Watu wa TCRA wakikata Internet nchi nzima hadi masaa mawili je huduma muhimu yaani Critical Services huwa salama kwa kiasi gani?

Watu wa TCRA wakikata Internet nchi nzima hadi masaa mawili je huduma muhimu yaani Critical Services huwa salama kwa kiasi gani?

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,630
Reaction score
25,586
Katika nchi yoyote ile huduma za internet ni huduma nyeti sana kwa maana kwamba mahospitali, miundombinu kama usafiri, njia za reli na sehemu zingine nyeti hii ni huduma muhimu isohitaji hata nukta ya sekunde kuhujumiwa.

Kitendo cha TCTA kukata mtandao wa internet nchi eti kwasababu ya kuzuia watanzania wasimsikilize Humphery Polepole ni cha kinyama, cha kutokuwa na uelewa wa mambo na ni cha kikatili.

Fikiria mahospitali, huduma kama za usafiri watu kuhitaji kutumia kadi mitandaoni, matumizi ya simu ka ajili ya shughuli mbalimbali, huduma za mabenki na sehemu nyingie zote nyeti, uzime mtandao kwa masaa mawili, je nchi itakuwa salama kiasi gani?

Najiuliza tu au wana JF nawauliza maoni yenu kama kuna mwenye idea hii ya TCRA ni ujinga, kutokuelewa au ni nini?

Tusema madaktari Mloganzila wahitaji kufanya checkups na membo mengine au katika hospitali zingine kwahitajika matumizi ya mitandao je hali huwaje huko watu hufa au vipi?

Je, pia nini madhara ya hii kitu kwa siku zijazo?

Au kuna njia mbili za internet au VPN zatumika kwa sehemu niyingi kwa siri?

Nani aamua kukata internet nchi nzima kwa masaa mawili?

Kwa sababu Humphery Polepole yeye husubiri masaa mawili yapite ndo hurusha video yake.

Sasa hizi games za TCRA wacheza na Humphery Polepole kwa kutumia maisha ya watanzania?

Humphery Polepole hachezi games bali yupo kwenye kazi ngumu ya kurekebisha uzozo uliopo.
 
Wana block sites tu
Kwahiyo TCRA wakiamuru ISPs wazime baadhi ya mitandao huwa wazima tu mitando ya kijamii na sio internet kwa ujumla?

Nnachofahamu na ambacho nimekiona ni kwamba serikali kupitia TCRA wana options mbili moja ni kuamuru watoa huduma yaani ISPs kuzima access kwa watumiaji wa mitandoa ya kijamii kupata kwenda Youtube, X au IG na kwingine.

Lakini pia la pili na ambalo ni la kutisha ni pale maagizo yanapokosewa ISPAs na kukuta internet imekatwa kwa bahati mbaya ( kwa saa mbili) bila kufahamu hivyo.

Ukifanya hivyo yamaanisha kwamba si tu mitandoa ya kijamii inakuwa imezuiwa kwenda kwenye interent bali pia apps zingine muhimu kama Uber zinakuwa zimedhurika.

Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu internet kukatwa ndani ya nchi badala ya social media tazama mitandao kama Netblocks ambao huweza kutoa tathmini ya ni kwa namna gani nchi fulani imekata internet.
 
Huwa haizumwi Internet, wanazima mitandao ya kijamii,
Mwaka 2020 kwenye uchaguzi serikali iliamuru internet na mitandao ya kijamii kukatwa/kuzuiwa yaani vyote kwa pamoja.

Na safari hii tutegemee kwamba hali itakuwa ni mbaya zaidi ya 2020.
 
Huu ni ujinga na upumbavu kuathiri huduma za internet kwa watu wengi kisa ni mtu mmoja anaongea siasa asisikilizwe. Ingekuwa nchi zingine yule mkurugenzi angefurushwa kazi kwa kutumiwa kisiasa. Huwezi kuzima internet eti kuna mwanasiasa mpinzani anaongea mtandaoni asisikilizwe. Kwa hulka za watanzania kutoshobokea mambo ya kisiasa kamwe hawastahili kuzimiwa internet.
 
Nakuunga mkono kwa 101%

Na uamuzi wa kujiuzulu wa DG wa TCRA huwa ni wa haraka mno.
 
anayewatesa ni huyo pole pole anayetoa hizo hotuba.
Kwanini asijitokeze hadharani na kusema kuliko kutumia mitandao ya kijamii na kuwapa watu shida
 
anayewatesa ni huyo pole pole anayetoa hizo hotuba.
Kwanini asijitokeze hadharani na kusema kuliko kutumia mitandao ya kijamii na kuwapa watu shida
Sasa anaeteseka na kuonekana wa hovyo ni yule anaezima mitandao au yule anerusha ujumbe?
 
Sasa anaeteseka na kuonekana wa hovyo ni yule anaezima mitandao au yule anerusha ujumbe?
Anayerusha ujumbe.
Vita vyao vya ujanja ujanja .na lao Moja hao.unadhani mwisho wa pole pole utakuwa lininwa kutoka hizo hotuba?
 
Anayerusha ujumbe.
Vita vyao vya ujanja ujanja .na lao Moja hao.unadhani mwisho wa pole pole utakuwa lininwa kutoka hizo hotuba?
Nilidhani utasema wamuachie aseme mwisho atachoka ila waache watanzania wasikie anachokisema.

Si hatoathiri chochote?
 
Nilidhani utasema wamuachie aseme mwisho atachoka ila waache watanzania wasikie anachokisema.

Si hatoathiri chochote?
Hao wenzako lao moja.huyo Pole pole sio wa kumuamini.wanaanzisha maigizo.
 
Back
Top Bottom