Zetes and NEC (Japan) and Tata Consultancy Services in collaboration with Ontrack Innovations Ltd (India). The statement further explained that the second screening will begin soon, and that it is expected to be finalized soon.


FONT]


Giesecke & Devrient FZE (Dubai)?

uwiiii nasikia kizunguzungu sielewi niko wapi Tanzania au Dubai. Moderator nisaidie nisianguke na kizunguzungu.Sielewi hata ninachoongea na sielewi wanachoongea hao walioyachagua makampuni.Nina wazimu nini.Hamna daktari humu jamii forum walau anipe panadol nitulize maumivu?
 
Vigogo wahaha kumwokoa Masha

[source mwanahalisi.co.tz]

Na Saed Kubenea

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, ambaye katika misingi ya utawala bora angekuwa ameshajiuzulu au amefukuzwa kazi, sasa ameanza kukingiwa kifua, MwanaHALISI limeelezwa.

Masha anakabiliwa na tuhuma nzito za kuingilia mchakato wa kutafuta mzabuni wa kutengeneza vitambulisho vya taifa katika mradi utakaogharimu zaidi ya Sh. 200 bilioni ulioko chini ya wizara yake.

Waziri anadaiwa kubeba malalamiko ya kampuni ya nje iitwayo Sagem Securite na kuyatumia kujenga hoja ya kurejewa hatua za mchakato ili naye awemo.

Katika wiki moja tangu kufumuka kwa taarifa za waziri huyo kuingilia mchakato, Masha ameripotiwa kuwa katika wakati mgumu kwa kuwa suala lake ndilo limekuwa “gumzo la Dodoma.”

Hakuna taarifa zozote juu ya alichokisema Rais Jakaya Kikwete alipokutana na Baraza la Mawaziri mjini Dodoma, lakini taarifa zisizorasmi zinasema alidokeza juu ya “mwenendo wa baadhi ya viongozi na misingi ya maadili ya uongozi.”

Aidha, kuna taarifa kuwa waziri Masha amekwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kukutana naye. Haijafahamika ilikuwa matembezi ya kawaida, kikazi au safari mahsusi ya “kutafuta kinga” kutoka kwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Bila ya kutaja majina, mbunge wa kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru, alikiambia kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kuwa “waweke mbele maslahi ya chama.”

Ngombale-Mwiru amenukuliwa akisema kuna wanaosema “maslahi ya taifa kwanza.” Alisema sharti waweke maslahi ya chama mbele na kwanza.

Hoja yake ilionekana kama majibu ya hoja nyingine kuwa kashfa inayomkabili Masha, inaweza kuwa mtaji mkubwa kwa vyama vya upinzani; na kwamba wabunge wa CCM wasiposimama pamoja, basi chama kitabomoka.

Wachunguzi wa siasa za CCM wanasema kauli ya Ngombale-Mwiru ni sehemu ya vitisho kwa wabunge na hata karipio kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa kitabu alichozindua (ambamo kuna sura aliyoandika) kiitwacho Bunge lenye meno ambacho kinasisitiza utaifa kwanza.

Hadi tunakwenda mitamboni, Kamati ya bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambayo ilipewa jukumu la kushughulikia hoja ya Masha kuingilia Bodi ya Zabuni ilikuwa haijatoa taarifa zozote kwa spika.

Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi ilitakiwa kusikiliza hoja binafsi ya mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa juu ya tuhuma dhidi ya Masha na hatimaye kuwasilisha matokeo kwa spika.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kamati zinasema wajumbe wake wamegawanyika kuwili. Upande mmoja unataka suala hilo lipelekwe bungeni na wengine wanataka liishie kwenye kamati.

Kinachofanya baadhi waogope hoja hiyo kwenda bungeni ni hofu ya kuundwa kwa Kamati Maalum ya kuchunguza tuhuma na hatimaye kuja na hitimisho kama lililomkumba aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa.

Naye baba yake Masha ambaye ni mbunge wa Baraza la kutunga Sheria la Afrika Mashariki, Dk. Fortunatus Masha, ameripotiwa kuwapo mjini Dodoma akikutana na baadhi ya wabunge na viongozi mbalimbali.

Taarifa zimeenea mjini Dodoma kuwa Dk. Masha amekuwa akiwaomba wabunge na viongozi wengine kumnusuru mwanae.

Waziri Masha anataka kukwepa, pamoja na mambo mengine, tuhuma za:

  • Kujipatia taarifa za maandishi juu ya mchakato wa zabuni wakati yeye siyo mjumbe wa Bodi ya Zabuni.
  • Kulalamikia hatua za Bodi ya Zabuni wakati yeye hayumo katika mlolongo wa wahusika.
  • Kutumika kama mlalamikaji wa mmoja wa wazabuni kutoka nchi ya nje kiasi cha kufikisha kilio kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  • Kushinikiza Katibu Mkuu wa wizara yake kutafuta ushauri wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi serikalini (PPRA) wakati suala hilo halihitaji kufikishwa huko katika hatua ya sasa.
  • Kutawanya taarifa za Bodi, ambazo haziko mikononi mwake kihalali, kwa waziri mkuu, katibu mkuu wa wizara yake, katibu mkuu kiongozi na PPRA.
  • Kujadili mambo yaliyomo katika Bodi ya Zabuni ambayo bado hayajatangazwa na hivyo kuingilia uhuru wa Bodi.
  • Kushindwa kufuata sheria ya ununuzi kwa kupokea taarifa za malalamiko, kama anavyodai katika barua kwa waziri mkuu, na kukaa na taarifa hizo bila kuziwasilisha kwa Bodi ya Zabuni.
  • Kushindwa kufuata misingi ya utawala bora ya kutofanya au hata kuonyesha upendeleo.

