SoC03 Matumizi ya Tehama katika ukusanyaji wa mapato na uwazi katika mgawanyo wa matumizi Serikalini

Stories of Change - 2023 Competition

The Real Kop

New Member
Jun 18, 2023
2
0
Teknolojia imezidi kukuwa kwa kasi kubwa sana, lakini ukuaji wake unasababishwa na uvumbuzi unaopelekea utatuzi wa matatizo na majanga yanayotokea katika jamii na ulimwengu kwa ujumla. Mabadiliko makubwa ya teknolojia yameletwa na wataalamu mbalimbali katika nyanja tofauti tofauti, wamejitahidi kwa kadiri ya uwezo wao katika kuboresha mifumo, uendeshaji na pia kuleta sera mpya ili kuleta matokeo makubwa chanya katika jamii yetu tunayoishi katika kuongeza ufanisi, thamani ya huduma na bidhaa, na urahisishaji wa maisha ya mwanadamu ya kila siku pamoja na uwazi.

Teknolojia pia imeambatana na madhara lakini inategemewa inatumiwaje katika jamii na kwa muktadha upi. Kwa hali ya sasa, teknolojia haepukiki kabisa licha ya kuwa na madhara. Teknolojia ipo kila nyanja lakini katika ukurasa huu, tutaeleza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, kwa ufupi inajulikana kama (TEHAMA) katika kuchochea ukusanyaji wa mapato na uwazi wa matumizi ya fedha za umma katika wizara, sekta, na taasisi mbalimbali serikalini.

TEHAMA inahusisha matumizi ya kompyuta na programu za kompyuta katika kuhifadhi data, kuchakata data, usambazaji wa data au taarifa. Teknolojia hii inasaidia katika kuunda, kutengeneza na usimamizi mzima wa mfumo wa data au taarifa. Tekonolojia hii imeleta uvumbuzi wa uundaji wa mfumo mmoja mkuu, unaoweza kusimamia mifumo yote midogo na mengine yote. Huu mfumo unaitwa KITUO CHA DATA (Data Centre).

Serikali ya Tanzania ilianza kutumia mfumo wa TEHAMA katika ukusanyaji wa fedha za umma mwaka 2017, ambao unaitwa GePG (Government e-Payment Gateway System) ambao umepelekea uongezekaji wa mapato serikali kuu, mfumo huu ulikuwa una lengo la kuongeza uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa mapato. Lakini mfumo umeshindwa kuonyesha ni jinsi gani fedha za umma zinavyotumika serikalini na taasisi zake. Na kutokana na ripoti mbalimbali za mkaguzi wa serikali (CAG) kuonyesha ubadhirifu katika fedha za umma. Hivyo hatunabudi kuleta mfumo mwingine wenye kuonyesha pia matumizi ya fedha za umma.

Mfumo wa GePG umefungamanishwa na mifumo yote ya kielektronki kutoka taasisi zote za serikali nchini, na unasimamiwa na kituo cha data ambacho kipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Mfumo hutoa bili ya malipo kwa kutumia ‘control number’ ambayo hubeba taarifa za malipo na huhifadhiwa ndani ya mfumo kwa muda mrefu, lakini haonyeshi jinsi gani mapato yalivyotumika. Tunapendekeza marekebisho au nyongeza katika mfumo wa zamani ili kuonyesha uwazi wa matumizi ya fedha za umma kupitia tovuti kwa upatikanaji wa data kwa wakati halisi (Real Time Data Acquisation)

Mfumo mpya huu utaunganishwa na mfumo uliokuwepo GePG ili kupata taarifa za kiasi cha fedha za umma zilizokusanywa na jumla za fedha zote za hisani na mikopo. Hivyo mfumo utaonyesha matumizi yote ya serikali kwa mwaka husika wa fedha, kwa mfano mwaka wa fedha 2024/2025. Na taarifa zitakuwa zinafanana au uwiano sawa na matumizi kutoka bajeti kuu (Wizara ya Fedha na Mipango). Na taarifa zitatumwa kwa wananchi kupitia kila tovuti ya wizara, taasisi, na kubandikwa kwa nakala ngumu (hard copy) katika ofisi zote za serikali kwa wananchi wasioweza kupata huduma ya tovuti. Na mfumo utaonyesha malipo yote yaliyofanyika tayari katika tovuti kuu ya serikali (Wizara ya Fedha na Mipango). Kwa mfano; ukitaka kujua malipo yaliyofanyika kwa mwezi husika, utapata taarifa za malipo yote kama malipo ya pesa za miradi, mishahara, na matumizi ya mafuta kwa magari ya serikali na n.k kutoka kila wizara. Malipo yote ya serikali na mahamisho ya kifedha yatafanywa na mfumo wa kielektroniki unaofanana kama wa GePG. Na utasimamiwa na kituo cha data kilichopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Faida ya mfumo huu mpya utaleta ufanisi wa kazi kwa sababu utakuwa unaratibu,kusimamia na kutoa muongozo kwa muda sahihi na kwa haraka, haijumuishi sana uwepo wa binadamu kwa asilimia kubwa katika utendaji wake. Hivyo itapunguza au kuondoa viashiria vyote vya rushwa na uhujumu wowote wa kimfumo au mapato. Na itapelekea uongezekaji wa uzalishaji na kuongezeka kwa mapato kwa sababu ya uwazi katika uendeshaji wake.

Pia italeta hamasa na chachu kwa wananchi katika kulipa kodi au ushuru panapohitajika, bila kukwepa kwa sababu wataona uwazi wa jinsi gani pesa zao zinavyotumika. Na kila kiongozi atatekeleza majukumu yake kulingana na fedha iliyopangwa kwa kuheshimu fedha za umma,kwa sababu ya kuwa huru au wazi katika utendaji wake katika ofisi yake.

Mfumo wa kituo cha data utatengeneza mazingira salama ya mfumo, mfumo utatengenezwa kwa kujilinda kwa kiasi kikubwa katika masuala yote ya udukuzi au kuharibiwa kwa kutengenezwa katika mfumo mzuri wa usalama wa mtandao. Na pia mfumo wa kituo cha data utatoa usalama wa kazi kwa kila mtumiaji kwa sababu, utaonyesha majukumu na uwajibu wa kila mtu kwa uwazi, hivyo kupunguza muingiliano wa majukumu katika kazi. Mfumo utahusisha katika usimamizi bora wa utunzaji wa taarifa au data kwa muda mrefu bila marekebisho yeyote ya taarifa.

Mfumo wa kituo cha data unatoa faida nyingi katika kuongeza au kuchochea utawala bora wenye uwajibikaji wa kila mtu katika jamii. Lakini unawezwa ukakumbwa na changamoto kama kutohingilia matumizi ya wizara ya ulinzi,taasisi na vitengo vyote vya usalama kwa lengo kulinda usalama wa taifa na masilahi yake kwa ujumla.

Mfumo mpya wa kituo cha data utapelekea ufanisi katika nyanja ya biashara na uchumi, hivyo kuleta maendeleo kwa jamii kwa sababu kutakuwa na mfumo wa uwazi katika uendeshaji kutoka ukusamyaji mpaka matumizi. Uwazi katka taarifa huchochea uwajibikaji na utawala bora, TANZANIA YENYE UWAZI WA TAARIFA INAWEZEKANA SASA.
 
Back
Top Bottom