FORTUNE JR
Member
- Mar 20, 2021
- 82
- 480
Wakuu, Natumai Mko Vyema na Mnaendelea Vizuri na Mapambano ya kila siku. Kwa wale ambao siku yao Haiko sawa labda kwa kuuguwa, kuuguliwa na kila Changamoto ambazo tunazipitia kama binadamu basi natoa pole kwao nikiamini kesho mambo yataludi kwenye mfumo.
Wakuu nimeona ni vyema nije Jamvini, kutokana na Mambo Kadhaa yanaondelea katika Maisha yangu, Nikiamini nitajengeka na kufanya maamuzi Stahiki katika haya ninayokabiliana nayo. Wahenga walisema "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu na Katazo la wengi ni onyo la Mungu"
Ni mwaka wa 3 sasa , nipo katika mafarakano makubwa yakutosemeshana, kutowasiliana na Wala kutoshirikiana kwa Chochote na Wazazi wangu.
Ni jambo gumu kidogo Kuingia akilini ila nitatoa maelezo ya kina na uhalisia ilihali Ushauri wenu uwe dawa sahihi ya Tatizo.
Kwa Utangulizi; Binafsi naweza sema nimepitia harassment katika Makuzi yangu. Mama Yangu kanihadabisha vilivyo pindi nikiwa Mdogo , Mara nyingi alinivua nguo na kuniadhibu nikiwa uchi hata mbele ya majirani na watoto wa Rika langu.
Ilikua ni ngumu sana kupita hata siku mbili sijaadhibiwa, na sio kwamba nilikua mtukutu sana, Laaah! Mama angu kiuhalisia ni katilii na Mshari sana,
Mara kadhaa alipigana na Wamama wenzie(majirani) kwa sababu ndogo sana na mara pengi yeye alitangulia kuwashambulia Wamama wenzie kwa makofi au ngumi na matusi juu. Pia mara kadhaa alikua akipigana na Mzee wangu nyumbani.
Kuna mda alithubutu hata kunipigia na ukuni wenye moto au hata mwiko wakati anasonga ugali. kifupi hasira yake iliwaka kiwepesi sana na Mkono wake ulikuwa mwepesi sana kutoa hukumu. Kuna mda nilisikia majirani wakimuuliza kama kweli Mimi nilikua Mwanae.
Mazingira hayo yalinifanya niwe na nidhamu ya Woga,Mnyonge nisiyeweza kudai haki yangu na mara pengi nilipenda tu kukaa pekeangu(Introvert) kwa kadri ninavozidi kukua.
Ahueni niliipata baada ya kuanza kukaa boarding(O-level na A-level).Mda mwingi wa likizo nilibaki shule kwa Kiteteo Cha Kujisomea twisheni. Kifupi nilikaa mda mchache sana Nyumbani .
Hatimae nikafanikiwa kujiunga na Chuo kikuu Cha Dar es salaam( UD) kuendelea na masomo ya ngazi ya juu. Baada ya kutamatisha masomo yangu ya Chuo kwa miaka mitatu nikaonelea Bora niludi nyumbani(Mkoani), ili nijipange na maisha yajayo.
Siku Moja nikiwa nyumbani, Nilipishana na Mother kitu kidogo Sana, Cha ajabu Alinifwata niliposimama, Sina hili Wala lile aliniwasha kibao Cha uso, Sijakaa sawa kaniongeza kingine Cha shavu , kiukweli hasira zilinipanda nikashindwa kujizuia nikajikuta nimemnasa kibao na Yeye Cha shavu.
Mzee hakuwa mbali, baada ya kuliona lile tukio , Alinifwata na Gongo la Muanzi alinipiga nalo Mgongoni mara mbili, Mara ya tatu alitaka kunipiga nalo kichwani as if Mtu anae uwa chatu, kwa bahati nzuri nilikwepa. Akiwa anajiandaa anipige tena, nilimshindilia teke la Kifua Mithiri ya Mtu aliedhamiria kuvunja mlango uliokataa kufunguka mara kadhaa, akadondoka chini.
Kiukweli, Hadi kufikia hatua hii, nilikua ni Mtu ambae sitambui hata ninalofanya Maana niliongozwa na Jazba na hasira ndani yangu.
Mzee aliamka pale chini, Kwa hasira akaingia ndani na kutoka na begi langu la Mgongoni akanitupia chini na kuniamuru niondoke, na kwakumaanisha alikiri kutonitambua tena kama mtoto wake na Maneno mengi ya kunilaani niendako.
Alinizui kuchukua vitu vyangu vilivyosalia ndani kwamfano begi langu kubwa la nguo akidai hivyo vyote ni juhudi zake. Wakati hayo yote yakijiri majirani wamejaa kama unavojua tena uswahilini.
Nilichukua Begi langu nakuondoka huku nikijiapiza Moyoni kama sitakaa niludi tena na Niendako nitapambana nifanikiwe adi niwashangaze.
Nilikuwa na Akiba kidogo kwenye Simu yangu, hivyo nikapanga kutumia fedha hiyo kama Nauli ya Kunifikisha Dar. Sikujua hasa, nikifika Dar nitaishije ilihali sikua na makazi tena.
Baada ya kufika Mjini, Ikumbukwe nilikua Sina marafiki wengi sana kipindi nikiwa chuo, kutokana na kuwa nilikuwa sio Mtu wa kujichanganya sana na mara nyingi nilikua sio mwongeaji sana(Introvert) kama Jinsi nilivyoeleza awali, hivyo niliamini katika marafiki wachache tu.
Nilipata hifadhi kwa Jamaa Mmoja ambaye yeye pia nilisoma nae, baada ya Ku graduate alisalia Mjini. Jamaa alinipa hifadhi ingawa ni kwashingo upande sana baada ya kumsihi sana kama nitaondoka baada ya mda mfupi.
Hiki kipindi, kilikua Kigumu zaidi kuliko kipindi chochote Cha maisha yangu. Nilizoea kuishi maisha ya shule ambayo kula uhakika na kulala uhakika. pia Chuo nilisaidiwa sana na wazazi na pia boom lilinifanya niweze kumudu maisha.
Niliishi kwa kula mlo Mmoja tu kwa siku Mithiri ya Mtu aliye kwenye mfungo, kifupi nilikuwa Sina tena fedha. Jamaa nae pale ghetto hakuwa na utaratibu wa kupika Mara nyingi alikula kwa Demu wake au kwa Mama ntilie.
Nyakati ngumu pia zilikua pale jamaa anakuja gheto na Demu wake, ilinipasa kukaa usiku kucha nje kwenye benchi yaani mbu wangu, baridi yangu Hadi kunapambazuka. na sio mara Moja ni mara pengi tu jamaa kanilaza nje.
Siku zilizidi kwenda, Mwili uliisha sana maana Chakula nilikula mara Moja tu Hadi nikazoea , Pia niliandamwa na misongo ya mawazo juu ya maisha yangu na suala la Wazazi wangu kifupi kiza kilitanda mbele yangu. Nilipatwa na vidonda vya Tumbo vikali sana.
Waswahili wanasema, Pata shida umjue rafiki. Binafsi katika kipindi hiki kila ninakochekeka kunagoma, kila ninaemwazima fedha ananikataa. Nimepiga Simu nyingi kwa ndugu, wajaribu kuongea na Mzee nyumbani Ajaribu kuludisha moyo Nyuma, lakini niliishia kukatishwa tamaa kwamba Mzee wangu kachoma kila kitu changu home na ameapa Mimi hanitambui.
Baada ya siku kadhaa kupita jamaa aliyenipa hifadhi aliniaga yakuwa anaenda Mkoani hivo niendelee kukaa pale kwake, lakini akiludi tu nitafute makazi mengine maana anataka kukaa pale na Demu wake.
