Mei Mosi ya mwakani tukiwa na Rais mwingine na akaja na sababu zake za kutoongeza mshahara,watumishi wa umma watapaswa kusubiri tena?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,919
2,000
Kwakuwa hakuna aijuae kesho kwa maana leo unaweza kuwa mzima na kesho ukatangulia mbele za haki au kupata ulemavu wa Kudumu, n.k, ni sahihi kuishi kwa kutegemea matakwa au fadhila za binadamu mwenzako hasa kwa mambo sensitive ya ktaifa kama hili la haki na masilahi ya watumishi wa umma?

Swala la mishahara ya watumishi na mambo mengine katika nchi, kwanini tuyaache yategemee utashi binafsi wa Raisi?

Je, kwa bahati mbaya mwakani tukawa na Raisi mwingine kwasababu yoyote ile kulingana na katiba yetu, na Mei Mosi Raisi huyo akaamu kutongeeza mishahara kwasababu yoyote atayoitoa, watumishi watapaswa tena kusubiri miaka saba ndio masilahi yao yaangaliwe?

Kama ambavyo leo hii Magufuli hayupo, nani ana uhakika mwakani Mama Samia atakuwepo au yeye mwenyewe atakuwepo?

Ukweli ni kwamba, anaweza asiwepo Mama Samia na hata makamu wake au wanaweza kuwepo lakini wote wasiwe fit kukalia hicho kiti.

Kama utadhani mimi nina mawazo mabaya, basi walioandika katiba yetu watakuwa na mawazo mabaya zaidi.

Wakati umefika, mambo ya msingi katika nchi yasiwe ni matakwa binafsi ya Raisi vinginevyo nchi hii na watu wake wataendelea tu kupiga mark time miaka nenda miaka rudi.
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
2,032
2,000
Kufa hamfi ila cha moto mtakiona, na ni wachache wenye udhubutu wa kuacha kazi, vumilieni mambo mazuri yanakuja.

Watz wanyonge kupandishwa mishahala ni takwa la kisheria ila kuweni wazalendo tujenge viwanda na ndege

Poleni sana kwa kwa mei mosi ya leo
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,842
2,000
Bavicha si mlisema matatizo yote kaondoka nayo Magufuli?

Hivi vilio vinatoka wapi tena?
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,358
2,000
Kama ambavyo leo hii Magufuli hayupo, nani ana uhakika mwakani Mama Samia atakuwepo au yeye mwenyewe atakuwepo?

Ukweli ni kwamba, anaweza asiwepo Mama Samia na hata makamu wake
Duh....!. Hii ni kama ile ramli chonganishi!. Tuchunge sana kauli zetu, kauli nyingine huumba hadi vifo!.


P
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,847
2,000
Gombea ubunge, huko ndiko kuna fedha za kutosha. posho za uhakika, hakuna malimbikizo.
kamwe hutosikia wabunge wakilalamika kuhusu malipo hata siku moja.
miaka 5 inatosha kupiga hatua.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,919
2,000
Duh....!. Hii ni kama ile ramli chonganishi!. Tuchunge sana kauli zetu, kauli nyingine huumba hadi vifo!.


P
Hakuna jipya nililoongea hapa lisiloelewaka/iisilowezekana kutokea zaidi tu ya ukweli kwamba binadamu tumeumbwa kusahau.
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,166
2,000
Afrika inaangamizwa na wanasiasa wa Afrika wenyewe.

Wale wale waliokua wanamsaidia rais yule aliyefariki ndio hao hao walopo Leo .
Basi tutegemee tu huruma na utashi viendelee kutuongoza.

Hata hivyo Mama yupo katikati ya mbwa mwitu wakali wanaojifanya kondoo.
Kwa asili na hulka na imani na mila za mama Samia ni mtu msafi kabisa mwenye kujua maana ya utu,haki,thawabu mbele za Mungu,wema , sadaka kwa wengine na kujali wengine kwa kile alichojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Cha msingi ni kumshauri namna bora ya kupata vyanzo vipya vya mapato na wapi pa kupunguza ili mwakani aweze kutimiza ahadi yake
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,358
2,000
Hakuna jipya nililoongea hapa lisiloelewaka/iisilowezekana kutokea zaidi tu ya ukweli kwamba binadamu tumeumbwa kusahau.
Yes hakuna jipya ulilosema, ila hata ile kuwaza tuu kuwa kuna uwezekano aliyeahidi asiwepo, na ukaenda mbali zaidi hata kwa makamu wake, then huko kuwaza na kuandika ni tayari umetoa kauli!.

Wanabodi,

Kauli huumba, hivyo tusishabikie sana kauli zenye negativity na kujikuta kumbe ni sisi tuna sababisha hizo negatives kwa kuziumba kwa kauli zetu. Badala yake tuwe positive kwenye kila jambo, hata tukihisi jambo fulani sio jema, tutumie kitu kinachoitwa affirmatives kubadili negatives kuwa positives.

Tupendane, tuombeane mema hata maadui zetu, tuwaombee mema hivyo kutengeneza positive karma effects.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa ...

Wasalaam.
Paskali
Sasa kauli kama hizi ni ramli ...zinaweza kutuumbia majanga tena, please!.
P
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom