MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,439
Ndugu zangu,
Jamii ya sasa imejaa watoto wanaolelewa na mzazi mmoja hasa akina mama. Hili tatizo kwa kiasi kikubwa linasababishwa na sisi wanaume wa zama hizi ambao kuzaa holela na kutelekeza mama na mtoto imekuwa kama kitu cha kawaida na tunakipa sababu rahisi tu.
Sasa hapa leo nataka nitoe angalizo muhimu kwa wanawake hasa single mothers. Mara nyingi baada ya kutelekezwa au kukosa maelewano na mzazi wa kiume kuna hatua mnachukua kwa hasira bila kujua matokeo yake.
Nimekuwa inspired kuandika hili baada ya kuona video ya mtoto wa msanii maarufu Anti Ezekiel akijiita jina la baba wa kufikia badala ya baba yake halisi. Sasa nisikieni kwa makini.
Mtoto ukizaa na mtu tambua hiyo damu inatambulika ni ya ukoo huo sio na Mungu tu, bali hadi miungu/mizimu ya huko kwenye ukoo. Vita yenu wazazi haiondoi uhalali wa hiyo bloodline na mambo ya kwao. Juhudi za makusudi kushiriki kumtenga mtoto na huko ni hatari labda wawe wamemkataa wenyewe lakini sio kupishana tu wazazi.
Hatari zaidi ni wewe mwanamke kumpakia mtoto chuki na baba yake, mtoto kwa kutokujua akashiriki kwa vitendo au kukiri kwa kinywa kumkataa baba yake halali huku baba yake akimtambua kama mwanae! Tofauti zenu za kimaisha ikiwemo matunzo hafifu tambua mstari hatari kuvuka ni kukana damu!
Sasa sikieni dada na mama zangu, mara nyingi hawa watoto wanaweza kukua vizuri ila wakishapata ufahamu wa kutosha hutokea matatizo ya ajabu! Utahangaika makanisa yote hutoboi na hapo sasa ni mpaka mtoto kwasababu ni mtu mzima mtumishi au Mungu mwenyewe amuonyeshe aina ya toba ya kufanya.
Hizi shida mara nyingi hutegemea na hizo familia za baba zao. Kama ni familia yenye miungu/ mizimu mikali ni hatari zaidi! Na ikitokea mtoto ni wa kiume ndio balaa maana ni wa urithi.
Kwenye ugomvi wowote upo mstari usivuke, usihusishe mtoto na kumuingiza kwenye maagano yatayokuja kumgharimu kuyafuta akipata ufahamu. Kama mzazi mwenzio amekutelekeza hizo hatua unazochukua hazitaleta ugali wala ada.
Mtegemee Mungu, kabidhi mtoto kwa Mungu aliyekupa then songambele hapo madhara ya huo uovu utabakia kwa baba pekee na familia yake kama imehusika.
Mwenye masikio na asikie! Mambo ya ukoo! Mizimu/miungu yapo. Wewe zaa alafu uenende bila kuchunga hatua zako na mtoto uone huko mbele msalaba utaobeba.