Watoto wa mwisho tukutane hapa

Watoto wa mwisho tukutane hapa

Nyie jiiteni tu Wa Mwisho,
Wakati hamna uhakika kama Dingi zenu hawakucheza "Nje Cup" wakachomoka na wengine ambao hamuwajui.
 
Kaka yangu yupo humu, anaijua id yangu ila mimi siijui yake. Yaani shamuwinda niijue ila sijafanikiwa bado.
Mimi kaka yangu mwenyewe nahisi yumo japo sina hakika kama anaijua I'd yangu maana kuna siku za nyuma huko nilikuwa sina bundle nikawa nasema please kaka ninunulie bundle kuna kazi nataka nifanye kaniambia huna lolote unataka uingie kuchat Jf, mimi macho yakanitoka heee
 
😂😂😂😂
 
Nyie jiiteni tu Wa Mwisho,
Wakati hamna uhakika kama Dingi zenu hawakucheza "Nje Cup" wakachomoka na wengine ambao hamuwajui.
Ndio maana Eli79 hapa alikuwa anasisitiza ye ni wa mwisho kwa mama
 
Yaani espy umetafuta kila namna ya kunitoa kwa MO11 hadi umefanikiwa[emoji57][emoji57][emoji57]

MO11 wangu mpuuze huyo mtoto wa mwisho atakusumbua bure, njoo kwangu mie mtoto wa katikati[emoji8]
Unapenda kunionea kweli jamani, ngoja niende tu darasa la make up.
 
Nyie mitoto ya mwisho mnakera sana... mivivu hadi mnakera!

Miaka kadhaa iliyopita si nikaenda kuishi na uncle wangu... mtoto wa mwisho kwa bibi na babu yangu!! Basi yule jamaa akawa anataka hadi nguo nimfulie! Akaacha kunipatia nguo zake baada ya kugundua naziloweka tu naenda kuzianika... sipendi ujinga mimi!

Yote 9, kumi unaweza kukuta anapiga kelele kishenzi kukuita! "Chigee! Chigee... njoo mara moja!" Nakumbuka enzi hizo nishamaliza Six, kuamka mapema sio lazima! Utashangaa kelele zote hizo anataka umpe viatu vyake ambavyo vipo chini ya 10 toka alipo... yaani kwavile anakunywa chai, ndo basi tena anaona taabu kuinuka na kwahiyo anataka mtu amletee!

Hayo yakapita! Nikiwa nimeshaanza maisha yangu huku nikiwa nikiwa naenda home siku za weekend peke yake; nikawa naumwa na hivyo kulazimika ku-settle kwa muda pale kwa wazazi! Hapa napo, tuna mdogo wetu wa mwisho!

Hili nalo, likinywa chai kila kitu litaacha hapo hapo! Likija kwenye meza yangu iliyojaa makokoro kibao, basi kama ni sinia au kikombe, hesabu ataacha hapo hapo!! Hili hata kuzima taa haliwezi! Sioni anachokiweza zaidi ya kufua na kupiga pasi nguo zake mwenyewe! Ngoja liumwe sasa... hata kumeza dawa, halitaki!

Aisee, nyie watu mnaboa sana!!!
 
nyie ma last born mnahatari sana wala msifurahie maana kama wazazi wenu wangesema hawaongezi mtoto kabla yenu mngekuwa wapi??????
 
mi hata sijielewi kama kifungua mimba,kitinda mimba au wa katikati
 
Mimi kaka yangu mwenyewe nahisi yumo japo sina hakika kama anaijua I'd yangu maana kuna siku za nyuma huko nilikuwa sina bundle nikawa nasema please kaka ninunulie bundle kuna kazi nataka nifanye kaniambia huna lolote unataka uingie kuchat Jf, mimi macho yakanitoka heee
Kama yupo humu anaweza kuunga matukio akajua wewe ndio mdogo wake.
Kaka yangu anaijua id yangu na ndio alinishauri nibadili jina la atoto. Nilistuka tu siku ananiambia "dogo kumbe wewe mtata eeh!!" Huku kashika simu anasoma comments jf. Kumuuliza ndio akaniambia, ila akagoma kuniambia id yake.
 
Atajua mwenyewe bwana asije akaja tu pm kupima upepo
 
Second born hapa..ingawa nilitamani niwe first born.. unfortunately my sister ndo first born
 
Back
Top Bottom