Simulizi ya Kijasusi: Giza la Wasaliti

Dec 27, 2018
57
104
SURA YA KWANZA

ASUBUHI YA HEKA HEKA

Utangulizi.
Richard Dawson, mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisikanda maalum ya Dar es salaam, miaka mitano tu tangu ajiungena jeshi hilo, lenye jukumu la kulinda raia na mali zao lakiniilitosha jina lake kusemwa katika korido za makao makuu yajeshi hilo na hata ripoti za majaladya kesi mbali mali alizopewakuzisimamia hazikuacha maswali pale ziliposomwa na wakubwa zake kicheo waliomtuma kuyafanyia kazi. naam unaweza kumuita majina kama mfanyakazi mwenye weledi wa hali ya juu katika kazi yake hiyo ya kipolisi.

Kwa kufanikisha kufichua uhalifu pamoja na kuwakamata wahalifu wakubwa na wadogo kitu kilichofanya sifa zake kuenea kote ndani ya jeshi hilo pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ndani ya Tanzania.
vaa viatu, fuatana nami.
kama ilivyo kawaida kwa wakazi wengi wa mji huo wa raha na karaha yaani Dar es salaam, asubuhi ya kila siku huanza kwapilika na heka heka nyingi sana ili mradi familia na waowenyewe wawez kupata chochote kitu.
grrrrhh grrrrhh……mlio wamtetemo wa simu juu ya meza unamstua bwana Richard aliekuwa ametopea katika usingizi mzito sana alioupata mara baada ya kumaliza heka heka na kuanza likizo

yake.”msyuuuu”nisauti ya kusonya na kuonekana msonyaji alikereka na huenda hakutarajia kupata bugudha akiwa kati raha yausingizi ule uliokuwa umemlevya kiasi cha kutosha, akaurefusha mkono wake kuichukua simu yake kwnye kimeza kidogo kilicho karibu na kitanda na hapo akapigwa na butwaa baada ya kuitazamanamba ile namba ya simu iliyokuwa imekatisha usingizi wake haikuwa nyingine bali ilikuwa ya kamishina msaidiziwa jeshi la polisi SACP Joseph cherehani ambae pia ni kamandawa polisi wa mkoa huo

ASP Richard: “jambo afande, niko timamu tayari kwamaelekezo.” aliongea kikakamavu afisa huyo wa jeshi la polisiakisubiri sauti ya bosi wake ipate kuunguruma lakini badalayake,upande wa pili ulipopiga simu ulikuwa kimya kupimautulivu kikafatia mkoromo wa kitu kama kikohozi cha kulainisha koo na ndipo kisha likasika neno kwa sauti tulivu ilailiyojaa mamlaka na amri.
"NAKUHITAJI OFISINI KWANGU NDANI YA MASAA MAWILI TOKA SASA" nakilichofatia ni mlio wa Tiitiiih tiiitiiih kumaanisha mpigajiamekwisha kubonyeza kitufe chekundu yaani ameshaikata simuhiyo.

"Kumetokea kitu gani mpaka nihitajike kwa haraka kiasi hikikatika ofisi ya kamanda ndiyo kwanza nina siku ya kwanza tangu nimepewa barua ya likizo " alijiwazia ASP Richard alijiwazia mwisho aliingia katika chumba anachofanyiamazoezi, akatumia dakika thelathini katika kupasha viungo vyamwili joto, akaingia bafuni kwake na kuosha mwili wake kishaakajiandaa na kutoka katika nyumba anayokaa ambayo nimiongoni mwa nyumba alizozinunua kutoka shirika la nyumbala taifa (NHC).

Akawasha gari lake na kutokomea katika ofisi yakamanda.Wakati h , ayo yakiendelea kwa upande wa ASP Richard, upande mwingine asubuhi hii iliingia shubiri na vitiwalivyovikalia vilikuwa vya moto hapo katika chumba hikokulikuwa na kiyoyozi Ila wajumbe katika kikao hichowalionekana kufuta jasho jembamba kila dakika mbele Yao alikaa mwanamke wa makamo, naam hakuna mwingine Bali Mheshimiwa raisi Gloria Steven, mwanamke mwenye msimamomkali na aside na mzaha kwenye mambo ya msingiyanayolihusu taifa, leo hii aliitisha kikao cha dharula kilichowahusu wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, mbele take kulikuwa na mkuu wa jeshi la wananchi, inspekta jenerali wa polisi, Kamishnaa wa idara ya uhamiaji, kamishna wa magerezana mkurugenzi wa idara ya ujasusi, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na jibu la kueleweka katika ripoti zao, wote ni kama walikuwa wamekalia kuti kavu Ambalo muda wowote lingekatika na kuwadondosha kwa uzito na ugumu wa mambo yanayoendelea kila Jua linapochomoza.

"Nina Imani kwamba mnafahamu na mmeweza kusikia mambo yanayotokea kila siku kwenye taifa hili, wananchi wangu wanaishi kwa hofu hawana uhakika wa usalama wao pamoja namali zao, uhalifu umekithiri kundi Fulani limeshajitangaziajamhuri na nyie wenye dhamana ya kuilinda Amani hiyommekaa tu ofisini mnazunguka tu na Ma V8 huku wanaofanyamuishi Maisha mazuri ninyi na Familia zenu kupitia kodi zaowanaishi kwa hofu huko mitaani"

"hakuna hata mmoja went hapa mwenye ripoti inayochimbakiini cha mambo haya, mmesahau majukumu yenu ya msingi, naKuna engine niliwapamba kwa speech nzuri wakati nawaapishakiasi Sasa najuta ni here ngeweka maneno Yale kama akiba, mzee wangu IGP unaweza kunambia ni kwanini mpaka leobiashara ya dawa za kulevya inazidi kushamiri, hakuna vitendeakazi?

Idadi ya watendaji wako ni pungufu kuliko ugumu wakazi? umebakiwa na muda wa mwaka mmoja na nusu iliutundike hizo buti ni chaguo lako kumaliza utumishi wako kwafuraha na bashasha au kumaliza kwa aibu na fedheha."

kiti alichokalia IGP kilikuwa ni kama kinawaka moto kwakufokewa kule na bosi wake na kuna muda alijilaumu kufanyakazi ya upolisi huenda sasa hivi angekuwa nyumbani kwake au mashambani kwake alipojiwazia kwamba sio ishu ya madawa yakulevya pekeake bali kuna mauaji ya mawaziri watatu ndani yausiku mmoja alijikuta akivuta punzi nyingi kwa ndanina kuzitoataratibu, alizama katika tafakari zito mpaka aliposhtushwa nasauti ya mheshimiwa raisi.

"mzee wangu wa magereza, unaweza kuwa na lolote kuhusu kutoroka kwa yule mshtakiwa wa kesi ya ugaidi tena katika gereza mnalojinasibu nyie watu wa magereza kuwa ulinzi wake ni kama ikulu hii, aliwezaje lutoroka gerezani ukonga kama hakuna watendaji unaowaongoza kushirikiana nae, hiii haikuoneshi picha ya wasi kwa namna yoyote vijana wako wasivyo na weledi na hatujuikwa muda huu gaidi huyo atakuwa bado nchini au kashaondokandiyo maana nimewaita wote hapa ili mjue madudu yenu"

"nahitaji mkurugenzi wa idara ya ujasusi uniletee ripoti yaupotevu wa fedha zilizokuwa zinapelekwa katika benki kuu tawila mwanza, mwalimu wangu katika medani hizi za usalamaaliwahi kusema kuwa usalama wa taifa ni akili sio ukali, kaziyake ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganishakwa makini, taarifa nyeti za ndani nje ya nchi kulilinda taifa nawatu wake, lakini mzee wangu hujafanya lolote kati ya hayomajukumu, unanishawishi kwa kipi nkuache ukitafuna kodi zao.Mzee wangu sihitaji kukukumbusha majukumu natambua uzoefu ulionao idarani na oparesheni ulizosimamia ndizozilizonifanya kukuweka hapo nakuomba tafadhari Sana usinitukanishe huko duniani.

"nawapa siku 14 muarobaini wa hili jambo uwe umepatikana naatakayeona ugumu wa jambo hili niko tayari kupokea barua yakujiuzuru kwa mikono miwili." akasimama na kuondoka hukuwalinzi na mpambe wake wakimsindikiza tayari kwa kwendakwenye kikao kingine na baraza la mawaziri.

viongozi wale wa ulinzi na usalama wakaamua na kukubalianakwa pamoja kuwa kiundwe kikosi maalum kitakachohusishawatu wa kazi kwa kila vyombo hvyo vya ulinzi na usalamawatakaoenda na kasi ya siku walizopewa kupata ripoti nan matokeo chanya yatakayo nusuru vibarua vyao kwani walijuajinsi mheshimiwa raisi alivyo na maamuzi magumu na hapepesimacho pale kunapotokea madudu, waliagana wakipeana mudawa saa moja kwa ajili ya kupendekeza jina kwa kila idara yaulinzi na usalamaa

Saa 10:05 asubuhi
ndiyo muda uliomkuta ASP Richard akiwanyuma ya mlango wa kamanda wa jeshi hilo kanda malum ya Dar es salaam baada ya kuwa amepewa maelekezo ya kutoshana katibu muhtasi wa kamanda huyo kwamba akifika apitilizemoja kwa moja ofisini kwake. akakinyonga kitasa cha mlangoule na sekunde iliyofatia alijikuta kwenye ofisi panailiyopangwa kwa ustadi wa hali ya juu huku ikinakishiwa nahewa safi inayopatikana katikana katika kiyoyozi kilekalichotengenezwa na kampuni ya LG (life is good) ubaridiwake kiasi usioumiza mfumo wa upumuaji wa mtu au watu, kwa aliebahatika kuivuta hewa katika ofisi ake hakustaajabu hilomaana ni kawaida kwa ofisi kama ile kuwa na mpangilio sahihiwa vitu na mazingira yanayoizunguka.

Alishtushwa na sura alizozikuta ndani ya ofisi ile, Naam kulikuwa na wanaume watatu na wanawake wawili waliokuwakatika mavazi ya suti zao nadhifu, pamoja na hurufu nzuri yamanukato ambayo iliwatambulisha kwamba watu hawa niwazito kinyadhifa na pia kiuchumi, ukiondoa wnaume hao nawanawake wanaofunga idadi ya kuwa watano mbele yao alikaamwanaume mmoja alionekana tu kuwa ni mkakamavu naasubuhi hiyo uso wake haukupambwa na tashititi yoyote yatabasamu. kwa ukakamavu wa hali ya juu alitoa heshima kwakupiga saluti mbele ya wakuu hao.

Hakuna hata mmoja alieshughulika nae badala vichwa vyao namawazo yao yalikuwa juu ya majalada matano ya kesi mbalimbali zilizotikisa vituo vikubwa vya polisi katika jiji hilo, kamanda wa polisi aliamua ukimya uliokuwa ndani mle uendelikizo kwa kumuomba kijana yule aketi na kisha akafunguamazungumzo yale kwa sauti ya utulivu.

SACP Cherehani:" ASP Richard nimekuita hapa nkiwa naimani kabisa ulikula kiapo cha kulitumikia taifa katikamazingira yote ya utumishi wako, nayasema haya kwasababunatambua umeanza likizo yako, lakini kikubwa tu nimepigiwasimu na afande IGP, akinitaka nkupe ujumbe kwambaunahitajika kufika makao makuu haraka iwezekanavyo, nkutakieutekelezaji mwema wa maagizo utakayopewa, mimi sina lolotela kukujibu kwa maana sijui utakachoelezwa huko ila wasiwasiwangu huenda ni haya matukio yanayoendelea kutupasuakichwa na kutunyima usingizi kila jua linapoamka na kuzama." ASP Richard akapiga salute na kuondoka kuwahi hukoanapohitajika.

*******************************

MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI

Saa 11:35 asubuhi, huu ndiyo muda ambao mrakibu msaidizi wapolisi bwana Richard alikuwa mbele ya mapokezi na kuambiwaapite moja kwa moja hadi ofisini kwa IGP, akatoa heshima kwamkubwa wake huyo wa kazi na kukaribishwa tayari kwa ajili yamaagizo

"ASP Richard nimelipitia jalada lenye taarifa zako na taarifa yamwisho inaonesha uko likizo, asubuhi ya leo kulikua na kikaonyeti ili kujadiliana kuhusu hali ya ulinzi na usalama nchinikiukweli hali ni mbaya na kichwa changu kinapata moto, simuza viongozi wengi zinaita huku nyingi zikiwa ni za maswaliambayo hata mimi sina majibu nayasema haya kwa msisitizo iliupate kutambua uzito wa mambo haya, bila hivo taifa litakuwagizani katika sintofahamu hizi pia wengine kama sisi nafasi zetuziko rehani, mbali na uzalendo na mapenzi katika kazi hii lakinisitakuwa tayari kuwaona wahalifu wakijitangazia jamhuri yaona mimi nikirudishwa makao makuu nkasome magazeti nakurudi nyumbani nkacheze na wajukuu. nnakupa muda wamwezi mmoja nipate ripoti kamili pamoja na washalifuwaliohusika na matukio haya kama yalivyoainishwa kwenyemajalada haya kufikishwa mahakamani, utapewa ushirikiano wakutosha na wenzako hapa lakini ripoti ya mwisho utanileteamimi ili niifikishe kwa mheshimiwa raisi ,yangu ni hayo labdakama una swali ila jua swali lako litajibiwa hukoutakapoenda. napewa ujumbe kwamba usafiri wakukupeleka huko unakusubiri kwenye maegesho ya magarihapo chini, nkutakie majukumu mema na ukatuwakilishevyema.

akapiga saluti na kutoka ofisini kwa kigogo yule wa jeshi zimala polisi, akashuka kutoka ghorofa ya tano iliyopo ofisi ile nakutumia ngazi huku akitumia dakika 5 kuyafikia maegesho namara aliona gari imewesha taa na kuizima, akajongea mpakakwenye gari lile dereva akamfungulia mlango siti ya pembenikwa dereva nae bila ajizi alikaa huku akiwaza ni wapianapopelekwa

"tutatumia muda gani kufika huko" alimuuliza dereva huyoambaye hakufumbua kinywa kusema kitu chochote zaidi yakuwa bize na usukani, kuona hivyo alijiongeza kuwa derevahuyo hakutaka maongezi, alizama kwenye fikra kali na ndipokumbukumbu zikaja kichwani kwake kuwa kesho yake ni siku ya kuzaliwa kwa mtoto wake kelvin, mtoto aliyezaa namwanamke kisha kutengana kwa sababu ambazo zilikuwa nje yauwezo wake, kazi zilimfanya awe bize kiasi cha kupata mudakidogo sana wakukaa nayo, na hiyo ndiyo sababu iliyofanyaatengane na mwanamke baada ya kukosa huduma za kimwilikutoka kwa mwanaume huyo kiasi cha kujutia kwanini aliwahikumpenda mwanaume huyo, mbnli na kuwa bize sana katikakupambana na wahalifu lakini hakuwahi kuacha kuikumbuka nakuijali familia yake, hata baada ya kutengana na mke wake aliendelea kuwajali huku akijua ipo siku watarudi mikononimwake kama zamani

"tumeshafika shuka na utasubiri hapa kwa taratibu zingine, mimikazi yangu imeishia hapa" akafanya na muda sio mrefu akatokeajamaa mmoja mwenye upara na mkakamavu akiwa kwenye sutiyake nadhifu ya rangi nyeusi, "tuongozane chief anakusubiriASP Richard" hakutaka kujiuliza jamaa huyo kalijuaje jina lake ila aligundua huyo mtu aliekuja kumpokea atakuwa na taarifazake"

wakaingia katika jengo la nyumba hiyo ya gorofa moja iliyokaakama makazi ya mtu,lakini kiukweli ni miongoni mwa nyumbasalama(safe house) za idara ya usalama wa taifa,na ilizungukwana ulinzi mkali wa watu ambao hakusumbua akili yake kujiulizaikiwa anatambua haiba ya watu wale kama makomandoo wajeshi la wananchi na idara ya usalama wa taifa, akajua kuletwakwake hapo ni kwa ajili ya kukabidhiwa kazi nyeti sana au kuoneshwa kitu nyeti sana, mlangoo uligongwa mara mbili nakisha wa ukafunguliwa na kuingia.

"karibu sana ASP richard ni sauti iliyotoka kutoka kwa mtualiyekuwa amempa mgongo hakuwa mwingine bali mkurugenziwa idara ya ujasusi ya taifa, chifu Desmondi mkosamali, mtu wamiraba minne na mwenye macho makali wakati huo tabasamulake lilikuwa likizo kufutia kikao kilichofanyika asubuhi hiyokatika ikulu ya Tanzania.

kuweka umakini kwa mtu yule kulimsahaulisha kwamba mlendani kulikuwa na sura zingine sita, chifu aligeuka na hapo ASP Richard alitoa heshima kwa kumpigia salute mtu yule, "karibuuketi, hawa unaowaona ni watu ambao utashirikiana naokwenye hili ambalo muda si mrefu ntawenda kuwaeleza, akameza mate kisha akasema huyo bidada mrembo unaemuonahapo mwanzoni kwako kulia anaitwa luteni sabina chacha, komandoo wa jeshi la wananchi na mdunguaji, akasimama nakupiga saluti kikakamavu kabisa, huyo anaemfatia ni sajentimayunga samson kutoka kikosi cha kuzuia na kupambana nakulevya, nae akasima na kupiga saluti, huyo dogo hapo anaitwajames shayo kutoka idara ya ujasusi ni mtaalamu wa mitambo nateknolojia,kushoto kwako uliekaribu nae ni meja sadiki tumbaku, komandoo wa jeshi la wananchi, anaemfatia ni dianachiwawa kutoka idara ya ujasusi na huyo wa mwisho ni inspektajafari malingumu kutoka jeshi la polisi makao makuu na wewehapo ASP Richard Dawson kutoka jeshi la polisi, timu ya watusaba inayohitajika lufanya kazi kama mchwa wajengapokichuguu." hawakuelewa maana ya mstari wa mwisho wamaneno aliyosema chifu, wakastaajabu ndani ya nyumbakulikuwa kuna eneoambalo lipo chini ya ardhi baada ya chifukugusa ukuta kisha ukafunguka kisha akawasha taa na eneozima huko chini likawa na mwanga wa kutosha watu wotewalistaajabu walichokiona kompyuta za kisasa, silaha na dhanambali mbali ziliwafanya kupigia mstari na kengele ya taadhariikalia vichwani kwao kwamba' TAYARI KUMESHAKUCHA'

" tusikilizane wote mliopo hapa mpo kwa sababu ya kutafutauvumbuzi wa haya yanayoendelea nchini, kwa kifupi kunamatukio yametokea na ripoti za awali zinaonesha kunamuunganiko kati ya tukio moja na jingine na hili kufanya hatawakuu wenzangu kuhisi mhusika au wahusika kuwa ni hao haowanaotukosesha usingizi, tukianza na tukio la tarehe 20 mweziwa saba mwaka huu wiki tatu nyuma la kutekwa na kuuwawakwa mawaziri wawili wa wizara nyeti za serikali na gavana wabenki kuu linatajwa kuwa na ushabihiano wa tukio la kuvamiwamsafara uliokuwa ukisafirisha pesa kuzipeleka tawi la benki kuumwanza katikati ya mapori nje kidogo ya mji wa manyoni nakisha mauaji ya walinzi waliokuwawnazisafirisha haitofautianisana na wizi uliofanyika katika ghala la silaha katika kambi yajeshi huko mafinga masaa manne baadae ishara tosha kwambawatu hawa walijipanga"

mbali na hayo tukio jingine linalotuumiza kichwa ni hili la kutoroka kwa MUSTAPHA ABDI NUR AHMED gaidi sugualietafutwa kwa takribani miaka kumi na mashirika mbali mbaliya kijasusi duniani, mwaka jana tulimkamata na kumfungiakatika gereza la ukonga huku akisubiri hukumu yake ndipoalipotoroka wiki iliyoisha na kisha majuzi tulishuhudiakulipuliwa kwa bomu kiwanda cha sukari huko morogoro najana taarifa zimetufikia kuwa kiwanda ki nguine cha maziwahuko Tanga kimelipuliwa usiku wa jana, matukio yote hayayanatisha na kuwatia watu hofu"

"mna siku kumi na mbili za kunifikishia ripoti ya mambo hayayote mezani kwangu, na wahusika wa haya matukio nahitajikuwaona kwa sura zao, oparesheni hii ni ya kukamatainapoonekana kuna ugumu wa kufanya hvo muwafute katika usowa dunia hii, mna baraka zangu na vitambulisho vyenumtavipata mara baada ya kutoka humu kama kuna chochotemtanitaarifu ili nirahisishe kazi yenu, ripoti yote itanifikia mimiili niiwasilishe kwa mheshimiwa raisi, mwisho napendakuwataarifu kwamba meja Sadiki tumbaku ndiyo atakayekuwakiongozi wenu, niwatakie utendaji mwema na wenye weledi ilimtuletee matokeo chanya"

wakashusha pumzi huku wakikuna kichwa kwa majukumu hayowaliyopewa waliona kazi iliyopo ilivyo ngumu na uchache wa muda ili kuwapata wahusika vile vile. ********* itaendelea………….:unataka kujua kilichoendelea vuta kiti kaa tayari kwa kuona giza lenye kivuli. Tchao
NB: Simulizi hii iko katika mfumo wa PDF kwa mwenye uhitaji wa kuisoma yote ikiwa ni kuburudika na kuelemika sogelea kwenye PM yangu ukiwa na Tshs 5000/= nkuoe njia ya malipo ukaburudike nwapenda sana!!!
 
Kabla ya kuanza kusoma hii simulizi, naomba kujua ratiba, ni lini muendelezo utakuwa unashuka??? 🤒 😎
Simulizi hii itakuwa inaruka karibu kila siku kulingana na maoni ya wasomaji na pia kwa kudra za Mwenyezi Mungu ili kuondoa kile kilio sugu cha arosto
 
NB: hadithi hii haihusisiani na mambo yoyote yaliyotajwa katika katika nchi husika au vyeo na majina ila ina lengo la kuelimisha na kuiburudisha jamii, karibuni tuendelee
SEHEMU YA PILI
Tayari ilikuwa imeshatimia saa 7 na dakika zake mchana huo, vijana hao wa kikosi maalum kilichoundwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, walikuwa wameketi katika ukumbi ule ulio chini ya ardhi huku wakikubaliana kwambawajigawe na kufika maeneo ambayo matukio hayo yalifanyika.
" kama tulivyokubaliana kwamba tugawane majukumu ilikuendana na kasi, sasa ni hivi inabidin tuwe wawili ili tukusanye taarifa na saa 5 usiku ya leo hii pwote tuwe hapa kupeana mrejesho ili tujue tunaanza na kipi siku itakayofatia. tutakuwa makundi matatu ilat utakuwa tunawasiliana kwa lolote lile litakalojitokeza, sajenti mayunga utaongozana na ajenti Diana katika eneo lilipotokea mlipuko pamoja na kukusanya taarifa ni wapi ule mzigo wa kilo 120 za dawa za kulevya utakapoingilia ili tuwapate wahusika mapema kabla hawajauingiza kwenye masoko yao, ASP Richard na Inspekta Jafari mtafatilia kilichotokea gereza LA ukonga nakutafta Intel zitakazofanikisha kumpata gaidi huyo, Mimi na luteni Sabina tutafatilia uvamizi na wizi wa silaha lakini vile Kuna timu ya idara ya ujasusi ya jeshi(Military Intelligence) ikiongozwa na kapteni Joshua, na chifu kanitumia ujumbe Kuna timu imetangulia katika eneo zilipoibiwa hizo pesa, naweza kusema hayo ndo majukumuku ya msingi tunatakiwa kuyafanyakwa weledi na kwa uharaka ili tusimuangushe chifu na viongoziwetu, tukayaanze majukumu bwana James utakuwa unatuparipoti ili tuendane na siku tulizopewa tukutane hapa saa tano ilituone kama kutakuwa na chochote kitakachotupa Mwanga kwenye mambo haya."
wakati kila mmoja akienda walipokubaliana huku chifu akiwawezesha kwa vitendea kazi na usafiri watakaotumia wakati wote wa oparesheni hiyo, meja tumbaku na luteni wakawahiuwanja wa ndege kwa ajili ya kuwahi kwenye kambi ya jeshi kulipotokea na wizi wa silaha ili kujua mbivu na mbichi tiketizao zilikuwa zishaandaliwa kuwafikisha mkoa wa isongwe nakisha kuunganuisha moja moja mpaka ilipo kambi ya jeshi la wananchi palipotokea na wizi huo mawasiliano yaliunganishwakwa wote sita na kisha maelekezo mengine yalitoka kutoka chumba cha oparesheni alichomo bwana james kutoka idara yajasusi.
wakati hao wakijiandaa kuanza kai hiyo ngumu, upande mwingine watu watatu wenye umri wa makamo waliokuwa wamekaa ndani ya sebule moja huku wakigonga glasi zilizobeba kimiminika cha bei mbaya, wakifurahia kazi nzuri iliyofanyika.
"sikutarajia kama mipango tuliopanga kikao kilichoishaingeenda hivi kweli hakukosea kupewa jina kobe nadhani hatanyinyi ndugu zangu konokono na kinyonga hamkutarajia kulala maskini na kuamka tajiri, tufurahie maisha, alafu kobe amenifahamisha kuwa hata nyayo hazitoonekana maana vijana wale walishazifuta hata waje majasusi wa CIA watakuwa wanatwanga ,maji kwenye kinu na wataishia kuibwaga kazihiyo."
"hahahaha umeongea vizuri bwana kiroboto. mipango imeendasawia nategemea muda wowote mheshimiwa anaweza kunipandisha cheo na nikawa bosi kamili wa wizara ile na ndipo tutaweza kujiweka nafasi nzuri ya kuimarisha uchumi wa umojawetu na kisha kobe akikaa pale juu tutakuwa tunajichotea tu, wajinga ndiyo waliao"
"kama mlivotangulia kusema wenzangu kiroboto na kinyonga, mimi nafuraha sana kuliko labda nyie na ndipo mpango wetu wapili wa kuingiza ile shehena ya coca unaanza leo usiku huku wenyewe wakielekeza nguvu kutatua hayo matukio ambayo hawatafanikiwa sisi tunaendelea kupiga bingo, na nimeamini kweli wale vijana ni watu wa kazi hahahaha"
"tutamuua yule mama kwa presha, maana sio kwa matukio yale hahaha, mzigo ukishaingia jumamosi ntakuwa dubai kwamatembezi madogo madogo na yule mchepuko wangu, kazininshaweka invoice tayari, sisi ndo wenye nchi bwana au nakoseabwana konokono"
"hujakosea kabisa bwana kiroboto tunywe tufurahi maanayajayo ni makubwa kuliko haya....cheers" wote watatuwakagonga glasi kwa furaha sana vigogo wale waliojipa majinaya uficho huku wakijinandi kuendelea kuweka mizizi mikubwakatika taasisi nyeti za serikali
GEREZA LA UKONGA
Saa 8:20 mchana
Huo ndiyo muda ambao inspekta jafari na ASP Richard walikuwa wakikagua eneo ambalo lilihisiwa mahubusu yule kulitumia kutorokea amabapo walijikita kuwahoji askari kadhaa waliokuwa zamu siku na saa ambayo mahubusu yule anayekabiliwa na kesi ya ugaidi alitoroka, mahojiano hayoyalianza baada ya yeye na mwenzake kujitambulisha kwa mkuuwa gereza na kisha kuanza kazi hiyo ya kuuchimba ukweli,
"tangu kutengenezwa kwa gereza hili haijawahi kutolea suala la mahabusu au mfungwa kutoroka na niwahakikishie kuwa mtuhumiwa hakupita katika eneo la mbele au nyuma yagereza...aaaahhhh sasa naanza kupata picha"
"unapata picha gani warden maana unanichanganya hebu nipemaelezo ya kutosha muda sio rafiki nina majukumu mengi sana kwa siku ya Leo umepya picha gani wewe mzee"
"nisahihi kabisa ASP Richard nimeanza kupata picha kwasababu wiki mbili zilizopita tulipata malalamiko kwambamfumo wa maji safi na taka katika upande wa ule wa kondemu(conderm) na zile selo za upande wa wafungwa wenye matatizo ya akili ulikuwa haufanyi kazi na ndipo walipokujawatu wakiwa na barua toka makao makuu kwamba wamepewa tenda ya kutengeneza mabomba hayo na walianza kazi hukuwakisimamiwa na baadhi ya maafande na siku tuliyo mkosa mahabusu huyo tulikuta shimo katika hapo linapokaa sinki la choo hivo ni ukweli kwamba alitorokea hapa na baadhi yamaafande walifatilia hili shimo linapoishia wakajikuta wanatokea katika jumba fulani kilomita moja kutoka hapa, hawakufanikiwa kupata alama yoyote aliyoacha nyuma na hatatulipofatilia jumba hilo tuliambiwa tangu limalizike miezi minne iliyopita halikuwahi kukaliwa na mtu "
"Daaaah!!! unaweza kunambia ni mafande wapi waliohusika kusimamia hilo zoezi na wako kazini hii leo" aliuliza inspekta mayunga kwa kukatisha maelezo ya mkuu huyo wa magereza huku akimkazia macho
"sijawaona leo ila nina imani sio muda watafika maana niliagiza maafande wote waliokuwa zamu wawe maeneo haya kama watahitajika kwa lolote ila mpaka mnaingia humu maafande watatu walikuwa hawajafika na ndiyo walihusika na zoezi hilola usimamizi vile vile walikuwepo lindoni siku iliyosadikika kwa mahubusu huyo alitoroka" akaweka kituo hukuakiwatazama ASP na Inspekta kwa chati.
"unaweza kutupa anuani za makazi wanapokaa maafande hao ilitujue kitu gani kipo nyuma hata ya wao kutokufika kazini kwasiku ya leo wadeni"
bila shaaka ASP Richard ngoja nimuite afande mmoja anaehusika na utunzaji wa kumbukumbu ili aweze kuwapa annuani hizo......dakika moja tafadhari akawaambia huku akinyanyua mkonga wa simu na kupiga sehemu akatoa maelekezo kisha akaikata simu ile, dakika sio nyingi mlango ukagongwa na akaingia askari magereza wa kike akiwa na majalada matatu na kisha kumkabidhi majalada yale akapiga saluti na kuondoka, mkuu wa gereza akatoa anuani za askari wale kisha akatulia kusubiri wageni wale watasema nini.
"wadeni tunahitaji jina ka hiyo kampuni ikiwezekana na baruahiyo waliokuja nayo tuna kazi mayo bila kusahau anuani ya hiyonyumba mnayohisisa ndiyo alitokea kabala ya kutokomea kusikojulikaa" alisema ASP richard huku akimkazia macho mkuu yule wa gereza.
" hakuna shaka ASP richard ntawapa kila mnachokihitaji ilimfanikishe suala hili maana bila hivyo ntapoteza kazi au kufungwa kabisa kwa kosa lisilo la kwangu," akawakabudhibahasha yenye kila kitu kisha akawaambia kama kuna chochote wasisite kumjuza.
inspekta mayunga na ASP Richard waliondoka eneo lile la magereza tayari kuanza kuwatafuta askari waliokuwa zamu siku ya tukio, wakati wao wakiendelea na uchunguzi wao upande wa mwingine pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya hindi katika jijila Dar es salaam wanaonekana mwanamke na mwanaume wakionekana kuzama katika mahaba mazito sana kiasi kwamba ungepita karibu yao ungeweza kudhani labda ni watu waliokokwenye fungate au ndiyo wanajiandaa kufunga ndoa lakinimahaba yale yalikuwa ni kuwatia watu upofu kwa maana walikuwa pale kwa ajili ya kitu fulani.
"itatuchukua muda gani kuweza kukamilisha hili kablahatujahamia kule kulipotokea yale mauaji sajenti" aliongea kwa kunong'ona mwanamke yule kiasi kwamba hata ungekuwa umesimama umbali wa mita mbili usingeweza kusikiaalichokitamka.
"unawaona wale jamaa pale wanachoma mihogo na wenginekule kwenye mitumbwi wote wale ni wenzetu na wanasubiri mzigo ufike ili tuwatie nguvuni watu hawa"
"lakini taarifa za msiri wetu alisema mzigo utaingia usiku iwejetuje kutega hapa muda wote na tulikubaliana saa tano tuwemezani na ripoti huoni kwamba tunapoteza muda na heri tungeanzia kwenye nyumba zilipotokea mauaji huendatungepata kitu"
"ni kweli kama usemavyo kwamba msiri wetu alisema mzigoutaingia usiku ili kuna taarifa zilifika ofisini kwamba mzigo umegawanywa mara mbili na hizi ni taarifa fiche ambazonimelazimika kukwambia tu ajenti Diana kwasababu wewe nipartner wangu kwenye kazi hii."
"sawa nimekuelewa sajenti........ngoja niende maliwato mara moja haja ndogo imenibana" alisema ajenti Diana huku akisimama na kuuelekea mlango wa kuingilia vyoo wanavyotumia jinsia ya kike alipofika alitoa ka simu kadogo nakuandika ujumbe mfupi kwenda kwenye namba moja.
"KUNA MJUSI ANATOA HABARI ZETU KWA NYOKA....PANYA WANASUBIRIWA KWA HAMU WAJAE KWENYE SHIMO HABARI ZAO ZIISHIE HAPO NA KILA LITU KIWE WAZI BADILISHA MPANGO HARAKA"
baada ya kutuma ujumbe ule hakusubiri ujibiwe aliizima simuile na kuondoka huku akijifanya kujiweka sawa kisha akarudi kwenye kiti chake huku akiendelea kupata kinywaji chaketaratibu "pole sana sajenti mnajifanya wajanja ila hakuna atakaeweza kuusimamisha mzigo huu usiingie sokoni naukithubutu hata kuusogelea risasi yangu moja itakuondoa haujui unapambana na watu wa aina gani, laiti ningekuwa mimi ningekuwa kijijini kwetu nalima viazi kuliko kupambana nawatu wazito ambao wanaweza kunipoteza hata kabla jua halijazama" aliwaza hivo ajenti Diana huku akinywa juisi yake
taratibu.****** itaendelea kesho Tchao
 
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
"pole sana sajenti mnajifanya wajanja ila hakuna atakaeweza kuusimamisha mzigo huu usiingie sokoni naukithubutu hata kuusogelea risasi yangu moja itakuondoa haujuiunapambana na watu wa aina gani, laiti ningekuwa miminingekuwa kijijini kwetu nalima viazi kuliko kupambana nawatu wazito ambao wanaweza kunipoteza hata kabla jua halijazama" aliwaza hivo ajenti Diana huku akinywa juisi yaketaratibu.
VAA VIATU TUONGOZANE
RASKAZONI- TANGA
katika eneo hili lenye nyumba nyingi za kifahari kuonesha nieneo la watu wanaojiweza, ndani ya nyumba moja hivi, wanaonekana wanaume watatu warefu na miili iliyoshibakutokana na kuzingatia ratiba ya mzoezi kikamilifu huku mwingine akiwa mfupi mwenye kipara na aliechonga ndevuzake kwa mtindo wa O na kufanya idadi kuwa wanne ndani yasebule ile.
" wazee tusikilizane nimepokea ujumbe nusu saa iliyopita kwamba kuna mtu anataka kutukamatisha kwa polisi mara tumzigo utakapofika kwenye destination yale, ina maana tuna wasaliti kati yetu,na alieutoa ujumbe huu ni mtu wetu na ni mmoja ya watu walioko kwenye mtego tukionekana tu tuwe matatizoni na nimefanya mawasiliano na bosi amenitumia ujumbe kwamba twende na mpango wa usiku huu wa mchana atatupa feedback nini kifanyike."
"ebhana eeennnhh mpaka nimesisimka, kinyundo hizi taarifaumetoa wapi mbona unanishangaza sana nilikuwa nshapiga hesabu zangu za kulala kwa yule demu wangu wa tegeta mara tutukifika mbwa gani huyo anaetia ndimu kwenye maziwa nikimjua mtu huyo ntakuwa wa kwanza kutumbukiza risasikwenye mdomo wake ili akifike huko awe bubu kabisa "
"hata mimi najiuliza sana mpango tupangie gizani hata sisimizi walikuwa wamelala hawakusikia neno hao wanaotusubiri wamejuaje?” alisema bwana yule mweusi na mwenye macho mekundu aliefahamika kwa jina la kala
kati ya wanaume wale wanne waliozungumza ni mmoja tu ndiyo hakuwa amezungumza aliwatazama wenzake kisha akasema
"msaliti hayupo kati yetu msaliti yuko juu na huenda ni kati ya mabosi zetu au watu wao wa karibu,sisi ni watekelezaji tu siyo wapangaji wa mipango na mikakati na kwa jinsi nnavyoonakuna harufu ya kuhujumiana kwenye mizigo hii kiondoa huu mzigo tulionao mzigo wa usiku anakuja nao nani na anatoka wapi ili tumzuie asiweze kufika mpaka upepo utulie" mtu huyualifahamika kama Kobelo
"mzigo wa usiku anakuja nao Vanessa kutoka pakistani na atafika hapa na ndege ya emirates saa tisa usiku na mpango ulisema tutamkuta hoteli ya longido pale kinondoni, nimejaribu kumtafta lakini hapatikani na kama mnavyojua akiwaga namzigo hawashagi simu mpaka akishaukabidhi na kupata pesayake taslimu ndiyo simu yake inapata uhai" alitoa maelezo hayomafupi bwana kinyundo.
"mimi namuaminia maana siyo mara moja kavuka na mzigo tena kwenye nchi zenye ulinzi mkali Kobelo” mwisho wakakubalia watulie ndani mle kuangalia upepo utakavyokuwa.
MAFINGA-IRINGA
Saa 11:45 jioni
huu ndiyo muda ambao maafisa wale wa jeshi yaani luteni Sabina na Meja tumbaku walifika katika kambi ile nakuchunguza uhalifu ulivyofanyika ndani ya kambi walipokea ripoti kutoka kwa majasusi kutoka idara ya ujasusi wa jeshi, kwamba kabla ya tukio kamera zote zile zinazoonekana na zile za siri ziliharibiwa na kisha kuuwawa wanajeshi wanne ambaomiili yao ilikutwa imefichwa kwenye kichaka jirani na uwanja wa kufanyia mazoezi, sio hivo tu kuna miili kumi na tatu imekutwa imeteketea na moto na wataalam wa milipuko kutoka makao makuu wamethibitisha kuwa milipuko hiyo inatokana nabomu la kurushwa kwa mkono kutupwa karibu na maegesho ya magari na kilichotokea ni kama hivi tunavoona.
"kwahiyo kapteni ni wanajeshi 17 tu wanaolinda hii kambi au wakati tukio linatokea ni hawa tu ndiyo walikuwa kambini"
"siku ya tukio tulikuwa tunafanya usafi maeneo ya mjini na niagizo ambalo aliliridhia mkuu wa majeshi kutokana na ombi la mkuu wa mkoa, hivo wakati nguvu kubwa iko mtaani huku kambini tukapigwa tukio, wamekuja kufika tayari watu washaondoka na mzigo wa silaa za kivita na mabomu"
"mmmmhhh ninaona harufu ya hujuma, luteni sabina hebu mpigie chifu atupe ripoti za walipofikia timu ilioko singida"
"haina tatizo meja tumbaku," alitoa simu na kuitafuta mamba yachifu na kuipiga ikaita kwa sekunde kadhaa Kisha ikapokelewa
"chifu shikamoo
"Marhaba luteni Sabina Habari za jioni, Kuna mlilopata mpaka Sasa kwenye upelelezi wenu"
"Havana chifu kwa sisi tuliokuja huku mafinga kiukweli adui kafuta nyayo zake kitu kinachotufanya kazi hii tuione Ina ugumu ila tutajitahidi kwa Kadri ya akili na nguvu zetu zote ilituweze kumaliza hili jambo kwa wakati, Vipin timu ulioituma singida imepata dondoo zozote"
"oooopps.... Huko napo hakuna ripoti ya kueleweka na hata walioenda Kule gerezani pia wamenipa Habari za kustusha kidogo, kama tulivyo kubaliana tukutane safe house tujadiliane"
HOSPITALI YA TAIFA- MUHIMBILI.
Saw 12:15 jioni
miili mitatu ya viongozi isyokuwa na uhai ilikuwa imelazwa huku daktari akimpa ASP Richard ripoti ya uchunguzi wa miili hiyo kabla haijachukuliwa na ndugu wa marehemu kwa ajili yakwenda kuzikwa
"Afande ripoti inaonesha muuaji/wauaji kabla ya kumpiga risasiya kichwa, alipuliza dawa kali ya usingizi iliyomlaza marehemu Kisha akatekeleza kile alichokusudia kiulaini, na hivo hivondivo alifanya kwa waziri wa fedha na hata kwa gavana."
"nimekuelewa daktari hiyo ripoti niwekee kwenye flashi, nkihitaji ufafanuzi ntakutafta, Uwe na jioni njema" alisema ASP Richard huku akitafta namba za sajenti Mayunga kujua ni hatua ipi waliyopiga na ajenti Diana lakini walichoambiwa kilizidi kuwaacha mdomo wazi kwamba mzigo waliokuwa wameutega wa madawa ya kulevya, mtego wao ulinasa kwa Jamaa waliokuwa wanauza ice cream, hata walipo wahoji hawakuwa naLA maana kusaidia kufikia jawabu"Wakaagana hukuwa kikubaliana wakutane nyumba Salama kwa ajili ya kupangamikakati mipya.
SAFE HOUSE- MIKOCHENI
saw 5:05 usiku
Watu wote walikuwepo kwenye chumba kile huku Vichwa vyaovikiwa Vinawaka moto, ni auti ya chifu ndiyo iliyowatoa katika tafakari kwamba ni siku ya kwanza ila giza ndivyo linazid kuwa zito, mbali na hao wenginew mawazo kujilita katikakazi iliyopo mbele yao ni ASP Richard peke yake aliyekuwa akimuwazia mdogo wake johnson, ambaye kwa tabia yake yaulevi amekuwa akikaa selo mara kwa mara, leo hii alitoka kupokea simu ya mkuu wa kituo cha polisi uwanja wa ndege kwamba mdogo wake huyo amempiga mkewe kiasi cha kumfanya mpaka apoteze fahamu kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi, mwili ulikuwa pale ila mawazo yake yalimpeleka mbali kiasi awaze ni jinsi gani ataweza kumbadilisha mdogo wake huyo ila akajikuta anajisonya moyoni kwamba kama jeshi hilo lenye viongozi chungu nzima wa jeshi hilo hilo la polisi wameshindwa kumlea na kumfunza adabu kiasi cha kubadilika yeye peke ake hatoweza kitu alichoazimia ni kikao kikiisha basi atatoka kwenda kumuonakituoni hapo. na ndiyo wakati huo huo sauti ya chifu ilimstua
"ASP Richard naona kama hauko na sisi unaweza kutuambia nikitu gani unakiwaza labda kuna kitu kitakachotupa mwanga"
"hapana chifu tuko pamoja nafikiria ni kwanini muuaji waaskari waliokuwa zamu katika gereza la ukonga wakati gaidi yule anatoroka na ndiyo waliosimamia utengenezaji ule wabomba la maji safi na taka alitumia mtindo wa aina moja sawa na kile kilichotokea kwa wale mawaziri wawili na gavana wabenki kuu hili linanifikirisha sana kuona kuna tatizo sehemu, japo uchunguzi wangu sio rasmi ila kwa kufikiria nje ya box naona kabisa vifo hivi vinahusiana matukio haya wacha tuendelee kuchunguza ila tutakuja kujua baadae na kinacho nitafakarisha ni kwamba uhalifu huu unaotengenezeka uko organized(kupangiliwa) chifu" alitoa maelezo ambayokidogo yalianza kumuingia chifu
"kama nimekuelewa vizuri ni kwamba mawaziri wale walihujumiwa na mwisho kupewa zawadi ya kifo hii inatupa picha kwamba katika maeneo yote kulipopigwa matukio kulikuwa na wasaliti waliokuwa nyuma ya uhalifu huu sasa mawazo yetu inabidi tuchunguze kwenye ofisi hizi ili tupate dondoo zitakazotufikisha kwenye jawabu......ghrrrrr ghrrrr mliowa simu ya chifu ilitoa mtetemo ambao ilimbidi kuingiza mkono mfukoni na kuitoa moyo wake uliingiwa na ubaridi baada yakuona ni namba ya mheshimiwa raisi akapokea na kutoaheshima kwa mkubwa wake wa kazi
"uko wap mzee wangu"
"nipo na vijana wangu tuna habarishana kwa kile walichokipata mpaka sasa kuhusu matukio haya"
"NAKUHITAJI OFISINI KWANGU SASA HIVI" simu ikakatwa ilibidi kikao kihairishwe na chifu kwenda huko anapohitajika na mheshimiwa raisi, huku ASP Richard akimuomba sajenti mayunga amsindikize uwanja wa ndege kwasababu mdogo wake amepata shida vile vile kuangalia haliya shemeji yake
"partner mbona usiku usiku kuna nini tena au ndiyo umeshammisi mama mtu" alichombeza ajenti Diana huku akidadisi kujua sajenti mayunga anaelekea wapi baada yakushindwa mchana ule kuwashika washirika wenzake baada yakuvujisha mpango waliowasukia wasafirishaji wale wa dawa za kulevya.
"hahahahah hapana bhana mbona mimi niko singo na kwa vile umeshakuwa partner wangu haizuii hata wewe kuwa mama mtu hahahaha"
" thubutu nani awe na mwanaume kama wewe muone ulivokamaa mikono imeota sugu kwa kukimbizana na wahalifu mtaani kwani huko vituoni kwenu hujaona unaefanana nae babu wewe unataka unichukue ukanizeeshe"
"naanzaje kusubiri elfu kumi yako utakayo pokea rushwa ndiyo inunue chakula na vipodozi si ndio mwanzo wa kupauka alafu mtu mwenyewe unaonekana una wivu si utanipiga risasi kama yule mwenzenu wa kule Mbeya akhaa babu wewe hayo maisha mimi siyahitaji hahahahah"
"ngoja nimuwahi Rich mdogo wake ana matatizo na kaniomba nimsindikize"
"wapi nyie hiyo ni janja janja tu mmeshawamisi wanawake zenu ndo kwanza siku ya kwanza na yatawashinda mwaka huu....ila polisi nyinyi mna nini mbona mnapenda chini hivo"
"kama huniamini tunaweza kuongozana na tukampa kampanimwenzetu"
"mnaenda wapi kwanza kama ni mbali mimi bora nijilaze tumaana siku ilikuwa ndefu alaf uliniudhi sana nakwambia tuondoke hapa tunapoteza muda hutaki kusikia unaamini intel za uongo....hivi unadhani nyie polisi mnaweza kuwa na intel za uhakika kutushinda sisi watu wa idara na nyingine sisi ndiyo tunaamua tuwape tu ili mkajipakulie minyama kwa waandishi wa habari na mlivyo na wala rushwa baada ya miezi kadhaa kesi inazimwa...muone kwanza lilivyokushuka haya tunaenda wapi".
"UWANJA WA NDEGE"
"hebu ngoja kwanza kwani mdogo wake ni mgonjwa na anapanda ndege kwenda kutibiwa nje au kuna nini huko UWANJA WA NDEGE kataitiwa na maafisa nini....." bado aliendelea kudadisi ili apate uhakika wa kile wanachoendakufanya maafande hao wawili.
"mimi mwenyewe sijui chochote nafikiri ntajua nkifika hukovipi tunaenda mrembo au unaenda kutoa uchovu kama ulivyosema"
"na mafoleni haya tunaweza kurudi asubuhi nkakosa kupata usingizi ngoja nimtafte dada wa kazi aniambie kwangu kumeshindaje" na ni wakati huo ambao ASP Richard alikuwaana toka kwa kiongozi wake Meja Tumbaku kumuomba ruhusana alimkuta sajenti anamsubiri basi wakachagua gari moja katiya mengi yaliyokuwa yame simamishwa kwenye maegesho yamagari, wakatoka na gari aina ya BMW X6 na kuyaacha makaziyale ya nyumba salama kuitafta njia ya uwanja wa ndege.
JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPOT
Saa 12:47 usiku
ndiyo muda uliwakuta geti la kituo cha polisi jirani na terminal one, wakajitambulisha na kutoa vitambulisho vyao wakaruhusiwa kuingia na baada ya kuipaki gari dakika iliyofata iliwakuta mapokezi na kutoa utambulisho mfupi kisha akaombakupewa utaratibu wa dhamana na afande wa mapokezi.
"kwa usalama wake na hali ya mgonjwa dhamana yake kiukweli mkuu imezuiliwa mpaka labda mgonjwa akionesha ahueni"
"nimekuelewa sajenti, kama itakupendeza ninahitaji nizungunzenae hata kwa dakika mbili tu afande " alikuwa anao uwezo wakutumia cheo chake kumuona mtu anaemhitaji ila kwa taratibuna kanuni ule haukuwa muda wa kuwaona watuhumiwa nahaukuwa muda wa kupiga nao stori ndiyo maana akatumia lughaya unyenyekevu kwa afande yule kiongozi wa wenzake waliokuwa chumba cha mashtaka.
"haina tatizo mkuu ngoja nimpeleke kule chumba cha CID mkapate kuongea mkuu wala sisi hatuna tatizo kwanza tuna furaha kwa kuwa umetutembelea, detektivu mayunga yeye tushamzoea na kiukweli hatukutarajia ujio wenu kabisa"
"haina tatizo afande ngoja sisi tutangulie atatukuta huko"
dakika sio nyingi akaletwa mdogo wake na ASP Richard ambaye kiukweli haikupaswa kupoteza sekunde kujua wawili hawa ni ndugu ijapokuwa walicho tofautiana ni tabia tu, mudawote ASP Richard alikuwa amekaunja ndita huku akionekana kuchukizwa na upande ambao mdogo wake amechagua"
"Dogo hii tabia ya ulevi umeshindwa kabisa kuidhibiti? na vipikumdunda mkeo unajiskia fahari" maswali mfululizo yaliyomfikia akiwa bado kasimama yalimpa picha ujio ule haukuwa wa kumfariji bali kuchochea kuni
"ntakujibu maswali yako yote mawili japo umenichukia ila ntakueleza kama kaka yangu na vile vile kiongozi wangu katika jeshi" muda wote huo detektivu sajenti mayunga alikuwa kimyaakiwasikiliza ndugu hawa japo alikuwa na uchovu na usingizi ila alijipa subira.
" kaka mke wangu kanishinda tabia, huwezi amini mama Dickson huyu wa sasa hivi sio yule uliekuwa unamjua, mama Dickson sasa hivi kawa na kiburi amekuwa mlevi kiasi kwamba ameanza kuwa mtoro kwenye kitanda tunachotumia kulala" akameza funda la mate huku akionesha ni jinsi gani yalivyokuwa yakipita kwa shida hiyo ilitoa tafsiri ya kile kilichomkaba kooni kuwa ni hasira alizonazo kwa mkewe huyo.
"alipokuja na wazo la Dickson kwenda shule za bweni nilionaana maono ya mwanetu apate elimu, kumbe haikuwa hivo alikuwa na ajenda yake ya siri ya kuwa huru na kufungulia tabia yake ya asili"
********itaendelea
Tukutane tena kesho
 
NISOME TENA UPATE KUJUA NI AJENDA GANI YA SIRI MAMA DICKSON ALIKUWA NAYO FUATANA NAMI.
“unavyosema ajenda ya siri na tabia ya asili una maana gani dogo hebu nyoosha maelezo muda siyo rafiki na ukicheza utafungwa na mimi sitonyoosha mkono wangu kukusaidia" aliongea kaka ake kwa msisitizo
"kaka sikujua kama naishi na mwanamke ambaye alistaafu ukahaba kwa muda, wakati amepumzika ndiyo muda niliompata na kuanza kuishi nae, ila sasa lile pepo lake la ukahaba limerudi kwa kasi, kiasi kwamba ninapotoka kuingia zamu usiku nae anatoka kwenda kufanya uchafu wake, huwezi amini usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9 usiku nilijiskia hali yangu sio nzuri, hivyo nikamueleza mwenzangu na akanishikia lindo, nkiwa nimerudi nyumbani nilikuta hali ya ukimya sana nkajua amelala nimegonga zaidi ya nusu saa ndipo nilipokumbuka nina ufunguo wa ziada nkjaribu kufungua na kikakubali ila cha ajabu chumba kilinilaki kikiwa chenyewe na kipweke hata shuka nililikuta liko vile vile kuonesha halikulaliwa usiku ule."
nilipotezea nkajisemea ngoja nipumzike ntajua kesho nililala nikiwa na maswali magumu kichwani mwangu ila kubwa zaidi ni hii tabia mpya ya mke wangu nilipitiwa na usingizi na ilipotimia saa 11 alfajiri niliamka na kujisogeza kazini tumbo lilikuwa limepoa kiasi ihivyo basi nilifika na nkikamukuta mwenzangu ilibidi niweke sura ya tabasamu na ulipofika muda nikakabidhi lindo naam ilikuwa ishatimia saa 12 asubuhi na baada ya zoezi lile nilizitupa hatua kurudi nnapo kaa ,niliporudi nilistaajabu kumkukuta mama dick amejilaza huku akionekana kama ana uchovu hivi hasira ilinifukuta nilitamani nimuamshe ili anijibu usku wa jana alikuwa wapi ila nkajipa subira. nilijilaza kitandani nikiwa na mawazo na uchovu, sikumuuliza chochote na tuliendelea na shughuli za siku kama hakijatokea kitu lakini kama Mungu ilipofika majira ya saa 11 jioni aliniaga anaenda kisimani kuchota maji bahati mbaya kwake na nzuri kwangu aliacha simu yake na ndipo nilipoishika baada ya ujumbe mfupi kuingia kwenye simu yake hakika kaka mama dickson nilikuwa sijamjua tabia yake vizuri nilipofungua ule ujumbe ulioingia nilichoka kwani kama ulivyo kuonesha kuwa hakukuwa naneno la siri ujumbe ulisomeka" leo umenipa penzi nusu nusu, kwanini usitengneze safari ya ghafla ili tule raha nimemis ikelele zako"
"ujumbe ule ulinifanya nifatilie meseji za juu na kweli niliona uozo anaofanya mke wangu na huyo mtu mwenye hiyo namba lakini siyo huyo aliyepelekea hayo yatokee bali nilipofungua mtandao wa whatsaap niliona namba moja ninayoifahamu nkapata shauku ya kufungua jumbe zake na hapo nkajikuta moyo unanisukuma nifungue jumbe zake la haula kaka nilikuta video za ngono za mke wangu na mkuu wangu wa kituo huku wakiambiana wamemisi kufanya mapenzi na mke wangu bila aibu anamwambia amemisi kuingiliwa kinyume namaumbile kwa hakika niliishiwa nguvu, niliwaza kumbe najinyima kula vya ndani humu kumbe kuna wengine wanapewabila hata kuomba na aliporejea nilimuuliza akakana akasema kuna mfanyakazi wa ndani wa nyumba ya jirani ndiyo anatumiaga simu yake kuchati na hao watu" akameza tena mate huku akiendelea kutiririka huku machozi yakimlenga.
"na hapo hapo simu yake ilitumiwa ujumbe na namba ya mkuu wa kituo huku akisema leo ndiyo ratiba itatoka na ameshamwambia meja anipange shift za kuunganisha ikiwa nipamoja na kunipeleka kwenye ukaguzi wa mizigo terminal three na leo kwa vile kuna ndege za kuingia saa 9 kutoka brazili basi itanifanya nkae muda mrefu kazini kwa sabab kuna ndege pia zinaondoka saa 11 alfajiri lutoka nchini hivo ntakuwa lindo hadisaa 7 mchana kwa kisingizio cha kumshikia mwenzangu ambaye kaenda nyumbani kwao kwa vile kuna msiba"
ilikuwa ni kama kisu chenye moto kupita kwenye ngozi nilihisidunia inanielemea sikuhitaji kukushirikisha kwa vile hili nijambo la familia yangu na ndiyo maana nkaamua kufanya vile na mimi ndiyo niliempeleka hospitali na baada ya dakika 5 tangu nifike hospitali niliwekwa chini ya ulinzi kwa amri yamkuu wa kituo na ndio maana nipo ndani mpaka sasa hivi"
"na unaeingia nae lindo kwenye kukagua mizigo amekwishakupata taarifa kwamba hutafika leo kazini kwasababu umekamatwa kwa kosa la kumpiga mke wako' aliuliza detektivusajenti mayunga.
"hapana hatambui hilo na hata kuongea na bro ni wema tuamenifanyia inchrge wa chumba cha mashtaka ila ukweli ni kwamba sikupewa haki yoyote ya kuwajulisha ndugu wakatiwananikamata"
mke wako ulimpeleka hospitali gani sasa ili tukajue na yeye haliyake iko vipi, maana nikicheza dogo utapotea na kuozea gerezani" alisema ASP Richard kwa masikitiko.
"nilimpeleka kwenye zahanati ya kambi yetu, sijajua bado yupo au katoka"
"sawa wacha sisi tukamuone kisha kesho ntakuja kukuona nakukueleza kilichojiri hata kwenye lindo lako" wakasimama wakapeana mkono huku maafande wale wakielekea upande wazahanati lakini nako hawakumkuta mlengwa daktari aliwapataarifa kwamba mgonjwa aliruhusiwa tangu saa nne usiku naalikuwa anaendelea vizuri.
alitafta amba za shemeji na kuipiga simu iliita ikakata akapiga tena simu ikawa haipatikani
"eeeebhana dah kweli wanawake ni kama mti wa porini sajenti"
"kwanini unasema hivo ukute yupo nyumbani kapumzika ASP Richard tusije tukawaza vingine tukawa tunachuma dhambi nauna maana gani kusema ni mti wa porini"
"mwanamke ni mti wa porini kwasababu hauna mwenyewe hataumuoe mwanamke ukae nae ndani siyo kwamba ndiyo umejimilikisha kwamba ni halali yako, kuna wajenzi wataukatiahata hapo ndani kwako sajentijapo unajiita mmiliki ni wewe"
"hilo nalo ni neno afande, hata dogo nilivomskiliza inaonesha tayari huyo mwanamke keshamzidi maarifa hivo anamsukuma tu kama mlevi"
ulinigusia suala la mizigo uliokuwa unafatilia kule ufukwenikwamba ulikuta wanauza samaki ilikuwaje kuwaje ikiwaunasema ulipata intel ya uhakika"
"hata mimi nilishindwa kuelewa alafu kwanini wasiuzie samakisoko la samaki feri waje kuuza ufukweni"
"ndiyo hapo nawaza ilikuwaje kuwaje afande na Intel ilikuwa yauhakika, yaani had nkaishiwa pozi"
"Daaah!!! Na haukumshirikisha mtu mwingine".
"mmmmmhh....hapana mkuu tuliokuwa tunajua ni mimi infomana ajenti Diana"
"na ulinigusia pia mzigo wa pili kutokana na intell ulikuwaunatoka wapi sajenti"
"mzigo wa pili ulikuwa unatoka pakistani kwa mujibu wa intel ila haikuelezwa unafika saa ngapi."
"unaonekana umechoka turudi kambini maadamu kuna mamlakaziko macho ukifika tu unanaswa" wakaondoka uwanjani pale iliwapate usingizi wa japo kwa muda uliobaki kabla ya jua kuchomoza kwani walikuwa na siku ndefu sana, ilia kuwamaking"
Ajenti Diana hakupata usingizi bali alikuwa anawaza maafandewale wamenda kufanya nini uwanja wa ndege akatoka nakuingia bafuni kisha akafungulia maji na kupiga simu kwakinyundo.
"wewe boya mbona simu inaita muda mrefu, mlifanikiwa kumpata Vanessa? na ameshaingia nchini kwani"
"hapana yule demu kazima simu na watu wetu hawajamuona kabisa viwanja vya ndege na bosi anasema yule demu yuko nawenzake sita waliobeba kilo tatu tatu hivo kilo kumi na nane zinatakiwa ziingie kwa ndege na zile 102 zinatakiwa zije kwakutumia mapipa ya kuwekea mafuta na mzigo utaachwa pale karibu na ufukwe kisha sisi tutayafata huko chini na tuta yafikisha kule kiwandani kabla ya kuingia sokoni.
"atakuwa wapi sasa huyu mpuuzi mimi machale yananicheza kwamba nahisi kama mzigo wetu utakuwa mashakani acha niende uwanja wa ndege kuna nyoka wawili wameenda kuzurura mitaa hiyo hiyo sasa wasije wakaibuka na kitoweo nasisi tumekaa tu hapa bosi hatatuelewa"********”Laiti wangejua watakachokutana nacho kila mmoja angekuwa ameshatafta wapi bilipo vilago vyake na kutimkia ughaibuni………………………::itaendelea
Tunazisi kuchanja mbuga kama ulikuwa unahisi kwamba uliwahi kusoma Riwaya mpaka ukahisi ni filamu inayopita kwenye fikra zako kaa hapa hapa muda wowote ule tunaweza kupata muendelezo NAENDELEA KUSISITIZA SIMULIZI HII NI YA KUFIKIRI NA KUTUNGA WALA HAIHUSIANO NA MATENDO,WATU AU TAASISI ZAKE ISIPOKUWA NI KAZI YA FASIHI KUELEWEKA KWA HADHIRA KWA URAHISI,
 
NAENDELEA KUSISITIZA SIMULIZI HII NI YA KUFIKIRI NA KUTUNGA WALA HAIHUSIANO NA MATENDO,WATU AU TAASISI ZA NCHI HALISI PAMOJA NA MAENEO YAKE ISIPOKUWA NI KAZI YA FASIHI KUELEWEKA KWA HADHIRA
SONGA NAYO………………..Loading
 
SAFE HOUSE
Saa 11:40 alfajili
Grrrrhh Grrrrrhh.... ni mlimo wa mtetemo wa simu iliyokuwa juu ya meza ya chumba alichokuwa amelala sajenti Mayunga, n isimu ndiyo ilumtoa katika dimbwi la usingizi uliochochewa na uchovu wa siku nzima akanyoosha mkono na kuivuta na hapojuu ya kioo cha simu palisomeka jina na namba ya mkuu wake wa kazi yaani Kamishna wa kitengo hicho akapeleka kidole katika kitufe cha kijani na kuiweka sikioni
"shikamoo Mkuu"
"marhaba......umeona kinachoendelea kwenye grupu letu la waasapp afande"
"hapana....mkuu nilikuwa na uchovu uchovu wa siku ya jana"
"fungua kisha ntakurudia baada ya dakika tano najua tutatuzungumza lugha tutakayo elewana"
"sawa mkuu" simu ikakatwa huku sajenti mayunga akifungua mtandao wa waasapp akastaajabu utitiri wa jumbezinazoendelea kumiminika katika grupu lao la kazini, "KUNA NINI" alijiwazia kichwani akafungua jumbe nyingi sana hukuzikiwa zime tagiwa picha ambayo hakuwa anaiona vizuri akaigusa picha ile ikafunguka na hapo ndipo alipostaajabu na kupigwa na butwaa
,"kweli umdhaniaye kuwa ndiyekumbe siye" ndilo neno lilimtoka mdomoni huku akiwa ametumbua macho kwani picha iliyokuwa kwenye kioo cha simu ile ilikuwa ni sura anayoifahamu
"BEATRICE NDELWA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA WAPI NA WAPI"
Alijiongelea mwenyewe kwani mtu yule aliyetaja jina lake ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, umaarufu wake ulitokana na uimbaji wake wa hisia na pia sauti yake nzuri aliyobarikiwa na mungu kwa ajili ya kumsifu sio hilo la umaarufu lililompa hamaniko bali binti huyo ni shemeji yake namakamu wa raisi ambaye alimuoa dada yake miaka kadhaa huko nyuma, historia inaonesh wao ni wazaliwa wa mkoa wa kagera katika wilaya ya muleba, binti huyo aliweza kupata elimu yakekatika shule ya msingi muleba na kisha sekondari ya ihungo nahuko ndipo nyota yake ilipoanza kuwaka na alianza kujulikana zaidi alipoanza elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo safari yake ya uimbaji ulipoanza na kishakuanza kuachia albamu huku akipewa sapoti na dada yake ambaye tayari alikuwa kwenye ndoa na mtu huyo mzito, nailigunduliwa kuwa na mahusiano na mwanamke huyo wa mtumzito katika taifa hilo wakati alipohojiwa katika kipindi cha lininga kiitwacho" the interview" kinachoendeshwa na mwandishi mwenye makeke sasa Joashi chogo,
ni baada ya kupitia komenti ya mmoja wa wafuatiliaji kwamba ana undugu na mtu yule ambaye serikalini anatambuliwa kama mwenzi wa makamu wa raisi na baada ya kuonesha kupata kigugumizi ndipo alipokubali na kuanzia hapo watu na magazeti mbali mbali yalianza kuandika na kufuatilia habari kumhusu, nyimbo zake zilivuma kwa kasi kiasi cha kumfanya kuanza kufanya matamasha nje ya nchi, kusafiri kwake ilikuwa kawaida na hakuna aliyemtilia mashaka zaidi kumuona mtakatifu kwa ule unyenyekevu na sura yake ya upole iliyojaa tabasamu mudawote sifa zote aliendana na dada yake isipokuwa vitu vichache kama kipaji cha sauti na umbo la mwili kwa sababu ya majukumu ya kitaifa kama mke wa makamu wa raisi lakini kama mama wa watoto wanne waliomfanya awe katika umbo la umama huyu ndiye ROSEMARY NDELWA.
Na hiyo historia iliyokuwa ikisimuliwa na meja tumbaku ikiambatana na picha mbali zilizokuwa zinaonekana kwenye kioo cha skrini iliyokuwa ndani mle, na hiyo baada ya asubuhi kupata ripoti kuwa wamekamatwa watu wanne waliokuwa wameshavuka npaka wa Tanzania wakitokea nchi jirani ya Kenya kwa kutumia gari la watalii na taarifa za awali zinasema walikuwa wanavusha mzigo wa kilo ishirini na tano za madawa ya kulevya yanayohisiwa kuwa heroin.
"sasa sisi kukamatwa kwa huyo binti inahusiana vipi na kazi ambayo iko mbele yetu" alisema kwa hamaki ajenti Diana
" inahusiana kabisa na kazi yetu huenda huo ndio mzigo wa pili kati ya ule tuliokuwa tunausubiri pale ufukweni ajenti Diana huoni kama huyu atatufungua na kazi yetu itakuwa nyepesi sio kwetu tu hata kwa timu nzima nna uhakika kabisa tutaweza kuwapata wahalifu wote" alisema hayo sajenti Mayunga hukuakiwa na tabasamu pana.
"laiti kama mimi na mwenzangu tungekuwa tumepiga hatua kama nyie tusingekuwa tuna muda wa kupoteza kwa kulumbana sasa hivi tungeshapiga kambi kituo cha kikuu cha polisi ikiwezekana tungekuwa tushafanya mpango wa kumleta huku kisha tumpeleke kule shimoni naamini angesema mpaka jina la utani la mkuu wao" aliongea kwa utulivu ila wenye kumaanisha ASP Richard huku akiwatizama wanausalama wale kwa zamu.
"nadhani hata mimi nilikuwa nilikuwa na wazo wazo kama hilohilo alilosema ASP Richard hii kesi ya huyo binti kama inawezekana itabidi tumuambie chifu watuachie tufanye nae mahojiano huenda kuna kitu atatufungua" alifungua kinywa luteni sabina baada ya ukimya mwingi huku akitoa ushauri.
"nadhani tulikuwa tunapeana brief tu ya siku ya leo uamzi wakuhojiwa na sisi au akabaki mikononi mwa waliomkamata bado sijapata taarifa kamili kutoka kwa chifu ila kwasasa tujikitekatika majukumu tuliopeana japokuwa tayari kuna tobo la mwanga limeanza kuonekana kikubwa tuongeze bidii katika kuwtafta wahusika sahihi" alitoa maelekezo meja tumbaku ambaye pia alikuwa mkuu wa kikosi kile kilichoundwa naviongozi wa ulinzi na usalama.
IKULU( Oval house)-DSM
Saa 10:30 asubuhi
"mwambie katibu mkuu aitishe kikao na ningehitaji awepo chifu, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, nahitaji awepo mkuu wa majeshi,nawahitaji sasa hivi" mheshimiwa raisi alimpa maelekezo mlinzi wake mkuu
"sawa mkuu" akapiga salute na kutoka ndani tayari kutekeleza maagizo
simu ya wito ilimkuta chifu akiwa ofisini huku akiwazua atalipatiaje jawabu suala hili, hivo hivo hali ilikuwa hvo kwa mkuu wa majeshi ambae muda huo alikuwa anatafakari ni nanimwenye uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa kiasi hiko, akamwambia mlinzi wake aandae msafara na ilipohitimu saa nne na dakika arobaini na tano alijikuta katika chumba cha mikutano huku sura mbili zikiwa zimemtangulia na kikao cha leo kiliongezeka mtu mwingine ambaye ni waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje ya nchi, dakika iliyofuatia mlango ukafunguliwa na akaingia mheshimiwa raisi akiwa na walinzi wake.wakatoa heshima na mheshimiwa raisi akaomba waketi na ndipo alipofungua kinywa chake.
" mnajua nilichowaitia asubuhi hii au mmeshadokezwa chochote, chifu vipi watu wako wa nje hawajakuingizia ripoti yoyote ya usalama wa nchi nje ya mipaka?
"kiukweli mheshimiwa tume focus kwenye haya maswala pamoja na kukimbizana na siku hizi ulizotupa ili tukimbizane na muda mheshimiwa sijui chochote huenda kama kuna taarifa itanifikia muda wowote kuanzia hivi sasa" aliongea chifu akiwana unyenyekevu mkubwa.
"tusikilizane saa moja lililopita ubalozi wetu ulioko burundi umelipuliwa kwa mabomu, na sasa hivi nauliza kuhusu taarifaza leo hakuna hata mmoja wenu aliye na ripoti kamili ya nini ni chanzo cha haya yote kutokea, nadhani kama kuna mmoja wenu anahisi kwamba kupitia misuko suko ya namna hii ntaanguka......nisiwafiche wazee wangu mimi haya hayajanirudisha nyuma zaidi nyinyi ndiyo mtapoteza vibaruavyenu na mtarudi mikoani kwenu kwa aibu, chifu tusikilizane idara yako ina shida kubwa sana japo ni idara ninayoitegemea kama jicho langu ila tunapoelekea ntaivunja idara hii nakutengeneza ile ambayo itaendana na kasi ninayo ihitaji mnapewa mabajeti makubwa alafu hakuna kitu" alisema raisi kwa kufoka sana.
"sasa ni hivi kuanzia hivi sasa jukumu zima la kusimamia upelelezi wa haya mambo na kuyaletea ufumbuzi nimemkabidhi mkuu wa majeshi, najua ndani ya jeshi kuna idara ya ujasusi waende wakafanye kazi hiyo kwa weledi na uharaka ambao ripoti zote zitanifikia mara moja, sitohitaji kusikia watuhumiwa wamekimbilia nje ya nchi au wapi ila nitakachohitaji ni kusikia watuhumiwa wamekamatwa au wote wapo kuzimu nadhan itumeelewana" alisema mheshimiwa raisi kwa kufoka huku akiwatazama wakuu wale. kisha akasimama akiwa amewekwa katiikati na walinzi wake kisha msafara wake ukaelekea katika makazi yake kwani mambo yanayoendelea kiukweli yanamchanganya sana.
"chifu nimepewa hili jukumu ila tambua kwamba mbali na kuwa idara ya ujasusi ya jeshi ina vijana hodari na wazuri katika medani za upelelezi, ila naona kabisa bado ninahitaji msaada wako mkubwa mbali na kuwa tumetengeneza timu ila ifike muda tutengeneze timu ndani ya timu itakayofanya kazi kwa haraka sana."
"ni timu ya aina gani unayohitaji CDF, hili suala litakuja kuchukua sura mpya huko mbeleni tutashindwa kutazamana katika nyuso zetu, umesema nikusaidie katika kulitatua hili ila mimi nitakushauri kwamba katika ulimwengu wa ujasusi kuna kitu kinaitwa bahati, ni kaama unavyocheza mchezo wa chess au draft jenerali pale unapocheza kete mbaya na kwa bahati iliyo mbaya hakika utajutia kwanini ulisukuma ile kete" alisema chifu huku akivuta pumzi nyingi sana
"ntahitaji kustaafu kwa heshima mara tu hili suala litakapoisha tena chini yako jenerali ila tunapopanga kulimaliza hili suala na umesema una vijana wengi tena hodari je wameweza kuja na suluhisho la kilichotokea kwenye kambi yako kule Mafinga? hilo la kwanza je unatambua uliniletea vijana wako wawili ambao kama ulikuwa hujui kwenye ile timu nina vijana wangu watatu ambao nina uhakika kabisa hata wakuu wao hawawajui na hiyo yote unajua sababu? hutakuwa na jibu ila kiufupi nikwamba katika idara zetu kuna hujuma nyingi sana" aliongea tena chifu kwa utulivu wa hali ya juu

