SoC03 Matumizi ya mitandao ya kijamii na watoto wetu

Stories of Change - 2023 Competition

hassan yahaya

Member
Aug 27, 2022
32
34
Ndugu msomaji

Napenda kukuletea makala hii unayohusu matumizi ya mitandao ya kijamii na matokeo kwa watoto wetu. Kwa miaka ya hivi karibuni nchini kwetu Tanzania matumizi ya mitandao ya kijamii yameongezeka kwa kasi sana ukilinganisha na miaka ya kabla ya mwaka 2000.

Watu wengi sasa wanatumia mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp, YouTube, Twitter, Instagram, Facebook, TikTok na mingine. Nimeitaja hiyo michache kwasababu ni maarufu, inatumiwa na watu wengi sana na mepesi kutumia.

Siku hizi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia vifaa vinavyoweza kuingia katika mitandao hiyo vinapatikana kwa urahisi mkubwa hali inayofanya kuruhusu watu wa rika zote wenye uwezo wa kutumi mitandao hiyo kuitumia bila kujali maudhui yanayopatikana kupitia mitandao hiyo. Lakini pia mabadiliko ya sera ya elimu ambayo inaruhusu matumizi ya mitandao kwa wanafunzi inapelekea wanafunzi hawa kutumia mitandao ya kijamii na kuacha kufuatilia maswala ya masomo wanapoingia mitandaoni.

Kwa mtazamo chanya mitandao ya kijamii ni mizuri sana kwani husaidia katika usambazaji wa habari na matukio mathalani lilipotokea janga la corona watu wengi walipata habari ya ugonjwa huu na hata kutafuta namna ya kujikinga kupitia taarifa zinazotelewa na mitandao mfano Ada health.

Mitandao ya kijamii husaidia kusambaza matangazo ya biashara mbalimbali na kufanya wateja hata walio mbali kuweza kupata taarifa na hata kufika hatua ya kusafiri kwenda kununua au kupata huduma mahali husika. Si hivyo tu watu wameweza kupongezana katika kufarahia matukio mbalimbali kama vile sherehe za ndoa na siku za kuzaliwa na wakati mwingine kupeana pole wakati wa majonzi kama vile msiba, ajali na maafa.

Lakini sambamba na faida hizi zilizoelezwa mitandao hii ya kijamii ndio njia kuu ya kuharibu jamii na kuleta mambo yasiyo faa, hivyo kupelekea kuonekana kama haina faida au faida yake kuingiliwa na mambo mabaya. Mfano leo hii kuna mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii ambayo sio mazuri hata kidogo.

Mfano wapo watu wanawasrma vibaya viongozi wetu wa nchi katika mitandao hii, wanaandika wasifu mbaya wa hawa viongozi wetu na kuwasema na hata wakati mwingine kuwatukana.

Kupitia mitandao ya kijamii pia wapo watu wanatoa taarifa za upotoshaji ambazo hazina ukweli wowote ila ni mtu tu amezihisi au kaskia juu juu mfano suala la kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, kabla mamlaka hazijatoa taarifa sahihi na kabla ya uchunguzi kufanyika zilizuka taarifa kuwa mwanafunzi huyo alipigwa na mpenzi wake na wengine wakasema kwa kadri walivyoweza.

Mbali na hayo kuna video ambazo zimehaririwa na hazina ukweli wowote ambazo zinaonyesha matukio ya ajabu kama vile mtu kujirusha kutoka juu ya ghorofa hadi kufika chini bila kufa, zipo video zinaonyesha watu wanachomana visu na nyingine nyingi.

Pia zipo video zinazoharibu maadili yetu kama watanzania mfano wapo watu wanatumia wajina ya kuwa wao ni washiriki wa vitendo vibaya mfano ukiingia katika mtandao wa facebook wapo wanajiita wasagaji na wengine wanatumia lugha za matusi moja kwa moja bila kupepesa macho.

Lengo la kuandika makala hii ni kuhusiana na mambo mabaya yanayofanyika katika mitandao ya kijamii ambayo tayari nimeyaeleza hapo juu kwa uchache.

Hebu tujiulize je, watoto wetu wanajifunza nini kuhusu mambo haya mabaya?

Ukweli ni kwamba hakuna mafunzo juu ya jambo baya ila upotofu tu. hivyo kupitia mambo haya machafu watoto wetu wanapotea.

Kupotea huku kwa hawa watoto unaweza usione kama utaangalia katika eneo dogo ila kama utaangalia kwa upana mfano katika ngazi ya wilaya, mkoa au nchi na ukilinganisha na miaka iliyopita utagundua kuwa watoto wanapotea.

Mfano tabia ya kiburi imeweza kukua kwa kiasi kikubwa sana, tabia hii hutokea pale mzazi anapomtuma mwanae, wapo watoto ambao hukataa moja kwa moja kwa kusema nimechoka na wengine kusema kabisa siendi. lakini pia wapo watoto ambao huwasonya wazazi na wengine kuondoka nyumbani na kurudi jioni ili kuepuka kutumwa.

Hii ni kwa upande wa kitabia lakini pia mitandao ya kijamii imesababisha kuongezeka kwa matukio ya kujiua mfana wanafunzi wa vyuo vikuu kama chuo kikuu cha Dar es salaam, wanafunzi hujinyonga, au kunywa sumu au kujiangusha kutoka juu ya ghorofa hadi chini na kupelekea kufa.

Hali hij hutokana na kuzoea kusikia na kuona matukio kama hayo kupitiw mitandao ambapo huona kupitia filamu za kuigiza kama vike filamu za kihindi kwani huwa na matukio ya hatari ambayo sio ya kweli kabisa. Lakini pia matumizi ya madawa ya kulevya hususani bangi, kushinikizwa migomo mfano kugomea kuchoma chanjo ya uviko 19 watu wengi walishinikizwa na wengine kupitia taarifa zisizo rasmi kwenye mitandao ya kijamii hivyo kupelekea kuwajenga watoto hata wao kuamini kwamba chanjo sio salama.

Lakini pia mitando ya kijamii huchochea kuongezeka kwa vitendo vya uasherati miongoni mwa vijana wengi walio katika rika la kuwa shule na vyuo vikuu na kupelekea kuongezeka kwa kufeli katika matokeo yao. Lakini pia mitandao hii inapelekea upatikanaji wa video na picha mbaya kama vile picha za utupu ambazo husambazwa kupitia mitandao hii. Picha na video hizo ni aibu kubwa na husababisha watoto kujengwa na tabia mbaya na kuwapeleka kutamani kuanza kufanya mapenzi wakiwa katika umri mdogo.

Kimsingi kila mitandao ina vigezo na masharti, na kila nchi inautaratibu wake hivyo serikali isiwafumbie macho wale wanaotumia vibaya mitandao hii kwasababu taarifa zao zipo kupitia akaunti zao, lakini pia Serikali kupitia kitengo cha mawasiliano inapaswa kudhibiti mitandao ambayo inatumiwa na waigizaji wa video za utupu kutotumiwa nchini kwetu na kwa wale wanaoigiza hapa nchini wachukuliwe hatua stahiki.

Watoto wetu ni wetu wenyewe na ni jukumi leo kuwalea katika maadili mema hivyo wazazi, walezi na watu wakaribu wanapaswa kukagua simu wanazitumia vijana wao ili kujiridhisha na matumizi yao, tusiwaachie majukumu serikali kwani haiwezi kuja kumkagua mtoto wako uliyenaye nyumbani.
 
Back
Top Bottom