Hakuna mtu aliyesema hakuna wabongo, wanamapinduzi wanaofanya kazi WB. Wao wanapata kazi kutokana na taaluma zao na mahitaji ya WB. Huyo rafiki yako, hata kama aliongoza machafuko dhidi ya Mabuto kama kitaaluma ana-fit mahitaji ya WB , ataajiriwa. Hakuna cha kushangaza hapo. Tofauti ya WB na uwaziri Tanzania ni kuwa ni Rais wa Tanzania halazimiki kuangalia taaluma ya mtu anapomteua kuwa waziri. Ni uamuzi wake pekee na sio wa mtu mwingine. Kama dereva wa Masha, akigombea ubunge akafanikiwa, basi Rais anauwezo na haki ya kumteua kuwa waziri kama akipenda. Lakini dereva wa Masha akitaka kazi WB, nafasi anayoweza kuajiriwa baada ya usaili na kuonekana ana uwezo na sifa stahili ni udereva na si ukurugenzi.
Ajira inaanza unaposaini mkataba na mwajiri. Kwa vile Masha hakusaini mkataba, basi hajawahi kuajiriwa. Mwajiri anachofanya ni kukupa ofa ya ajira ambayo unaweza kukubali au kukataa. Ukikubali, unaingia nae mkataba na hapo ndio ajira inaanza. Pamoja na hili ulisema kuwa Masha alikuwa anasubiri Green Card ndiyo akaanze ajira. Hii imethibitishwa kuwa ni uongo maana hauhitaji Green Card kupata ajira WB. Ulichopaswa kufanya ni kutuhakikishia ni kuwa Green card ni condition moja wapo ya kuajiriwa na WB. Kitu ambacho hauwezi maana tunawajua wengi walioajiriwa na WB ( watanzania waliosomea Marekani) bila ya kuwa na Green card.
Nitamchukiaje masha ambae simjui? Kuwa waziri Afrika akiwa na umri huo nacho ni kitu cha kustaajabikia? Mimi nawaonea wivu wakina Robert Nesta Marley, Malcolm X, Martin Luther King, Julius Nyerere,Thomas Sankara, Mandela, Tupac Shakur, Bill Gates na wengine wengi walio-achieve mengi katika umri mdogo kuliko huo wa Masha. Masha ana Master's. Wewe unajua mimi nina elimu gani? Au kwa sababu najiita Fundi Mchundo? Na hata kama nina FTC, kwa nini nimuonee wivu Masha? Sasa hao wakina Dr. Slaa, Obama, Rice basi si itabidi nikatafute kamba nijinyonge kwa wivu?
Masha amekuwa Meneja wa Amusement Park, Corporate Secretary na MD wa kampuni ndogo ya serikali ambayo aliiacha ICU, amekuwa patna katika kampuni ya kisheria inayotuhumiwa mengi tu, amekuwa mbunge na amekuwa waziri. Katika yote haya sijaona cha kumwonea wivu maana mimi si wakili wala mbunge. Namheshimu kwa mafanikio yake lakini simuogopi, simnyenyekei, simsujudii wala kumwonea wivu maana haleti hata iota moja ya tofauti katika maisha yangu. Simjui. Hanijui.
Matatizo yako ni kuwa kila unaposhindwa hoja unaingiza maneno yasiyo stahili. Unasema namchukia Masha kwa sababu nasema hajawahi kuajiriwa na WB? Unasema namchukia Masha kwa sababu nasema amekosea kwenye kauli yake dhidi ya Mengi? Mbona hata huyo Mengi nilipinga kauli yake ya mwanzo? nae namchukia? Unasema namchukia Masha kwa sababu nakataa kuwa katutendea fadhila kurudi na kufanya kazi Tanzania? Kama ni hivyo, basi nitawachukia wengi maana si Masha peke yake aliyerudi Tanzania. Narudi tena, sina ugomvi, wala uhusiano wowote na masha au mtu yeyote tunayemjadili katika hili jamvi. Mimi namkosoa ( na kumsifia ikibidi)mtu kwa vitendo vyake na si kinginecho. Masha akifanya jambo ambalo linastahili pongezi sitachelea kumsifia. sasa wewe unamsifia Masha kwa sababu uliwahi kumuendesha, ni rafiki wa familia, unamjua na kuaminiwa na mama yake na baba yake, alikufanyia pati kubwa n.k. Kwangu mimi vyote hivi unavyovisema havimfaidii mtanzania wa kawaida. Nitamsifia akifanya vitendo vya kumsaidia huyo mtanzania. Hayo ya ukaribu nakuachia wewe.
Kama nilivyokuasa hapo awali, nionyeshe katika mabandiko yangu wapi nimeonyesha kuwa nina wivu au chuki dhidi ya Masha au wewe? Kupingana na kukosoana si chuki. Ni katika kujaribu kusaidiana. Nimempinga Mkandara kwa maneno makali tu hivi karibuni lakini hajawahi kusema kuwa namwonea wivu au chuki binafsi. Jifunze kwake ili ujue maana ya mjadala na utu uzima.
Sasa wewe unayeniambia maneno yangu ni ya chooni, irrelevant, nonesense ( BTW ni nonsense) n.k. ndiyo niseme unanichukia na kunionea wivu? Kwa kitu gani? Ufundi mchundo wangu! Basi itakuwa kazi. Ningekuwa Profesa ingekuwaje basi? Maisha ni mafupi mno na tupo hapa kuelimishana na kufurahishana. Hakuna haja ya kuingiza chuki na matusi. Haimsaidii mtu.
Amandla.....
Da! Amina baba.
huwa najisikiaga raha sana mtu akiweza kufikisha ujumbe ki mantiki zaidi bila kuchomeka vijembe-vijembe visivyosaidia kuweka uzito wowote kwenye hoja yake. Inapendeza sana ...