"idara ninayoiongoza ndiyo mhimili wa ulinzi katika taifa hili vile vile vijana wako wengi katika idara yako ya ujasusi ya jeshi, wengi ripoti zao zinanifikia mezani kabla hazijafika mezani kwako, nakwambia yote haya ili utambue kwamba kazi uliopewa ina uzito kiasi gani? na mimi siwezi kukubali mtoto wa mwalimu aliyenifundisha mbinu za kimedani akidondokea pua."

muda wote huo CDF alikuwa akimsikiliza tu, bila kutia nenokwa maana alijua kazi aliyopewa ni ngumu sana kulinganisha muda na siku zinavyozidi kuyoyoma bila kupata mwanga, hivyo alikuwa akikutegemea chifu na idara yake kumsaidia kufikia majibu.sahihi na kwa wakati sahihi
"ukimya wako unanipa picha kuwa tuko pamoja katika haya ninayokueleza sasa basi katika timu ya watu wachache uliotakiwa uunde ikuletee majibu sahihi na wakati sahii basi usiache kuwachukua vijana ntakaokutumia majina yao kwenye barua pepe vile vile ile timu ya mwanzo isijue chochote mimi ndiyo ntajua jinsi ya kuivunja, nadhani tumeelewana ndani yasaa moja kutoka hivi sasa utafungua barua pepe hiyo na chondechonde kama unataka kufikia majibu ya mambo hayo ni kubaki kama hujui kitu, nakwambia hivo kwasababu nimeshanusa harufu ya hujuma hapa"
********************************
Tuweke kituo hapo huku tukijiuliza
Je hiyo barua pepe inahusisha watu gani, Je hao wasaliti Chifu alionusa harufu yao watajulikana na je? Kwa murndelezo wa matukio ndani ya siku kumi na nne watamaliza kazi hii nzito Nisome tole lijalo Tchao
 
NAPENDA NICHUKUE FURSA HII KUENDELEA KUWASHUKURU WANA JAMII FORUMS KWA KUENDELEA KUYASOMA MAWAZO YANGU KATIKA SIMULIZI HII YA KUSIMAMIA PIA NAKARIBISHA MAONI NA USHAURI ILI KUBORESHA ZAIDI NA ZAIDI ILI TUENDELEE KUPATA PICHA HALISI KWENYE FIKRA ZETU KUPITIA MAANDISHI.FUATANENI NAMI
Viongozi wale wakaagana kisha kila mmoja akaingiakwenye gari lake na kisha wakaondoka na kila mtu na msafarawake kurudi ofisini kwake kuendelea na majukumuyanayoendelea kupasua vichwa vya viongozi wale
SURA YA TATU
SANAA YA MAISHA KATIKA JAMII.
KIJIJI CHA KISANGURA-SERENGETI DISTRICT
Saa 2:15 asubuhi.
"mwalimu Musa naona leo upo mbio mbio shida nini? umeshinda biko nini?"
"hapana mwalimu janet kuna maswala nashughulikia hapa sema naona muda umekuwa jinai kwangu kila sekunde inayopita nahisi ni askari wananitafta wanikamate, na mimi najitahidi niwe mbele ya huo muda madam janet"
" nkipata kaupenyo ntakupigia tuzungumze madam janet achaniwahi kipindi nkawafungue hawa wadogo zetu ubongo waijuenchi yao"
"sawa mwalimu mwenye somo lake la civics......ila mwalimu Musa samahani naomba nkuulize kitu nsamehe sana kama litakukera" alissema hivo madam janet huku akimtazama usoniakitarajia mabadiliko ila hakuona chochote isipokuwa tabasamutu.
"haina tatizo uwanja ni wako madam janet" alisema hukuakiendeleza tabasamu lake lile lile
"kwanini ulichagua kufundisha somo hili wakati wanaume wengi wamezoea kufundisha masomo yale magumu magumumfano si unaona mimi nafundisha kiswahili tu."
"hahahahaha ntakujibu swali lako mara nitakapotoka kuwafundisha kidato cha tatu maana leo nina mzuka sana wakufundisha, ngoja niwahi mood isijekukata madam janet."
mwalimu yule alionekana kupiga hatua za haraka kuwahikipindi chake hicho ambacho kilikuwa cha kwanza kwa siku hiyo kwa wanafunzi wa kidato cha tatu, na ndiyo kipindi cha kwamza tangu shule ilipofungu siku hiyo kuanza muhula wapili, hali ya darasa ilikuwa ya minong'ono iliyochanganyikanana kelele huku lugha iliyokuwa inazungumzwa ni ya kabila la kikurya kwa asilimia kubwa kwa wanafunzi wa kiume na wakike, upepo wa ukimya ukafuata huku kelele zile zikiendalikizo baada ya mwalimu Musa kusimama mbele ya darasa akawatizama akatikisa kichwa kwa masikitiko kwamba ana kaziya kufanya japo ni darasa lililoonekana kuwa na vipaji kwenye engo ya michezo ila upande wa taaluma darasani ni watu kumi tu ndiyo walionekana kuwa na mwanga kwenye masomo waliobakia taaluma kwao lilikuwa giza zito kwenye macho yaona hawakujisumbua kulitoa giza hilo kwani waliridhika na hali hiyo.
"GOOD MORNING SIR"
"GOOD MORNING CLASS, HOW WAS THE HOLIDAY" kufikia hapo wengi waliangaliana wakitegea kufatilizia sauti yawatakaojibu.
"WAS FINE"
"OKAY YOU MAY SIT"
akaandika mada anayoenda kufundisha, katikati ya ubao chakavu yalisomeka maneno 'POVERTY' kisha akawageukia wanafunzi na kuwaambia.
"mbona mnanitazama hivo.....mada ya leo tutaijadili kwa pamoja nasema hivo kwa sababu hata mimi nataka kuongeza kitu kutoka kwenu, kwa ambao hamjui lugha ya malkia hilo neno linamaanisha "UMASIKINI" heey kule nyuma tunaelewana .
"NDIYOOOO" zilisikika sauti nzito za wanafunzi hao wa kiume na kufanya darasa liangue kicheko kilichodumu kwa sekunde kadhaa kisha ukimya ukarejea.
"zakaria unaelewa nini kuhusu umaskini au neno umaskini" aliuliza swali lililomlenga mmoja ya wanafunzi wale waliokaa kwenye siti za nyuma inayetambulika kwa jina la zakaria, kijana mwenye umbo la kawaida na jina lake liliingia katika kumbukumbu za mwalimu huyo baada ya kumkosha kwa uchezaji wake wa mpira katika timu ya shule, ndiye mfungaji tegemezi wa timu hiyo, leo alikuwa akiulizwa swali kupimwa uelewa wake huku wanafunzi wakisubiri atajibu nini.
"khoo khoo alikohoa kidogo kulainisha koo lake kisha akaendelea kwa lugha ya kiswahili kilichoelekea kunyooka ila yenye rafudhi ya kikabila
“UMASIKINI ni ile ya mtu au watu kushindwa kujipatia mahitaji yake muhimu kama chakula,mavazi bila kusahau malazi" kisha akaketi mwalimu alimtazama kisha akayagandisha kwa mwanafunzi wa kike aliyekuwa katika vazi nadhifu la shule
"Ghati wewe una maoni gani kuhusu jibu la zakaria au unakubaliana nae" alisema hivo mwalimu akianza kulichangamsha darasa hilo kwa mjadala huo,
"nakubaliana nae kwa upande mmoja ila kiuhalisia halijakamilika" ikafuatia miguno na minong'ono iliyodumu kwa dakika nzima kisha mwalimu akawatuliza ili mwanafunzi yule aweze kumaliza hoja yake nae bila kusita na kwa ujasiri akaendelea kuitetea hoja yake.
" mwenzangu ameongelea umaskini katika mlengo mmoja, kauzungumzia umaskini kuwahusu watu au mtu mmoja mmojal akini hajazungumzia umaskini wa nchi, nchi pia zinakuwa classfield kama maskini ndiyo maana nkasema tafsiri yake bado haijatoa picha ya maana halisi ya neno UMASKINI"
"chacha mwisike une akili"
"matiko hata uni nimanyili musani ighaaa mkali huyo negetuna neteri"
"umobhoso naenkulotelee" mwenzake alimjibu hivo huku wakihitimisha mazungumzo hayo kumhusu Ghati kwa lugha ya kabila la walurya, walielewana kwakuwa marafiki hao walikuwa wazawa wa kijiji hicho na wote walikuwa wakurya kwa asili.
"matiko maha ekewele kelaheta" alisema hivo chacha kwa hamaniko na sauti kiasi cha kuibua hisia za darasa kutazama dirishani ma'am kulikuwa na wanyama pori Aina ya nyumbu walikuwa wakipita karibu na eneo Ile ambalo mbele yake kidogo kulikuwa na kabwawa kadogo kalikotumika kunyweshea mifugo maji na nyumbu wale walikuwa wakielekea huko kwaajili ya kupooza kiu Chao na kupita Kwao shuleni pale kulileta taharuki wanafunzi wa kike kwa kiume walipita madirishani ilikujaribu bahati zao kama watapata kiteo huku wakiungana nawanakijiji wa pale walioshika silaha za jadi wakijaribu kuwaangusha nyumbu wale watatu.
"hii ndo maana ya umaskini... Kama taifa kiukweli linasafari ndefu Sana kuwapata wasomi sahihi" alijiwazia mwalimu Musa huku akikusanya vitabu vyake huku madawati pekee ndo yaliokuwa yakimuangalia tofauti na mwanzo alipofika darasani pale ni nyuso za bashasha ndizo zilimpokea ili Sasa alikuwa analiacha darasa likiwa tupu na mada yake ya umasikini ikiwa bado inang'aa ubaoni akatikisa kichwa na kujilaumu kufundishakwenye shule Ile.
"Mwalimu mbona umerudi kabla ya kipindi chako kuisha.....umepatwa na nini"
"madam hivi mnafundishaje wanafunzi wasiojali hatma za ndoto zao"
"Mmmhuh..mwalimu Musa wamekukimbia darasani wanafunzi nini?"
"matoto mengine yalikuja kukua tu Tena mengine Yana mitihani kesho kutwa yanaacha kusikiliza eti yanakimbiza nyumbuu tadhani Rambo kawaona wanamgambo wa vietnam" alisema hivyo mwalimu Semeni aliekuwa amesimama mlangoni katika ofisi Ile ya waalimu wa shule hiyo ya sekondari.
"umasikini ndiyo chanzo cha haya yote na wala hata siwalaumu wanafunzi" alisema mwalimu Musa huku huku akipanga vitabu vyake tayari kwa kuondoka shuleni hapo,
"shauri zao kikubwa mwisho wa mwezi naenda wilayani kuvuta maokoto yangu nabadilisha na mboga basi Maisha ni buly buly kwanza mtoto wangu siwezi kumsomesha shule za bure " aliongeza mwalimu semeni kwa madaha huku akiendelea kuperuzi kwenye simu yake aina ya Samsung S9.
"Janani Mimi wacha nifike nyumbani nkapumzike kidogo" alisema mwalimu Musa.huku akiondoka ofisini pale kwa mwendo wa taratibu.
"Huyu nae anajifanya Ana mzuka wa kufundisha....wanafunzi wenyewe wale mbona atachoka kabla ya muda hehehehe" aliongea mwalimu semeni kwa kebehi
"shoga yangu mimi mwenyewe sioni jipya naenda zanguwilayani kufatilia mkopo wangu"
"ukipata kitu kizuri niletee basi"
SAA12:15 jioni
***********************************
Kunani saa 12:15 jioni, unahitaji kufahamu? Hahahahaha hata mimi sifahamu tukutane kesho panapo majaliwa
 
USIPENDE KUAMINI HABARI ZA UPANDE MMOJA, KWASABABU UONGO UNA TABIA YA KUFIKA HARAKA KULIKO UKWELI HALISI, USISHANGAE KWASABABU KUNA KURASA ZITAVUKWA NA MSIMULIAJI AU KUSAHAULIKA UNATAKA KUFAHAMU MAANA YA MANENO HAYA VUTA KITI KETI ALAFU NISOME………
Ilipoishia sehemu ya SITA
Huyu nae anajifanya Ana mzuka wa kufundisha....wanafunzi wenyewe wale mbona atachoka kabla ya muda hehehehe" aliongea mwalimu semeni kwa kebehi
"shoga yangu mimi mwenyewe sioni jipya naenda zanguwilayani kufatilia mkopo wangu"
"ukipata kitu kizuri niletee basi”
SONGA NAYO SEHEMU YA SABA
SAA 12:15 jioni
Huu ndiyo muda uliomkuta mwalimu Musa nyumbani kwake huku akiwa amewasha radio take akisikiliza taarifa ya Habari kupitia idhaa ya Kiswahili kutoka kituo cha Voice of amerika(Sauti ya marekani) huku mjadala mkubwa ukiwa ni shambulizi LA ubalozi WA Tanzania nchini Burundi, alikuwa akifatilia matamko ya wanazuoni mbali mbali huku wengi wakiishutumu nchi ya Burundi kwa kushindwa kusimamia Hali ya usalama kitu kilichopelekea mashambulizi hayo huku Wengine wakienda mbali na kuihusisha serikali hiyo na mashambulizi hayo kwasababu hakuna hata mtu mmoja aliyetiwa mbaroni kwa kitendo hicho.
"ticha shikamoo.....mbona kama una mawazo nimekuletea mboga jioni upike" aliongea zakaria moja ya wanafunzi waliokuwa karibu na mwalimu Musa na waliishi kama kaka na mdogo wake
"hiyo mboga ndiyo ilikufanya ukaruka dirisha na kusahau kile ninacho kusisitizia kila siku"
"hapana mwalimu sio sababu ya mboga ila.......ni familia yangu mwalimu napambana huku na huko ili mradi tu tupate walau milo miwili kwa siku lakini usisahau ticha mimi ndiyo kijana wa kwanza hivo nyumbani wananitegemea"
"bado hujanipa sababu ya msingi kwanini ulikimbilia nje wakati nafundisha.....zaka huo si ni utovu wa nidhamu tena wa wazi kabisa umeona haitoshi umekuja kunitukana kwa kuleta hiyo mboga unaniambia nipike usiku" aliongea mwalimu musa akiwa amekasirika mategemeo yake alihisi ataonekana shujaa ila matokeo yake ikawa tofauti
"wewe ni mhujumu uchumi kama walivyo wengine.....unaniletea hii nyama ili nishiriki katika dhambi yako......unahisi wakija askari hapa wakaikuta hiyo nyama si utaniharibia kabisa kazi yangu pamoja na maisha yangu, sikiliza mdogo wangu kwa makini kama huwezi kunipa walau robo ya heshima yangu ni heri usiwe unatia mguu hapa, nafumba macho nkifumbua uwe umepotea kabla sijakufanya ujutie kuingia kwenye mikono yangu" alifoka tena mwalimu musa tena kwa jazba sana
zakaria aliondoka mahali hapo akiwa mwenye uoga sana maana kwasababu hajawahi kumuona mwalimu huyo akiwa katika hali hiyo njiani alikutana na rafiki yake aitwae Marwa
"inakuwaje zaka mbona kama umebeba mfuko wenye vitu vitamu vitamu"
"ni kweli ndugu yangu ila nilikuwa nimempelekea ticha musa ilaikawa tofauti huwezi amini alinifokea sana na kaikataa kabisa wakati sio kawaida yake kuwa vile huenda kuna vitu vinamchanganya"
"sikia zaka huenda umemkuta ashasizi mibangi ndiyo maana.....wewe tufanye hivi kuna yule bibi pale bondeni tukamuuzie tupate hela ya kuchezea bonanza mshikaji wangu"
"hivi una akili wewe unadhani hizi pipi unauza tu si bora niirudishe nyumbani tu itatusaidia siku mbili tatu"
"haya bhana wewe mwenye akili umefika wapi acha ujinga wewe changamkia fursa acha mawazo ya kimaskini mshikaji wangu"
zaka hakutia neno zaidi ya kukaza mguu na kuzipiga hatua ndefu zilizomfikisha nyumbani kwao huku akiwa na mawazo huku akijiapiza kuwa siku itakayofata atakwenda kumuomba mwalimu wake msamaha
wakati hayo yakiendelea huko mjini mambo yalizidi kupambamoto vichwa vya magazeti vilipamba taarifa za mashambulizi ya ubalozi wa Tanzania nchini Burundi huku viongozi wa ngazi za juu wakipendekeza maofisa wa kwenda kufanya uchunguzi huo huku taarifa za awali zikieleza hata maafisa waandamizi wa ubalozi ule hawakujulikana walipo huku mwili wa afisa usalama wa ubalozini ulikutwa ukielea kwenye kingo za mto nchini humo, mbali na kifo hicho pia ulikutwa mwili wa afisa aliyetumwa kufanya uchunguzi ukiwa umefungwa kwenye buti ya gari alilokodi kutumia kwa shughuli hiyo hiyo ilikuwa kama ujumbe kwamba adui yupo sebureni kwao na anapiga hatua pamoja nao.
"chifu hili suala mbona limeanza kunipasua kichwa kiasi hiki"
"jenerali siku zote ukiona giza linatanda ndiyo mwanzo wa mapambazuko......kuna kijana wako mmoja anafaa kwenye hili"
"kijana wangu.......mbona sikuelewi chifu unanichanganya"
"huwezi kunielewa kwa maana kijana huyo hayuko kazini kwa sasa na yupo mahali anaendelea na mambo yake mengine, ni kijana niliyemtengeneza mimi na nina mfahamu vizuri sana laitika majukumu hili ningekuwa nimepewa mimi nisningesita kumuita katika hili, ni mmoja wa majasusi niliowatengeneza wakafika viwango mithili ya El cohen yule jasusi wa mossad, Nikita wa KGB, ki ufupi ni kiumbe hatari sana kuwahi kutokea katika vyombo vyetu nilishangaa sana mlivyomuachia kirahisi komandoo na luteni kanali yule kirahisi hivo"
"siajajua unazungumzia nini kwakweli chifu bado unaniacha njia panda "
"huwezi ukanielewa ila utanielewa pale utakaposoma "FAILI JEUSI" kwa maana sidhani na ujenerali wako katika kipindi ulichokaa ofisini kama uishawahi kusoma au kugusiwa japo habari kiduchu kuhusu yaliyomo kwenye faili hilo" upande wapili wa simu ulivuta pumzi ndefu na kuzitoa.
"na imani mpaka saa 2 usiku utakuwa umesoma na kukielewa kilichomo na ntakuja kwenye makazi yako" alisema chifu nakukata simu hapo hapo jenerali aliinua mkonga na kumpigiamsaidizi wake.
"nalihitaji"FAILI JEUSI" ofisini kwangu sasa hivi"
"what..............'
"hujasikia au dharau sikiliza tena ‘NALIHITAJI FAILI JEUSI HARAKA IWEZEKANAVYO"
"mkuu sidhani kama simu hii ni salama kuijibu nahitaji nije nkupe maelezo kuhusu faili hilo ofisini."
******************************
Faili Jeusi lina nina nini? Na linahusiana na kitu gani? Je wataweza kuwasha mwanga kwenye giza hili zito la wasaliti na wazandiki wa taifa lao……..tukutane toleo lijalo
 