Siku ya pili toka jamaa kaondoka, nikiwa pekeangu gheto majira kama ya Saa 5 usiku nikiwa nmejilaza kitandani kutafuta usingizi, Mara gafla nikaanza kujisikia maumivu kifuani upande wa kushoto wa moyo, Maumivu makali kama moto ndani ya Kifua, Mwili ukaanza kuishiwa nguvu pia, Jasho linanivuja Mithiri ya Mtu aliyekaribu na Tanuru la moto.
Mda unavyozidi kusogea na Hali ndivyo inavyozidi kua mbaya, Mto niliolalia umelowa jasho, pumzi nayo inanibana nashindwa kupumua kwa pua hivo natumia mdomo kurahisisha upumuaji, Nilikua na kisimu kidogo ambacho jamaa aliyenipa hifadhi aliniazima baada ya mimi kuuza yangu ili nipate fedha ya kujikimu, Kilikuwa na namba 3 tu, zingine zote nilifuta maana niliamini Sina watu, Niko mwenyewe. Moja ya namba ilikua ni ya mpangaji wa pale tulipokua tunakaa.
Wazo likanijia nimpigie huyo mpangaji nimwombe msaada, Wakuu, ni Ivi Simu naiona Iko kwenye pembe ya Kitanda lakini siwezi kuinua mkono, kusogeza Mguu Wala kiungo chochote Cha mwili. Akili inawaza lakini mwili hauna uwezo wa kufanya lolote. Hakika niliamini ule ulikua ni mwisho wangu.
Nilikaa kwa Hali hio kwa takribani kama masaa matatu hivi, ndipo nikaanza kupata nguvu kidogo kidogo Hadi nikaweza kuinuka kitandani na kutoka nje. Baada ya kupigwa upepo nje Hali ilizidi kutengemaa ,ilikua ni saa 8 usiku kwa mda huo.
Nikiwa katika Hali hii, nilikata tamaa na kujihisi Niko pekeangu jangwani. Lakini niliamini Kuna tumaini Moja limesalia, ni Mungu tu.
Nililudi ndani, nikawasha feni iniongezee hewa. Wakuu, Mimi sikuwa Mtu wa Kuzingatia sana maombi kabla, lakini Usiku huu nashindwa hata kuelewa ule msukumo nilitoa wapi.
"Katika kitabu cha Daniel 2: 13-23, Maandiko yanaelezea Jinsi Danieli na wenzake walivyotakiwa kutafsili ndoto aliyoiota Mfalme Nebukadneza, na Mfalme alihakikisha kuwauwa Daniel na Wenzake endapo watashindwa kutafsili ndoto hio. Danieli aliingia kwenye Maombi ili Mungu ampe tafsili ya ndoto ya Mfalme"
Wakuu, Unaweza kuvuta Picha ni maombi Gani Daniel alimwomba Mungu ilihali anajua kabisa Mungu asipomjibu tu basi anauawa. Haya maombi Ya Daniel naweza yaita Mungu shuka, usiposhuka Mimi nitapanda. Ndivo hivo na Mimi nilivyoomba takribani masaa mawili nikiamini msaada wa Mungu usipotenda kazi mda huo basi Hali ingekuwa ngumu zaidi.
Baada ya kumaliza maombi yale ya mda mlefu kwangu ambayo sijawahi omba kabla, Nilijilaza kitandani nikiendelea kutafakari, kifupi usiku mzima sikulala kabisa, ulikua ni usiku wa hekaheka na mda huu tayari kulikua Kuna pambazuka.
Wakuu, Hiki kipengele hapa Najua itawawea vigumu ninyi kunielewa maana hata Mimi bado Hadi Leo sielewi vizuri ila naamini alikua ni Mungu tu na Si vinginevyo; ni hivi Kuna akili ilikuja ndani yangu nikajikuta nafungua begi langu dogo la Mgongoni na kutoa notebook yangu ya Toka nikiwa chuo.
Nilijikuta nafungua kurasa ya mwisho ya Notebook na nikakutana na namba ya Simu. Ni namba niliyoiandika mwenyewe na siku niliyoandika ilikua hivi;
Wanaume hapa mtanielewa mapema, Ulishawahi kumwona Mwanamke Ukampenda Kupitiliza lakini ukashindwa kumfwata ukiamini yeye Si level yako yaani kuanzia kimwonekano, Kwa kipato na kwa kwa kila Hali kakuzidi.
Basi hili lilinikuta Mimi, Siku ya kwanza kabisa Kuingia Darasani(Venue) mwaka wa Kwanza chuoni, Kuna Dada nilimwona nilitokea kumpenda sana kupita kiasi, na ilikua hivo siku zote, kila nilipomwona akili yangu ilihama kabisa.
Alikua ni Mpole, Mstaarabu na mara pengi aliongozana na rafiki ake Mmoja. Hakuwa Mtu wa kujionyesha sana(Show off) ingawa haikufichika kwa mwonekano wake kuwa katoka familia bora. Dakika ya mwisho nikaja kujua kumbe sio Mimi tu bali Wanaume wengi waligwaya kufikisha hisia zao na wachache waliojitosa hawakufua dafu.
Kwa mwaka wa Kwanza na wapili sikumbuki hata kuwahi kuongea nae Zaidi ya kummezea mate tu.
Tukiwa mwaka wa Tatu, siku Moja Chuo tunasubiri Test, kila Mtu kakaa Kona yake nje, anapitia notes zake. Nilimwona yule dada kakaa pekeake, nikamfwata na ndio ilikua kwa mara ya kwanza napiga nae story.
Nilimsalimu, akaniitikia kwa Tabasamu, baada ya story kidogo akanipa namba yake yeye mwenyewe pasina Mimi kumwomba. Na kwakua tulikua tunaingia kwenye test Simu yangu niliacha gheto hivo nikaandika Nyuma ya Notebook.
Kuanzia siku hio ndio ikawa Mwanzo wa kuzoeana nae japo sio kivile. Tukikutana ni salamu tu story kidogo harafu kila Mtu anapita Kona yake, ingawa kila Mtu kufikia hatua hii alikua na namba ya mwenzake. Ikawa hivo Hadi tuna maliza masomo.
*****
Naendelea, Hapo nimewaludisha Nyuma ili twende sambamba Kuhusiana na hii namba ya kwenye notebook. Ikumbukwe Simu yangu kubwa nilishakwisha iuza na nipo na laini Mpya kwenye kisimu kidogo na nina namba tatu tu.
Akili inanisukuma nipige hii namba ya kwenye notebook ya yule Dada. kifupi nashindwa hata kuelewa ni akili Gani ilikua inatumika kufanya haya maamuzi.
Baada ya kupiga Kweli ilipokelewa na nilijitambukisha kwakua nilikua na laini Mpya.
Her: Ooh! Umepotea jaman. Uko poa Dr ?
Me : Siku Poa kabisa Rafik ang,
Her: What's Wrong Dr?
Me: Ni story ndefu best
Her: Uko wap Kwani
Me: Niko town .
Huyu Dada yeye anaishi Dar na Wazazi wake, Baada ya maongezi mafupi akataja location na Time ili tukutane.
Hadi kufikia hatua hii Sina hakika na kitu ninachokifanya lakini Kuna akili inanambia, Ukifanikiwa kukutana nae mwambie kila kitu.
Mda ulipofika mapema sana nikawa nimefika location. Baada ya mda Fulani bi dada nae akafika pale.
Na kweli, Sikupunguza Wala sikuongeza jambo nilimweleza kila kitu yule dada, Kuna mda nikaona yule dada anatoa kitambaa kwenye pochi na kufuta machozi " She was very emotional than me".
