Matumizi ya nepi za kutupa (diapers) yatajwa kusababisha UTI kwa watoto

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
pampo.png

Matumizi ya muda mrefu ya nepi za kutumia na kutupa za watoto maarufu pempasi yamekuwa yakisababisha athari kwa kundi hilo huku walio wengi wakipata magonjwa ya ngozi na mfumo wa mkojo yaani UTI.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Oktoba 23, 2023 na Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Lilian Mnabwiru wakati akitoa mada wakati wa mafunzo maalumu kwa vyombo vya habari yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya kuhusu umuhimu wa huduma za uchunguzi na vipimo kupitia maabara za afya ya binadamu ili kuwezesha matibabu sahihi kwa wagonjwa.

Kwa mujibu wa Dk Mnabwiru, pempasi zina kiwango maalumu cha kujaa na hujaa kulingana na namna mama anavyomlisha mtoto wake lakini haitakiwi kuachwa ivaliwe kwa zaidi ya saa nane.

pampazzz.jpg

“Wengi pempasi wanazitumia vibaya, mtoto anakaa nayo kwa muda mrefu. Unatakiwa uwe unaangalia sasa hivi zipo nyingine zinatoa ishara ukiona mstari umebadilika rangi inabidi umbadilishe.

“Wengine wanafanya hivyo kwa kuhakikisha asitumie nyingi anamuacha mtoto anakaa nayo asubuhi mpaka jioni, mtoto anakojoa mkojo unaendelea kuwa pale pale unapokuwa umejaa unajikamua kwenye pempasi, tunawatesa watoto,” amesema Dk Mnabwiru.

Amesema zamani ilikuwa kinamama wanawavisha vitambaa watoto ambavyo vikiloa lazima vibadilishwe au nepi za kawaida, “Sasa hivi wanawaacha na mkojo wanakaa nao pempasi mpaka limechafuka madhara yanakuwa ni mtoto kupata UTI.”

Dk Mnabwiru amesema wazazi wengi wamekua wavivu na kushauri kwamba ni vema mtoto kuvishwa chupi peke yake mchana akae nayo na kupata hewa ilia pate afya bora.

“Mvalishe mtoto kichupi akojoe, umtoe msafishe futa ili mtoto awe huru na awe na afya, wakati wake ukifika akajua kwenda chooni anaendelea kama kawaida lakini amekuwa vizuri bila changamoto yoyote,” amesema.

Mbali na magonjwa mbalimbali yanayowapata watoto, pempasi bado zimekuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira ambapo wazazi wamekuwa wakizitupa ovyo katika maeneo bila ya kuzihifadhi.

Wataalamu wa afya duniani wanasema kuwa pempasi ni chanzo kingine cha maradhi ya mlipuko (Kipindupindu) ambapo kuna baadhi ya wazazi na walezi huzitupa kwenye vyanzo vya maji na kusababisha kusambaa vinyesi katika maji na baadaye kupelekea maradhi ya kipindupindu, matumbo na kuharisha damu.

Pempasi ya kwanza iliingia sokoni mwaka 1961 nchini Marekani baada ya Victor Mills kuja na wazo mwaka 1956 baada ya kuchoshwa kubadili nepi za mjukuu wake. Sasa pempasi imesambaa duniani kote na wazazi wanaona ndio njia rahisi zaidi ya kudhibiti haja za watoto.

Tanzania pempasi zilianza kutumika mwaka 2000 na zimezidi kuenea kwa kasi hasa maeneo ya mijini na hivi sasa wazazi wamekuwa watumiaji wakubwa wa pempasi ili kurahisisha matumizi ya mipira, nepi na vitambaa.

Zamani ilikuwa kila mzazi lazima achane vipande vya kanga lakini pia anunue nepi kwa ajili ya kumvisha mwanaye lakini sikuhizi ni kawaida kila nyumba yenye mtoto kuwa na pempasi kama ndio nguo ya ndani ambazo hutumika kuvishwa watoto kwa ajli ya kuzuia kinyesi na mikojo kutapakaa.
 
Wasomi siku hizi bana wameelimika.ngoja wawalishe soseji na azamu juisi ,maziwa ya unga,ngano ya azamu iliyokobolewa,aje anywe soda, ale kiepe yai kizungu,aende English medium aongee English a dadi na junior, ale white bread na blue band, aje ale chocolate, big bom, aloweke juisi kula anywe, aje ale kitumbua.

Aangalie series,acheze game kwenye computer,apewe pop corn,na corn flakes zikichanganywa na maziwa ya dukani,aje ale samaki aliyekaa kwa.friji miaka,atembelee beibi woka, anunue Jambo ice cream, Azam 🍨, ale yogati ya asasi anywe Ceres na sayona juisi na mo energy,abembee kwa shuleni na afuatwe na gari ,shuleni apikiwe bread na chai sukari Kama yote. Ndio raha ya utajiri jamani acha mtt afurahie kuzaliwa na kulelewa na msomi
 
Sidhani kama kuna mwanamme aliweza kukaa na mimba miezi 9 hajui hili
 
Kama kayaongea haya. Huyo mwanamama ana matatizo kidogo kwenye kuwasilisha na kuongea vitu. Asante.
 
Back
Top Bottom