Aendelee kukaa marekani tu awe kama rais Paul Biya wa Cameroon anayeongoza nchi akiwa zake Paris hotelini.Afrika imerogwa Afrika imejaa wapumbavu,utawasikia mitaa fulani wakisema mama anaupiga mwingi
 
Shime shime shime watumishi wenzangu ...asiye na mwana aeleke jiwe.

Tunapoelekea Mei Mosi ya kwanza ya Rais Samia S. Hassan akiwa katimiza mwaka mmoja kazini si vibaya tukatanguliza yale tunayotarajia kusikia toka kwake.

Kama alivyotuahidi nyongeza ya mshahara mwaka huu bila shaka hilo limeisha ila ni wazi haki za watumishi zimekandamizwa kwa muda mrefu sana.

Basi si vibaya tukimueleza Mama nini hasa tungependa toka kwake. Ningependa kusema machache.

1. Haki ya Mtumishi kuhama kituo cha kazi
Hili limekuwa ni tatizo sugu na la muda mrefu sana. Watumishi wa serikali hasa walimu wamekuwa wakipokwa haki yao ya kuhama kwa hiyari. Serikali imekuwa ikitoa kigezo kuwa itasababisha upungufu wa watumishi huko watokako. Sijui hoja hii ina mashiko gani maana wengine wakitoka wengine wanakuja.

Lakini hata sababu ya msingi kabisa ya kwenda unganisha familia watumishi hawasikilizwi hii hupelekea kuibuka kwa matapeli na watumishi wanapigwa sana pesa wanapopigania uhamisho.

Tungependa Mama alitizame hili kwa uzito wake.

2. Fao la uzazi
Nyinyi ni mashahidi nafikiri wengi hapa mnafahamu haki hii ambayo watumishi wamepunjwa. Tungependa Mama alitizame hili pia kwa macho yake mazuri kabisaa.

3. Annual increment
Hapa wala hakuna maneno mengi nafikiri ninyi ni mashahidi Awamu ya tano ilichofanya...ilifutilia mbalii.. hili nalo litizamwe kwa macho yake yootee

... Endeleeni na mapendekezo ni nini Tumwambie Mama.
Acheni ujuha wa kufanya kazi kama msukule. Muwe mnaweza kuhoji hasa ile msukule kule halmashauri
 
Back
Top Bottom