Watoto kutegeana kutunza m/wazazi na kuwatelekeza ni janga linalokua kwa kasi nchini. Wewe umejipangaje?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
WATOTO KUTEGEANA KUTUNZA M/WAZAZI NA KUWATELEKEZA NI JANGA LINALOKUA KWA KASI NCHINI. WEWE UMEJIPANGAJE?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Niliwahi andika, sio lazima (wajibu) wa mtoto kutunza wazazi wake. Nikaongeza mzazi angalau afikishe miaka 60 ndio unaweza kumfikiria kumtunza na kubeba huo wajibu kama haumwi au hana matatizo yoyote.
Niliandika hayo nikiwa na dhamiri ya kuwa Watu wafanye kazi. Watu wakiwa umri wa kufanya kazi yaani miaka 20- 60 wasiwe mizigo kwa wengine kwa kisingizio chochote kile. Isipokuwa ugonjwa au ajali. Hayo yanaeleweka.

Sio kwa vile ni mzazi na unaumri chini ya miaka 60 utake kusumbua watoto. Yaani kila kitu unapigapiga simu kusumbua watoto. Umri huo unapaswa kufanya kazi. Mtoto mwenyewe kwa hiyari yake ndio anatakiwa akukumbuke walau kwa vocha. Hii inaenda sambamba na mtoto ukishafikisha miaka kuanzia ishirini unapaswa ujitegemee. Hakuna cha kisingizio sijui wewe ni mtoto wake ama nini.

Pia, Kuwa mke sio kisingizio cha kutaka kuhudumiwa kama maiti au mdoli fulani hivi. Mke sio kuwa tegemezi na kuwa mzigo kwa mumeo, familia na taifa. Mke ukiwa na umri wa kufanya kazi yaani 20 mpaka 60 Unaowajibu wa kufanya kazi kusaidia familia yako na kulisaidia taifa.

Utegemezi ni unyonyaji. Utegemezi ni ubinafsi na ukandamizaji wa haki za wengine. Utegemezi ni kulihujumu taifa.

Hayo yote niliyasema. Nasisitiza.
Usioe Mwanamke asiye na kazi na asiyetaka kufanya Kazi. Lazima awe mbinafsi. Na lazima unyanyasaji utatokea tuu. Binadamu asiyefanya kazi anakosa sifa ya kuitwa MTU. Ni aidha ni Mtoto mdogo, mgonjwa, au mzee au Maiti.

Kuoa Mwanamke asiye na kazi ni kuwa mtumwa. Ni kama kuwa Koloni la mtu mwingine. Yaani unanyonywa. Watu na jamii yenye uungwana, inayojali HAKI, Elimu (akili), Upendo na Kweli lazima Watu wafanye Kazi. Lazima wazalishe Mali.

Mweleweshe mzazi kabisa kuwa kama yupo umri chini ya miaka 60 huna wajibu wa kumhudumia na kumtunza. Ila utafanya kwa hiari yako tuu.
Kama ilivyo kwake yeye kama mzazi pindî alipokulea na ukafikisha umri wa kujitegemea alivyokuwa anakuambia umekua na hana wajibu wa kukutunza ndio hivyohivyo.

Kuna janga la wazee wengi kutelekezwa na watoto wao. Wapo watoto wanategeana kutunza wazazi wao. Hasa wale wazazi ambao ni kweli sasa ni wazee na wanahitaji uangalizi wa karibu kutokana na changamoto za magonjwa ya UZEENI.

Tatizo hili linasababishwa na mambo mengi lakini kubwa kabisa ni suala la Malezi Mabaya.
Watoto kutokulelewa kwa HAKI, UPENDO NA KWELI ndio chanzo kikuu cha watoto kutelekeza wazazi wao.

Wazazi lazima tuelewe kuwa Haki haina Baba wala mtoto. Haki ni haki tuu. Kuwa mzazi haikupi Haki ya kumfanyia mtoto wako mabaya. Alafu unakuja kuongopa kuwa Mzazi hakosei au wakati mwingine wazazi wanalazimisha Msamaha.

Utasikia majitu yasiyo na Haki yakisema,msamehe tuu, ni Baba yako yule, ni Mama yako yule. Huna Baba au Mama mwingine. Katika ishu ya haki hakuna neno Msamaha. Ila kwenye upendo kuna msamiati Msamaha.

Kwenye haki, Kile unachopanda ndicho utakachovuna. Ila kwenye upendo kuna neema ambayo hutokea by chance, Yaani umefanya mistake lakini unajikuta umesamehewa jambo ambalo sio HAKI.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Watoto watakusamehe ikiwa uliwafundisha UPENDO. Lakini hawatakuwa na wajibu wa kusamehe kwa sababu sio Haki.

Kumtunza na kumlea mtoto ni zaidi ya kumpeleka shule, kumpa chakula, kumfanya avae vizuri n.k.
Upendo haupimwi kwa mambo hayo. Hayo yote ni HAKI ya mzazi kuyafanya kwa mtoto wake kulingana na uwezo wake.
Lakini kuna zaidi ya HAKI ambayo ndio huitwa UPENDO.

Sio ajabu Wazazi wengi kwa kukosa upendo ila wanahaki kwa sababu ni wajibu wao kukulea na kukutunza ukawasikia wakisema, Ninakulisha, ninakusomesha nimekulea kwa shida alafu baadaye uje uhonge pesa kwa wanawake au alafu usinikumbuke.

Upendo hauhitaji malipo. Ila Haki inamalipo ndio maana ya Haki. Sasa malipo ya kumlea mtoto ni kupewa heshima kama mzazi. Yaani Wajibu wa mtoto kwa mzazi ni kumheshimu na kumtii lakini akiwa mtoto kwa sababu sio miaka yote mzazi atamtunza na kumlea mtoto wake. Kuna kipindi mtoto atakua na kujitegemea.

Upendo haulipwi popote na haiwezekaniki kuulipa. Ila haki inalipwa.

Kama Baba Unaowajibu wa kuwalea watoto wako kwa Haki kumaanisha kutakuwa na Malipo. Lakini pia kuwalea kwa UPENDO hii ndio kubwa zaidi.

Mtu anayekupenda hawezi kutegea au kukutelekeza ati akuache tuu hapo. Never Ever. Ile wenye Haki huweza kutumia haki zao kukutelekeza kwa sababu huenda wanastahili kufanya hivyo au hawana wajibu wa kukuzingatia au kukutunza.

Sijui kama naeleweka.

Katika kumfunza mtoto kuna kumpa adhabu kwa Haki na kumpa adhabu kwa Upendo. Lazima kuwe na uwiano mzuri katika mambo hayo.
Unaweza usimpe mtu haki yake kwa sababu unampenda kwa nia nzuri.
Upendo inalenga Nia njema. Haki kuangalia zaidi kile ulichopanda na ni lazima ukivune.

Ukatili wa watoto ndani ya familia, mara nyingi huongozwa na kile kiitwacho HAKI. Lakini haki ya kibinafsi inayoongozwa na mitazamo ya mtu husika.
Mzazi huweza kujipa haki ya kukuadhibu na kukutolea maneno machafu, kukupiga kikatili mpaka wakati mwingine kuua kwa sababu tuu yeye ati ni mzazi. Jambo ambalo sio sahihi.

Kutegeana kwa watoto kunaenda sambamba na kile kiitwacho haki kwani watoto wanaona fulani kwa vile ni kwanza au mkubwa ndiye anastahili kumtunza mzazi. Au kwa vile fulani anakipato kikubwa basi yeye ndio anastahili na kuwajibika kutunza mzazi.

Lakini kama upendo ungekuwepo, basi kutegeana na kutelekezwa kwa mzazi kusingekuwa kwa sababu watoto automatically watashirikiana kumtunza mzazi wao kwa sababu wanapendana.

Haki ni nzuri hasa ikiongozwa na upendo.
Haki bila upendo huweza kuvunja familia na taifa.

Acha Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Wewe ukiwa kijana unao unazaa watoto unawapanga kama team ya Mpira, huwapi sapoti ya maana, unaongeza michepuko na vimada.

Pesa zinaishia kwenye Pombe unasubiri baadae uanza kulalamikia watoto?

Huono Kikwete hadi leo anampigania Mwanaye apate mafanikio?

Hujaona 2010 hadi 20215 jinsi Mzee Mwinyi alivyokuw akimpigania mwanawe ili awe rais?

Hujaona Jinsi Mzee January Makamba alivypambana kuhakikisha Mtoto anabaki kwenye Mfumo?

Mafanikio ya Watoto kwa asilimia kubwa hutokana na malezi na sapoti ya Wazazi.
 
Ukweli ni kuwa maisha ya watz wengi ni ya kuunga unga hivyo swala la malenzi kwa wazee ni changamoto sana hasa wazee wanaoishi mjini hawa..
 
Wewe ukiwa kijana unao unazaa watoto unawapanga kama team ya Mpira, huwapi sapoti ya maana, unaongeza michepuko na vimada.

Pesa zinaishia kwenye Pombe unasubiri baadae uanza kulalamikia watoto?

Huono Kikwete hadi leo anampigania Mwanaye apate mafanikio?

Hujaona 2010 hadi 20215 jinsi Mzee Mwinyi alivyokuw akimpigania mwanawe ili awe rais?

Hujaona Jinsi Mzee January Makamba alivypambana kuhakikisha Mtoto anabaki kwenye Mfumo?

Mafanikio ya Watoto kwa asilimia kubwa hutokana na malezi na sapoti ya Wazazi.

Upo sahihi kwa asilimia 99%
 
Back
Top Bottom