Nilichanganywa kabisa na Kitu alichoniambia huyu Dada,na ilinichukua dakika kadhaa kuamini kama alimaanisha "..... Unasikia X(alitaja jina langu), Hii week haitaisha nitakusaidia kupata Chumba, nitajitahidi kuhakikisha unakula na kupata huduma za Msingi, Lakini kabla ya yote naomba Leo hii, Mda huu twende hospital ukapime ili Ujue shida iliyokukuta usiku ilisababishwa na Nini......."
Alooo! Niliamini huyu Dada atanijenga tu kwa mawazo lakini sio kwa hili alilotamka,. Alitoa Simu yake, akampigia Mtu kutaka kujua Yuko wapi, Baada ya kumaliza kuwasiliana na huyo Mtu akanambia, alikuwa anawasiliana na Boyfriend wake ni Doctor Specialist wa hospital "X " , Ni hospital maarufu sana tu hapa Dar.
Ali request Tax ambayo ilitusogeza Hadi hospital X. Baada ya kufika, Boyfriend wake alitoka, Dhahiri ilionekana ni jamaa furani mwenye pesa zake, kwa kumkadilia ni kama kanizidi Miaka 4, 5 au 6 kifupi alikua brother kwangu.
Bidada akanitambulisha kwa jamaa kama Mimi ni mtoto wa Bamdogo wake, Then akaniambia nimwelezee Jamaa ake Kuhusiana na Changamoto iliyonikuta usiku. Baada yakujielezea, jamaa alinipa pole na kunishauri anipeleke kwa specialist mwenzie wa Moyo anicheki.
Nilipimwa vipimo kadhaa na nilionekana na Heart attacks na vidonda vya Tumbo, Ingawa ndo ilikua kwenye stage ya Mwanzo. yule specialist alinishauri kwa mda Mrefu kidogo juu ya ninavyopaswa kuishi na alinisistiza sana nisiendekeze misongo ya mawazo.
Niliandikiwa Dawa za karibu Mwezi mzima, Bill jumla ilitoka 380,000. ikumbukwe nilifanya vipimo vikubwa na sikua na bima na Ile hospital ni ghali. Yule dada alichukua pochi yake ni kama alitaka kutoa Kadi ya Bank, Jamaa ake akamwambia aache atalipa, Hivo kwa kifupi yule Jamaa alilipa Ile fedha yote.
Baada ya kupata dawa zote nilizoandikiwa, Bidada Ali request tena Tax na akanambia Twende tukamshushe kwao then Mimi niendelee Hadi ghetto. Mda wote huu nashindwa hata kuelewa namshukuruje huyu Dada, Yani Kuna Jinsi kama machozi yananilenga.
Bidada alimwelekeza Dereva Hadi kwao, Sikuamini kwaweli, Yule dada ni wa kishua kuliko nilivyodhani, Kwao ni Bonge la mjengo wa kifahari. Alinionyesha kama pale ndo kwao then akatoa pochi yake na kutoa elfu 40 , then akanambia nitakuongeza nyingine kwenye Simu ikusukume tunavyoendele na mchakato wa kutafuta makazi .
Aliminya kengere ya mlango, na mlinzi akatoka, wakati huo nimebaki na Dereva tax akiwa anageuza gari tuondoke. Mlango ulifunguliwa nilichungulia vizuri kwa ndani hakika kulikua kuzuri sana huku Gari 3 zikiwa zimepaki. Sikutembea umbali Mrefu kwenye tax, Muamala ukasoma kwenye Simu yangu 120,000.
Wakuu, Napaswa kufupisha baadhi ya matukio ili tufike lengo. Haya yote yakiwa kama ndoto kwangu juu ya huyu malaika wa Mungu aliyejitokeza kwangu, Bidada alinipangia Room Kali sana, Akawa ananichukua tunaenda kufanya shopping ya vitu vya ndani ya room. kifupi alininunulia Kitanda, Friji La kati, Tv nch 32, na vitu vingi Hadi Chumba kikakamilika na kodi alishanilipia ya mda Mrefu.
Bidada alikua anakuja mara pengi pale ghetto maana hapakuwa mbali sana na kwao, Ananiletea matunda, Sometimes ananipikia na akiondoka Elfu 50 au 60 lazima anipe. kifupi niliishi maisha Mazuri. katika kipindi chote hicho najitahidi kutafuta sehemu ya kazi ya kujishikiza na Mimi niwe napata walau chochote kitu, pia bidada anajitahidi sana kuniulizia kazi sehemu mbalimbali.
Naweza sema toka nmekutana na huyu Dada ni kama milango ya Baraka ilifunguka kwangu, maana haikuchukua hata mda Mrefu nikawa nimepata kazi ya mkataba mahala Fulani.
Siku zimepita, Mambo yamebadilika, Kazini nimetokea kupendwa na wafanyakazi wenzangu na Maboss wangu, nalipwa fedha ambayo inanikimu kabisa ki maisha na Akiba naweka. Ghetto kwangu nimeweka Picha ya frame kubwa ya bidada aliyenifanya nifike hapa nilipofika,
Bidada Kawa rafiki angu Mkubwa sana Hadi sasa , ingawa ndani ya moyo nimempa dhamani ya zaidi ya Rafaki,Mama au niseme Malaika na Hadi sasa nafikiria nitamlipa Nini kulingana na kile alichonifanyia .
Lakini Kuna Greenlights zinaonyesha kama anahisia za kimapenzi na Mimi , maana anapenda ku play part ya mke sana kwangu kwa kunipikia, Kunisaidia kufua sometimes, Mara anipige Mabusu kwenye paji la uso
Ingawa naziona izo greenlights zote lakini sometimes napata wakati Mgumu licha yakuwa huyu Binti Mimi nilitangulia kumpenda sana mda Mrefu na ndivo hivyo Hadi sasa, Lakini bado Yuko na mahusiano na Mchumba wake na ni wametoka mbali sana,na mshikaji anaonekana kumpenda sana huyu Dada Kupitiliza.
na pia sometimes nawaza isije ikawa Mwenyezi Mungu kanitumia malaika wake msaidizi, Mimi nikaleta tamaa na Hasira ya Mungu ikawaka juu yangu. maana Iko wazi huyu Binti alikuja baada ya maombi, hivo bado Sina hakika kama Mungu Kaniletea Mke au Malaika masaidizi.
Wakuu ni hitimishe kwa kusema hivi, siku zimepita na sasa ni takribani naenda kufunga miaka mitatu toka Mafarakano yatokee, lakini bado Wazazi wangu hawataki Tumalize tofauti zetu. Nimefanya juhudi za kutosha, Kupitia ndugu, Wazee wenye hekima wa kule nyumbani ili wasaidie kumaliza tofauti zetu lakini wapi.
Kuna mda natamani nilipe hata kidogo Fadhira kwa Wazazi wangu kwa kunisomesha, kunilea napia nimetambua nilitumia Hasira kwa kipindi kile. Maisha yakudanganya akili kuwa Sina Wazazi ilihali ninao sioni sawa. Kuna time natuma fedha home, zinaludishwa, kifupi hawataki Hela yangu yoyote.
Kuna baadhi ya wazee na watu tofauti wanadai niendelee tu na maisha yangu kwakua nishateseka vya kutosha kutafuta suruhu lakini sijapata, wengine wanadai niendelee kupambana huenda siku juhudi zitazaa matunda, lakini Kuna wengine wanaungana na Wazazi wangu kwa kuamini Mimi ni mkosaji nilietukuka, Kuwapiga Wazazi tena wote wawili sistahili msamaha.
wanajamvii kama nilivyotangulia kusema Mwanzo Sauti ya Wengi ni ya Mungu, naomba Ushauri wenu katika hili ninalokabilina nalo.
ASANTENI NA POLENI KWA MAELEZO MAREFU.