Taarifa zilizopatikana Jumapili jijini Dar es Salaam zinaendelea kumshindilia Masha kwenye tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Inadaiwa kuwa Oktoba mwaka jana, alikwenda Geneva, Uswisi kuhudhuria mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi ambako baada ya mkutano, alipata wasaa wa kukutana na wenye kampuni ya Sagem Securite.

Imefahamika kuwa Masha aliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya kampuni ya Swissair. Mjini Geneva alikutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Jean Lin Fournereaux hapo 5 Oktoba 2008 kwa muda wa saa mbili kuanzia saa 12 jioni.

Taarifa zimeeleza kuwa Masha alifikia chumba Na. 0306 katika hoteli ya Mandarin Oriental na kutembelea ofisi za Sagem siku iliyofuata, katika eneo la Max Schmidheiny, Mtaa 202 CH 9435 Heerbrugg, mjini Geneva.


Naye Dk. Slaa, mwenye hoja binafsi juu ya waziri Masha kuingilia mchakato wa zabuni, aliiambia MwanaHALISI juzi Jumatatu kuwa kwa kuwasilisha hoja hiyo kwa spika, ametimiza wajibu wake na kwamba anasubiri jibu.

Kanuni za Bunge Na. 47 na 48 zinasema spika akiridhika, hoja binafsi yaweza kuwasilishwa bungeni. “Mpaka sasa hajanijibu,” amesema Dk. Slaa.

Mfumuko wa pilikapilika za kumtetea Masha ulianza pale Dk. Slaa alipoweka wazi kwamba ataomba maelezo bungeni kuhusu waziri kuingilia mchakato wa zabuni ya vitambulisho.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila aliiambia MwanaHALISI juzi kuwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilitarajiwa kuendelea na kikao chake jana na kupeleka ripoti yake kwa spika.

Alikataa kusema hatua gani imefikiwa hadi juzi na kuongeza kuwa shughuli za kamati hiyo ni za siri. Mkutano wa 14 wa Bunge unamalizika leo.

Wakati tuhuma dhidi ya Masha kuhusu kuingilia mchakato wa zabuni zingali mbichi, kampuni binafsi nchini imetishia “kumlazimisha kufuata sheria.”

Kampuni ya Power Roads (T) Limited inamtuhumu Waziri Masha kufuta amri ya Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji ya kumwondolea uhalali wa kuishi nchini Mwingereza aitwaye Douglas Hume Claxton.

Mkurugenzi wa Uhamiaji alifuta kibali cha Claxton, Daraja A Na. 018076 cha 30 Oktoba 2007, kwa barua Kumb. Na. 272673/31 ya tarehe 15 Septemba 2008, ambayo MwanaHALISI imeona.

Mkurugenzi amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa Claxton alipata kibali cha kuishi nchini kwa kutumia hati batili na iligundulika kuwa baada ya kupatiwa kibali, alikuwa akifanya kazi zisizolingana na kibali chake.

Lakini katika hali inayotia shaka, Waziri Masha alifuta amri hiyo ya Mkurugenzi wa Uhamiaji na badala yake akaruhusu Mwingereza huyo abaki nchini hadi sasa.

Katika barua yake Kumb. Na. DN 272673/32 ya tarehe 15 Oktoba 2008, Mkurugenzi wa Uhamiaji anamweleza Claxton juu ya uamuzi wa waziri.

Anasema, “…waziri ameelekeza kwamba uendelee kuishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia hati hiyohiyo na kwamba mahakama ndizo zilizomo katika nafasi nzuri ya kushughulikia matatizo na migogoro inayokabili Power Roads (T) Limited.”

Barua ya mkurugenzi imesainiwa na M.P. J. Ulungi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uhamiaji.

Hoja ya Power Roads kwa waziri, kupitia barua Kumb. Na. proads/08/16 ya 21 Oktoba 2008, ya kupinga hatua yake na kusema watahakikisha wanamlazimisha kufuata sheria, haikujibiwa hadi jana.

Baada ya kuona hawapati majibu, kampuni imemwandikia Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani na kumwomba afikishe nakala ya barua yao ya awali kwa waziri.

Katika barua hiyo, Kumb. Na. roads/09/01 ya 22 Januari 2009, kampuni inamwomba Katibu Mkuu kuwasilisha nakala ya barua yao kwa waziri kwa kuwa yeye, katibu mkuu, “ni mtekelezaji wa utawala bora, mu-wazi na muwajibikaji.”

Barua hiyo imesainiwa na Abba P. Mwakitwange, mkurugenzi na mwenye hisa 51 katika kampuni hiyo.
 
Mkuu Wildcard, sijapenda jinsi ulivyowarundika advocates kwenye chungu kimoja na kuwahukumu kwa pampja namna hii. Siamini kuwa wote wanaweza kuwa ghivyo, lazima watakuwepo angalau wachache wenye tabia tofaut na hizo

MN,
Sina nia kuwaweka ma-Advocate wote kwenye chungu kimoja ingawa karibu wote kwa sababu ya kushindana kuwa matajiri wameivuruga mno fani hii nyeti ya utoaji haki kwa wananchi. Chunguza kidogo maisha yao na mali wanazojilimbikizia kwa muda mfupi tu mara wanapoingia kwenye fani hii. Angalia fani hii inavyotaka kumchafua hata Jaji Waryoba ambaye aliishi maisha ya kiadilifu mno kabla kujiingiza huko. Tuiache hii kwa sasa kwani sio mada yenyewe.
 
Back
Top Bottom