Watoto wanaokuja nyumbani na vitu vya kuokota (Pesa, Midoli, Mipira,). Je, ni sahihi kwa wazazi kuruhusu tabia hii?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
12,135
2,000
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Watoto wanaokuja nyumbani na vitu vya kuokota (Pesa, Midoli, Mipira). Je, ni sahihi kwa wazazi kuruhusu tabia hii?

Mimi siwezi kujisifia kwamba nilikuwa na wazazi makini sana katika suala la malezi kwa maana wakati nipo mdogo nilikuwa sioni kama wapo makini. Nilichokuwa ninakiona kwao ni kile ambacho sisi vijana wa wakati huu (watoto wa zamani) tulikuwa tunakiita ni unoko. Mzazi akiwa anakujengea nidhamu unamuona adui badala ya kumshukuru.

Katika kipindi changu chote cha utoto kabla sijaanza secondary hakuna kitu ambacho mama yangu alikuwa hapendi kama tabia ya kurudi nyumbani na kitu cha kuokota. Yaani unarudi home ukiwa na pesa au mpira ambao baba/ mama hajakununulia kwa pesa yake. Unaanzaje anzaje kwanza kuja nao kwa mfano?

Just imagine unarudi nyumbani kwa furaha huko unamwambia mzazi wako "mama nimeokota hela barabarani shilingi mia tano" kitu ambacho mtoto yoyote anategemea kupata credit (kupewa sifa) kutoka kwa mzazi lakini badala yake inakuwa ndivyo sivyo.

Mama yetu alikuwa na tabia ya kuuliza swali moja la msingi endapo utakuja na kitu cha kuokota kama pesa. Atakuuliza hivi, "Kwa watu wooooote waliopita hapo barabarani, kwanini hiyo hela uione wewe tu na sio wengine? Sasa niambie hii hela umeiiba wapi? Kama haujaiba basi irudishe hapo hapo ile aje aokote mwingine"

Tuachane na hayo ya mimi na wazazi wangu na sasa niwape kisha cha mtoto wa mtaa wa pili huku ninapokaa. Kuna dogo mmoja aliyekuwa anasoma kidato cha nne aliwahi kuuwawa yeye na mama yake mkubwa kwa maana inasemekana huyu dogo alikuwa kila akiiba kitu basi lazima apeleke kwenda kuficha kwa mama yake mkubwa huko Temeke.

Huyu dogo alikuwa yupo na mwenzie ambaye ni dereva wa bodaboda na walikuwa wanatumia pikipiki katika kufanya ukwapuaji wa vitu kama mikoba, simu za mikononi pamoja na cheni. Baada ya kukwapua mali hizi alikuwa anampa yake amuwekee kwa kisingizio kwamba alikuwa anaokota sokoni tandika.

Mwisho wa siku dogo akiwa peke yake bila yule mwezie akachukua pikipiki kwenda kufanya dili zake hizo ila hakufanikiwa kukimbia, kwa maana inasemekana pikipiki ilitereza akaanguka chizi wananchi wakamkamata. Kabla ya kummaliza wakamuuliza maswali mengi mpaka akawapeleka kwa mama yake huyo ambapo huwa anaficha vitu vya wizi.

Wadau ile kuficha tu kwa yule mama, hawakumuita mjumbe wala mwenyekiti wa mtaa. Walichojua wao ni kipigo tu kwa yule mama na mwanaye. Wananchi waliwapiga sana kwa maana walikuwa ni wezi wanaopenda kuiba karibia na wanapokaa. Mtoto anakaa Tandika au Temeke alafu anaenda kuiba Yombo.

Kwanini mzazi unaruhusu mtoto kuja nyumbani na vitu vya kuokota? Unajuaje kama ni kweli ameokota au ameiba?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

mwanamanzi

JF-Expert Member
Feb 15, 2017
216
500
Hii ni kweli kabisa. Watoto wana tabia ya kujaribu na usipokuwa making nae basi anajenga mazoea.
 

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,229
2,000
Huenda amemwomba mwenzie ila hapo hujui.

Huenda amenyang'anya wenzie, hapo hujui.

Huenda ameokota, hapo hujui.

Huenda amepewas shuleni na walimu, hapo waeza fwatilia

La muhimu mnunulie vya kwakwe na umwambie akiona vizuri zaidi akwambieee na asiokote wala kunyang'anya wenziee

wawaza mtoto anapotamani vya wengine hata sie wakubwa tatamani vya wengine ijapokuwa atumudu rudi navyo omee
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,345
2,000
INSHORT:
Si sahihi kwa mtoto kuokota ovyoovyo hivyo vitu tena vikiwa siyo vile vya nyumbani, huko nje kuna mambo mengi.
 

Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,542
2,000
kuna mwingine kaokota makaratasi ya kura hasa yale ya urais yaani ni mengi sana, sijui niyapeleke wapi mimi(joke)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom