Wanawake wenzangu wenye vitanzi (IUD), mnaendeleaje?

Wanawake wenzangu wenye vitanzi (IUD), mnaendeleaje?

Miaka yake inahusika nin na alichokiandika
Na unadhan mtu unaweka njia ya uzaz wa mpango bila kumshirukisha mwenza wako ? Mbona watu mnapurupukaga huko mkadhan mnajua maisha ya watu? Au hizi mada za jamii forum zinawatoa akili zenu
😂😂😂😂😂
 
Habari,

Hii ni kwa wanawake wenzangu ambao wanatumia uzazi wa mpango aina ya IUD (Intra-uterine Device) au Kitanzi.

How are you guys? Vinawapa maudhi kama kilivyoninyoosha mimi au mmetulia?

I have to say nili-opt kutumia IUD sababu niliambiwa haina maudhi, na niliweka a copper IUD nikiambiwa ni non-hormonal yaani hakiingilii mifumo ya homoni. Miaka miwili ya mwanzo naona niliishi nacho tu poa.

Kuanzia around February 2025, nikaanza kupata periods zinazodumu siku 8 hadi 10, tumbo likawa linauma Mungu hapendi, nikipona yeast infection napata BV na mzunguko unaendelea hivyo.

Nimetoa IUD tangu November 2025. Kila kitu kimetulia! Yaani periods zangu zimerudi kuwa normal, sipati infections anymore na wala siumwi tumbo.

Tatizo ni kwamba; NIMEKIMISS. Namiss maisha yangu ya kuwa siwazi kupata ujauzito. Maana huku kwenye ndoa muda wowote unamwagiwa ndani, sipendi kukaa roho juu kabisaa. Niweke tena nikitumaini nitatulia miaka miwili mingine?
Aisee
 
MNANYOISHWAAA HIO STATA BADO PICHA.MNASHINDANA NA MUNGU

MNAAMBIWA MKAIJAZE NCHI MNATAKA KUJAZA NA KUCHEZEA SPER ..S ZA WATU ZA BURE AISE
 
Pole kwake, fibroids hazina sababu ya kitabibu inayojulikana ila kuna vichochezi vinavyoweza kuchangia ikiwemo historia ya fibroids kwenye familia, upungufu wa vitamin D na unene kupitiliza.

Sisi wanawake wa kiafrika ndiyo kundi linalozipata zaidi kuliko wanawake kutoka maeneo mengine. Shangazi yangu ameondolewa kizazi kwa sababu ya hili tatizo 😢.

Tiba inategemeana na fibroids zimejiotea wapi na kwa ukubwa gani. Kuna dawa za kuzifanya zinywee au operation. Pia kuweka IUD inasaidia kupunguza bleeding kipindi cha period.
Asante dear! Nitampa huu ushauri.. namuonea huruma anaenda fanyiwa operation nyingine next week!
 
Naona mleta mada anashambuliwa sana kwa kuamua kutumia njia ya uzazi wa mpango!!! Hii sio sawa,tumeshapita zama za kuzaa kama wanyama .

Kama mimba ingekuwa inatunga kwa mtu yeyote baada sex lazima na sisi wanaume tungetumia uzazi wa mpango. Bahati nzuri ni mwanamke anaye beba mimba,kitu pekee tunacho weza kufanya ni kutoa support ya njia salama za kupanga uzazi.
Hao hao wanaomshambulia mleta mada ndo viongozi wa kuzalisha bila kutoa huduma.
Kwa mtu anehusika na malezi full katika zama hizi hawezi kushabikia kuzaa hovyo kama bata.
 
Kitanzi cha Copper ni kweli hakina hormone za uzazi lakini usichoambiwa ni kwamba Copper ina uwezo wa kuathiri hormone za uzazi hasa estrogen ndio maana kuna hayo maudhi unayapata.

Hiyo sentensi kwamba " hakina homoni ni maneno tu ya kutia watu moyo ili waone kina uafadhali".

Mbaya zaidi kitanzi cha copper kinatoa kiwango kikubwa cha copper mwilini kuliko kiwango kinachoruhusiwa kwahiyo kinaleta " copper toxicity". So unaepuka hormones unapambana na copper toxicity.

Kuna group Facebook la wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani wanaotumia hizo Copper IUD, simulizi wanazotoa hao wamama sio poa. Ukipata nafasi kalitafute usome,utaona hayo mambo wanayopambana nayo.Hayo majitu ni masumu.

Bora njia za asili kama Billings Ovulation Method au kujipima joto mdomoni au homoni kwenye mkojo. Unazuia mimba kiuhakika bila madhara yoyote.
Tuzungumzie genye za ovulation jamani mimi ndo nakua msumbufu wal sio baba mjengo, kuna namna ya kuzizuia? 🥹
 
Communication matters. Mnajiandaa kabisa kwamba kuanzia kesho siku za joto zinaanza tuchukue tahadhari hii na hii na hii.

Sio rahisi jamani maana hizo siku unakuwa unatamani umgande mumeo kila wakati,lakini kulinganisha na madhara ya kutumia vijiti au sindano ni bora kuteseka kwenye siku za joto.

Kuna mwingine anachoma sindano anatoka damu mfululizo,anakuwa hapati hata chance kidogo ya kusex, sasa si bora kuvumilia hizo siku chache za hatari,zikiisha upo huru kuliko kukaa muda mrefu bila kusex kisa sindano zinafanya uvuje damu kila siku.

Mawasiliano na makubaliano yakiwepo,inasaidia ingawa ukweli utabaki kwamba sio rahisi kupambana na hisia zile siku za joto
Nilijaribu sindano aiseh hapana ina mauzi na nilinenepa kama tembo nikaitoa!
 
Tuzungumzie genye za ovulation jamani mimi ndo nakua msumbufu wal sio baba mjengo, kuna namna ya kuzizuia? 🥹
Wenzako wananunua madawa ya gharama kupata urges we unaomba ushauri upunguze usumbufu, ukiacha kuwa hivyo utaimiss hiyo moment.. utaichukia ndoa!
 
Bora njia za asili kama Billings Ovulation Method
Mimi mwanaume, nilijifunza kuhusu hii njia tangu nikiwa miaka 17 kupitia kitabu fulani.
Kwa uzoefu wangu hakuna njia ngumu kufuata kama hii. Afadhali withdrawal method.
Mwanaume ukae na mwanamke chumba kimoja, hauumwi kitu, rijali kamili, umri kuanzia 42 kushuka chini 18 ujizuie ngono siku 5 mpaka 7 huo mtihani mgumu sana.
 
Wanadamu wa sasa tunapenda ngono kama chakula.

Siku za hatari kwa mwanamke ni 7-10 tu. Kuanzia siku ya 10 hadi ya 18 au 20 mkiweza.

Sasa hizo siku 10 mwanaume eti anashindwa kuvumilia, ni uzembe wa kifisi.

Na wanaume inabidi wajue kukaa japo wiki 2 straight kwa mwezi bila kusex inakufanya u-recharge mwili na inner energy yako inakuwa kubwa.

Kiasi kwamba siku ukimkamata mkeo anafeel kama kakutana na mtu mpya.
Bila shaka hujaoa brother😀
 
Ndiyo, shida ni muda. Nishindwe kuwasiliana na washirika wangu wa biashara nikae kupokea simu za wanawake niliozaa nao kila wakati badala kutumia simu yangu kuwasiliana na madili ya biashara

Mapenzi au mahusiano yanahitaji

1. Muda
2. Pesa
3. Nguvu za kiume

Kwahiyo unapokuwa na wanawake wengi ni rahisi kutumia vibaya muda wako, pesa zako hata nguvu zako za kiume.
Matajiri bilionea Elon Musk na Pavel Durov wana watoto wengi kama taka taka.
 
Wenzako wananunua madawa ya gharama kupata urges we unaomba ushauri upunguze usumbufu, ukiacha kuwa hivyo utaimiss hiyo moment.. utaichukia ndoa!
Mkuu mchezo mtamu ila matokea ya ule mchezo sio matamu naogopa sana mimba alooh 😭
Situation kama hizi nawaonea sana wivu wanawake wa kizungu wenzetu wanaeleweka kiurahisi na wenza wao, shughuli iko huku sht holes countries
 
Tuzungumzie genye za ovulation jamani mimi ndo nakua msumbufu wal sio baba mjengo, kuna namna ya kuzizuia? 🥹
My dear hazizuiliki,hiyo ni kawaida. Mwili wako unakuwa unataka mtoto kwa kipindi hicho kwa lazima, kwahiyo usumbufu kwa baba mjengo muhimu. Ni hivi zile homoni zinakufanya unakuwa kama chizi fulani hivi. Ndio maana mawasiliano ni muhimu na yeye awe anakusapoti. Ni kukabiliana nazo tu kwa kujiwekea taratibu fulani za kufuata kwa kipindi hicho cha usumbufu. Ovulation ni kiashiria kwamba wewe ni mwanamke uliyekamilika na mwili wako unafanya kazi vizuri. Binafsi ukitoa ule usumbufu kwa baba mjengo, ovulation naipenda kwa sababu ndo kipindi ambacho ninakuwa na furaha muda wote,ngozi inakuwa nzuriii pia nakuwa na nguvu nyingi za kufanya kazi kwahiyo kazi zote zinazochukua muda mrefu hapo nyumbani nazifanya nikiwa ovulation. Ovulation ikikata tu nakuwaga na hasira hasira na pia nakuwa mvivu wa kazi si kazini wala si nyumbani na usingizi debe. Nakuwa binadamu mwingine kabisaaa. Nikiwa kwenye Ovulation huwa naishi, ovulation ikikata nakuwa nasogeza siku😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom