Matumizi mabaya ya pesa changamoto ya maendeleo katika nchi na hata familia

bitare

Senior Member
Jul 13, 2023
192
563
Nimeona niandike japo kwa kifupi kuwa, chanzo kikubwa cha huduma duni za kijamii nchini kwetu kunasababishwa na matumizi mabaya ya pesa yanayofanywa na vingozi wa umma. Ukiachana na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serilikali ambazo kila mwaka zinaonesha pesa nyingi kupotea na mbaya zaidi ni kutochukuliwa hatua kwa wanaosababisha upotevu huo.

Pesa nyingi zinatumika visivyo sahihi, fikiria kama kununua magoli kwa moja million 5 hadi 10 wakati huo watoto wakikaa chini madarasani kwa kukosa madawati au kama huyu aliemleta Diamond Mwanza kutumbwiza ili CHADEMA wasipate watu huku jiji hilo likiandamwa na mgao wa maji.

Hivi kweli viongozi mnaotuongoza mnauzalendo kweli?
 
Kwanza hii nchi watu hawapo serious hiyo kiujumla tupo hivyo ila pia hatuna viongozi bali tuna watawala kwa maana tunatawaliwa hatuongozwi.

Kama mna viongozi ambao wanaweza kuwajibu wananchi tena bila hofu kuwa kama hautaki hamia nchi nyengine, kama hao viongozi wanaweza kuwatukana wananchi mitusi mikubwa kisa umewakosoa mitandaoni, kama wananchi wanapinga jambo ila wanazuiliwa kuandamana hapo bado utasema una viongozi au watawala na upo kwenye utawala ukitawaliwa?
 
Back
Top Bottom