Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Hawa wetu wa siku hizi ukifanya kama tulivyo fanyiwa sisi jela inakungoja mayai si mayai matoy si matoy watu tulikuwa manunda kweli kulikuwa na mchezo mbaya sana unachukua jiwe la mviringo kama mpira unalivisha soksi yaani kama chandimu vile kisha unamlia timing jamaa unamwambia piga jamaa anajikunjua huko ule ulikuwa uuwaji.

Hii kitu siwezi sahau niliumiza msela wangu miguu alikaa ndani kama wiki mzima
 
Nakumbuka siku iyo tulikua kama watoto wanne tunakula na babu yetu, bahati nzuri ule mchele ulikua una mawe, ukila humalizi tonge mbili basi umetafuna jiwe na kulia ko. Ikawa kila mwenzetu aking'ata jiwe sie tunacheka, tabia ya kucheka mwisho mzee alikasirika, akasema ole wake acheke mtu, baada ya kama tonge tatu nikaja kung'ata jiwe kwenye tonge, acha kuna mwenzangu pembeni anicheke, alikosewa bonge ya kibao na kama kingempata basi angefanya alama kwenye shavu, apo tukabaki kimya, baada ya kama tonge nne hivi mzee akaja kutafuna jiwe zamu yake, na ilikua kubwa kidogo basi sauti ilitoka KOO, tulishindwa kuvumilia na tuliondoka kwenda mbio huku tunacheka. Duh kitambo sana
 
Dah namkumbuka mzee wangu Mungu amlaze mahali pema peponi,Aaaminn .
Sikumbuki kama nilliwahi kupitisha siku 3 home bila mzee kunipa mikwaju labda kama kasafiri lakini kama yupo lazima nile mikwaju tu
 
Dah namkumbuka mzee wangu Mungu amlaze mahali pema peponi,Aaaminn .
Sikumbuki kama nilliwahi kupitisha siku 3 home bila mzee kunipa mikwaju labda kama kasafiri lakini kama yupo lazima nile mikwaju tu
Yaani wazee wa zamani ndio hivyo, mimi mother bwana alikuwa kama simba, sasa huwa namkumbusha anacheka sana ,anadai ndio maana nipo leo labda angeniacha ningekuwa keko mpaka leo,maana nilikuwa mwizi wa mia mia za kula mihogo schule.
 
Mimi mshua alikuwa ana bakora zake special kwa ajili yangu kwanza anaficha juu tena sio bakora za mti,kuna stiki fulani wanatumia mafundi Garage kuchomea Gas basi nyembamba zile haangaiki kuagiza bakora,raha zaidi alikuwa football player sasa nikifanya kosa wala sihangaiki kukimbia mwenyewe nasogea maana hata nikikimbia simuachia atanikamata tu kwa mbio
 
Mie siku mmoja Nilimsifia mama wa jirani ananenepa kwa sababu ya wanakura ubwabwa kila siku niliongea mbele ya mama NIKACHAPWAA ! Niliambiwa Nina tamaa !
Unanikumbusha mbali sana nikiwa mdogo kijijini kwetu mwana ,nilikuwa nikilala kwenye vile viwanda vya kamba bibi ananikuta chini nimeanguka kila siku asubuhi, akamuua kutafuta vigogo vinne bhna, nikawa na lala kama kwenye kishimo cha mraba, sasa bakora zako asubuhi kabla ya hii mbinu ya 2 ninomaaa, nikatamani kuhama kijiji nipoteleee nisipokujua .
 
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.

Hapa ndo palikuwa panasababisha nijiuliza wazazi wanataka nini.

Halafu kuna ile ukiibiwa kalamu ukaja kuomba nyumbani unapigwa, ukiwa huombi kabisa kalamu kwa kipindi kirefu unajulikana unaiba unachapwa.
 
Yale maisha yalikuwa ya uzima mkuu, na kila aliyezaliwa kuanzia 88 kushuka chini alikutana na kibano toka kwa wazazi. ..sasa watt wetu digital life, ukimfinya atalia wiki nzima na majilani watajaaa
 
Yale maisha yalikuwa ya uzima mkuu, na kila aliyezaliwa kuanzia 88 kushuka chini alikutana na kibano toka kwa wazazi. ..sasa watt wetu digital life, ukimfinya atalia wiki nzima na majilani watajaaa

Ukifanya kosa wazazi hawapo mama wa jirani anakupa fimbo, jioni akija kusema kwamba alikupa adhabu kwa kosa fulani unaongezewa zingine, siku hizi jirani akichapa mtoto ambaye siyo wake polisi inamhusu.
 
Back
Top Bottom