Baada ya serikali kuwa inakataa kuonyesha mikataba ya madini hata kwa wabunge na kamati yake inayohusika na madini, na sasa kusoma kuwa mkakati wa kumfilisi Mengi ulijadiliwa katika kikao kimoja cha viongozi wa cha serikali, ninajiuliza maswali matatu:
(a) Je tuna sheria inayolazimisha records za serikali kama vile agenda za vikao vyote vinavyofanywa na viongozi, barua na email wanazoandika, na maongezi yao ya simu kuwekwa kumbukumbu ya kudumu? Nina wasi wasi kuwa huenda hapana kwa vile Ikulu yetu inatumia e-mail ya Yahoo, na hakuna uthibiti wa matumizi ya simu?
(b) Je tuna sheria inayolazimisha vyombo vya habari na rai wa kawaid kupewa habari zozte zinazuhusu serikali? Yaani kitu kama "Freedom of Information Act" ya marekani.
(c) Kama hatuna utaratibu wa kutunza records za serikali, na hatuna Freedom of information act ya kuilazimisha serikali kutoa habari za uhakika, na serikali ikaamua kudanganya wananchi kwa kudai kuwa kikao hicho hakikuwapo, na hivyo Mengi ni mwongo, je itakuwaje? Je Mengi ana uwezo wa kuthibitisha kuwa kikao hicho kilifanyika kweli iwapo serikali itakikana (hata kama kweli kilikuwapo)?