BABA WA TAIFA LA TANZANIA MWALIMU JULIUS K. NYERERE, ALIWAHI KUSEMA KWAMBA “HESHIMA NA TAMAA HAVIKAI CHUMBA KIMOJA, CHAGUA KIMOJA” MMMHHH MSEMO WENYE KISU KWA KILA PANDE ILIYOCHAGULIWA NA MHUSIKA. UNATAKA KUPATA JIBU NA PICHA YA HILI JAMBO UNGANA NAMI KATIKA MUENDELEZO HUU.
Ilipoishia……..
"mkuu sidhani kama simu hii ni salama kuijibu nahitaji nije nkupe maelezo kuhusu faili hilo ofisini."
JIPAKULIE
tukutane kwenye maegesho baada ya dakika tano" alisema hivohuku akiakata simu na kumtaarifu mlinzi wake kuandaa msafara tayari kwa kwenda nyumbani kwake alitazama saa yake yaukutani na ilionesha imekwisha kutimia saa kumi na mbilikasoro akatizama ofisi ile nakuiacha huku akiwekwa kati nawalinzi wake tayari kwa msafara wa kwenda nyumbani kwake.
naomba mnipishe nina mazungumzo muhimu" aliongea jeneralihuku akiwatazama walinzi wake na dereva wa gari lake, wakasogea pembeni wakitii amri ya mkubwa wao.
"niambie ni kitu gani kinaendelea mpaka faili hilo hujalifikisha ofisini kwangu" aliongea jenerali huku akimkazia macho msaidizi wake.
"Mkuu FAILI JEUSI lilipotea katika mazingira ya kutatanishasana na hata aliekuwa akilihifadhi kapteni masiaga pia hajulikani ni wapi alipo na hakuna anaejua kilicho kuwemo ndani yake zaidi ya watu watatu, jenerali aliyepita, chifu wa sawa sawa idara ya ujasusi na kanali masiaga ambaye alikuwa katibu wa jenerali na pia inasemekana ni nyaraka ya siri sana ambayo hata raisi mstaafu na huyu wa sasa hawajui kilichomo zaidi ya viongozi hao wa vyombo vya ulinzi na usalama na ndiyo maana hata wewe umenishangaza sana ulipoliulizia mkuu"
"mbona mnanichanganya sana na hizi habari mpya na umesema chifu wa sasa anajua kuhusu faili hilo"
"ndiyo mkuu na habari hiyo niliisikia katika siku za mwisho mwisho kuonekana kwa kanali masiaga na ilikuwa kama bahati kwangu baada ya kukuta akiongea na watu hao ofisini kwa jenerali na niliyasikia kwa bahati mbaya na mara baada ya kugundua nimesikia maneno machache kanali masiaga akinambia nibaki na siri hiyo yenye maneno machache tu niliyoyasikia na siku ntakaofungua mdomo wangu tu ndiyo siku ntakayokutana na shetani macho kwa macho" aliongea maneno hayo kwa sauti ya kitetemeshi luteni usu yule akiwa hana uhakika wa kuishi baada ya kusema siri Ile aliyo onywa asiwahi kusema popote na watu wale wenye nguvu kipindi kile na hata sasa.
"Nimekuelewa kijana na chukulia kama hujafanya mazungumzona mimi na siku hii haijawahi kutokea maishani kwako nakingine cha kuzingatia hata kama Kuna mtu alikuona kwa bahati mbaya basi uwaambie ulikuwa na shida binafsi na mimi.... Unaweza kwenda" alimaliza jenerali huku luteni yule akiteremka kurejea kwenye shughuli zake ofisini huku jenerali akiendelea na msafaara wake.
"tuelekee nyumbani nahitaji kupumzika na saa mbili ntakuwa na kikao na chifu hivyo waambie Vijana waimarishe ulinzi"
"Sawa mkuu ntatekeleza" alisema mlinzi mkuu wa jenerali.
****************
Wakati hayo yakiendelea watu wanne waliosadifu ukwasi wanao umiliki walikuwa katika sebule wakisherekea kitu Fulani, Kwani walizungukwa na Meza iliyobeba pombe za bei ghaliSana huku mabinti warembo wakiendelea kuikanda miili Yao ilimradi tu watimize maana ya. neno starehe.
"chatu amenipigia muda ule anausifu Sana utendaji wetu wa kazi, na ameniambia kama wataendelea kumkatalia basi Kuna zawadi Yao amewaandalia na amenihakikishia wataipenda watake wasitake hahaha"
"una nini wewe nae ukishalewa kidogo mambo ya chumbani unayaleta kwenye mkutano wa Kijiji hebu furahia au Binti ameshindwa kazi yake"
"Hapana hapana sijakusudia kuyaleta hapa ila nilikuwa nakujulisha tu"
"nimekuelewa nenda kapumzike"
"mapema yote hii anyway haina shida tajiri" aliposema hivo wenzake Wakamcheka Sana huku wakisema bwana yule Hana kichwa cha pombe
"umefikiria nini mpaka kumruhusu yule mjinga akaondoka na Malaya una uhakika akipewa miuno feni hawezi kuropoka mkuu" mlinzi wake alimnong'oneza hivo.
"Kobe nina mfahamu vizuri usiwe na wasiwasi nae"
"Sawa mkuu"
"Asante kwa kujali" alisema hivo huku akinyanyua glasi nakuipiga funda Zito la pombe Ile brand ya Jack Daniels
MWENGE-DAR ES SALAAM
Saa1:45 jioni
" Askofu bwana yesu asifiwe"
"Amina kondoo wa bwana.......naona Leo umeona uje kwenyeIbada ya jioni Diana"
"ni sahihi baba askofuila najua unatambua kilichomkuta Vanessa na unajua athari sake ni kubwa kiasi gani kama wakimtapisha kwa njia zao naamini hakuna atakayesalimika"
"unadhani chatu atakubali Hilo litokee nadhani unajua jinsi hayamambo yalivyo katika mpangilio na Kanika maagizo jumapilihii ntaenda kutimiza kile tulichokiongea na chatu so unatambua jinsi nilivyo na ushawishi hivo jumapili ntaenda kumpakamatope yule mwanamke huku kama kanisa tutamshinikiza Vanessa aachiliwe Mara moja na usisahau yeye ndiyo Ana nusuya mpango kazi wa kumuangusha kile kimama pale nyumba nyeupe"
"kuwa makini Sana baba askofu mbwa wamesambazwa Sana mjini na kazi Yao ni kunusa chochote kinachotokana namipango yetu na ninavosikia oparesheni nzima inasimamiwa najeshi"
"hahaha Binti Landa tu kama huelewi huu mpango ulisukwa nawatu wajuzi Sana wa mambo wewe kwa kwa kutulia na uonenchi yako inavyokwenda kama Gari bovu na dereva wake Hana siku nyingi za kuvuta hewa hii ya bure"
Ni Saudi ya mlango kufunguliwa ndiyo uliowatoa katika maongezi Yale Mazito na kubadilisha mada kiasi cha kumfanya muinjilisiti yule kutokuelewa chochote kile.
"baba askofu ndoa yangu imefikia pabaya imefika muda mpaka mme wangu hataki nije hapa badala yake anataka nimsindikize kwenye masuala ya ushirikina na mimi nimeokoka nisaidie kwenye hili." Aliongea mwanamke yule huku akiwa na sura yah uzuni na iliolawana kwa machozi huku ikiambatana na kiliocha kwikwi kitendo kilichomfanya hata muinjilisti kulaani kituhicho na kumsisitizia asianguke na kuiacha Imani yake na hata akiona matendo hayo yamezidi asisite kuomba talaka na kanisa litakuwa na Baraka zote kufanya hivo.
"nenda Mimi ntawasiliana na mme wake na jumapili jioni mtafika kanisani hapa nipate kusikia nae anasema nn Kisha ntawaombea nyote kwa pamoja.....unaweza kwenda kwa amani kondoo wa bwana.”
"nashukuru baba Askofu ngoja niwahi nisije nkatolewa masikio mwanaume mwenyewe Ana wivu kama mini?" Alimaliza kwa kung'aka na kuvuta mlango wa ofisi Ile na kuondoka katika jengo LA kanisa lile la JEHOVAH AMESHINDA.
********************************
KATIKA MAISHA KILA MTU ANA HADITHI YA UPANDE WAKE WENYE NGUVU AU UKAWA NA CHAGUO LA KUZAMA AU KUOGELEA ITATEGEMEANA NA KIWANGO CHA UVUMILIVU ULICHONACHO UISHIE KWENYE MAUMIVU YA NADHIMU AU UCHAGUE UPANDE WA MAJUTO UWE UNAJILIZA MPAKA UNAENDA KABURINI,……… SASA TUCHANJE MBUGA.
 
USIWAHI KUWAOGOPA WATU KWA KUCHUKULIA VILE WANAVYOKUFANYIA IWE MEMA AU MABAYA NA KURUDISHA SAWIA NA VILE WANAVYOKUFANYIA, KWA SABABU GLASI NI CHOMBO KIZURI CHA KUWEKEA KIMIMINIKA CHA MAJI MAJI ILA NI HATARI PALE INAPOVUNJIKA, BADO HUJAELEWA, USPIPATE TABU UNGANA NAMI UPATE KUELEWA.
Ilipoishia SEHEMU YA SABA
nashukuru baba Askofu ngoja niwahi nisije nkatolewa masikio mwanaume mwenyewe Ana wivu kama mini?" Alimaliza kwa kung'aka na kuvuta mlango wa ofisi Ile na kuondoka katika jengo LA kanisa lile la JEHOVAH AMESHINDA.
VUTA KITI TuENDELEE NA SIMULIZI
SEHEMU YA NANE
Wakati hayo yakitukia huko upande mwingine wa jiji eneo la Masaki lilipata ugeni mzito wa chifu wa idara ya ujasusi yaTanzania, picha lilianza kwa umeme kukatwa huku gari tatu brand ya Land cruiser(LC300), zenye rangi nyeusi zilipita kwa mwendo wa kasi kiasi cha kufanya ushindwe kuelewa waliokuwemo na pia kulingsna na muda ule ukichangwiza na kiza kilichokuwa kimeanza kushika hatamu na ni sahihi kwamba kwa mtu wa kawaida anaweza kujisifu anaona ila kwa Hali Ile hakuna ambacho angeona labda tu wale watu wachache ambaowamepitia mafunzo ya Hali ya juu ya kimedani za kulifanya Giza Zito kuwa kama mchana na kuweza kung’amua kilichojificha kama tu anatazama kitu kwenye Mwanga wa Jua ingali ukiwa umetamalaki. Dakika sio nyingi umeme ulirejea huku gari zilishapotelea kwenye geti la jumba Fulani huku Hali ya utulivu ikiwa imetamalaki kwenye kitongoji hiko.
"jenerali Habari za muda huu"
"Salama chifu nadhani tutembee tembee tukifanya mazungumzo kwa maana hata kuta siku hizi zina masikio" aliufukuza ukimya Chifu mara tu alipomtia machoni jenerali
"hahahaha tangu lini hayo masikio yakaota kwenye nyumba ya mtu anaeogopwa na kuanzia sisimizi hadi hadi na cabinet.....hehehe basi isiwe shida Chifu tunyooshe miguu" walivyonyanyuka walinzi wakitaka kuwasindikiza ila wakagoma vigogo wale wenye maamuzi magumu katika nchi hii kila siku linapoamka Jua mpaka linapomka tena.
"sikufanikiwa kushika achilia mbali kilichopo kwenye ‘FAILI JEUSI’chifu kiufupi nimechanganyikiwa sababu kumeanza tabia ya upotevu wa nyaraka muhimu Sana na za Siri ndani yajeshi, na jenerali hajulishwi chochote kuhusu upotevu huo, je zikiuliziwa nyaraka zingine za nchi zikakosekana si wataninyonga Mimi kwa kukihisiwa nimeisaliti nchi na kiapo na Kuiasi nchi.....hebu nifafanulie chifu ni kitu gani kinaendelea"aliongea jenerali kwa unyenyeku mkubwa huku akisubiri Majibu ya hiko kinachomuumiza kichwa
"FAILI JEUS’I liliibiwa miaka mitatu nyuma kabla ya uchaguzimkuu, nyaraka zilizomo ndani ya jalada Hilo zilikuwa zikiwahusu Vijana wanne ambao naweza kusema walikuwa the best katika idara ya ujasusi ijapokuwa wote ni vijana wangu, na ilipokuja kujulikana wana kofia mbili yaani ya kwanza ni komandoo kutoka kikosi cha wanamaji (navy) ambao walikuwa ni special force haswa lakini vile vile ni ma ajenti kutoka idara ya ujasusi na walikuwa na Code name ambazo ni idara ndiyo ilipendekeza yawe hivo bila jeshi kujua ni watu wangu.
Wakati wa vita ya nchi ya Congo na waasi wa kundi la M23, ni kikosi hiki ndicho kilipeleka vilio kwa Familia za waasi wale nakurudisha baadhi ya sehemu zenye vyanzo vya Maputo katika serilali ya Congo huku wakibeba kiasi Fulani hivi cha vifukovya dhahabu na hapo ndipo kilipotumwa kikosi cha Siri Sana kwa lengo LA kuwamaliza watu wale wanne , kilichotokea Kule Congo kilitisha Sana maiti mbili Kati ya nne zilipokelewa uwanja wa ndege, vijana wa kikosi kile cha siri ndani ya serikali iliyopita walirudi na madini badala ya wale waliotumwa mwanzo " akameza mate kulainisha koo kisha akaendelea.
"na imani mbali na wewe kuwa jenerali wewe ni jasusi na usisahau code name yako ni "Shepherd" ni sifa hiyo ndiyo ilinifanya nikupendekeze jina lako kwa mheshimwia raisi na leo hii uko hapo ulipo......actually hilo silo lililonileta naimani umegusiwa kilichomo kwenye FAILI JEUSI.
" hapana kwa kweli chifu bado sipati muunganiko kiufupi moja haikai mbili haikai"
"hahahaha huwezi kuelewa jenerali mambo haya yalifanywankwa usiri na ndiyo maana hata baada ya kushika hatamu ya ujenerali ilibidi faili lile lihamishwe kwa sababu ya hicho ulichonacho kilichofanya idara ikupe code name ya"shepherd ", watu waliolihamisha hawakutaka kabisa uweze kunusavhata harufu ya karatasi na kilichoandikwa na kiufupi nakwambia haya kwa maana mambo yamekwisha kuharibika na adui alikuwa anacheza na kunywa sebuleni kwetu hivi sasa yuko pahali anatuchezesha kama keyboard za kompyuta.......Jenerali nimekudokeza kwamba ni maiti mbili ndizo zilitambuliwa na kuzikwa kwa heshima katika mikoa ya mbeya na kigoma. Katina kikosi kile kilichokuwa chini ya luteni jenerali Yamungu Shayo kilisalitiwa Dakika za mwisho za oparesheni, hebu jiulize Nani alikuwa na ubavu wa kumfikia luteni jenerali Yamungu jitu lile lenye Roho ya kikatili na aliogopeka hata na jenerali aliyepita ila maiti yake ilikutwa kwenye jokofu lake huku kichwa kikiwa kimechemshwa kwenye sufuria, ukatili ulioje."
Nadhani baada ya wewe kutoka masomoni nchini China ndiyo ukakalia ofisi Ile iliyokuwa ikitumiwa na luteni jenerali Yamungu, huku idara ikisaidiana na wewe beta kwa beta na utendaji wake wa kasi ndiyo uliokufikisha hapo Leo."
"kama idara ilikuwa inanisaidia kwanini hawakuwahi kuniambia kuhusu FAILI JEUSI, chifu"
"fikiria kama jasusi kuwa jambo nyeti kama lile, siyo kila mtu alitakiwa kujua hebu fikiria hata raisi mstaafu mwenyewe alikuwa halijui Nani mwingine aliweke masikioni kwake ili baadae aje kuleta usumbufu hahaha.......ninasema hivi kwamaana hata wale vijana walio wamaliza kikosi kile Kule Congo nao waliuawa kikatili na kikosi maalum cha............GrrrrrGrrrrrrr simu ya chifu iliita kwa mtetemo ndani ya mfuko wa suruali ya suti iliyokuwa imemkaa vizuri.
"Habari za Sasa hizi mheshimiwa raisi"
"Salama, chifu nimekupigia nikutaarifu kuwa kesho asubuhi ntakuwa kwenye ofisi zako nkifatilia mahojiano ya yule Binti shemeji yake na makamu wa raisi"
"Sawa lakini mbona hata jeshi LA polisi lilikuwa linaweza kumhoji tu kwani wanao vijana wazuri linapofika suala LA upelelezi"
"chifu linapokuja suala LA madawa ya kulevya Tena kwa kiwango kama kile linakuwa suala LA usalama WA taifa hebuji fikirie kama jasusi mbobevu na usitake kuniambia umekuwa mzee kiasi cha kutokufikiria nje ya box na kukumbusha Leo ni siku ya pili hujaweka ripoti mezani kwangu.......uwe na wakati mwema" ilisikika sauti nyororo ila yenye mamlaka
"saw........tititititi" kuashiria mazungumzo yameisha na Simu imekatwa
"Jenerali nimepigiwa simu na mheshimiwa raisi nadhani ngoja nkaandae mazingira maana kesho anakuja ofisini kwangu Kuna paka mmoja anatakiwa atapike samaki aliye muiba jikoni"
"Sasa vipi kuhusu hili umenipa taarifa nusu nusu alafu unaondokaje kama hivo"
"shule ya sekondari Kisangura Serengeti utapata nusu iliyobakia" akapiga hatua kuelekea kwenye gari lake
"hahaha majukumu mema Chifu" alicheka kicheko cha kuukubali uwezo wa chifu katika kufupisha mazungumzo hasa anapokuwa na majukumu nyeti.
Grrrr Grrrrrr.......simu ya jenerali iliita na aliepiga alikuwa ni mheshimiwa raisi
"jenerali"
"naam mheshimiwa raisi Habari za saa hizi"
"zitakuwa Salama pale utakapo nikabidhi watu wangu either wakiwa wanapumua au wakiwa maiti na ripoti nzima zimebaki siku kumi na mbili nilihutubie taifa LA si hivo nitawaambie wananchi mmeshindwa kuwalinda Maisha Yao na malizao........majukumu mema titititi" Simu ilikatwa huku akiachwa katika tafakari nzito huku mkanda wa kujutia kukikalia hiko kiti cha ujenerali ukipita katika fikra sake akatoa simu mfukoni
"niandalie ndege nataka kufika kufika kwanza kabla usiku hujawa mzito"
"Sawa mkuu kila kitu kiko kama inavohitajika"
"Sawa andaa msafara" Simu ikakatwa huku walinzi wake wakijipanga tayari kwa safari
Wakati hayo yakiendelea huku kijijini kisangura, Zakaria aliona akamuombe msamaha akiwa njiani alikumba na na pande LA mtu likamtupia Bahasha ndogo ya kaki na kumwambia ampeleke mwalimu Musa usiku huo huo na kama asipofanya hivo litamnyonga huku likiikamata shingo ya Zakaria kiasi cha kumfanya ashindwe kuvuta pumzi vizuri Kisha likamuachia nakuangua kicheko kikubwa na likapotea kama spidi ya mwanga machoni kwa zakaria , alikimbia kuwahi nyumbani kwa mwalimu Musa na alimkuta amekaa ndani anasikiliza mzikihuku akionekana kuzama katika msongo mawazo alisogea mpaka mlangoni.
"Ticha samahani naweza kuingia"
"wewe dogo nilikuambia mini muda ule unataka kunizoea so ndiyo" mwalimu Musa alifoka huku akionekana kukasirishwa na kitendo kile cha Zakaria Kuja Tena kwake, muda huo kilitokea kitendo cha ajabu kwani Zakaria alipiga magoti huku akitoa Bahasha Ile mfukoni huku akiinyoosha kwa mbele. Mwalimu Musa akaichana kwa juu na kudondosha kilichokuwemo ndani, kikadondoka kitambulisho chenye Jina lake halisi alilokuwa analitumia akiwa jeshini kikiwa kipya hakikuwa kitambulisho tuBali ilidondoka diski muweko ndogo aliiokota na kuingia ndanina kuwasha kompyuta yake ya mpakato na bajada ya dakika kadhaa akaichomeka diski mweko Ile na akakutana na faili dogo akaifungua na kukutana na faili LA pdf alipofunguaakakutana na maandishi "KESHO SAA 5 KINGDOM HOTEL-MWANZA CHUMBA NAMBA 104" na Kisha maandishi yalionekana kujichora kwa herufi ndogo ndogo kabla ya kutoa kamlio kadogo ka tahadhari kwamba atoe flash au kila kitukitafutika kwenye kompyuta.
*******************************
Sehemu ya nane inaishia hapa, Je? Chumba namba 104 Kingdom Hotel-Mwanza, Je? Atafika huko ujumbe unapotaka afike nini hatima ya ukomo wa matukio yanayoendelea kuiandama taifa la Tanzania na suluhisho…….. usikae mbali kwa maana
SHAMBULIZI NI KUJILINDA KWA SIRI LAKINI VILE VILE NA KUJILINDA NI KUJIANDAA NA KUPANGA SHAMBULIZI.
 
HUWEZI KUTAMBUA MADHARA YA UBAYA ULIOMFANYIA MTU MPAKA PALE UBAYA HUO UTAKAPOKURUDIA, NA KAMA MOYO WAKO NI VOLKANO IWEJE UTEGEMEE UTACHANUA KAMA MAUA, BADO UNAJIULIZA KWANINI KIPANDE HIKI KIMEANZA NA MANENO YAKUTOKUELEWEKA KWA MTU UNAYESOMA BILA KUVUTA PICHA KWA KILA NENO MOJA SENTENSI HATA KAMA HUJAELEWA FUATANA NAMI UNISOME.
ilipoishia sehemu ya nane…….
"KESHO SAA 5 KINGDOM HOTEL-MWANZA CHUMBA NAMBA 104" na Kisha maandishi yalionekana kujichora kwa herufi ndogo ndogo kabla ya kutoa kamlio kadogo ka tahadhari kwamba atoe flash au kila kitukitafutika kwenye kompyuta.
SONGA NAYO……….
Alipotoa flash Ile na kuizima kompyuta Ile ndiyo wazo LA kuwa Kuna mtu yupo mlangoni likaja kwenye fikra zake.
"aaahhh dogo zaka bado tu hujaondoka?" Aliuliza mwalimu Musa huku muda huu Sauti yake ikipungukiwa ule ukali.
"nimeogopa kuondoka Tena bila kuaga kwani sitaki utumie ule Msemo wake kuwa kosa linalojirudia Mara mbili ni kusudio(maamuzi) ya mtendaji.
"hahaha dogo zaka unajua kwanini Niko karibu na wewe kuliko mwanafunzi yoyote shuleni pale?"
" Hapana ticha ila naweza kukisia labda ni kwa sababu damu zimeendana"
"La..hasha.....hiyo siyo sababu, unajua nkikuona najisikia faraja kwa maana wewe ni mwanafunzi mwerevu Sana ila kabla yayote nataka kujua umekutana nao wapi mpaka wakakupa Ilebahasha"
"nimekutana na mtu Ana sura inatisha akanikaba akanipa hiyo bahasha na alinambia kama nisipo kufikishia Leo basi Jua LA kesho litachomoza na Habari mbaya ya msiba wangu shuleni na kijijini hapa" kufikia hapo akavuta pumzi nyingi na kuzishushakabla ya kuuliza swali.
"kwani yule mtu ni Nani au mnajuana labda na kile kikadi kilikuwa na maana gani mbona kama ni kitambulisho usiniambie umepata kazi mpya" aliuliza kwa utulivu na shauku bwana mdogo Zakaria.
"sijapata kasi mpya mdogo wangu......ila ni mambo tu ya Maisha ukipata likizo njoo Dar es salaam utayajua mengi Sana ila kwa Sasa keep focusing on studying Sawa dogo"
"nimekuelewa tich........" Alikatishwa
"Mimi sio mwalimu hii ni cover tu ya kazi yangu halisi, kiufupi taifa linanihitaji nirudi kwenye majukumu yangu ya awali hivo usiku huu huu ntakiwa niwe Mugumu tayari kwa safari ya alfajiri, hivo tutaondoka wote na Kisha wewe utarudi na pikipiki uitunze ili ikusaidie kwenye mishe mbili tatu mpaka ntakaporejea ndiyo utanirudishia hebu zunguka uwani uitoe wakati mimi najiandaa tuondoke Sasa hivi" alisema kwa utulivu mwalimu Musa huku akinyanyuka kuingia ndani.
" ni chifu ndiyo atakuwa amefichua utambulisho wangu maana hakuna ambaye alikuwa anajua kuhusu hili LA Mimi kuwa huku mafichoni, nilishaapa sitafanya hizi kazi Tena"Kubalii wito kataa neno" ndiyo neno lililopita kichwani kwake lakini alipotupa macho kwenye kitambulisho alicholetewa mwili uhlimsisimka kwamba ni Rasmi amerudi kulitumikia taifa kwani kwa kupenda au kutopenda, hakuwa na chaguo zaidi ya kupanga vitu vyake muhimu.Mpaka anamaliza alikuta Zakaria ashaiwasha tayari kwa safari.
"haupiti kumuaga madam Janet"aliuliza huku akitabasamu bwana mdogo zaka
"Hapana atanichelewesha kwa maswali ambayo Sina jibu hata moja LA kumpa na miiko ya kazi yangu hainihitaji niropoke kwa kila mtu"
"miiko ya kazi...... Mbona Kila mtu hapa kijijini anajua wewe ni mwalimu na hata madam Janet analijua Hilo"
"usilolijua ni Sawa na usiku wa Giza.....jambo unalo likomalia mdogo wangu sio saizi ya umri wako na usalama wako pia una kumhuka umekutana na mtu wa Aina gani, Sasa huyo uliyekutana nae mimi kwangu anapiga saluti......kiufupi mdogo wangu mimi ni komandoo niliyefuzu karibia mafunzo yote katika medani za ujasusi, nimepata kupita katika mikono ya mashirika ya kijasusi ya huko duniani kama CIA ya marekani, MI6 ya uingereza na lile la urusi FSB na kozi yangu ya mwisho nimeimalizia israel chini ya mossad, nimekwambia hivo kwa sababu ninakupenda kama mdogo wangu na nimekwambia ili uelewe upande wa pili wa kaka yako na kama nilivyokuahidi tukutane Dar wakati wa likizo ya kufunga muhula wa pili namba yangu ni Ile Ile nipigie wakati wowote ukiwa na shida yoyote nadhani tumesomana"
"ndiyo ticha Musa"
"siyo ticha Musa Bali luteni kanali charz busungu"
Dogo Zakaria alitumbua macho na kutetemeka kwa wakati mmoja kwani mtu aliyemchukulia ni mwalimu tu wa kawaida alikuwa na upande unaotisha Sana kwani amekuwa akiwaogopa wanajeshi na hata muda mwingine kujificha pale anapomhisi mtu ni mwanajeshi.
"mbona.unaniangalia hivo......aaahhh jambo LA msingi Kabisa kuliko hata hayo niliyokwambia na uliweke kichwani mwako na libaki kifuani kwako mpaka siku unazikwa ni utambulisho wangu, panda nyuma tuondoke muda ushasogea" alisema kwa msisitizo luteni kanali Charz busungu huku dogo Zakaria akikaa nyuma ya pikipiki na kuondoka walifika mjini majira ya saa 4 kasoro usiku na Kisha kutafuta nyumba ya kulala wageni, mji ulionekana kuchangamka kwa heka heka nyingi hasa ukizingatia ilikuwa siku ya maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru hivyo mji uliupata ugeni kutoka kwa wapiga kura(wananchi) wa wilaya na vijiji tofauti tofauti
"inabidi kesho nnapoondoka nawe uhakikishe unaitafta njia ya kisangura asubuhi ni darasani eeeennn, nahitaji utimize ndoto zako siku moja uje kuwa mtu mkubwa, Sawa dogo na usimwambie madam Janet kama tulionana usiku huu nahakikisha husogei Yale maeneo ya nyumba Ile niliyokuwa naishi kazi ikiwa nzito maadui watakuja huku Sina Familia zaidi ya Familia niliyoipata ukubwani ambayo ni wewe, ntakuingizia pesa kesho nikifika mwanza tumeelewana.
"ndiyo kaka" dogo Zakaria kwa Mara ya kwanza akamkumbatia luteni kanali charz ambaye alilipokea kwa hisia kali kiasi cha machozi kwanza kumlenga lenga, kwani katika Maisha yakeyote hajawahi kukutana na kitu hiko.
"usiku mwema nenda kapumzike una siku ndefu kesho"
"Na wewe pia kaka tutaonana saa 11 alfajiri." Alijibu hvo zakahuku wote wakiingia katika vyumba vyao katika nyumba Ile ya wageni.
Kompyuta ya jenerali ilitoa mlio kuashiria Kuna ujumbe umeingia akayafungua mafaili matatu yaliyopewa code name,akaamua kufungua faili lenye code name "ANGEL OF DEATH" na hapo akakutana na picha ya mwanadada mwenye rangi ya uweusi wa kung'aa, Jina lake lilitambulika kama CHAUSIKU JUAKALI, jasusi wa shirika LA Tanzania Secrete Service, huku akiwa na rekodi ya kutisha kwa kufanya oparesheni mbalimbali baada ya mafunzo Makali na mashirika ya kijasusi ya Cuba(DI),
alihusika na oparesheni ya idara ya ujasusi ya marekani katika kumkamata gaidi wa kundi LA islamic state aliyekimbilia Kenya katika kaunti ya Machakos, vile vile alifanikisha kukombolewa kwa majasusi wa FSB waliokwama katika magereza ya kijeshi huko Ukraine wakati WA vita hivyo na alijizoelea sifa kem kem kutoka ikulu ya Kremlin, wasifu wake unaonesha kwa muda ule alikuwa akiiongoza idara ndogo ya kupambana na ugaidi kwenye shirika Hilo LA kijasusi. Na code name hyo imetokanana kazi chafu za mwanadada huyo katika ulengaji wa shabaha kiasi cha kufananishwa na jasusi nguli wa ujerumani Gabrielle Kröcher,
Aliporidhika na maelezo hayo, akahamia kwenye faili LA pili lilikuwa na code name "MAKAVELI" hapo ndipo alipokutana na picha ya mwanaume aliyeonekana kwa muonekano wa nje tu kama mkakamavu huku Jina lake kamili akiwa ni kapteni Jumanne saidi kutoka idara ya ujasusi ya jeshi(Military intelligence) huku akiwa na wasifu ulijaa oparesheni Za kutisha katika misitu ya Congo kwa miaka miwili mfulululizo na amekuwa akitumiwa kwenda kusafisha chokochoko za waasi na baada ya hapo alihamshiwa rasmi katika ubalozi wa nchi ya Rwanda kama afisa mkuu wa ubalozi, wasifu unaeleza jinsi alivyokuwa malaika wa kifo baada ya kusambaratisha ngome ya waasi iliyokuwa imesimika mizizi yake katika jumbo LA kivu kaskazini na kusababisha kiongozi wa waasi kutorokea kusikojulikana ndipo idara ikampa utambulisho huo na kumpangia majukumu katika ubalozi nchini Rwanda.
Aliridhika na maelezo Yale kwani anamtambua ni moja ya vijana wake ambao alihakikisha wanaenda kozi za kijeshi katika nchi zilizoendelea kama China ambapo alishirikiana na idara ya ujasusi ya nchini humo yaani military secrets service(MSS) na kozi ya mwisho aliifanya nchini Cuba huku akimaliza kozi hiyo ya mafunzo ya ukomandoo kwa Alama za juu na oparesheni aliyofanya na wanajeshi wa Cuba wakiungana na majasusi wa marekani kumtafuta kiongozi wa kundi LA kigaidi LA Al qaeda huko Afghanistan, ashraf bin Mansoor iliwafanya mabosi waliokuwa wanaongoza oparesheni Ile kumuona kama malaika wa kifo( the angel of death) kwa unyama alioufanya mtu yule Hakika ilikuwa ni heri magaidi wale wangekutana na simba katikati pori lililoshona kwa miti mingi kuliko kukutana mwanaume huyo, hakukaa Sana kulisoma faili Hilo kwa maana analifahamu akafungua faili lingune lenye code name ilimfanyafikra zake kupata shauku ya kumjua mtu huyo. BLACK COBRA ndiyo code name iliyosomeka kwenye faili hlona alilifungua kwa pupa na shauku lakini hakuambulia chochotekwenye faili Hilo zaidi ya kuonekana likiwa tupu akafikicha macho yake kuwa huenda macho yake hayaoni vizuri lakini mwisho wa siku akili yake ilipitisha jibu kuwa lilikuwa tupuhapo hapo alinyanyua simu na kumpigia chifu kwani aliona anachezewa akili huku siku zikizidi kuyoyoma tu bill majibuhuku jukumu zima LA kuwatafta wahusika likiachwa kwake.
"chifu tusifanyiane utani muda wa kazi, una maana gani kunitumia mafaili nusunusu na unajua Kabisa siku zinayoyoma na hakuna lolote mpaka sasa"
"nilijua utapiga simu hii kuniuliza hivo ila nimeliacha makusud ikwa maana huyo mtu sitaki taarifa zake zijulikane popote hata kwa bahati mbaya na nkuhakikishie ntakukutanisha nae Mara tu baada ya kutoka huko ulipo"
************************************
Je ni nani huyo ambaye Chifu hataki taarifa zake zijulikane? Siku zinakimbia na hakuna majibu ya kueleweka na watu wanazunguka kwenye viti vya ofisini……….tukutane tena toleo lijalo ninakuapia hutajutia kuisoma simulizi hii TCHAO

USIWAHI KUWAOGOPA WATU KWA KUCHUKULIA VILE WANAVYOKUFANYIA IWE MEMA AU MABAYA NA KURUDISHA SAWIA NA VILE WANAVYOKUFANYIA, KWA SABABU GLASI NI CHOMBO KIZURI CHA KUWEKEA KIMIMINIKA CHA MAJI MAJI ILA NI HATARI PALE INAPOVUNJIKA, BADO HUJAELEWA, USPIPATE TABU UNGANA NAMI UPATE KUELEWA.
Ilipoishia SEHEMU YA SABA
nashukuru baba Askofu ngoja niwahi nisije nkatolewa masikio mwanaume mwenyewe Ana wivu kama mini?" Alimaliza kwa kung'aka na kuvuta mlango wa ofisi Ile na kuondoka katika jengo LA kanisa lile la JEHOVAH AMESHINDA.
VUTA KITI TuENDELEE NA SIMULIZI
SEHEMU YA NANE
Wakati hayo yakitukia huko upande mwingine wa jiji eneo la Masaki lilipata ugeni mzito wa chifu wa idara ya ujasusi yaTanzania, picha lilianza kwa umeme kukatwa huku gari tatu brand ya Land cruiser(LC300), zenye rangi nyeusi zilipita kwa mwendo wa kasi kiasi cha kufanya ushindwe kuelewa waliokuwemo na pia kulingsna na muda ule ukichangwiza na kiza kilichokuwa kimeanza kushika hatamu na ni sahihi kwamba kwa mtu wa kawaida anaweza kujisifu anaona ila kwa Hali Ile hakuna ambacho angeona labda tu wale watu wachache ambaowamepitia mafunzo ya Hali ya juu ya kimedani za kulifanya Giza Zito kuwa kama mchana na kuweza kung’amua kilichojificha kama tu anatazama kitu kwenye Mwanga wa Jua ingali ukiwa umetamalaki. Dakika sio nyingi umeme ulirejea huku gari zilishapotelea kwenye geti la jumba Fulani huku Hali ya utulivu ikiwa imetamalaki kwenye kitongoji hiko.
"jenerali Habari za muda huu"
"Salama chifu nadhani tutembee tembee tukifanya mazungumzo kwa maana hata kuta siku hizi zina masikio" aliufukuza ukimya Chifu mara tu alipomtia machoni jenerali
"hahahaha tangu lini hayo masikio yakaota kwenye nyumba ya mtu anaeogopwa na kuanzia sisimizi hadi hadi na cabinet.....hehehe basi isiwe shida Chifu tunyooshe miguu" walivyonyanyuka walinzi wakitaka kuwasindikiza ila wakagoma vigogo wale wenye maamuzi magumu katika nchi hii kila siku linapoamka Jua mpaka linapomka tena.
"sikufanikiwa kushika achilia mbali kilichopo kwenye ‘FAILI JEUSI’chifu kiufupi nimechanganyikiwa sababu kumeanza tabia ya upotevu wa nyaraka muhimu Sana na za Siri ndani yajeshi, na jenerali hajulishwi chochote kuhusu upotevu huo, je zikiuliziwa nyaraka zingine za nchi zikakosekana si wataninyonga Mimi kwa kukihisiwa nimeisaliti nchi na kiapo na Kuiasi nchi.....hebu nifafanulie chifu ni kitu gani kinaendelea"aliongea jenerali kwa unyenyeku mkubwa huku akisubiri Majibu ya hiko kinachomuumiza kichwa
"FAILI JEUS’I liliibiwa miaka mitatu nyuma kabla ya uchaguzimkuu, nyaraka zilizomo ndani ya jalada Hilo zilikuwa zikiwahusu Vijana wanne ambao naweza kusema walikuwa the best katika idara ya ujasusi ijapokuwa wote ni vijana wangu, na ilipokuja kujulikana wana kofia mbili yaani ya kwanza ni komandoo kutoka kikosi cha wanamaji (navy) ambao walikuwa ni special force haswa lakini vile vile ni ma ajenti kutoka idara ya ujasusi na walikuwa na Code name ambazo ni idara ndiyo ilipendekeza yawe hivo bila jeshi kujua ni watu wangu.
Wakati wa vita ya nchi ya Congo na waasi wa kundi la M23, ni kikosi hiki ndicho kilipeleka vilio kwa Familia za waasi wale nakurudisha baadhi ya sehemu zenye vyanzo vya Maputo katika serilali ya Congo huku wakibeba kiasi Fulani hivi cha vifukovya dhahabu na hapo ndipo kilipotumwa kikosi cha Siri Sana kwa lengo LA kuwamaliza watu wale wanne , kilichotokea Kule Congo kilitisha Sana maiti mbili Kati ya nne zilipokelewa uwanja wa ndege, vijana wa kikosi kile cha siri ndani ya serikali iliyopita walirudi na madini badala ya wale waliotumwa mwanzo " akameza mate kulainisha koo kisha akaendelea.
"na imani mbali na wewe kuwa jenerali wewe ni jasusi na usisahau code name yako ni "Shepherd" ni sifa hiyo ndiyo ilinifanya nikupendekeze jina lako kwa mheshimwia raisi na leo hii uko hapo ulipo......actually hilo silo lililonileta naimani umegusiwa kilichomo kwenye FAILI JEUSI.
" hapana kwa kweli chifu bado sipati muunganiko kiufupi moja haikai mbili haikai"
"hahahaha huwezi kuelewa jenerali mambo haya yalifanywankwa usiri na ndiyo maana hata baada ya kushika hatamu ya ujenerali ilibidi faili lile lihamishwe kwa sababu ya hicho ulichonacho kilichofanya idara ikupe code name ya"shepherd ", watu waliolihamisha hawakutaka kabisa uweze kunusavhata harufu ya karatasi na kilichoandikwa na kiufupi nakwambia haya kwa maana mambo yamekwisha kuharibika na adui alikuwa anacheza na kunywa sebuleni kwetu hivi sasa yuko pahali anatuchezesha kama keyboard za kompyuta.......Jenerali nimekudokeza kwamba ni maiti mbili ndizo zilitambuliwa na kuzikwa kwa heshima katika mikoa ya mbeya na kigoma. Katina kikosi kile kilichokuwa chini ya luteni jenerali Yamungu Shayo kilisalitiwa Dakika za mwisho za oparesheni, hebu jiulize Nani alikuwa na ubavu wa kumfikia luteni jenerali Yamungu jitu lile lenye Roho ya kikatili na aliogopeka hata na jenerali aliyepita ila maiti yake ilikutwa kwenye jokofu lake huku kichwa kikiwa kimechemshwa kwenye sufuria, ukatili ulioje."
Nadhani baada ya wewe kutoka masomoni nchini China ndiyo ukakalia ofisi Ile iliyokuwa ikitumiwa na luteni jenerali Yamungu, huku idara ikisaidiana na wewe beta kwa beta na utendaji wake wa kasi ndiyo uliokufikisha hapo Leo."
"kama idara ilikuwa inanisaidia kwanini hawakuwahi kuniambia kuhusu FAILI JEUSI, chifu"
"fikiria kama jasusi kuwa jambo nyeti kama lile, siyo kila mtu alitakiwa kujua hebu fikiria hata raisi mstaafu mwenyewe alikuwa halijui Nani mwingine aliweke masikioni kwake ili baadae aje kuleta usumbufu hahaha.......ninasema hivi kwamaana hata wale vijana walio wamaliza kikosi kile Kule Congo nao waliuawa kikatili na kikosi maalum cha............GrrrrrGrrrrrrr simu ya chifu iliita kwa mtetemo ndani ya mfuko wa suruali ya suti iliyokuwa imemkaa vizuri.
"Habari za Sasa hizi mheshimiwa raisi"
"Salama, chifu nimekupigia nikutaarifu kuwa kesho asubuhi ntakuwa kwenye ofisi zako nkifatilia mahojiano ya yule Binti shemeji yake na makamu wa raisi"
"Sawa lakini mbona hata jeshi LA polisi lilikuwa linaweza kumhoji tu kwani wanao vijana wazuri linapofika suala LA upelelezi"
"chifu linapokuja suala LA madawa ya kulevya Tena kwa kiwango kama kile linakuwa suala LA usalama WA taifa hebuji fikirie kama jasusi mbobevu na usitake kuniambia umekuwa mzee kiasi cha kutokufikiria nje ya box na kukumbusha Leo ni siku ya pili hujaweka ripoti mezani kwangu.......uwe na wakati mwema" ilisikika sauti nyororo ila yenye mamlaka
"saw........tititititi" kuashiria mazungumzo yameisha na Simu imekatwa
"Jenerali nimepigiwa simu na mheshimiwa raisi nadhani ngoja nkaandae mazingira maana kesho anakuja ofisini kwangu Kuna paka mmoja anatakiwa atapike samaki aliye muiba jikoni"
"Sasa vipi kuhusu hili umenipa taarifa nusu nusu alafu unaondokaje kama hivo"
"shule ya sekondari Kisangura Serengeti utapata nusu iliyobakia" akapiga hatua kuelekea kwenye gari lake
"hahaha majukumu mema Chifu" alicheka kicheko cha kuukubali uwezo wa chifu katika kufupisha mazungumzo hasa anapokuwa na majukumu nyeti.
Grrrr Grrrrrr.......simu ya jenerali iliita na aliepiga alikuwa ni mheshimiwa raisi
"jenerali"
"naam mheshimiwa raisi Habari za saa hizi"
"zitakuwa Salama pale utakapo nikabidhi watu wangu either wakiwa wanapumua au wakiwa maiti na ripoti nzima zimebaki siku kumi na mbili nilihutubie taifa LA si hivo nitawaambie wananchi mmeshindwa kuwalinda Maisha Yao na malizao........majukumu mema titititi" Simu ilikatwa huku akiachwa katika tafakari nzito huku mkanda wa kujutia kukikalia hiko kiti cha ujenerali ukipita katika fikra sake akatoa simu mfukoni
"niandalie ndege nataka kufika kufika kwanza kabla usiku hujawa mzito"
"Sawa mkuu kila kitu kiko kama inavohitajika"
"Sawa andaa msafara" Simu ikakatwa huku walinzi wake wakijipanga tayari kwa safari
Wakati hayo yakiendelea huku kijijini kisangura, Zakaria aliona akamuombe msamaha akiwa njiani alikumba na na pande LA mtu likamtupia Bahasha ndogo ya kaki na kumwambia ampeleke mwalimu Musa usiku huo huo na kama asipofanya hivo litamnyonga huku likiikamata shingo ya Zakaria kiasi cha kumfanya ashindwe kuvuta pumzi vizuri Kisha likamuachia nakuangua kicheko kikubwa na likapotea kama spidi ya mwanga machoni kwa zakaria , alikimbia kuwahi nyumbani kwa mwalimu Musa na alimkuta amekaa ndani anasikiliza mzikihuku akionekana kuzama katika msongo mawazo alisogea mpaka mlangoni.
"Ticha samahani naweza kuingia"
"wewe dogo nilikuambia mini muda ule unataka kunizoea so ndiyo" mwalimu Musa alifoka huku akionekana kukasirishwa na kitendo kile cha Zakaria Kuja Tena kwake, muda huo kilitokea kitendo cha ajabu kwani Zakaria alipiga magoti huku akitoa Bahasha Ile mfukoni huku akiinyoosha kwa mbele. Mwalimu Musa akaichana kwa juu na kudondosha kilichokuwemo ndani, kikadondoka kitambulisho chenye Jina lake halisi alilokuwa analitumia akiwa jeshini kikiwa kipya hakikuwa kitambulisho tuBali ilidondoka diski muweko ndogo aliiokota na kuingia ndanina kuwasha kompyuta yake ya mpakato na bajada ya dakika kadhaa akaichomeka diski mweko Ile na akakutana na faili dogo akaifungua na kukutana na faili LA pdf alipofunguaakakutana na maandishi "KESHO SAA 5 KINGDOM HOTEL-MWANZA CHUMBA NAMBA 104" na Kisha maandishi yalionekana kujichora kwa herufi ndogo ndogo kabla ya kutoa kamlio kadogo ka tahadhari kwamba atoe flash au kila kitukitafutika kwenye kompyuta.
*******************************
Sehemu ya nane inaishia hapa, Je? Chumba namba 104 Kingdom Hotel-Mwanza, Je? Atafika huko ujumbe unapotaka afike nini hatima ya ukomo wa matukio yanayoendelea kuiandama taifa la Tanzania na suluhisho…….. usikae mbali kwa maana
SHAMBULIZI NI KUJILINDA KWA SIRI LAKINI VILE VILE NA KUJILINDA NI KUJIANDAA NA KUPANGA SHAMBULIZI.
 
