Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Sidhani kama Watanzania ni wanafunzi wazuri. Muda si muda utasikia viongozi fulani wamefanya dili fulani na wamekula hela kishenzi. Sana sana mafisadi watakachofanya ni kuboresha zaidi mbinu zao za ufisadi ili wasiweze kugundulika kiurahisi.

Au kwa mtazamo mwingine, mafisadi watakuwa wamejifunza kutokana na makosa ya Masha na hivyo kuwalazimu kubadilisha tactics zao lakini.

Kwa hiyo sidhani kama fundisho walilopata ni la kuwafanya waogope na waache michezo yao michafu!

Kwa mtizamo wangu, "Waziri Kijana" sio tishio tena. Keshajichafua kama sio kuchafuliwa vya kutosha. Kila siku yuko kwenye media na kashfa mbalimbali, kuanzia issue ya albino, kuwatembelea watuhumiwa magereza, kupanga kumfilisi Mengi na nyingine nyingi. As far as I'm concerned, he is politically off the track. Tuwaachie wananchi wa huko Nyamagana 2010 wafanye maamuzi ya kina. Lakini kupitia CCM, msishangae wananchi wanachagua chama na sio mgombeaji. Huyu dogo anaweza kurudi na kupewa u PM. Did I just say that? Masha for the next PM? Sounds insane, but possible in Tanzania only!

Adios!
 
Nyani Ngabu,
Mkuu unajua hakuna kitu kigumu duniani kama utatumia elimu yako ya darasa kwa wale ambao hawana elimu..Na ukijaribu kuwa kama wao ndipo unapozidi kuharibu...
Acha elimu tu exposure pia unaweza kuchekesha vilevile, nakumbuka mwaka 1995 nilitaka kupeleka nyumbani matairi ya gari tubeless jamaa wakanambia hayawezi kuuzika Tanzania..Nikajaribu kuwaelekeza hawakunielewa zaidi ya kuona kuwa Mkandara kachanganyikiwa! Ikabidi nianze kutafuta matairi ya tube... mkuu kila mtu niliyemuuliza huku aliniona hamnazo na dunia gani naishi..

Wanabodi,
Tatizo la Masha naweza kuliweka sehemu mbili, kwanza aidha yupo ktk Mtandao na alikuwa anafanya deal Ama alikuwa akijaribu kubadilisha mentality ya watu ktk udanganyifu na ma deal ambayo hayana maslahi ya Taifa. Kwa kufanya hivyo amejikuta akifanya makosa ambayo sii makosa ila kwa yule mwenye kukisia kuna mchezo!
Nina hakika hata mimi katika position yake ningejaribu kuhakikisha nakwenda sambamba na taasisi ya tender kwa sababu record ya taasisi hii ni mbaya sana na ndiyo iliyotuingiza ktk hasara nyingi kubwa za kitaifa hasa nikipata malalamiko ya shirika hata moja tu..Hivyo Masha kachemsha kweli lakini hadi leo nashindwa kuelewa kama alichemsha kwa nia nzuri au mbaya!
Ajabu basi pamoja na makosa yote ya Masha, sisi wananchi na hasa hapa JF tumemkalia Masha kooni tumesahahu kabisa kwamba Taasisi hii ya tender ndiye yenye scandals kubwa sana na ulaji wote huanzia pale..
Ni rahisi sana kumkamata Masha au kiongozi yeyote nje ya board ya tender kuliko kufahamu kinachoendelea humo na hakika kama mnakumbuka tuliwahi kusema kama kweli viongozi wetu wanataka UWAZI basi tender yoyote ya kitaifa ni lazima ipitishwe na Bunge... Hili limeshindikana na limepigwa vita sana na viongozi tena wamelijengea hema kuwa ni siri ya serikali.. WHY?..
 
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Mwandishi Wetu Sarah Mossi na Mkurugenzi wa Gotham International Limited, Jack Steven Gotham

SWALI: Ulipataje hii tenda? Mlishindanishwa na kampuni nyingine?

JIBU: Mradi ulikuwapo siku za nyuma, ulipitishwa na Bunge mwaka 1986, akini wazo la kuwapo vitambulisho vya Taifa lilizaliwa 1968 na nchi nne za Tanzania, Kenya, Malawi na Zambia. Marais wa nchi hizi walifikiria juu ya kuwapo Muungano lakini baadaye wazo hili likakwama.

Mwaka 1972 wazo hili likaibuka tena lakini bado likakwama. Mwaka 1995 wakati nchi ilipoingia katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kila chama kikilalamikia chama kingine kwamba kilipandikiza watu toka nje ya nchi kupiga kura, wengine wakapiga kura zaidi ya mara mbili na wengine walipiga kura chini ya umri wa miaka 18. Wewe ni shahidi wa yaliyokuwapo Zanzibar. Likaja wazo la kuwe na vitambulisho vya Taifa ambalo lingeweza kuondoa malalmiko haya. Lakini likaja wazo jingine kwamba hatuna hela wala teknolojia na wakasema tujigharimie watu wanunue vitambulisho.

Mwaka 1996, Serikali wakaita tenda ya wazi na kampuni ya Regional Services Ltd ikashinda tenda hiyo. Kampuni hii ilisajiliwa katika visiwa vya Isle of Man nchini Uingereza. Ni ngumu sana kuitress kwani kampuni kama hizi husajiliwa kwa ajili ya kupata unafuu wa kodi na unaweza kufungua kampuni kwa saa tu. Mmiliki wake alikuwa Nairobi akiitwa Horatius Dagama-Rose, huyu alikuwa muasia wa Kabila la Goa.

Wakati akiwa katika mjadala na serikali alitaka kujua idadi ya Watanzania atakaoshirikiana naye pamoja na idadi ya watu nchini lakini serikali ikayumba katika majadiliano, ilikuwa haina uhakika na idadi ya watu. Na alikuwa mjanja baada ya kuona serikali inayumba akapandisha bei ya tenda aliyoshinda na kuruka mara mbili.

Serikali ikakataa na kutaharuki na kumtaka aandike hayo kwa maandishi kwa sababu hakukuwa na proper procurement procedure. Hii kampuni ikaipeleka serikali mahakamani na mahakama ikasema pande zote mbili zirudi mezani. Ndipo serikali ikashinda kwa kampuni ile kushindwa kuthibitisha gharama kubwa waliyoipandisha.

Wakati wote huo kukawa na shinikizo kubwa kutoka kwa nchi wahisani wakisema ni lazima iwepo vitambulisho kwa ajili ya uchaguzi, ili kutatua migogoro inayojitokeza wakati wa chaguzi.

Na wakati wote huo nilikuwa Special Envoy wa Rais Laurent Kabila DRC niliwavutia watu nyumbani wakasema naweza kusaidia kutatua tatizo la Vitambulisho vya Taifa nikaitwa na serikali kuja kutoa ushauri juu ya nini kifanyike.

Kutokana na uzalendo kwa nchi yangu niliishauri serikali mambo manne. Moja ni kwamba mradi huu asipewe mtu binafsi kwa sababu ni la usalama wa taifa. Jambo la pili nikashauri kiundwe chombo cha Serikali kitakachosimamia huo mradi.

Nikashauri pia vitambulisho vitolewe bure na tuwapigie magoti wahisani watusaidie kwani kwa kuwa na vitambulisho nchini tutakuwa tunajua nguvu kazi zetu ni za namna gani, tupeleke maendeleleo kwa kina nani, utakuwa unajua idadi ya watumishi ulionao serikalini pamoja na idadi ya walimu uliyonayo.

Nikashauri pia kitambulisho kilenge kumsaidia Mtanzania katika uchaguzi na kitaondoa kelele za watu kupiga kura mara mbili au kupiga kura chini ya umri. Nikawaaambia tukiyabeba haya tutapata fedha mara moja toka kwa wafadhili na hatutotumia fedha katika bajeti yetu.

Na ili kuyaweka haya vizuri nikashauri uwapo utafiti wa kina ili tuyaweke haya kimaandishi na iwepo andiko ambalo serikali italitumia kuelimisha watu wake juu ya umuhimu wa vitambulisho vya taifa.

Nikawaeleza serikali watafute mtu wa kufanya feasibility study na mimi nitaendelea kumshauri huyo mtu lakini nitakachosaidia ni kutengeneza hadidu za rejea utafiti huo. Nikatengeneza nikawaeleza nitaendelea kutoa ushauri ili kuendelea kuleta yale tunayohitaji Tanzania.

Lakini niliwashauri pia watafute kampuni kama za National Statistic Bureau na TISCO katika hili hawa kwa miaka mingi walikuwa wakitengeneza project nyingi za serikali, pia nikashauri wawatafute wataalamu pale UDSM wa kitengo cha Research Economic Bureau ambao hawa ni wataalamu wa mfumo wa mawasiliano wangewasaidia sana kwani ukija na huu mradi lazimi ujue nani duniani amewahi kuwa na vitambulisho kama hivi.

Serikali ikasema wakitangaza tenda hawana bajeti ya ufatifi huo ingawa walikuwa wakiamini hii ni muhimu. Wakati huo mimi nikaanza kupiga ndogondogo Jumuia ya Ulaya. Hawa wakasema tuko tayari kufadhili mradi ila tuletewe feasibilitu study yenu.

Nikaona aibu kurudi kwa EU kuwaambia hatuna hata hela ya kufanyia feasibility study. Wakati wote huo nilikuwa nikiendelea kushauriana na serikali nini kifanyike.

Ushauri wangu kwa serikali wazichukue taasisi nilizozitaja ili wajadiliane nao kiserikali. Bado mimi milikuwa naendelea kushauri bila malipo.

Walipokwenda ikaonekana hizi taasisi wanahitaji kulipwa ndipo serikali wakaomba niwasaidie niongee na EU. Nikawaambia waende kwa Rais lakini bado wakawa wagumu. Wakati huo Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Mohammed Seif Khatib baadaye akaja Omar Mapuri.

Na wakati wote huo nikiwa katika hali ngumu huku EU wakizidi kunitia presha ndipo nikasema nione nitakavyoweza kusaidia na kuanza kuzungumza na rafiki zangu hapa Tanzania nikawaeleza hali halisi wakaahidi kuona itakavyokuwa, hiyo ilikuwa 2003-04.

Nikawaeleza Serikali nipo tayari kufanya feasibility study kwa kushirikiana na timu yangu lakini je nitalipwa vipi? Kwa vile nakopa hela za watu, Serikali ikajibu tutakulipa na kunihakikishia kunilipa baada ya kuwa approved. Ndipo tukashauriana na rafiki zangu tuisaidie serikali. Nilifika mahali nikaacha shughuli zangu. Ilitugharimu na ikafikia kuogopa iwapo serikali haitolipa hela za watu lakini kwa kujenga uaminifu kwa watu waliotoa fedha zao bila riba kwa nia ya kuisaidia serikali.

Nikaanza kuangalia katika Afrika kuna vitambulisho katika nchi za Kenya na Afrika Kusini na Switzerland na kuanza kuwasiliana na watu wangu kule. Nikaendea Afrika Kusini kuangalia vitambulisho vyao na kupata picha ya wenzetu wanavyofanya. Kenya hatukuridhika sana, lakini hata Afrika Kusini nako tukaona havikidhi haja.

Tukaanza kuzunguka dunia nzima kila tunakosikia kuna vitambulisho na sapoti ya serikali katika safari zetu zote ni kupata connection ya nchi tunayokwenda ili tusaidiwe kiserikali.

© New Habari (2006) Ltd
All rights reserved

Jack Steven, save me all that waxing historic about the old century attempts to unite Tanzania and Malawi, question is how did you win the government deal and whether you were competed against anyone.

So, you somehow won this deal after you started out advising the government for free on how to navigate this murky ID project. You got into talking with them about securing funds and all that because they were impressed on your work as an envoy to a warring President of neighboring country! You were consulting free of charge because of your "patriotism." As a free consultant you perpetually lobbied the European Union in behalf of the government of Tanzania for aid.

So, at some point you go back and tell the Tanzanian officials that the Europeans need a feasibiliy study, and you Mr. Gotham, can run the study! This time you were gonna charge the government. And you seal the "tender." The deal is that you use your own money and the government promises you reimbursement. You don't have money so you go out and borrow other people's money banking on this promise from the government! The story ends there!

Now folks, if this chicane is telling the truth, then our government gave a consultancy deal to a weasel who told them that they need a consulted study! Do you hear that?

This character advised that the national ID project should not be handled by private parties because of its national security dimensions but there he is, a private individual named Jack Steven, running around carrying high stake sensitive messages of Tanzania to the European Union. (Nasema ni sensitive message kwa sababu unapoenda kuomba fedha kwa wahisani sio lazima uwaambie kila siri na kila kitu. Kwa mfano, uamuzi wa kuwa na national ID unaweza kuuweka kama ni kukuza demokrasia lakini ukweli tunaujua kwamba maamuzi yalishafanywa zamani zile hata kabla hatujui kutamka neno democracy! Na kwamba katika chaguzi zilizopita kumekuwepo na wizi wa kura lakini hakukuwa na ripoti za massive fraud zinazohusiana na voter identification. Kwa hiyo, unahitaji ku couch maombi yako ya hela kitaalam, na cha ajabu ni kwamba huyu mtu binafsi Jack Steven ndio anadai akaaminiwa kazi ya kubeba ujumbe huu wa Tanzania kwa wahisani. Yeye ambae anadai ndio alishauri hili dili lisifanywe na watu binafsi!)

So then, this Jack Steve, this is what makes me wanna go through the wall, this nark told the government to choose among three public stastistical entities (TISCO, a DSM University entity, and the Statistical Bureau) to do some consulting work but that he would be the one to advise them, all this in order to avoid private competition against himself! That's the chicanery here! And then at the end he emerges with the deal, or if you wanna call it a tender!

Who is this Jack Steve Gotham guy anyway? His company's website is designed to be shadowy as hell (look it up here). What does his work advising a warring president up in Congo have to do with a Tanzanian national ID tender deal? What is so incredibly expert that he advised here, that we need national IDs so that the government can be able to count its teachers? This "patriotic" liaison is shuttling between Tanzania and Europe doing our bidding for free, he says! Why weren't our paid officials stationed in missions across Europe in charge of begging the money? When, where and what entity processed the government tender to this Jack Steven consultant? Who done it?

Now, Mr. Gotham, listen here, and you listen good, for your own good, you two bit slick weasel of a consultant, taking advantage of unwary and corrupt government officials and lightweight journalists: You wanna start packing your rags and riches in quickness and head out to the nearest port of exit instead of giving all these condescending, mind-numbing, self-incriminating interviews before the Director of Prosecutions Feleshi reads your blabber and be right after your back side.

The people are apoplectic, up to the threshold, can't stand yet another Jim Sinclair and all these modern day Karl Peters who come here masquerading as messiahs of poor people even as they keep looting and raping the country's resources for years on end. You wanna go live with Sailesh Vithlani, the grim fugitive, warned! Enough, okay, enough!
 
Last edited:
Jack Steven, save me all that waxing historic about the old century attempts to unite Tanzania and Malawi, question is how did you win the government deal and whether you were competed against anyone.

So, you somehow won this deal after you started out advising the government for free on how to navigate this murky ID project. You got into talking with them about securing funds all that because they were impressed on your work as an envoy to a warring President of neighboring country! You were consulting free of charge because of your "patriotism." As a free consultant you perpetually lobbied the European Union in behalf of the government of Tanzania for aid.

So, at some point you go back and tell the Tanzanian officials that the Europeans need a feasibiliy study, and you Mr. Gotham, can run the study! This time you were gonna charge the government. And you seal the "tender." The deal is that you use your own money and the government promises you reimbursement. You don't have money so you go out and borrow other people's money banking on this promise from the government! The story ends there!

Now folks, if this chicane is telling the truth, then our government gave a consultancy deal to a weasel who told them that they need a consulted study! Do hear that?

This character advised that the national ID project should not be handled by private parties because of its national security dimensions but there he is, a private individual named Jack Steven, running around carrying high stake sensitive messages of Tanzania to the European Union. (Nasema ni sensitive message kwa sababu unapoenda kuomba fedha kwa wahisani sio lazima uwaambie kila siri na kila kitu. Kwa mfano, uamuzi wa kuwa na national ID unaweza kuuweka kama ni kukuza demokrasia lakini ukweli tunaujua kwamba maamuzi yalishafanywa zamani zile hata kabla hatujui kutamka neno democray! Na kwamba katika chaguzi zilizopita kumekuwepo na wizi wa kura lakini hakukuwa na ripoti za massive fraud zinazohusiana na voter identification. Kwa hiyo, unahitaji ku couch maombi yako ya hela kitaalam, na cha ajabu ni kwamba huyu mtu binafsi Jack Steven ndio anadai akaaminiwa kazi ya kubeba ujumbe huu wa Tanzania kwa wahisani. Yeye ambae anadai ndio alishauri hili dili lisifanywe na watu binafsi!)

So then, this Jack Steve, this is what makes me wanna go through the wall, this nark told the government to choose among three public stastistical entities (TISCO, a DSM University entity, and the Statistical Bureau) to do some consulting work but that he would be the one to advise them, all this in order to avoid private competition against himself! That's the chicanery here! And then at the end he emerges with the deal, or if you wanna call it a tender!

Who is this Jack Steve Gotham guy anyway? His company's website is designed to be shadowy as hell (look it up here). What does his work advising a warring president up in Congo have to do with a Tanzanian national ID tender deal? What is so incredibly expert that he advised here, that we need national IDs so that the government can be able to count its teachers? This "patriotic" liaison is shuttling between Tanzania and Europe doing our bidding for free, he says! Why weren't our paid officials stationed in missions across Europe in charge of begging the money? When, where and what entity processed the government tender to this Jack Steven consultant? Who done it?

Now, Mr. Gotham, listen here, and you listen good, for you own good, you two bit slick weasel of a consultant, taking advantage of unwary government officials and lightweight journalists: You wanna start packing your rags and riches in quickness and head out to the nearest port of exit instead of giving all these condescending, mind-numbing, self-incriminating interviews before the Director of Prosecutions Feleshi reads your blabber and be right after your back side.

The people are apoplectic, up to the threshold, can't stand yet another Jim Sinclair and all these modern day Karl Peters who come here masquerading as messiahs of poor people even as they keep looting and raping the country's resources for years on end. You wanna go live with Sailesh Vithlani, the grim fugitive, I would advice. Enough, okay, enough!

Okay, what about Dr. Masau?
 
...200m USD kwa ID? hivi kuna emergency gani ya huo mradi,hatuna umeme,Dar haina maji,shule zetu chakaa mbaya mbovu,barabara za lami muhimu za kuunganisha mikoa yote hatuna...kwanini tusitumie hizo pesa kwanza kuongeza umeme na barabara zetu na hizo ID zikafanyika baadaye,sioni sababu kabisa ya kutumia 200m kwa ajiri ya Id huku mambo muhimu kama umeme ambayo yangeongeza uchumi wetu kwa kiasi kikubwa na kupunguza umaskini hayafanyiki,huu mradi usimamishwe tuu na hizo pesa ziwe diverted kwenye infrastructure haraka sana
 
Changa la macho hilo, ili kuziba makelele kwa Masha imeonekana bora watangaze kila kitu na kuipiga kumbo ile kampuni ya sagem ,hivi ndio itakuwa yamekwisha au ndio kulindana huku ,CCM wameshamwokoa mwenzao.
 
...200m USD kwa ID? hivi kuna emergency gani ya huo mradi,hatuna umeme,Dar haina maji,shule zetu chakaa mbaya mbovu,barabara za lami muhimu za kuunganisha mikoa yote hatuna...kwanini tusitumie hizo pesa kwanza kuongeza umeme na barabara zetu na hizo ID zikafanyika baadaye,sioni sababu kabisa ya kutumia 200m kwa ajiri ya Id huku mambo muhimu kama umeme ambayo yangeongeza uchumi wetu kwa kiasi kikubwa na kupunguza umaskini hayafanyiki,huu mradi usimamishwe tuu na hizo pesa ziwe diverted kwenye infrastructure haraka sana

Kwa sababu Miafrika Ndivto Tulivyo!
 
Wanabodi,
Naomba kuuliza kitu kimoja.. Hivi kama wewe ni waziri na umenusa harufu ya rushwa ktk taasisi ya tender - ni hatua gani utakazo chukua kisheria wakati huna ushahidi wa kimaandishi zaidi ya barua ya mhusika mmoja..
Sina maana naungana na Masha isipokuwa najaribu kutazama swala hili upande wa pili..
Let's say, Masha au mtu mwingine yeyote ktk nafasi yake angeona kuna maonezi ktk utendaji kazi wa board hiyo tya Tender na umeambiwa kuwa watu wanahceza mchezo utafanya nini?..
Je, utasubiri hadi deal limepita..
Utalizuia kabla halijafanyika na kwa njia gani ambayo itakubalika...
Je, Bunge ni sehemu ya kwanza ikiwa tender zinasemekana kuwa ni siri za serikali!..
 
Masha acts on ‘libelous’ newspapers

Monday Feb 16, 2009 DAILY NEWS Reporter, 16th February 2009 @ 10:29

Home Affairs Minister Lawrence Masha said today that he has instructed his lawyers to take legal action against newspapers that carried articles linking him with graft. The newspapers reported that Mr Masha was using his position to influence the tendering process in the multi-billion shillings national identity cards project.

The minister told a news conference in Dar es Salaam that he has instructed IMMA Advocates to initiate legal action against all those involved in the accusations. Mr Masha also used the opportunity to challenge those who claim they have proof of his interference in the tender process, which is against the law, to bring forward their evidence.

The news conference comes after recent media reports that he had interfered with the tendering process to find the company to produce the country’s first national identity cards using smart-card technology. Mr Masha refuted reports that he was in Geneva on October 5, last year with Sagem Securite Company executives negotiating the offer.

He showed his passport to journalists that indicated that he entered the country on October 5. The minister also said October 5, was a Sunday and UN offices were closed on that day. “This is something they could have checked with me, but since there is something else they are looking for they did not bother to do that,” said Mr Masha.

He further said that in his life, he has never set foot in the hotel cited in newspapers that the meeting between him and Sagem executives took place. He said the confidential document leaked to the media and the internet was an official document, but does not prove that he interfered with the tendering process. “There is no place in the letter that I said which bidder should win the tender, I just advised my Permanent Secretary to seek further advise from the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), who agreed with my observations of the said faults,” he explained.

Mr Masha said that it is not only the Sagem Securite, but four companies, which told him that there were irregularities in the tendering process, however, the minister said that he advised them to adhere to the tendering procedure and forward their complaints to the proper authorities. He said that one of the complaints was that information from the confidential tendering screening procedure was leaking out. However, the minister said that his ministry has tightened documentation and security at the ministry to ensure that such information remains confidential.
 
Kwa haraka haraka, japo sipo upade wowote kwenye hili, kwani SAGEN na kufunguliwa kwa ofisi za UN kuna uhusiano gani wadau?
 
hivi hakuna mtu aliyemuuliza malalamiko ya hayo makampuni yeye aliyapata wapi, lini, na kwa njia gani?
 
hivi hakuna mtu aliyemuuliza malalamiko ya hayo makampuni yeye aliyapata wapi, lini, na kwa njia gani?

Nadhani hii mikutano na 'waandishi wa habari' huwa sio 'interactive' ni kama unaangalia taarifa ya habari kwenye TV?
 
Jamani huyu Masha ni waziri wa serikali. Kaeleza wazi ni nini alikifanya kwa mujibu wa kazi zake za uwaziri.-

1. Aliona mchakato wa kuchagua wazabuni una kasoro kwa hiyo akamwambia Katibu
Mkuu wake achunguze na apate ushauri wa PPRA na PS akafanya hivyo na PPRA
ikathibitisha kuwa kweli kulikuwa na kasoro kama alivyoziona waziri Masha. Jee hapa
waziri Masha kaingilia mchakato vipi? Mlitaka aachie kasoro hizo ziendelee na akina Dr.
Slaa waje kumsulubu baadae?

2. Baada ya Waziri Masha kuona mapungufu hayo na kumjulisha PS wake, pia alimjulisha
boss wake waziri Mkuu katika utaratibu wa kawaida wa kutoa ripoti za utekelezaji. Jee
hapa Wziri Masha ameingilia mchakato upi? Au mlitaka Waziri Mkuu amjie juu baadae
na kumshutumu kwa kutotoa taarifa?

3. Dr. Slaa naye akakurupuka kutaka kuleta hoja binafsi bungeni bila kufanya utafiti
wa kutosha. Speaker na wabunge wote wakiwemo wa CCM, wakahamasika na kwa
kuwa lengo lilikuwa kummaliza Masha, wakaungana na wapinzani. Wakapeleka haraka
haraka hoja hiyo kwenye kamati ya Bunge ili iamuliwe katika kikao hicho hicho na
kummaliza Masha kwa kutoa azimio la kutaka ajiuzulu. Mpaka bunge linamalizika
Masilingi akawa bado amepatwa na kigugumizi. Natumai baada ya kutolewa kwa hoja
tulizozisikia leo. Dr. Slaa akatoka kalowana na kafunga mdomo hadi leo. Jee hapa
waziri Masha kujihami anakosa gani?

4. Magazeti ya IPP yakaandika kuwa Masha alikutana na wawikilishi wa Sagem Geneva.
Waziri Masha amethibitisha beyond doubt kuwa tarehe zilizotajwa hakuwa Geneva bali
alikuwa njiani toka Far East. Tena keleza kuwa hajafika tangu azaliwe katika Hoteli
iliyotajwa huko Geneva na kuonana na watu hao na ushahidi anao. Hivi watu
hawajiulizi ni kwa nini magazeti ya IPP yaandike uongo wa namna hii kwa waziri wa
serikali? Hapa ni nani anaingilia mchakazo wa Zabuni ni Waziri Masha au IPP? Kwa
kweli mimi naunga mkono hatua ya waziri Masha kuwashtaki kwani sasa hawa jamaa
wamezidi uzushi. Mara waziri kijana kasema hivi mara tumetishiwa maisha. Wakiombwa ushahidi
hawana. Inaonekana kuwa mambo mengi ya hawa jamaa ni uzushi mtupu.

5. Waziri Masha amesema wazi kuwa, kama waziri katika wizara yake, anawajibika kwa
mambo yote, anayoyajua na asiyo yajua. Kwa hiyo ni wajibu wake kuhakikisha kuwa
mambo yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu zilizopo kwa
kurekibisha yale yanayomfikia. Kinyume cha hivyo itabidi awajibike. Mtakumbuka
Raisi Mstaafu Mwinyi alipokuwa waziri wa wizara hiyo hiyo, ilibidi ajiuzulu kwa mauwaji
yaliyofanywa na askari mikoani wakati yeye yuko Dar es Salaam.

6. Hongera waziri Masha. Wewe mi mfano wa mawaziri bora, wenye uwezo na upeo mkubwa
na unaitumia vema elimu yako kusaidia taifa kwani hii ni mara ya pili kuokoa jahazi
ukianzia ripoti yako ya madini.
 
TK.. I really hate to bust your bubble.. but there are more to this than SAGEM and Masha...

CLUE: MRADI HUU WA VITAMBULISHO ULISIMAMISHWA HUKO NYUMA NA MCHAKATO KUANZA UPYA. WHY AND WHAT HAPPENED THEN?
 
Kwa sababu CCM wanatafuta pesa ya kampeni next year.
 
Jamani huyu Masha ni waziri wa serikali. Kaeleza wazi ni nini alikifanya kwa mujibu wa kazi zake za uwaziri.-
Hongera waziri Masha. Wewe mi mfano wa mawaziri bora, wenye uwezo na upeo mkubwa na unaitumia vema elimu yako kusaidia taifa kwani hii ni mara ya pili kuokoa jahazi ukianzia ripoti yako ya madini.

Hongera tk. Wewe ni mfano wa mawakili bora, wenye uwezo na upeo mkubwa na unaitumia vema elimu yako kumtetea Waziri Masha kwani hii si mara yake ya kwanza kupindua jahazi ukianzia ripoti ya kuvinjari Keko usiku.
 
tk,
Ripoti gani hiyo ya madini? Siye huyu huyu Masha aliyekuwa wakili wa kampuni ambazo hivi sasa zinapora madini ya Watz?
 
Back
Top Bottom