Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Elimu ya kutunza pesa wengi wetu imetushinda. Hakuna umasikini mbaya kama kujutia maisha yaliyopita, kama ungetumia pesa vizuri ungefika mbali. Hii elimu ni muhimu kuwafundisha watoto. Wakipata pesa wasihamaki.
Ni kama vike unavyokunywa chai kila siku, hata ukiwa mkubwa chai unakua umeizoea, mtoto akizoea matumizi mazuri ya pesa tangu akilwa mdogo ukubwani haitampa shida.
Wenye uwezo huanza kumpa mtoto shilingi 10,000 kwa wiki kwa matumizi ya shule ya msingi. Lakini ikifika weekend akueleze matumizi yake ya Juma zima. Hapa ukaribu na mtoto unahitajika. Mtoto asikuogope akueleze kabisa alikula mihogo ya kuchoma, chips dume nk. Muulize pia sababu ya kula vitu hivi wakati nyumbani kuna chakula.
Ukiona mrejesho wa 10,000 ni mzuri unaaweza kumpa laki moja, hapa akiwa A level, pia mhimize umuhimu wa kujiwekea akiba. Pia kama una uwezo waweke watoto wawe nadhifu. Watoto waliokuwa na mavazi duni huwa wanapata shida kupata control ya kununua mavazi.
Kuna watu wana milioni 40 bank lakini ana mashati matano na viatu pair mbili, pair nyungine ni trainers 👟. Hivi vinamtosha kabisa. Na wengine watakuambia tangu wakiwa sekondari mzee Christmas aliwapa laki moja ya shopping kila mtu na alijifunza kununua nguo za kumtosha kwa mahitaji yake.
Kuna watoto wana drop out chuo kwakua wanashika boom na hii inakua mara yake ya kwanza kumiliki pesa ndefu. Anafikiri haitaisha, matokeao yake anashindwa kumudu gharama za kujikimu.
Kila mtu anayo style yake ya maisha lakini, lakini kuna vi bibi au wamama wenye class na wana hand bags tatu nzuri. Sasa inamkuta binti ana handbags 20, hizi zote ni za nini na kila msimu una fashion yake. Ukizoea matumizi mazuri ya pesa unajifunza ku balance maisha yako vizuri.