KAMA HUWEZI KUELEWA THAMANI YA UTII, KAMWE USIJE KUTEGEMEE UKAPATA KUELEWA THAMANI YA USALITI. LAKINI KATIKA MAISHA YOTE IPO SIKU MOJA AMBAYO UTAJIFUNZA KWA KILA USALITI ULIOFANYA, NINI? MAANA YA HAYA MANENO UNGANA NAMI KWENYE SIMULIZI HII YA KUSISIMUA.
Ilipoishia sehemu ya tisa
“nilijua utapiga simu hii kuniuliza hivo ila nimeliacha makusud ikwa maana huyo mtu sitaki taarifa zake zijulikane popote hata kwa bahati mbaya na nkuhakikishie ntakukutanisha nae Mara tu baada ya kutoka huko ulipo"

Fuatana nami katika sehemu hii ya kumi.
unataka kusema ni tofauti na huyu niliekuja kumchukua huku"
"Hahaha hauko mbali sana na jibu la swali lako huyo "BLACK COBRA" ni kwa sasa yuko kwenye umiliki wake na data zinaonesha kitambulisho chake cha kazi kiko active, sitazungumzia mtu ambaye taarifa zake nilikuelezea nusu na nusu nilikwambia atakupa yeye, nilikuambia ntakupa vijana wanne ambao wote ni serial killer wa kimataifa na Ile timu ya mwanzo nishaivunja ila elewa tu ntakupa huyo kijana mmoja ambaye hana faili hapo kwenye hizo data kesho, kama unataka kupata ripoti ya kazi nzima kabla ya hizo siku kumi na moja zilizosalia basi wasikilize wanachohitaji na kaa na utazame kazi inavyofanyika.
**************************
ARUSHA-NORTHEN- TANZANIA
saa 5:40 usiku
Pande la jitu lenye kipara na rangi nyeupe kwenye ngozi lilingia bafuni na kuiwasha simu yake, kitendo cha kuwasha simu tu akakutana na sms kutoka kwa mfadhili wao ikimtaka mpango uende kama walivyopanga na baada ya hapo atampa maelekezo mengine na baada ya kusoma ujumbe huo atajua cha kufanya. gaidi yule baada ya kuusoma ujumbe na kuuelewa aliitoa laini na kuivunja vunja kisha akatupa simu katika sinki la choo na kuflashi kwa maji mengi kiasi cha kutokuonekana tena katika upeo wa macho yake akashusha pumzi nyingi kishaakarudi kitandani kwake kuendelea kufurahia usingizi alioukosa muda mrefu toka ametoroka gerezani alikuwa mtu wa kuhama hama kila alipoweka maficho kwa hofu ya kukamatwa na serikali ya Tanzania.
"Ile nchi na watu wake watajuta kwanini waliingiza mkono wao na kunifungia kwa huo muda wote Hakika watajuta na ntafurahi Sana Nikiona Ile hashtag ya pray for Tanzania, ntahakikisha nusu ya jiji la Arusha linakuwa majivu.....vijana wana morali ya kutosha hussein?"
"ndiyo mkuu wanasubiri amri yako tu Tanzania inuke harufu yamoshi"
"hahahaha ni muda wa makafiri kusilimu na atakaegoma ntafurahi kuona damu yake ikimwagika mbele ya kamera ili dunia itambue kwamba sisi islamic state hakuna mzaha kwa makafiri Kisha yule bibi kizee atanizalia mtoto kabla sijamchinja kama kuku"
"lakini ungepumzika kidogo mkuu Hali iwe shwari ....tukifanya sasa hivi hatutafanikiwa mkuu"
"fanya nilichokueleza kuanzia kesho vijana waanze kusogea mjini kwa shughuli ya wikendi hii naskia Kuna tamasha kubwa hivo target ya kwanza ni uwanjani na target nyingine ntakwambia siku ya tukio"
"Sawa mkuu"
"Hussein sitaki makosa kwenye hili, wafadhili wetu wana mpango wa kuongeza day baada ya hili tukio hivyo usiniangushe na usimwambie mtu yoyote kama nimejifichahuku......alamski"
"Abdi nur mkuu....allah akutangulie kwenye njozi" alisemahuku akifunga mlango tamari kutekeleza majukumu aliyopewa na kiongozi wao MUSTAPHA ABDI NUR AHMED

TANZANIA SECRETS SERVICE(TSS)-HQ
Saa 2:15 Asubuhi
asubuhi hii ofisi ya idara ya ujasusi ilikuwa na pilika pilika nyingi kwani walikuwa walikwisha taarifiwa na chifu ya kwamba kutakuwa na ugeni mzito wa mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano
msafara wa gari zilizokuwa na nembo ya ikulu kumaanisha kuwa mkuu wa nchi alikuwa hapo huku eneo zima likiwa limeimarishwa na ulinzi wa kutosha na baada ya hapo ilichukua takribani dakika kumi za utambulisho kisha mheshimiwa raisi akapewa daftari la kusaini wageni wanaofika ofisini kwa chifu na kisha wakaketi kwa mazungumzo kidogo.
" kama nilivyokueleza jana mzee wangu nataka nishuhudie mahojiano hayo maana makamu alinipigia simu asubuhi akiniuliza habari zisizo na kichwa wala miguu, anadai huyu binti anasingiziwa kutokana na umaarufu wake na taarifa alizopewa na mke wake ni kwamba huyu binti aliachwa na ndege ndiyo akatumia option ya kupanda gari la watalii waliokuwa wanakuja huku Tanzania kutoka nchi ya jirani" alisema mheshimiwa raisi huku akipiga funda zito la kahawa aina ya capucino.
"nadhani kuna zaidi ya hilo mheshimiwa utalitambua muda mchache ujao na pia usinikatalie kwa maamuzi ntakayoichukua"
"bado sijakuelewa chifu unamaanisha nini"
"tunaweza tukaongozana kwa pamoja kwa lengo la kutambua hayo ambayo hata mimi yalininyima usingizi usiku wa jana'
"ni sawa je jenerali ameshakupa ripoti yoyote yenye kutoa mwanga wa haya matatizo"
"nadhani umesahau mheshimiwa kama jukumu hilo ulishamkabidhi mtu mwingine na anaripoti moja kwa moja kwako"
"mzee wangu naona unazeeka kwa haraka kiasi hiko umesahau suala la ulinzi na usalama wa taifa hili liko mikononi mwako kukuondolea jukumu sio tija ya wewe kuto kufuatilia hatua kwa hatua na najua kinachoendelea na hata hiyo timu mpya nimeibariki na nina imani kwamba wataikamilisha ndani yamuda.
wakasimama wakiongozana mpaka karibu na chumba kingine kilicho karibiana na chumba mahojiano huku kilichotenganisha ni kioo kigumu cha rangi nyeusi ambacho walioko kwenye chumba cha mahojiano huona kama ukuta lakini walioko upande wa pili wanawatazama vizuri kabisa.
" kamera ziwashwe tafadhari" alisema chifu huku akimpa maelekezo mkurugenzi msaidizi ambaye alimpa mrejesho kila kitu kiko sawa.
ndani ya chumba cha mahojiano kulikuwa na watu wawili jinsia ya kike huku mmoja akionekana ni mtu wa mazoezi, mwili wake uliojikata ulisadifu urembo aliobarikiwa na mungu, nywele zake alizikata mtindo wa low cut, asubuhi hiyo alikuwa ndani ya suti nadhifu ya rangi ya kijivu mbele yake kulikuwa na binti aliyefikishwa muda huo akiwa katika ulinzi mkali wa maafisa wa idara ya ujasusi.
"mfungueni mikono na miguu awe huru tu, najua ana mengi ya kunambia si ndiyo binti yangu?" aliwapa maelekezo na kulitupa swali kwa binti yule ambaye alifunuliwa na kukutana sura ya mwanamke mrembo mbele yake ambaye hakuacha tabasamu liende likizo muda wote alionesha tabasamu la kirafiki.
"vanessa ndelwa niliyoko mbele yako naitwa ajenti Chausiku juakali naomba tuishie kwa njia hii ya mahojiano ya kirafiki tafadhari ila kama pia hauta kubaliana na urafiki huu wa muda baina yangu na wewe zipo njia zingine ambazo sikushauri ufike huko " aliongea kwa sauti ya upole yenye kumaanisha kile alichokisema
"nipo wapi hapa?"
"rafiki yangu kujua hapa ulipo sio muhimu sana.......ninacho kitaka kutoka kwako ni ushirikiano tunakunipa majina ya wahusika wala hutaona hata kipande cha ngozi yako kinabadilika rangi achilia mbali kupata maumivu, vanessa nambie unashirikiana na nani kwenye haya matukio"
"mimi sijui unaongelea nini kiufupi unanichangany......"
"nazungumzia kilo 25 za madawa ya kulevya aina ya Heroine"
"siwezi kuongelea lolote mpaka mwanasheria wangu afike, nisaidie simu nimjulishe dada kwamba mmenishikilia muone hata kama nitamaliza saa 1 niko humu, mnanibambikia kesi alafu mnaninyma haki zangu kisheria.....namhitaji mwanasheria wangu ndiyo ntakujibu maswali yako"
ajenti chiku kama walivyozoea kumuita akaiangalia kamera na punde mlango ukafunguliwa akaingia mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania akiwa na tabasamu murua na kumfanya vanessa nae atabasamu kwani alijua kila kitu kitaisha hasa kutokana na utambulisho aliopewa mheshimiwa raisi na makamu wake kwamba huyo ni shemeji yake kilifanya awe karibu nae kiasi kwamba hata matukio muhimu ya kitaifa yaliyokuwa yakifanyika alikuwa akipata mualiko moja kwa moja kutoka ikulu.
"vanessa binti yangu usishangae nimekuja hapa na kofia mbili, moja kama mlezi wako na ya pili kama mwansheria wako na siko hapa kama raisi ndiyo maana hujanuona mlinzi wangu hata mmoja jisikie amani kabisa na ujibu maswali utakayoulizwa na dada chiku Sawa"
"nahitaji kumjulisha dada na shemeji kuwa nimekamatwa japo bado sijajua niko wapi"
"shemeji yako nimeshazungumza nae asubuhi na hivi sasa yuko ethiopia ananiwakilisha katika mkutano wa umoja wa afrika unaofanyika Adis Ababa, hivyo nkuondoe wasiwasi binti yangu kuwa hakuna baya litakalotokea mimi nikiwa humu binti yangu mrembo na nitakusaidia uweze kushiriki tamasha lako huko jijini Arusha nadhani tumeelewana"
"nimekuelewa mama" alisema hivo kwa upole huku mheshimiwa raisi akimuangalia dada chiku kama ishara ya kuendelea na mahojiano.
***********************************
UONGO NA SIRI NI KAMA KANSA YA NAFSI HIVYO BASI INAKULA YALE MAZURI NA KUACHA UHARIBIFU NYUMA YA PAZIA, JE? ATATAJA WAHUSIKA AU ATAKUBALI KUFA NA SIRI YAKE, TUKUTANE TOLEO LIJALO
 
KIUHALISIA NI SAHIHI KWAMBA MAJI YALE YALE YALIYOCHEMSHWA YANAVILAINISHA VIAZI MVIRINGO(ULAYA) LAKINI PIA NDIYO HAYO HAYO MAJI YANALIFANYA YAI LA KUCHEMSHWA KUWA GUMU, INATEGEMEANA NA JINSI ULIVYOUMBWA NA SIYO MAZINGIRA KUWEZA KUKAA NA SIRI MOYONI UNGANA NAMI.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
"niandikie hapo wahusika wote wa mtandao wa dawa za kulevya nataka wale wanao watuma kuyaingiza na kwa taarifa tu ambaoulikuwa hujui wenzako uliokuwa nao sasa hivi nahisi watakuwa wamesha kuwa kuni huko jehanamu"
"whaaat......mmewaua wale watalii maskini mungu atawaadhibu vibaya san......"
"binti tusipotezeane muda nipe majina ya wahusika muda wakumtaja mungu ukiuhitaji nao tutakupa ili umtaje vizuri" alifoka ajenti chiku huku lile tabasamu mwanana likienda likizo nakukaribisha mikunjo ya ngozi katika uso wake"
"fanya hivo Vanessa" aliongea mheshimiwa raisi kwa sauti yakusihi
"mimi sijui chochote mama nachokumbuka nilichelewa ndege majira ya saa 7 usiku na hii ni kutokana na maandamano mpaka usafiri niliyoukodi unafika uwanja wa jomo kenyatta airpot saa 8 na robo tayari nilikuwa nyuma ya muda wa dakika 45 tangu ndege niliyokuwa natakiwa kurudi nayo Tanzania kuiacha ardhi ya kenya sikuwa na chaguo zaidi ya kurudi hotelini na hapo ndipo dereva taxi yule aliponambia kuna gari ya watalii inakujat anzania kupitia arusha nilipoona hivyo niliona hiyo ndiyo njia rahisi kwa mimi kuweza kufika Arusha hata kama ni usiku mzito ningepata muda wa kupumzika na muda wa maandakizi ya tamasha langu lililokuwa likidhaminiwa na kanisa la JEHOVAH AMESHINDA nilibahatika kupata usafiri ule lakini bahati mbaya tulipovuka mpaka wa Kenya kuingia tanzania tulisimamishwa na dereva aka.........." alikatishwa sentensi yake
"akakanyaga mafuta mengi kuwakimbia maofisa wa polisi mpaka mlipokuja kukamatiwa jirani na benki ya KCB gari lilipopata hitilafu katika harakati zenu za kuficha mzigo uliokuwemo ndipo mlipojikuta mmezingirwa na askari polisi na kikosi cha wanajeshi" alimalizia kusoma kile kilichoandikwa kwenye maelezo aliyotumiwa kwenye tablet, mheshimiwa raisi kitu kilichomshitua vanessa kwamba mheshimiwa kayapata wapi hayo maelezo ikiwa wenzake tayari wameshatangulia mbele za haki, kupitia nyuso zao vanessa alitambua kuwa ndani mle hakukuwa na mtu aliyekuwa upande wake kabla ya kushtukizwa na swali lililoutia ubaridi mwili wake na kumfanya apigwe na butwaa kwa dakika nzima.
"Vanessa binti yangu nambie ukweli unashirikiana na nani, na ni taarifa ngapi umeshazituma kwa wakubwa zako"
"mama sijui unachoongelea, mimi ni muimbaji tu wa nyimbo za injili sijui chochote kuhusu buiashara mnayoisema ya dawa za kulevya sasa hivi imebadilika tena kuwa nimetoa taarifa za nchi kwa watu ambao ni wakuu wangu....labda niwaambie tu mkuu wangu ni Mungu wa mbingun..........." alikatishwa kwa kibao kikali kilichotoa sauti kiasi cha chumba kizima kubaki na mwangwi, hata mheshimiwa raisi alifumba macho maana anajua kazi chafu za bidada huyo linapofika suala la mahojiano ni mrembo ila ana roho mbaya sana anapokutana na wahalifu, ni heri hata ukutane na afisa wengine katika mahojiano ila siyo huyu bidada aliyesoma shahada yake ya udhamili katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya patrice Lumumba huko urusi na taaluma ya upelelezi aliipatia huko huko chini ya shirika la ujasusi la nchini humo yaani KGB
"sasa huyu binti mkuu mbona amevamia chaka la simba na anachokutana nacho atatamani hata muda urudi nyuma waongeekama marafiki." alisema mkurugenzi msaidizi
"jasusi ni jasusi tu na ukiona raisi ameliingilia hili ujue kwamba hili suala ni zito na huenda linahusiana na kile kinachoendelea nchini burundi, tuma watu wakamwangilie dada yake na kama watamkuta basi atakuwa chini ya uangalizi wa idara mpaka pale na yeye atakapo tapika taarifa tutakazo ziona zitatusaidia kupata. mwanga"
"huoni tutakuwa kwenye mgogoro na makamu wa raisi hasa ukizingatia huyo ni mkewe na amezaa nae watoto......mimi ningeshauri tukomae na huyu kwanza kisha tutamuingia dada yake taratibu"
"mgogoro huo mimi ntaumaliza wewe cha kufanya hivi sasa tekeleza kile nilichokwambia tuko nje ya muda, hayo ya makamu wa raisi ntazungumza na mheshimiwa raisi tena ikionekana analeta ubishi nae pia ashikiliwe huko huko na aletwe hapa ahojiwe kikamilifu."
"sawa mkuu" hayo yalikuwa maongezi ya chifu na msaidizi wake
"binti nipe jina tuokoe muda ili mheshimiwa akaendelee na majukumu ya kitaifa"
"unataka jina la mkuu wangu si ndiyo" akachukua kalamu na ile karatasi akaanza kuandika majina na akampatia karatasi ile chausiku lakini raisi akawahi kuichukua na kuitazama kwa makini kisha akamuangalia yule binti kwa masikitiko.
"nikiwa na umri kama wako miaka ya 1998, niliwahi kumkamata gaidi aliyeweza kuhusika na mlipuko wa mabomu katika treni ya abiria, mtu huyo alikimbilia kenya na alikuja kunasa baada ya kuzuzuka na urembo wangu na hata njia niliyotumia kumkamata hata wakuu wamgu wa kazi kipindi hicho walikuwa hawajui kilichofanyika mpaka nikamdaka mtu yule, alikaa kwenye kiti kama hicho hicho na tena akiwa huru kama wewe hivo sikutaka kumfanyia mahojiano akiwa amebanwa na vitu na hata nilipompa karatasi aniambie maeneo aliyotega mabomu mengine aligoma kusema."
"nilimpa ofa ya pesa nyingi sana endapo angenitajia mkuu wake na wapi anapopatikana aliniandika vitu kama ulivyoandika wewe tofauti yeye alitumia ‘Allah’wewe umetumia ‘Mungu’, na nyote mmesaidifu kitu kimoja ........ndiyo ni sahihi Mungu ni mkuu hata mimi nalitambua hilo ila namhitaji mtu akiwa na majina kamili na wapi anapatikana mwenzako alinitajia majina yote ya wahusika na mabomu yalipo na hivi sasa yupo guantanamo anakolia usiku na mchana” alisema mheshimiwa raisi kwa sauti ile ile ya kusihi
"sasa na wewe usitake nitoke hadharani mbele ya waandishi wa habari nkutangaze kama gaidi na vile vile muuza madawa ya kulevya na ushahidi ninao wa kutosha na kama haitoshi ntautangazia ulimwengu kwamba wewe ni jasusi wa burundi uliekuwa unaihujumu nchi na umehusika na shambulizi la kulipua ubalozi na kubwa zaidi ntakukabidhi kwa CIA wakashughulike na wewe hivyo chaguo ni lako nina dakika tano tu za kukusikiliza" aliongea mheshimiwa raisi kwamsisitizo
"hahahahaa sina cha kukwamb..........." alipigwa kofi la mgongoni kiasi cha kushindwa kuzivuta pumzi vizuri.
"siku nyingine usijaribu kuleta mzaha watu wakiwa kazini'
"mzaha....mimi na nyie nani analeta mzaha mnapoteza muda kuniuliza maswali ya ajabu ajabu na ukute wewe sijui ndio chiku sijui nani ukute ulimnyima mmeo tendo la ndoa kuhofia angekumaliza nguvu za kunihoji haya mpaka sasa umepata nini"
"Chiku mpeleke huyu gereji bado ana mengi ya kutuambia"
"pole sana binti yangu nataka uuone upande wangu wa pili ambao ninauhakika ukimaliza kuuona utakuwa na siku chacheza kuvuta pumzi hii ya bure....mpelekeni Shimo la tewa"
***************************************
"chifu nnimeletewa taarifa kwamba watu waliokwenda nyumbani kwa makamu wa raisi hawajamkuta mkewe wala watoto kwenye shule wanazosoma pia walichukuliwa jana na ripoti inavoonesha tayari wameshaikimbia nchi....."
"whaaaat na makamu wa raisi yupo wapi wakati mkutano ulikwisha tangu jana na ndege aliyoondoka nayo mbona nimepata taarifa imetua siyo muda mrefu kutokea adis ababa ethiopia""
"ni sahihi mkuu ila kwa taarifa nilizopewa ni kwamba hata makamu pia na kikosi chake cha walinzi wanao mlinda nao pia wametorokea kusipojulikana"
"ooooohhh shit mpigie simu jenerali na uniunganishe nae mojakwa moja"
KINGDOM HOTEL-MWANZA
Saa 4:53 asubuhi
huu ndiyo muda Luteni kanali Charz Busungu alikuwa aliwasili mapokezi ya hoteli ya kingdom jijini mwanza akitokea wilaya ya serengeti na kabla hajasema chochote sura ya mrembo aiyekuwa mapokezi ilimlaki kwa bashasha na tabasamu pana.
"karibu kingdom hotel kaka mzuri, kuna kila huduma uitakayo na itakufanya usijutie kuja hotelini kwetu" alifunguka dada yule huku tabasamu likiendelea kuchanua vile vile kama mwanzo
"nisaidie funguo ya chumba namba 104 tafadhari"
"bila shaka wewe ndiyo mwalimu Musa"
"ndiye ila umechelewa kumjua ila ndiyo hivo anaenda kubadilika kuwa mtu mwingine, Tena hotel hii ndiyo Ina bahati kunihifadhi kwa Dakika chache, Sauti Yako ni tamu Sana mrembo nilitamani iniburudishe kwa nyimbo tamu na uchovu huu na Imani ungetoroka Mara moja kwa mmeo kuja kuiba huba tamu kutoka kwangu,"
"una vituko wewe kaka hebu chukua funguo zako ukamuwahi huyo anaenda kufaidi huo mwili....hujawatia mimba wanafunzi wako kweli?.
"ni heri ningekuwa namuwahi huyo unaesema anaenda kufaidi, ilia nipe namba ili nikikabwa na jinamizi nikuite uje kunisaidia"
"huna lolote......hiyo naijua hebu nenda bhana, bosi asijenikuta napiga soga wakati huu ni muda wa kazi akanifukuze na Maisha yalivyo magumu sitaki nirudi kijijini kwetu nkacheze na nyani"alimaliza kusema huku bado akiwa na tabasamulile lile kama mwanzo
"haya bhana chumba changu kiko ghorofa ya ngapi"
"unaona Sasa unanipigisha soga kiasi kwamba nimesahau hata kukwambia sehemu kilipo chumba chako ni ghorofa ya tatu mkono wa kulia"
"nisindikize tukamwone wote anaenda kuufaidi huumwili" alisema luteni kanali huku akianza kuzipiga hatua.
"thubutu aje anichome kisu....wewe nenda tu wanawake wenyewe wa siku hizi washari Shari utakuta kwenye pochi ametembea na kisu" mpaka anamaliza kuongea alipotupa macho aliambulia patupu baada ya kukuta ni kweupe ikiwa Ina maana luteni kanali Charz alikuwa amekaribia korido lenye chumba anachotakiwa kwenda, alitikisa kichwa huku akiendelea kuitupia macho siku yake aliyokuwa anaitumia kuperuzi katika mtandaowa tick tock
********************************************************
SHIMO LA TEWA (TSS-HQ)
saa5:15 asubuhi.
"karibu kwenye hatua ya pili ya mahojiano ambayo kwa moyo wako mkunjufu Kabisa mtumishi wa bwana, umechagua fungi LA kukosa na kwatarifa yak........"
"iwe taarifa yangu au taarifa ya Habari mimi sijui mnachoniuliza munapoteza muda tu ila siku yenu ya kulia na kusaga memo, Tena utaanza kulia wewe Malaya" alikatishwa na Binti yule nakumaliza na tusi lililomlenga ajenti Chausiku.
"wow.....siku hizi naona mmejisahau mlokole anatukana hadharani, Binti Huoni kwamba Kuna tatizo sehemu haya naona umebadilisha Gia angani kutoka kutaja Mungu Sasa unataja Malaya lakini nikuhakikishie Leo umeyakanyaga Binti" aliongea mheshimiwa raisi huku akimtazama ajenti Chiku
"Angel of the death show her what a person saw in a seconds before his death"
"yes madam....ni muda wa kutapika taarifa Binti nadhani kwenye vitabu vyenu vya dini umewahi kusikia kitu kinaitwa malaika wa kifo na sifa zake si ndiyo Binti"
"sijui chochote labda uniue na hata ukiniua utakuwa umefaidika nini"
"hutakufa kikawaida watu wanaishi Mara moja ila kwa wahalifu wanaofikia hatua hii waga wanaishi Mara mbili"
"usijida......."
"sijamaliza Binti.......ni hivi unaishi Mara moja ukishazaliwa ilakwa muhalifu kama wewe utaishi Mara mbili Mara ya kwanza ulivyozaliwa na Mara ya pili utaishi utakapokutana na Malika wa kifo kama wewe Leo hii Kisha Hao utakao wasema utake usitake Tena ukiwa na maumivu, Nakata kuanzia kwenye unyayo mpaka kwenye ncha ya mzizi mwisho wa nywele zako" alisema hivo ajenti Chausiku huku akiwa amegeukia Sanduku lenye kila Dhana ya kumfanya mtu achukie na kujutia kuzaliwa ama kuingia eneo Hilo.
"hahahaha unajisumbua tu Dada ang...........aaaaahhhh Mungukidole changu " alilamika huku akisikia maumivu baada ya pingili ya kidole chake shada.kukatwa kikatili
"nipe majina au tuendelea kuzidondosha pingili zote za mkono wako wa kushoto na nitahamia mkono huo wa kulia ukiwa mgumu wa kuwataja nitahamia miguuni.....nakuonea huruma bint........"
"kamwambie hizo ngonjera zako baba yako nilishavuka hatua zote za mateso na yesu atanifunika kwa damu yake nyie fanyeni mnachofany.........oooooohhh shit mama angu nakufa"
**********************************
Unadhani alikufa? Waswahili wana kamsemo kao ya kwamba kufa hufi ila cha moto utakiona, je friji lake litaendelea kugandisha au gesi itaisha na kujikaza kwake kutakuwa nguvu ya soda ungana nami toleo lijalo
 
“SIKU ZOTE WATU WAJINGA NA WAPUMBAVU HUJIONA NI WENYE BUSARA LAKINI MTU YEYOTE MWENYE BUSARA ANAJUA NI KWA NAMNA GANI YEYE NI MJINGA, NA HAKUNA UONGO MBAYA KAMA ULE MTU ANAOONA. UNASEMA KWELI” BADO HUJANISOMA UNGANA NAMI SASA UPATE KUELEWA MAANA YA HAYA MANENO
Ilipoishia sehemu ya kumi na moja
"nipe majina au tuendelea kuzidondosha pingili zote za mkono wako wa kushoto na nitahamia mkono huo wa kulia ukiwa mgumu wa kuwataja nitahamia miguuni.....nakuonea huruma bint........"
"kamwambie hizo ngonjera zako baba yako nilishavuka hatua zote za mateso na yesu atanifunika kwa damu yake nyie fanyeni mnachofany.........oooooohhh shit mama angu nakufa"
FUATANA NAMI KATIKA SEHEMU YA KUMI NA MBILI
"na utakufa kweli huku ukiwaacha unao waficha wakila kuku kwa mrija huku wewe ukiwa kilema wa Maisha huko gerezani nadhani unaelewa" alisema mheshimiwa raisi huku akimkazia macho Vanessa aliyekuwa anasikilizia maumivu.
"ki kawaida kila baada ya pingili mbili tunamwaga dawa ya kuulia bacteria sisi hatutaki upate shida ya kuoza kidonda na kiufupi tunakupenda ndiyo maana tuko hapa na wewe"aliunguruma tena ajenti Chiku
“Tutakukata vidole vyote Kisha tunaenda kwa Dada yako tutamleta hapa achague Kati ya kutupa majina au akushuhudie ukikata Roho Kisha na yeye atakufata huko, haya muda wa story umeisha" akaanza kumimina kimiminika kilichokuwa kwenye kikopo cheusi na muda na huo huo baada ya kumwaga kimiminika kilicho kuwemo ndani ya kikopo na matone kadhaa yalikifikia kidonda kibichi cha binti yule na kusababisha apige yowe la maumivu na hofu kwa wakati mmoja.
"hahahaha unadhani utampata dada yangu au makamu wako wa raisi mnapoteza muda wenu tu sasa hivi watakuwa mbali na jiandaeni kwa shoo itakayokuwa ni burudani machoni mwenu hahahaha......unataka kufanya nini "
"muda wa jeuri umeisha sasa ni muda kusikiliza matokeo ya njia uliyoichagua na nikuhakikishie mpaka utakapo nipatia hayo majina ndiyo utatoka humu tofauti na hapo tutakesha humu ndani," alisema hivyo mheshimiwa raisi huku akiwa na sindano iliyokuwa na kimiminika kama dawa, ambacho hutumika kumpa maumivu makali mtu. wakati anajiandaa kufanya zoezi hilo mlango ukafunguliwa na chifu anaingia akiwa na simu mkononi
"mheshimiwa kuna simu imeingia dakika mbili zilizopita kwa private number na inahitaji kuongea na wewe tu" mheshimiwa raisi akaipokea simu ile na kuiweka sikioni huku akipiga hatua mbili na kusikiliza upande wa pili utasema nini napo kulikuwa kimya mpaka alipoanza yeye
"ni nani wewe mtu muoga mpaka unatumia private number ndiyo unipate kwani hujui ofisi zangu"
"hahahaha kunijua siyo tija mheshimiwa raisi nilitegemea utaishi kwenye status yako ya uraisi na sasa hivi huenda ungekuwa mikoani unazindua hata mashimo ya choo ila sasa ni saa la tatu uko kwenye ofisi za chifu unamuhoji binti mdogokama huyo mliye mbambikia tuhuma nzito kwa busara tu ningependa kukuomba umuachie tu huyo binti akaendeleze kazi zake za uimbaji wa nyimbo za injili"
"kwahiyo unanipangia kitu cha kufanya si ndiyo hilo halita wezekana kwasababu serikali yangu haifanyi makubaliano na wahalifu kama wewe au huyu mhalifu mwenzako na sipokei amri kutoka kwa mtu ambaye simfahamu njoo ofisini kwanguulete hizo amri zako nami ntakusikiliza by the way kuna ka kazi kadogo nakafanya nadhani baada ya nusu saa unaweza ukafika ofisini kwangu"
"hahahahah nimeshakuwa mhalifu tena kwa upole kabisa nimekwambia muachilie huyo binti ndani ya nusu saa hiyo unayosema uhakikishe unapotoa mguu wako katika hizo ofisi nae anatafuta njia ya uwanja wa ndege akapumzike akiwa huru na hakikisha hana hata jeraha"
"hahaha labda hujui tu tunavyozungumza huyu binti hana kidole cha shada sijui hata atakaye funga nae ndoa huko kuzimu ataweka wapi pete, hivyo nadhani muda wa kuongea na mpumbavu kama wewe umeisha"
"subiri labda ni kwa vile hujui unalo lisema ndani ya saa 24 zijazo jiji la Arusha litakuwa moshi na majivu ‘BOOOOOM’ hahahaaha najua watu wako wanatafuta hii simu inapotokea ila niwajuze tu hawataweza kuipata mna machaguo mawili kuyazuia mabomu ambayo hamtaweza kuyapata hata nikiwapa mwezi mzima na hata mkiomba usaidizi wa nchi marafiki hamtanusa hata harufu yake au mmuachie huyo binti na kisha ntakuacha uendelee na uongozi wako salama"chifu akampa ishara kwamba aendelee kuzungumza nae vile vile bila kuonesha tashtwitwi yoyote.
"hahhaha nimependa unavyozungumza kwa kujiamini ila ningependa unipe muda kidogo nitafakari kwanza na watu wangu"
"masaa matatu yanakutosha vinginevyo urafiki baina yangu na wewe kwenye hili suala litabaki historia na huko mbele unaweza kulalamikiwa kuwa hukufanya maamuzi sahihi" alisema mtu yule aliyekuwa anaongea kwa sauti nzito kiasi cha kushindwa kutambulika sauti yake na hata utambulisho wake ni nani bado wana usalama walikuwa wakishughulikia, baada ya simu kukatwa mheshimiwa raisi akamrudishia chifu wa idara ya ujasusi aliyeipokea akiwa na shauku ya kujua wamesema nini
"hawa wajinga wana niamrisha nimuachilie huyu malaya na wamenipa masaa matatu nataka umueleze jenerali kwamba mipaka yote iwe kwenye ulinzi masaa 24 na huu mji wa Arusha upekuliwe vilivyo najua akili za hawa wapumbavu ni kutufanya tuweke umakini sehemu moja najua una vijana wa kutosha katika pembe ya kila nchi waaminifu na wenye tamaa, na ndiyo maana hata ujio wangu ofisini kwako na kila ninachokifanya taarifa zinawafikia maadui nataka mutafute simu iliyotoa hayo mawasiliano mara moja nataka niwafundishe kwamba nchi imara kama Tanzania haichezewi chezewi ovyo na wajinga wajinga tumeelewana"
"ndiyo mheshimiwa vijana, wanalishughulikia hili na baada ya muda mfupi tutakuwa tumempata"alisema chifu huku akikiacha chumba hicho.
"nimerudi binti utanipa majina au bado umeshikilia msimamo wako ule ule wa kuzoea maumivu si ndiyo "
"mheshimiwa raisi wangu naona unapoteza muda ungemsikiliza uliyekuwa unaongea nae kwenye simu ili nchi itawalike kwa amani unadhani ukishindwa kufanya hivo nchi ikawa kwenyeharufu ya moshi na vifo huyu malaya pembeni hapo unadhani ataweza kumkatia kiuno basha wake hahahaha eti anajiita malaika wa kifo nikitoka hapa ntakuua mbwa wewe na maiti yako ntaichemsha niwape mbwa wangu wanywe kama supu" mheshimiwa raisi alivyotaka kuchukua ile sindano ajenti chiku akampa ishara ya mkono kwamba aache
"hiyo itakuwa ya mwisho kabla hajavuta pumzi yake ya mwisho sasa hivi ninachotaka kukifanya ni kumpatia ladha ya kifo kabla hajakutana na kifo chenyewe" muda huo alikuwa anatoa chuma kilichokuwa na uwekundu kwa mbele ikiwa na maana yakushika moto katika katika kiwango cha kuibadili rangi yake ya asili na kuwa nyekundu.
"mungu wangu aaiiiiii mama nakufa mungu wangu" alilalama kwa maumivu yule binti wakati chuma kile kilichoshika moto kilipoigusa ncha ya chuchu kwenye ziwa lake la kulia kisha kikatolewa
"utasema au bado ni mgumu tuendeleze zoezi sasa hivi nashuka hapo kwenye kitovu"
"mungu hapendi unavyofa..........aiiiiiiii mama angu nakufa, wewe malaya nkitoka mzima ntakufanya kitu kibaya"
"unadhani utatoka hapa ukiwa mzima sahau kuhusu habari za duniani hapa uko kuzimu na nilikueleza muda wa kupiga soga hakuna, alisema hivo ajenti Chiku huku akiifata sindano ile mezani
"najua wewe ni jasusi na unajua maana ya dawa iliyoko humu ndani. itakupa maumivu makali ambayo sidhani na urembo wako unaweza kuyahimili utakufa ukiwa kwenye maumivu makali sana na hakuna wa kukusaidia utafia kwenye kitanda na mwili wako ntauyeyusha mle kwenye lile pipa hahahaha binti pole sana kiburi cha kutokufunzwa na wazazi wako vizuri mimi ntakusaidia kukupa somo la kuwa mtoto mwema hata ukifika motoni mpaka shetani ahisi labda umekosea njia kwa tabia njema na utiifu utakayoipata hapa hapa kabla roho yakohaijauacha mwili wako" alisema mheshimiwa raisi huku akisogelea meza
"siwezi kuongea chochote kwa maana so......oooutch son of b*tch"
"umeshatoka kwa mungu na Sasa hivi tunazungumza lugha moja ya kuzimu si ndiyo Binti" alifoka ajenti chiku
"aaaahhhhh mama nakufa" alisema Binti yule huku Saudi yake ikitoka kwa kukwama kwama kutokana na maumivu ya dawa Ile na kama haitoshi jasho lilikuwa likimtoka kwa wingi.
"nisaidieni ntasema ntasema" aliongea Binti yule kwa pupa huku akiwa amekakamaa kama mgonjwa mwenye degedege, Hali ilidhihirisha maumivu anayopitia ama ana ukaza mwili kuupa nafuu dhidi ya maumivu lakini Sasa inaonekana ni kama vile friji lake lilizidiwa na joto kiasi cha kushindwa kugandisha kimiminika yaani Siri,
"nipe majina Yao chap chap Binti" aliongea mheshimiwa raisi huku akimsogelea binti yule aliyekuwa kwenye maumivu makali alitamani kuuloweka mwili wake kwenye barafu ili apate ganzi ila uwezo hakuwa nao alikuwa kwenye kumi na nane za watu wakatili
"Hapana kwa Hali....hii si..wezi ni...pe dawa kwaanza Dada angu"alitia huruma huku akimtazama Chiku
"hahaha si umeona Sasa ungesema tangu mwanzo usingekuwa kilema wa Maisha mpumbavu Sana wewe" alifoka mheshimiwa raisi huku akimchoma dawa nyingine ya kuounguza maumivu kama sio kuyaondoa kabisa
"oooouch.....oooops angalau Sasa maumivu yameenda likiz....." alivuta pumzi nzito binti huyo
"weeeeeewe....acha ngonjera hizo twende na muda Binti nipe majina chap"
"naomba nikunong'oneze mheshimiwa raisi wewe peke yako kwa sababu hichi ninachoenda kukwambia ni cha hatari hata mimi pia sidhani kama ntaishi.” Aliongea binti yule kwa sauti ya kukata tamaa
"nambie Mimi nitakulinda" alisema mheshimiwa raisi huku akilichukua koti lake alilokuwa amelitundika sehemu ndani ya chumba kile
"huwezi kunilinda mheshimiwa wasinifikie ni kikundi cha hatari Sana ambacho kina mtandao mkubwa Sana Ina watu katika kila pembe ya serikali yako na nje ya nchi hivyo nina ombi moja tu haya majina ntakwambia kwenye gari lako tukiwa wawili tu ukiwa na kalamu na karatasi"
"Hilo haliwezekani.....naona Binti unanunua Tena muda na tuna massa 2 na Dakika zake kabla mheshimiwa raisi hajawajibu ma bwana zako kwa kuwatangazia kifo chako" aliongea tena chiku huku akimtazama kwa jicho la usongo
"chiku muache tu afanye hicho anachohitaji andaa utaratibu atanikuta kwenye gari na mwambie chifu aniletee ripoti ya kile alichokipata kuhusu aliyetoa taarifa za uwepo wangu hapa...." Alitoa maagizo hayo raisi kwa ajenti chiku huku akiwa anavaa koti lake LA suti naKisha kukiacha chumba hicho cha mahojiano na kupita koridoni walipo walinzi wake katika korido zile za ofisi ya ujasusi, hatua kadhaa mbele yake chifu nae alikuwa akija upande huo huo na kwa utiifu mkubwa.
"hongera Sana mheshimiwa kwa hatua uliyofikia itatufungua sana kama siyo kutuwezesha kuufikia mzizi" alifukuza ukimya Chifu
"mtu wangu mmekwisha mpata?"alijibiwa kwa swali ambalo alilitegemea hapo kabla
"mpaka jua linazama tayari ripoti itakuwa ishafika kwako mheshimiwa vijana wangu wanashughulikia nikuondoe wasiwasi kwenye hilo mheshimiwa" alisema Chifu huku akianza kuongoza njia kwa safari ya ofisini kwake
**************************************
Je? Ni nani anayetoa siri kwa maadui tena katika ofisi nyeti inayodhaniwa kama jicho la taifa, je majina yanayotafutwa kwa usongo na mheshimiwa raisi yatatolewa na binti huyo? Kwani huyo binti hasa ni nani? Majibu yote utayaoata toleo la 13 Tchao
 
“DUNIA NI SEHEMU YA HATARI SANA, SIYO KWA SABABU WAISHIO KUFANYA MAOVU, NI KWASABABU WATU HUONA UOVU NA
KUNYAMAZA BILA KUFANYA CHOCHOTE” haya ni maneno ya mwanafikizia anayekadiriwa kuwa na akili nyingi kiasi cha kutengeneza ‘theory’ mbalimabali huyu si mwingine bali ni Albert Einstein
Ni maneno yanayogusa asilimia kubwa ya kipande hiki cha kumi na tatu, Fuatana nami……………..
niandalie mazingira niongee na huyo binti kama mama na mtoto wake" alisema hivyo mheshimiwa raisi huku akimnong'oneza chifu
"nilishaandaa mheshimiwa kule underground nahisi patakuwa salama kwa unyeti wa jambo hilo na imani unapatambua vizuri mheshimiwa"alisema Chifu
"sawa acha nitangulie huko na huyo binti muachie ajenti chiku amlete kwa usiri mkubwa hata walinzi wangu waishie mita mia moja na wasijue kinacho endelea huko" alisema hivyo huku wakiendelea kutembea kana kwamba wanaingia ofisini kwachifu lakini katika ofisi hiyo kuna mlango wa ziada utakaomfikisha huko wanapopaita underground ya ofisi ile ya idara yaujasusi
baada ya kumfikisha raisi ofisini kwa chifu, aliwapa ishara ya kutoka nje huku akiwapa ishara walinzi wake kutoka nje ya ofisi hiyo kwani alikuwa na mazungumzo nyeti na chifu.

*************
MAKAO MAKUU YA JESHI-LUGALO DAR ES SALAAM.
SAA 6;12 MCHANA
ilisomeka katika saa ya jenerali kwamba sasa imekwisha timia saa sita mchana ya siku ya nne kati ya kumi na mbili alizope wana mheshimiwa raisi, lakini alikuwa amekwisha pewa dondoo kwamba lile giza zito karibu linaelewa kutoweka kuupisha mwanga utawale.alikuwa ofisini kwake akitazzamana na kijana ambaye alishawahi kupita katika mikono yake wakati huo akiwa na cheocha kanali huko kambi ya 92 KJ huko ngelengele lakini leo hii alikuwa mbele yake huku akiwa na mavazi ya kawaida sana na baada ya salamu aliufukuza ukimya kwa kufungua kinywa chake kwa swali lililomlenga kijana yule ambaye hata kwa macho ya kawaida yana sadifu kwamba ni mtu wa kufanya mazoezi makali na kuufanya mwili wake kuumuka misuli na kuwa na umbo kama la mchezaji wa mpira wa kikapu (hayati) kobe bryant.
"nilipata taarifa chumba namba 104 uliwekewa mavazi ya kuvaasasa mbona umekuja ofisini kwangu kama hivo au maisha ya uraiani yamekufanya ukengeuke na kusahau miiko ya kazi natamani sana kujua wakufunzi wako mara mwisho walikufunza vitu gani....unadhani maofisa wengine wanajifunza kitu gani kutokana na tabia yako tena mtu mwenye cheo cha luteni kanali kama wewe ulifaa kuwa mfano.........mbona umejisahau sana na hizo nguo nazipataje mbona unahatarisha sana oparesheni kijana kama unahisi hujisikii kuchukua misheni ni heri urudi ukaendelee na kazi yako na mimi ntawaambia wakuu kwamba umekiasi kiapo chako" aliongea kwa sauti ndogo ila yenye msisitizo huku muda wote akiwa habandui macho kwa kijana yule kabla ya kumalizia sentensi ya mwisho na kugida maji yaliyokuwa kwenye glasi na kupiga mikupuo miwili hukua kishusha glasi ikiwa nyeupe na kitendo cha kushusha glasi sauti kavu na nzito ya kijana yule iliunguruma
"naona sasa jeshi limepata kiongozi anaekaa kwenye kiti nameza kubwa kiasi huku uwezo wake wa kufikiri ukiwa ni mdogo sana, kwenye hili jeshi unalo liongoza wewe kwa sasa aliwahi kukaa mzee mmoja mkatili sana na mwenye akili sana, aliwez kupanua akili yake kiasi cha kuizidi hiyo meza, katika utumishi wangu sikuwahi kusikia matishio makubwa kamayanayotokea hivi sasa, sisemi kama uongozi wake ulikuwa mkamilifu sana la hasha kulikuwa na mapungufu ila sio kama sasa..........." alimeza fundo la mate huku akimtazama mzee yule aliyechafukwa vyeo kwenye gwanda nadhifu alilolivaa kiongoziyule.
"jeshi letu siyo kisiwa kiasi cha kushindwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.....sikiliza mzee haya yote yanasababishwa na mpasuko uliyopo baina ya jeshi na vyombo vingine”
"nyamaza mjinga wewe.......hivi umesahau miiko ya kazi kiasi cha kunipandishia sauti mimi kiongozi wako.....umatakiwa kufata amri tu na unajua athari ya kupinga amri ya mkubwa wako na unakumbuka kiapo chako siku unaingizwa rasmi katika data za jeshi huko kambi ya navy kigamboni? siku nyingine ukiwa unaongea na mimi sauti yako isiwe juu kama sidiria bali iwe chini kama chupi unaniuliza maswali ambayo natambua huna unalolijua na hii ni kutokana na kushinda ukiimba nyimboza kuwafurahisha watoto wa shule nadhani umesahau kwamba hapa sio shule na mimi siyo mwalimu mkuu bali unaongea na jenerali wa jeshi la wananchi tanzania tumeelewana " alifoka tena jenerali
"walioshiriki katika mauaji ya wenzangu bado wamo katika utumishi wa jeshi hili, waliohuika na mauaji ya luteni jenerali Yamungu shayo, wapo wanakula pensheni na wengine wapo humu humu na huko duniani, lakini pia watu waliohusika na kunibambikia tuhuma za kuwa nimepatwa na ugonjwa wa akili nikafukuzwa kazi na pia malupulupu yangu na pensheni vilizuiwa mpaka leo tunavyoongea nao pia wapo humu humu kwenye jeshi unaloliongoza lakini pia nimekuja kwa heshima yako kwasababu nilipata ujumbe wa mtu aliyenifanya leo navuta pumzi kuwa nchi ina matatizo na ninahitajika mara moja kufanya majukumu yangu sijaja hapa kukuuliza kama luten ikanali wa jeshi bali nimekuja hapa nikiwa kama raia wa kawaida tu.......mbali na madhira yote hayo sijawahi kusikia uchunguziwowote unafanyika walio utoboa mwili wangu kwa risasi sio waasi bali walikuwa ni kikosi maalumu kabisa cha kumlind..............grrrrrr grrrr grrrr simu iliita na alipoitoa alikutana na namba ya mheshimiwa raisi
"mheshimiwa raisi habari za sasa hivi"
"ni njema jenerali kuna taarifa na majina ya wahusika nimeyapata ila kiufupi nahitaji nkutane na wale vijana uliopewa na chifu saa 11:00 jioni nataka niwakabidhi hao watu mimi mwenyewe wapi ntakutana nao ntakujulisha dakika 20 kabla ya muda wa kukutana nao kikubwa waambie tu wakae tayari.....nkutakie mchana mwema.........tititi tititi"
"hata vijana sijawaona wote anyway ngoja niwajulishe" alijisemea jenerali huku akiwasha kompyuta yake na kushika simu yake ili ampigie kila mmoja akae tayari ni simu ya luteni kanali Charz ndiyo iliyomshtua kuwa kumbe mtu yule aalikuwa humo ndani, luteni kanali alimwangalia akasikitika sana.
"unajua nini kuhusu faili jeusi, luteni kanali charz"
"nadhani tunarudi pale pale kwamba mimi mwanajeshi wa cheo cha kati najua nini kuhusu mafaili yanayokaa na kutunzwa na watu wazito kabisa wenye maamuzi ndani ya jeshi, mbali na majalada yanayotunzwa masijala ila hili lilikuwa na upekee rafiki yangu mmoja aliyekuwa na cheo cha kapteni aliwahi kuniambia kwamba faili hilo linatunzwa ofisini kwa jenerali na hiyo ni baada ya kufukuzwa kazi na kumbukumbu zangu kufutwa na hata katika data zenu sidhani kama Luteni kanali Charz busungu ana exist ila kuna idara nyingine inayonithamini sana ndiyo maana hata taarifa zangu zipo huko na walikunyima makusudi kwa maana wanajua mamluki wapo kila kona hata kwenye ofisi yako"
"kwahiyo unataka kusema nini huna imani hata mimi"
"sio wewe tu hata kivuli changu pekee sikiamini, kwasasa nafsi yangu na mwili wangu hautatumika tena kufanya kazi ya upendo wa mshumaa tena kwenye gwanda kama ulilovaa wewe na baretiya zambarau achilia buti nyeusi au kaki ila huo upendo umesha zimika na mimi siko kwenye huduma ya jeshi kama data zenu zinavyosema kwenye nchi hii ninawasikiliza watu wawili tu,,,,,,,nkutakie mchana mwema usisahau kunipa location utakayopewa na mheshimiwa raisi" alisimama na kukitoa kitambulisho chake mfukoni na kukitupa kwenye ndoo ndogo ya kuhifadhia taka taka ofisini mle na akalifungua begi lake nakutoa gwanda safi la jeshi na kuliwea juu ya meza na kisha akatoa suti safi nyeusi hiyo alisita kuiweka juu ya meza aliirudisha ndani ya begi lake dogo akasimama na kutoa heshima kisha akauelekea mlango
"tutaonana saa 11 kijana nadhani ntajua ukweli wote na nikuhakikishie ntawabana wewe na chifu mpaka mniambie ukweli"
"huna ubavu wa kumbana kiongozi wako au na wewe umesahau miiko yako baada ya kulewa madaraka ya ujenerali mzee wangu......wacha tuone" akaufungua mlango na kuondoka ofisini hapo akiwa amevaa kofia na miwani kuficha utambulishowake, alijitahidi kufanya hivyo ila siyo macho ya watu waliopikwa na kuiva katika medani ya intelejensia mmoja wao alitoa simu na kutuma ujumbe mfupi "KOBRA MWEUSI AMEONEKANA KWENYE KIOTA AKIWA ANAPIGA SOGA NA NDEGE ILA ANAONEKANA HAJAONDOKA NA YAI, NAFUATILIA KUJUA KILICHOMLETA KAMA ANA MENGINE NAFIKIRI SASA HIVI HATAKUWA NA BAHATI, ATAKUTANA NA YAKOBO MUBASHARA HUKO MAWINGUNI. upande wa pili uliusoma ujumbe huo huku taa nyekundu zikiwaka kichwani mwao.
*************************************
NO COMMENT ⚠️⚠️⚠️
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom