Watoto wa mwisho tukutane hapa

Watoto wa mwisho tukutane hapa

Kuwa last born kuna raha yake ila huwa natamani ningekuwa na mdogo wangu. Yaani angekuwa mwanangu kwakweli.
Nimejikuta hadi wakubwa zangu nawaita "dogo" lol.
Ndio maana bas unatusumbua kaka zako
 
Nyie mitoto ya mwisho mnakera sana... mivivu hadi mnakera!

Miaka kadhaa iliyopita si nikaenda kuishi na uncle wangu... mtoto wa mwisho kwa bibi na babu yangu!! Basi yule jamaa akawa anataka hadi nguo nimfulie! Akaacha kunipatia nguo zake baada ya kugundua naziloweka tu naenda kuzianika... sipendi ujinga mimi!

Yote 9, kumi unaweza kukuta anapiga kelele kishenzi kukuita! "Chigee! Chigee... njoo mara moja!" Nakumbuka enzi hizo nishamaliza Six, kuamka mapema sio lazima! Utashangaa kelele zote hizo anataka umpe viatu vyake ambavyo vipo chini ya 10 toka alipo... yaani kwavile anakunywa chai, ndo basi tena anaona taabu kuinuka na kwahiyo anataka mtu amletee!

Hayo yakapita! Nikiwa nimeshaanza maisha yangu huku nikiwa nikiwa naenda home siku za weekend peke yake; nikawa naumwa na hivyo kulazimika ku-settle kwa muda pale kwa wazazi! Hapa napo, tuna mdogo wetu wa mwisho!

Hili nalo, likinywa chai kila kitu litaacha hapo hapo! Likija kwenye meza yangu iliyojaa makokoro kibao, basi kama ni sinia au kikombe, hesabu ataacha hapo hapo!! Hili hata kuzima taa haliwezi! Sioni anachokiweza zaidi ya kufua na kupiga pasi nguo zake mwenyewe! Ngoja liumwe sasa... hata kumeza dawa, halitaki!

Aisee, nyie watu mnaboa sana!!!
Boss sio kwa kutukandia huku daah
 
Raha ya kuwa wa mwisho watu wote macho yanakuwa kwako ila kero yake ni kwamba hata uwe na mvi kama zangu watakuona mtoto tu na usiombe itokee mkusanyiko wa kifamilia may be msiba yaani kila kitu utakuwa unatumwa wewe aargh hupati hata wasaa wa kukaa chini, halafu wazo lolote utakalotoa linaonekana la kitoto. Mimi wa mwisho ila nimekua kigumu balaa huwezi hata kunijua
Ukikutana na mimi wa kwanza

what a nice combination!!
 
Wa mwisho wanaonewa huluma ukimsema utasikia mama ake muache mtoto,mara mbona unapenda kushindana na mtoto,usile hayo machungwa yamebaki kidogo ya mtoto
 
Mnh! Kumbe na wewe!! Tell me kwamba nimedanganya hayo niliyosema kuhusu nyie viumbe!!
Sio kweli kumbuka sisi ndio wa kutumwa na kila mtu yaani ilifika mahali nilikuwa natamani kuwa na mdogo wangu mradi nipate mtu wa kumtuma yani nione how it feels kunwambia mtu fanya hivi, nenda kule, njoo hapa maana sijawahi kupata hiyo chance
 
Sio kweli kumbuka sisi ndio wa kutumwa na kila mtu yaani ilifika mahali nilikuwa natamani kuwa na mdogo wangu mradi nipate mtu wa kumtuma yani nione how it feels kunwambia mtu fanya hivi, nenda kule, njoo hapa maana sijawahi kupata hiyo chance
Hiyo kweli tabu ya wa mwisho kutumwa tuna mtuma huyo mpaka analia haiwezekani dada zake/kaka zake wainuke yy kakaa
 
Umeona eeh? Yaani namshangaa huyo anayesema mtoto wa mwisho alikuwa anatuma mimi siwezi hata hapa nyumbani naweza nikakaa na mtoto labda wa ndugu huwa siwezi hata kumwomba anifulie nguo hata kama nahitaji msaada huo yaani nashishindwa kabisaa
Hiyo kweli tabu ya wa mwisho kutumwa tuna mtuma huyo mpaka analia haiwezekani dada zake/kaka zake wainuke yy kakaa
 
Back
Top Bottom