Watoto wanaokuja nyumbani na vitu vya kuokota (Pesa, Midoli, Mipira,). Je, ni sahihi kwa wazazi kuruhusu tabia hii?

Katika udogo wangu nimewahi kuokota mia mia na mia 2 nyingi sana..

Kuanzia siku hiyo nikawa naokota hela kila siku kwa kipindi karibu na mwezi...

Kuna wanaodondosha bahati mbaya na wanazitupa makusudi kwa sababu wazijuazo wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna level ikifika hata panga inabidi umshikie sembuse plaizi?

Tuombe Mungu atujalie kuzaa watoto wastaarabu, wasio na matatizo ya usumbufu, la sivyo lazima umshikishe adabu angali mdogo ama wewe ukishindwa basi walimwengu watamfunza.
Mmmh kushikia panga tena jamani
 
Hivi unadhani wale wanaopiga watoto wao mpaka wanawaumiza ni kupenda kwao?
Hakuna mzazi anataka mwanae aharibikiwe na bahati mbaya hakuna formula ya kulea, kila mzazi analea vile anaona mtoto atakua kwenye maadili sahihi kulingana na jamii husika.

Lakini sikubaliani na kupiga watoto mpaka kuwaumiza. Mimi nimelelewa bila kupigwa lakini nilikua namuogopa sana baba angu kutokana na nilivyokua naona akipiga kaka zangu. Kwahiyo akisema tu kitu hiki hakifanyiki hapa kwangu, nilikua natii bila shuruti. Kwahiyo naamini katika malezi ya fimbo na malezi ya kuongea na mtoto. Kwahiyo katika kutumia fimbo au nguvu kuwajibisha mtoto itumike kwa kiasi sio unapiga mtoto kama unapiga mwizi. Au sijui mtoto kaiba nyama unamchoma mikono. Siamini katika hilo na nadhani wanaopitiliza kutumia nguvu kwa watoto wao kuna shida mahali, wanakua na stress flani inawasumbua.

Kwahiyo mimi nimekua katika ile baba akisema neno lake ndio sheria na unatakiwa kutii bila shuruti. Kwahiyo ukiona mpaka unashikia mtoto panga sijui nini ujue umeshindwa kuwa kiongozi wa familia kwa namna flani. Neno lako halionekani kama ni sheria.
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Watoto wanaokuja nyumbani na vitu vya kuokota (Pesa, Midoli, Mipira). Je, ni sahihi kwa wazazi kuruhusu tabia hii?

Mimi siwezi kujisifia kwamba nilikuwa na wazazi makini sana katika suala la malezi kwa maana wakati nipo mdogo nilikuwa sioni kama wapo makini. Nilichokuwa ninakiona kwao ni kile ambacho sisi vijana wa wakati huu (watoto wa zamani) tulikuwa tunakiita ni unoko. Mzazi akiwa anakujengea nidhamu unamuona adui badala ya kumshukuru.

Katika kipindi changu chote cha utoto kabla sijaanza secondary hakuna kitu ambacho mama yangu alikuwa hapendi kama tabia ya kurudi nyumbani na kitu cha kuokota. Yaani unarudi home ukiwa na pesa au mpira ambao baba/ mama hajakununulia kwa pesa yake. Unaanzaje anzaje kwanza kuja nao kwa mfano?

Just imagine unarudi nyumbani kwa furaha huko unamwambia mzazi wako "mama nimeokota hela barabarani shilingi mia tano" kitu ambacho mtoto yoyote anategemea kupata credit (kupewa sifa) kutoka kwa mzazi lakini badala yake inakuwa ndivyo sivyo.

Mama yetu alikuwa na tabia ya kuuliza swali moja la msingi endapo utakuja na kitu cha kuokota kama pesa. Atakuuliza hivi, "Kwa watu wooooote waliopita hapo barabarani, kwanini hiyo hela uione wewe tu na sio wengine? Sasa niambie hii hela umeiiba wapi? Kama haujaiba basi irudishe hapo hapo ile aje aokote mwingine"

Tuachane na hayo ya mimi na wazazi wangu na sasa niwape kisha cha mtoto wa mtaa wa pili huku ninapokaa. Kuna dogo mmoja aliyekuwa anasoma kidato cha nne aliwahi kuuwawa yeye na mama yake mkubwa kwa maana inasemekana huyu dogo alikuwa kila akiiba kitu basi lazima apeleke kwenda kuficha kwa mama yake mkubwa huko Temeke.

Huyu dogo alikuwa yupo na mwenzie ambaye ni dereva wa bodaboda na walikuwa wanatumia pikipiki katika kufanya ukwapuaji wa vitu kama mikoba, simu za mikononi pamoja na cheni. Baada ya kukwapua mali hizi alikuwa anampa yake amuwekee kwa kisingizio kwamba alikuwa anaokota sokoni tandika.

Mwisho wa siku dogo akiwa peke yake bila yule mwezie akachukua pikipiki kwenda kufanya dili zake hizo ila hakufanikiwa kukimbia, kwa maana inasemekana pikipiki ilitereza akaanguka chizi wananchi wakamkamata. Kabla ya kummaliza wakamuuliza maswali mengi mpaka akawapeleka kwa mama yake huyo ambapo huwa anaficha vitu vya wizi.

Wadau ile kuficha tu kwa yule mama, hawakumuita mjumbe wala mwenyekiti wa mtaa. Walichojua wao ni kipigo tu kwa yule mama na mwanaye. Wananchi waliwapiga sana kwa maana walikuwa ni wezi wanaopenda kuiba karibia na wanapokaa. Mtoto anakaa Tandika au Temeke alafu anaenda kuiba Yombo.

Kwanini mzazi unaruhusu mtoto kuja nyumbani na vitu vya kuokota? Unajuaje kama ni kweli ameokota au ameiba?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
SIYO SAHIHI ASLANI!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom