Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Mwanakijiji mtafute Gerald Hando wa Clouds umpatie maswali
+255713266388

All the best
 
Ana lipi jipya?

Jana tumemsikia na amezungumza yote aliyokuwa nayo sasa hii kampeni ya vyombo vya habari itabadilisha nini?

Angalia asije akachemsha tena!
 
Nziku,
..
Time will tell!

Time i-tell mara ngapi kaka? Mwenye macho haambiwi Tazama.

Yaani watu kwa kuzoea vya kunyonga, kubanikiwa, kutafuniwa halafu mwisho kuanza kuuliza kama inatakiwa kumeza au kutema!
 
Ukimkosa Gerald nishtue nikurushie ya PJ - Paul James

Ila nimemcheki anapatikana sasa hivi.
 
Capo di tutti Capi Kuhani,

Anayetakiwa kusaini mkataba ni Katibu Mkuu na si waziri! Yeye ndiye accounting officer. Kujiingiza mawaziri kwenye hili matokeo yake ndiyo hayo tuliyoyaona Buzwagi!

Mimi sipingi waziri kuonyesha concern. Ninachopinga ni kuingilia utaratibu uliowekwa. Kwa kufanya hivi tunakosa wa kumlaumu mambo yakienda kombo. Waziri anasema yeye alifanya kwa nia njema tu na si mtaalamu. Wataalamu wanasema walishindwa kumpinga waziri kutokana na kumheshimu. Mwisho ya yote ndiyo hayo tunayoyaona kila siku; barabara zinajengwa anakotoka waziri wa infrastructure, vyuo vya elimu vinajengwa alikotoka waziri wa elimu n.k. Mbaya zaidi, kutokana na kuamini nia njema ya hawa wanasiasa, watendaji wanakubali business card kama ishara ya power of attorney! Wote hawa, bila shaka, walifanya hivyo kwa nia njema na uzalendo kwa nchi yao!

Amandla.........
 
hoja ya masha kujiuzulu haiepukiki....maana hata huko kunyofolewa kwa taarifa nyeti na kuvuja kwa taratibu za tenda kwenye jambo nyeti kama hili ni sababu tosha ya kujiuzulu leave alone his connections with Sagem
 
Hivi huyu bwana Masha anavuruga kweli au Media ndo zinamfanya za kufanya?

Kuna kamkono ka mtu hapo, nina muhisi Mengi.
 
Poa poa mwanakijiji. Tupo pamoja kuhakikisha hili litaifa la wadanganyika linaelekea mwelekeo sahihi.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mimi kila siku najiuliza, huyu Masha ana wazimu au ndio ujana wenyewe...
Yaani jitihada zake za kujisafisha ndio anazidi kuharibu...kwa sababu wananchi wanazidisha maswali akilini..
Kwa mfano mara zote anapojitetea husema kuna mashirika mengine manne.. Yataje basi hataki!..
Nina hakika akiyataja yote (kama yapo) na watu wakafuatilia itagundulika hakuna kitu kama hicho pia akiombwa ushahidi hana!..
 
Nadhani mwanakijiji alikuwa anatoa maswali.

Ila Gerald ni mzuri na ana uwezo wa kujipanga na kuuliza maswali ya maana. Ila uwezi jua labda Masha amenunua air time hapo clouds ajisafishe.

Masha ni kijana na Joseph Kusaga ni kijana wanaelewana kaka.

Tusibiri kesho tusihukumu kabla lakini.
 
Nadhani kama Waziri hata backdown.. tomorrow could be a very historic day. Kama itakuwa inavyofikiriwa, I would be able to stream the PB show baada ya saa sita za usiku huku...
 
Masha anatapatapa tu, Lazima atang'oka tu, unafanya mchezo na Dr Slaa nini?

Atakaye mng'oa ni Mangi, sio Dr. Huyu ni kipenzi cha Mkulu, na Mkulu mwenyewe kavaa miwani ya zege na kutia pamba masikioni, haoni, hasikii na kelele zikizidi zitapenya kwenye pamba na kusikika kama kelele za mlango, hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi.
Atakaye mkosesha usingizi ni magazeti ya Mangi yakiona kilio hakisikiki, yatamchafua mpaka baba ili amwadabishe mwanae kipenzi.
 
narudia kauli yangu....hoja ya masha kujiuzulu haiepukiki....maana hata huko kunyofolewa kwa taarifa nyeti na kuvuja kwa taratibu za tenda kwenye jambo nyeti kama hili ni sababu tosha ya kujiuzulu leave alone his connections with Sagem
 
Mzee Mwanakijiji,
Mimi kila siku najiuliza, huyu Masha ana wazimu au ndio ujana wenyewe...
Yaani jitihada zake za kujisafisha ndio anazidi kuharibu...kwa sababu wananchi wanazidisha maswali akilini..
Kwa mfano mara zote anapojitetea husema kuna mashirika mengine manne.. Yataje basi hataki!..
Nina hakika akiyataja yote (kama yapo) na watu wakafuatilia itagundulika hakuna kitu kama hicho pia akiombwa ushahidi hana!..

Mkuu Mkandara, huyu jamaa inaelekea anataka kuendelea kudanganya umma na ku-change the goal post. Kauli zake zinaanza kuingiza mambo mapya ambayo anadhani zitawafanya wasikilizaji/wafuatiliaji/wasomaji wa habari hizi kupoteza lengo.

Kuhusiana na kampuni 4 zilizolalamika: Hakuna mahali zaidi ya wakati huu ndipo hili linajitokeza. Kampuni inayojulikana na ambayo ameipigia kelele ni moja tu nayo ni Sagem Securite. Hizi nyingine hazipo kwenye lawama zake za utekelezaji wa kumtafuta contractor wa national ID. Labda kama anataka kuziingiza kwenye hiyo barua sasa.

Vile vile, hoja ya lini alikwenda uSwis, haina maana. Haina maana kwa kuwa hakuna anaejali alikwenda lini huko uSwiss. Anaweza alikwenda tarehe yoyote na bado hoja ikawa na nguvu ile ile. Nadhani katika hili, anaamini kuwa jamii itaona lawama zote zinazopelekwa kwake ni uzushi mtupu (just because the date is wrong).
 
Back
Top Bottom