Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Katika miaka 10 ya awamu ya nne ya JK (2005 hadi 2015), kila mwaka ilikuwa ifikapo tarehe mosi Mei serikali ilikuwa ikitamgaza ongezeko la kiasi fulani kwenye mishahara ya watumishi wake wa serikali. Watumishi hawa walikuwa wakifurahi sana ifikapo Mei mosi kwa sababu hiyo.
Ukweli ni kuwa kitendo hicho kilikuwa ni danganya toto tu kwani ongezeko lililokuwa likitolewa lilikuwa sawa au chini ya annual increments za mishahara yao. Annual salary increments zao stahiki walikuwa hawazipati, badala yake walipata hiyo ongezeko la Mei mosi ya mishahara yao. Kibaya zaidi upandaji wa ngazi katika salary scales (aka promotion) ulikuwa wa nadra sana. Hivyo mtumishi wa serikali alijikuta kwenye ngazi moja ya mshahara kwa zaidi ya miaka 6 au 10. Kwa mjibu wa standing orders za utumishi wa umma, annual salary increment inapaswa kutolewa kila mwaka na mtumishi anapaswa kupanda ngazi moja kwenye salary scales zake kila baada ya miaka 2 au 3. Waliokuwa wakizidai walipewa visingizio mbali mbali - km taarifa zao za siri au opras zao kutokuwapo etc. Upandaji ngazi umekuwa wa upendeleo au kwa kutoa cho chote (rushwa) kwa maafisa utumishi etc. Watumishi wengi wamekuwa wakistaafu bila kufika mwisho wa salary scales zao.
Badala ya ongezeko la mishahara la kila Mei mosi serikali ingalifaa ifanye yafuatavyo:
1. Annual salary increments za mishahara ya watumishi wa umma zitolewe kila mwaka. Kusiwe na kisingizio cho chote.
2. Serikali ihakikishe mtumishi anapanda ngazi moja kwenye salary scale yake kila baada ya miaka 2 na isizidi miaka mitatu kama ambavyo standing orders zinavyoelekeza. Kusiwe na kisingizio cho chote. Mambo ya opras yafutwe. Kama mfanyakazi hafai ni wajibu wa mwajiri wake kujua hilo na kumchukulia hatua za kinidhamu ikiwamo kumwachisha au kumfukuza kazi. Kwa wale watumishi wengi ambao wamedumu kwenye ngazi moja kwa zaidi ya miaka mitatu warekebeshiwe ngazi zao za nyuma na kupata accelerated promotions zitakazowaweka walikostahili kuwa hadi sasa.
3. Posho ya usafiri wa kwenda na kurudi kazini: Watumishi hawa wanatumia kiasi kikubwa cha mishahara yao kwa gharama za usafiri wa kwenda na kurudi kazini. Waraka wa posho ya usafiri (transport allowance) urejeshwe kama ifuatavyo:
- Watumishi wa ngazi za chini stahiki yao ni daladala = Sh 40,000 kwa mwezi.
- Watumishi wa ngazi ya kati stahiki yao ni bodaboda = Sh 100,000/ kwa mwezi.
- Watumishi wa ngazi za juu stahiki yao ni mafuta ya gari = Sh 200,000/ kwa mwezi.
NB: Watumishi wa umma wa kisiasa wanapata posho hii tena kwa kiwango kikubwa sana eg wabunge. Ndiyo maana uchaguzi mkuu unapokuja kila mtumishi wa umma anatamani kwenda kugombea ubunge!
4. Posho ya kutoishi mijini (Out of town residential allowance): Watumishi wanaoishi mijini wana fursa nyingi za kutengeneza kipato halali cha ziada nje ya kazi zao za umma. Wanaoishi mbali na miji hawana fursa hizo na hivyo wengi wamekuwa wakikataa kwenda kufanya kazi huko au kutafuta visingizio vya kuhama maeneo hayo. Ikumbukwe kuwa huko mbali na miji (vijijini) ndiko asilimia 80% ya watanzania wanaishi. Posho hii itolewe kama ifuatavyo:
- Watumishi wa ngazi chini = Sh. 50,000/ kwa mwezi.
- Watumishi wa ngazi ya kati = Sh 100,000/ kwa mwezi.
- Watumishi wa ngazi ya juu = Sh 200,000/ kwa mwezi.
5. Kiwango cha pensheni inayolipwa kila mwezi kwa wastaafu waliokuwa watumishi wa umma: Hali ilivyo sasa licha ya kiwango hiki kuwa kidogo, kiko fixed na hivyo thamani yake hupungua kila mwaka. Kama ilivyofanyika kwa viongozi wakuu serikalini, ingalifaa kiwango hiki kikawa pegged kwa asilimia fulani ya incumbant salary ya existing equivalent officer. Ile ya mkupuo ndiyo iendelee kwa kikokotoo kilichopo cha denomator ya 540.
NB: Posho hizi zisikatwe kodi.
Haya yakifanyika watumishi wa umma watanufaika na hakutakuwa na haja ya kupandisha mishahara kila Mei mosi wala kubadilisha salary scales za mishahara ya watumishi hawa mara kwa mara au kubadilisha miundo ya mishahara ya watumishi hawa mara kwa mara. Miundo na salary scales za watumishi hawa ni mizuri sana (compared to most private sector), tatizo ni utekelezaji wake inapokuja kwenye promotions, annual increments, allowances and penssion.