Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Discussion in 'JF Doctor' started by Gudboy, Aug 20, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Maelezo ya Awali...

  Njia za uzazi wa mpango hutumika na wanaume na wanawake kuzuia ujauzito kwa madhumuni ya kupanga uzazi ili kuwa na familia bora. Ni vigumu kusema kuwa kuna njia iliyo bora zaidi ya uzazi wa mpango kwa kuwa kila njia ina faida na hasara zake. Wote kati ya mwanamke na mwanaume wana maamuzi juu ya mipangilio wa kupata watoto.

  Kufanya uchaguzi utumie njia ipi kwa ajili ya kupanga uzazi siyo kitu rahisi kwa kuwa kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya kufanya maamuzi yeyote. Lakini awali kabisa, inabidi ujifunze njia mbali mbali, ili kuweza kubaini ni njia ipi itakayokufaa pamoja na mwenzi wako kupanga uzazi. Mnaweza pia kuwasiliana na muuguzi au daktari anayeusiana na masuala ya uzazi wa mpango kwa ushauri, ili muweze kuchagua njia sahihi itakayowafaa.


  Kabla ya kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango, inabidi ufikirie kuhusu mambo yafuatayo:
  • Afya yako kwa ujumla.
  • Ni kwa kiwango gani njia husika ya uzazi wa mpango inafanya kazi.
  • Unajamiiana mara ngapi?
  • Matarajio ya kupata mtoto siku za usoni.
  • Je ni nini faida na madhara ya kutumia njia husika ya uzazi wa mpango?
  • Je unafurahia kutumia njia husika uliyochagua?
  Yakupasa kufahamu kuwa, hata kama njia unayotumia ni bora zaidi, wakati mwingine njia hiyo yaweza kushindwa kufanya kazi. Lakini uwezekano wa kupata ujauzito utakuwa mdogo sana endapo njia uliyochagua itatumika kwa usahihi wakati wa kujamiiana. Pia ikumbukwe pia, njia za uzazi wa mpango za kutumia homoni na dawa, hazitakukinga na maambukizi ya HIV na magonjwa ya zinaa.

  ======
  Dawa au vifaa vya uzazi ni baadhi ya taratibu zinazotumiwa kuzuia mimba kutungwa. Ikiwa msichana au wanamke atafanya mapenzi pasi na kutumia mojawapo ya mbinu hizo basi, kuna uwezekano wa theluthi moja kwamba atapata mimba.

  Hata hivyo aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.


  Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV, na magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi.

  Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti tofauti, ni muhimu basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.

  Mbinu za kuzuia mimba (Contraception)
  Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono. Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa mda mrefu. Nyengine hufanya kazi papo hapo na nyengine huitaji maandalizi ya muda.

  Kondom au tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba.

  Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumuwa kwani mbali na kuzuia mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu asiambukizwe vurusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.


  Tuangalie kwanza vifaa vya kuzuia mimba:
  Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa lengo kuwa mbegu ya mwaname na ile mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume ndio isilifikie yai la mwanamke.

  Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya kuambukizana kupitia ngono.Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za wanawake ndio vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa vyenginevyo viitwavyo diaphragm na caps kwa kimombo ambavyo vinaweza kutumiwa na wanawake.


  Kondom za wanaume: Hivi hutengenezwa kutokana na aina maalum ya mpira uitwao latex, au plastiki nyembamba. Kondom ya mwanaume huvaliwa kwenye uume iliyosimama, tena kabla ya uume kuingizwa ukeni. Ikitumiwa kama inavyotakikana inakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98. Kwa kawaida kondomu hupatikana kwenye vituo au kliniki za upangaji uzazi, kwenye maduka ya madawa au hata maduka ya kawaida.

  Kondomu za wanawake: Halkadhalika hutengenezwa kwa mipira laini ya latex au plastiki nyembamba maalum. Huvaliwa ndani ya uke, huku sehemu iliyowazi ikichomoza nje kidogo. Kwa kawaida kondom za wanawake ni ghali, na pia utendaji kazi wake unakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 95.

  Aina nyenginezo na vifaa vya kuzuia mimba huwa hazipendekezwi kwa vijana lakini ni vyema kuvijua.Kuna aina nyenginezo za vifaa vya kuzuia mimba viitwavyo diaphragms na caps. Hivi hutengenezwa kutokana na kitu kiitwacho silicone au mpira laini maalum. Vikiwekwa ukeni hutumika kama vizibo vya kuzuia mbegu za mwanamme kupenya hivyo basi haiwezi kukutana na yai la mwanamke.

  Kwa kawaida caps ni ndogo kuliko diaphragms lakini kwa vile wanawake pia wana maumbo tofauti, ni sharti upate saizi utakayokutosha. Hapa ni sharti upate usaidizi wa daktari wako, au muuguzi, kuiweka.

  Inapowekwa mahali pake ndani ya uke, iwe diaphragm au cap, huziba kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanamme haitapatanafasi ya kupita. Ukishaonyeshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadae unaweza kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.


  Kwa matokeo bora zaidi, diaphragms na caps hutumiwa pamoja na dawa iitwayo (spermicide) ambayo huuwa mbegu za uzazi za mwaname. Hapo diaphragms au caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati ya 92 na 98.

  Hata hivyo itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati mwengine pia hutumiwa na gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la asilimia moja kuzuia mimba.

  Faida yake nyengine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na saratani ya (cervix) lango la nyumba ya uzazi.

  Ikiwa wewe hutumia vifaa kama diaphragms au caps, au hata kondom, ni vyema kujipangia mapema ndio usikose akiba, ndio haitakuwa karaha kuvitafuta pale unapovihitaji.


  Mbinu nyingine za kuzuia mimba
  Kuna chembe chembe za kimaumbile, zinazojulikana vyema kama homornes ambazo hutumiwa kutengeneza tembe au chanzo ya kuzuia mimba.

  Chembe chembe hizi kwa jina maalum progestogen yaani mchanganiyko wa oestrogen na progestogen, huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa mpangilio na kiwango maalum ili kuzuia mimba kutungwa. Hufanya kazi kwa namna hii:


  * Kwa kuzuia ovari kuangua mayai
  * Kwa kuzuia mbegu za mwanamme kulifikia yai (kwa kufanya majimaji ua ukeni kuwa mazito na kunata hivyo kuzuia mbegu ya mwanamme kupenya)
  * Kwa kulizuia yai kujipachika kwenye kiota cha nyumba ya uzazi.


  Tembe mchanganyiko - huwa ni kidonge cha dawa kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa chembe chembe za oestrogen na progestogen. Hii huzuia mimba kwa njia zote tatu tulizozitaja hapo juu na ikitumiwa itakikanavyo, vinategemewa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

  Tembe ni rahisi kutumia - Mradi tu unakumbuka kumeza vidonge kulingana na maagizo. Wakati mwengine pia huifanya hedhi, kupungua na kupunguza pia maumivu wakati wa hedhi.

  Lakini athari zinazoandamana na utumiaji wa vidonge hivyo ni pamoja na kuchafukwa na moyo, kuongezeka unzani, na athari mbaya zaidi ni iwapo itatokea hali ya kuganda kwa damu kwenye mishipa ya kupitisha damu.

  Vidonge vya Progestogen pekee (POP) - Aina hii ya Tembe huitwa pia "mini pill" na huwa ina chembe chemba za progestogen pekee. Huzuia mimba kwa njia kama zile zile zinazozuia tembe za mchanganyiko, na ina utendaji kazi wa kati ya asilimia 96 na 99. Hata hivyo kama una uzani wa zaidi ya kilo 70 uwezo wake wa kuzuia mimba hupungua

  Faida kuu ya kutumia vidonge hivi ni kwamba vina athari ndogo za kiafya. Lakini tatizo ni kuwa ni sharti tembe imezwe wakati ule ule kila siku , kama umechelewa basi isipitishe zaidi ya masaa matatu.
  Sindano - Hii ni chanjo ya kuzuia mimba inayotengenezwa na chembe chembe hizo hizo za homoni ya progestogen. Tofauti na tembe, ambazo ni sharti kumeza moja kila siku, sindano pindi inapodungwa inakupa kinga dhidi ya mimba, kwa mda wa kati ya wiki nane hadi 12 kuambatana na aina inayotumiwa.


  Hudungwa takoni, na dawa kuingizwa ndani ya mishipa ya damu na ina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 99.

  Faida kuu ya njia hii ya sindano, ni kwamba hutakuwa na wasiwasi wa kupata mimba unapofanya ngono, kwa mda wa angalau wiki nane au 12.

  Lakini pia ina athari zake - ni kwamba huenda dawa hii ikavuruga mpangilio wako wa kawaida wa kupata hedhi, au ukatoka hedhi kiwango kisicho cha kawaida cha damu, au kwa mda mrefu, au hedhi ikapotea kabisa. Pia inaweza kusababisha kuongezeka uzani.

  Homoni au Vidonge vya kupachika chini ya ngozi Hapa dawa kama ile ile ya tembe au chanjo, hutengenezwa na kuwekwa kwenye kifaa cha plastic mfano wa kijiti cha kiberiti. Hupachikwa ndani ya ngozi chini ya kwapa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo.Hii ni njia ya mda mrefu ya kuzuia mimba. Inaaminika kuzuia mimba kwa aslimia 99 na inaweza kufanya kazi kwa mda wa hadi miaka mitatu.
  Kuna aina nyenginezo za upangaji uzazi ambazo, ingawa kwa hali ya kawaida hazipendekezwi kwa vijana, si vibaya kuzijua.


  Kitanzi au koili, ambacho kwa lugha ya kitaalam kinajulikana kama Intra-uterine device au IUD hutengenezwa kwa plastiki na shaba, na hupachikwa kwenye mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.Vitanzi huanza kufanya kazi pindi kinapopachikwa. Hufanya kazi kwa njia mbili kuu. Kwanza, kwa kuzuia mbegu za kiume kutangamana na yai, na pili kuzuia yai kukubaliwa kujipachika ndani ya mfuko wa uzazi.

  Kitanzi au koili kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 98 na 99. Na pindi kikitolewa asili ya uwezo wa wanamke wa kushika mimba anapofanya ngono, unarudi vilevile.

  Hata hivyo moja ya matatizo ya kitanzi ni kwamba vinaweza kuifanya hedhi yako kuwa nzito (damu kutoka nyingi) na pia huenda ukapatwa na maumivu, mara nyengine inaweza kutoka mahali kilipowekwa na kusukumwa nje ya mfuko wa uzazi.Hivyo ni vyema kumuona daktari mara kwa mara ili kama imechomoka, ipachikwe tena vyema.

  Njia asilia ya mpango wa uzazi:
  Njia hii inahitaji makini sana kuitumia. Kwani inafanya kazi tu ikiwa wanamke anafanya mapenzi tu wakati ule ambao kiasilia hawezi kushika mimba.

  Hii inawezekana kwa kutayarisha tarakimu za siku za hedhi, na kupima hali ya joto la mwili. Njia hii inahitaji uangalifu na uzoufu mkubwa – Kwa vile ni ya kubahatisha haipendkezwi kwa vijana ambao hawako tayari kupata mtoto.


  Kwa bahati mbaya watu wengi hudhani kwamba kutoa uume kutoka ukeni, pindi tu kabla ya kufikia kilele cha kumwaga manii, ni moja ya njia za kuzuia mimba.

  La sivyo kwani mara nyingi mbegu za kiume hutangulia kutoka hata kabla kufikia kilele katika hali ya kufanya mapenzi. Hivyo basi hata ukitoa uume huenda umeshachelewa!Vasectomy au Tubuligation, Hii ndiyo njia pekee ya kudumu ya kuzuia mimba.

  -Vasectomy ni njia ya kumfanya mwanamme asiwe na uwezo wa kutunga mimba ilhali Tubuligation ni njia ya kumfanya mwanamke asiwe na uwezo wa kushika mimba. Hii inafanyika kwa njia ya upasuaji mdogo.Mwanamme anafanyiwa upasuaji kwa kukata vibomba vinavyopitisha mbegu za kiume kutoka kwenye makende hadi kwenye uume. Upasuaji huu kwa mwanamke unahusisha kukatwa au kuzibwa kwa vibomba vinavyopitisha mayai kutoka kwa ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi.

  Baada ya upasuaji huu, ni vigumu mwanamke au mwanamme kurudishwa tena katika hali ya mwanzo ya kuweza kuzaa, kwa hivyo njia hii inatumiwa tu kwa sababu za kimatibabu au ikiwa mhusika amefikia uamuzi wa hakika kwamba hataki tena kupata watoto (zaidi).

  Kitanzi cha Intra uterine system au IUS - Hiki nacho kimetengezwa kwa plastiki, yenye muundo wa T kikiwa na chechembe za homoni ya progestogen ndani. Kinaweza kupachikwa ndani ya mfuko wa uzazi na daktari au muuguzi.

  Kitakapopachikwa, progestogen pole pole huingia ndani ya mwili, na kuzuia mimba katika njia ile ile kama vinavyozuia tembe. Kinaweza kutumika kwa mda wa miaka 5, na kinakadiriwa kuzuia mimba kwa asilimia 99.


  -Kitanzi cha IUS ni kizuri kwa wale walio na matatizo ya maumivu wakati wa hedhi, kwa sababu kinapopachikwa (ingawa wakati wa kupachikwa huenda ukapata maumivu kidogo) baadaye husaidia kupunguza hedhi au hata kuisitisha kabisa, kutokana na homoni hizo za progestogen. Madhara ya njia hii nayo ni kama, kuongeza uzani, kuumwa na kichwa, kutokwa na damu kusiko na mpango, na mabadiliko ya majira ya hedhi. Pia inaweza kuchopoka, hivyo itabidi kumwona muuguzi au daktari kila mwezi kuhakikisha kiko sawa.

  Ni vyema kujadili juu ya aina mbalimbali za mpango wa uzazi ili kuchagua vyema. Daktari wako au muuguzi atakushauri ipasavyo. Hata hivo kumbuka njia hizi za kuzuia mimba hutumiwa zaidi kwa minajili ya mpango wa uzazi, hivyo basi haziwezi kukukinga dhidi ya maambukiko ya virusi vya Ukimwi, au magonjwa mengine yayayosambazwa kupitia ngono.

  Ni busara kutumia kondom kila unapofanya mapenzi na mtu ambaye afya yake ya uzazi huifahamu - Hakikisha pia unaufahamu vizuri jinsi ya kutumia kondom na unajua jinsi ya kufanya ngono salama kwa jumla.


  Threads zinazofanana


  CONFESION: Madhara ya Vidonge vya Uzazi Wa Mpango...

  Njia ya uzazi wa mpango wa asili (natural birth control)
  Vikwazo vya Viongozi wa Dini kuhusu kampeni ya uzazi wa Mpango
  Athari za kutumia njia za uzazi wa mpango za kisasa
   
  Last edited: Aug 20, 2009
 2. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Habari zenu wana MMU.

  Mimi ni buheri wa AFYA njema kabisa.Hapo nyuma tuliangalia athari kubwa zitokanazo na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango.

  Member wengi humu hasa wamama kwa wadada walijumuika nasi katika kushuhudia madhara ambayo kimsingi ni matatizo makubwa sana kwa afya za hawa mama zetu.Ingawa serikali na vyombo vyake vya afya vimekuwa vikitumia fedha nyingi katika kuhimiza matumizi ya hivi vidonge.Kwa mchango wa wadau humu MMU tutajifunza mengi sana na Mwishoni kila mdau atachagua njia sahihi ya uzazi wa mpango.

  Leo tena tutapata muda wa kutafakari hayo maudhi madogo madogo ambayo ndio msingi mkubwa wa matatizo ya kiafya ya uzazu ya hawa mama zetu.

  Ntaziangalia njia mbali mbali na matatizo yake kwa ufupi sana, na wadau wengine wataongezea katika kufanikisha somo letu.

  NJIA mbali mbali......kama zifuatavyo...

  1.KITANZI
  Kifaa cha plastiki inakaa kwenye mji wa mimba.Inafaa kwa wale wenye mume mmoja mwaminifu

  INAVYO FANYA KAZI

  Inazuia yai la mwanamke lisikutane na mbegu za mwanaume

  MAUDHI YAKE

  Watu wengine kutokwa na damu nyingi,Kusababisha magonjwa ya zinaa yaingie kwenye mji
  wa uzazi kwa urahisi ikiwa umeambukizwa.

  2.KUFUNGA KIZAZI
  Ni operesheni kuziba njia ya mayai ya mama au mbegu za baba ili zisikutane
  Inafaa kwa wale ambao wamekamilisha familia


  MAUDHI YAKE

  Huwezi kuzaa daima
  Ni rahisi zaidi kwa baba kwa sababu njia yake ni juu juu kuliko ya mama, lakini zote ni operesheni ndogo tena bure.

  3.Vidonge (Combined Oral Contraceptive)
  4.NJIA YA SINDANO(DEPO PROVERA)
  5.VIPANDIKIZI

  Vidonge vya Uzazi wa Mpango vyadaiwa kusababisha upofu,Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha ugonjwa wa macho ujulikanao kama Glaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.

  Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

  Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

  Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

  Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen vina umuhimu katika seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

  "Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho," anasema Dk Pasquale.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

  "Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge," anasema(Mwananchi 20/jan/2014)

  .....Kwa wale walotumia njia hizi watuambie hayo maudhi madogo madogo kama wanavyo yaita wenyewe wahusika ni yapi.

  ------------------------

  --------------------------------

  Kwa Ushahidi wa madhara ya matumizi ya njia hizi - https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/336309-confesion-madhara-ya-vidonge-vya-uzazi-wa-mpango-8.html#post8429829

  Mjadala juu ya nini Madhara ya njia hizi - https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/212274-msaada-jamani-nini-madhara-ya-vidonge-vya-uzazi-wa-mpango.html
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280


  [​IMG]uzazi wa mpango ni jambo muhimu sana katika jamii yetu, lakini kuna njia nyingi sana ukitaka kupanga uzazi na familia nyingi waliotumia uzazi wa mpango wanasema hawajutii kutumia njia hizo....

  lakini najiuliza ni njia gani nzuri ya kutumia? kwasababu watu wengine hupendelea kuweka vijiti japo wengine husema vijiti hivyo hutembea mwilini na kuleta madhara ya cancer.

  wengine hutumia kitanzi, hiki hukaa muda mrefu wa miaka kumi lakini pia wengine huniambia tatizo la kitanzi style yako kamwe ni kifo cha mende maana ukijifanya unatoa machejo kinafyatuka, na wengine wanasema mwenza wako akiingia kinamtia kero kwa kumgasi...

  na wengine wanatumia vidonge, lakini wengine husema ukikosea kumeza kimoja tu na ukacheza basi goli lazima liwe lako, na wengine wamepata ujauzito pindi wanatumia hizi dawa...

  ama kutumia condom? sawa kwa mwanzoni mnaweza kutumia condom lakini mpaka lini, maana wanaume wengi wanasema yani mke wangu mwenyewe nimvalie condom???????????? ama kwa wale walevi najua pindi pombe zimekolea nivigumu sana kukumbuka condom....

  je wewe umeshawahi kutumia njia za uzazi na ni ipi na je kunamadhara gani uliyokutana nayo???? maana kunawanawake wanaotaka kutumia njia hizi lakini hawajui ipi ni salama maana maneno yanasemwa mengi...


   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ahsante Mzizi-Makvu kwa hii thread. Watu wengi sana wana 'negative attitude' kwa njia mbali mbali za uzazi wa mpango, lakini wengi kati ya hawa sio watumiaji wa njia za uzazi wa mpango, lakini wako mstari wa mbele kuhakikisha watu hawatumii njia za uzazi wa mpango.

  Natumai kupata real testimonies za watu/wanawake ambao wanatumia/wametumia njia za uzazi wa mpango kupitia thread hii!
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Njia salama kabisa ni kalenda
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Mzizimkavu,

  "Usalama/salama" ni nini katika muktadha wa swali lako? Je unakusudia kusema ufanisi (effectiveness) - yaani kufanya kile inachotakiwa kufanya kwa wakati unaotakiwa? Au usalama kwa maana ya kutokuleta madhara kwa mtumiaji?
   
 7. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe Malaika....kalenda ndio njia salama kupita zote, lakini ndio njia ngumu kueleweka na kuifuata kwa uhakika kwa watu wengi tu. Kuna nyingine inaitwa 'coitus inturruptus'...hii ni ile mwanaume akikaribia 'kukojoa' (kumradhi lugha) basi anachomoa uume na kumwaga nje. Nayo ni salama lakini ina ugumu kwenye timing especially kwa wanaume wanaopenda kusikilizia bao. Na si reliable kama mwanaume ni mtu wa mabao zaidi ya moja.
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal, katika Mkutano wa mwaka wa Uzazi wa Mpango, Oktoba mwaka huu. Katika Mkutano huo Tanzania ilionekana bado ina matumizi ya chini ya dawa za uzazi wa mpango. Picha na Maktaba
  KWA UFUPI

  • Kupanga uzazi ni jambo muhimu katika kujenga familia bora lakini njia za uzazi wa mpango zinatajwa kuzua changamoto kadha wa kadha kwa watumiaji.


  Pamoja na kuwa ni njia nzuri ya kuzuia ujauzito, vidonge vya Uzazi wa Mpango vinatajwa kusababisha ugonjwa wa macho ujulikanao kama Glaucoma, unaoelezwa kuwa ni chanzo kikuu cha upofu.

  Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.

  Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

  Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

  Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

  Wanawake zaidi ya 3,400 wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walifuatiliwa kwa zaidi ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utafiti huo.

  Profesa Shan Lin wa Chuo Kikuu cha Carlifonia, San Francisco anasema wanawake wanaotumia vidonge hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatakiwa kupima maradhi ya macho aina ya Glaucoma na afya zao zifuatiliwe kwa uangalifu na wataalamu wa macho.

  Utafiti huo umebaini kuwa wanawake waliotumia vidonge hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu walikuwa na hatari kwa asilimia tano ya kupata upofu usababishwao na glaucoma ukilinganisha na wasiotumia vidonge hivyo.

  Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen vina umuhimu katika seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

  “Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho,” anasema Dk Pasquale.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

  “Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge,” anasema Dk Masawe anasema si vyema watu kuzitumia dawa za Uzazi wa Mpango kwa mazoea na endapo wataona ni vyema kufanya hivyo, washauriane na wataalamu wa afya.
  Anasema kuwa elimu inahitajika kwa kina kuhusu matumizi ya dawa hizo kwani wapo baadhi ya watu wanaozitumia bila mpangilio wala utaratibu maalum.

  “Hizi dawa zinasaidia lakini zisipotumiwa kwa uangalifu, huenda zikasababisha madhara,” anasema Dk Masawe.

  Kwa upande wa utafiti huo uliojikita kuangalia madhara ya vidonge hivyo kwa wanawake, watu wanaovitumia wanatakiwa kuwa makini na uhusiano uliopo kati ya afya ya uzazi na maradhi ya macho hasa kama mtumiaji amefunga hedhi mapema.

  Matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa katika mkutano wa kila mwaka wa Chuo Kikuu cha Mfumo wa Macho Marekani (USP), yanasema wanawake zaidi ya 3,046 walifanyiwa uchunguzi kuhusu afya ya uzazi na maradhi ya macho.

  Pamoja na sababu nyingine za maradhi ya macho, wanasayansi waliofanya utafiti huo wanasema kutumia vidonge vya uzazi kwa muda mrefu, ndicho chanzo kikuu cha upofu na kutaja sababu nyingine kuwa ni historia ya familia, shinikizo la ya macho na kisukari.

  Watalaamu wa afya nchini wanasema bado madhara ya dawa hizo yanatofautiana kulingana na aina ya dawa anayotumia mhusika.

  Madhara mengine ya dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu, kichwa kuuma, matiti kuuma, kuongezeka uzito na kupata hedhi bila mpangilio.

  Dk Joseph Matiku wa Kituo cha Afya, Mugumu, Serengeti anasema, hatari zaidi ni kwa binti wanaotumia dawa hizo kwa muda mrefu kabla hawajaanza maisha ya ndoa.

  “Wapo wanawake ambao wanapata uvimbe kwenye kizazi kutokana na matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi. Ingawa hakuna utafiti uliofanyika kuthibitisha hili, lakini wanawake wengi wanaotumia dawa hizi hapa nchini wanapata uvimbe maarufu wa Fibroids” anasema.

  Hata hivyo, Oktoba mwaka huu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi anasema Wizara ya Afya ipo kwenye harakati za kutafuta fedha ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanawake wanaostahili kupanga uzazi wanapata dawa husika.

  Mwaka jana wakati wa Mkutano wa Uzazi wa Mpango uliofanyika London Uingereza, Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuwa hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania itafikisha asilimia 60 katika huduma za uzazi wa mpango. Vilevile katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Uzazi wa Mpango uliofanyika Oktoba mwaka huu, Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal alisema juhudi za ziada zinahitajika kuhakikisha kiwango cha watumiaji wa huduma za uzazi wa mpango, kinaongezeka ili kutimiza lengo la kimataifa ya kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma hiyo.
  Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kuwa, kiwango cha matumizi ya huduma za uzazi wa mpango kwa nchi zilizoendelea ni asilimia 72, huku Tanzania iliyo kwenye kundi ya nchi zinazoendelea ikiwa ni asilimia 27 tu.

  Dawa za uzazi wa mpango hufanyaje kazi?

  Vidonge vya uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuweka uwiano katika kiwango cha vichocheo.

  Katika hili, kazi kubwa ni kuzuia homoni za estrogen kuongezeka na kufikia kiwango cha kati au cha juu.

  Bila homoni ya estrogen, tezi ya pituitari haiwezi kuifanya mirija ya uzazi kuruhusu mayai yaliyochavushwa kwenda kukutana na mbegu za kiume kwa ajili ya utungishwaji wa mimba.  Ugonjwa huu unaelezwa kuwa sababu kubwa ya kusababisha upofu kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi kwa muda mrefu.

  Hayo yamebainishwa kwenye Utafiti wa Afya na Lishe uliofanywa na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa cha Marekani(CDCP).

  Utafiti huo unasema kuwa, seli zilizoko katika neva za macho zina homoni za estrogen ambazo hufanya kazi ya kulinda macho, vidonge hivyo huingilia mchakato huo wa ulinzi kwa kupunguza kiwango cha homoni hizo.

  Unasema kuwa wanawake wanaofunga hedhi mapema au wanaotumia vidonge ambavyo huzuia kuzalishwa kwa vichocheo vya estrogen, na dawa za saratani ya matiti, huweza kupata upofu.

  Wanawake zaidi ya 3,400 wenye umri wa zaidi ya miaka 40 walifuatiliwa kwa zaidi ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utafiti huo.

  Profesa Shan Lin wa Chuo Kikuu cha Carlifonia, San Francisco anasema wanawake wanaotumia vidonge hivyo kwa zaidi ya miaka mitatu, wanatakiwa kupima maradhi ya macho aina ya Glaucoma na afya zao zifuatiliwe kwa uangalifu na wataalamu wa macho.

  Utafiti huo umebaini kuwa wanawake waliotumia vidonge hivyo kwa miaka zaidi ya mitatu walikuwa na hatari kwa asilimia tano ya kupata upofu usababishwao na glaucoma ukilinganisha na wasiotumia vidonge hivyo.

  Kiongozi wa utafiti huo, Dk Louis Pasquale wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Havard anasema vichocheo vya Estrogen vina umuhimu katika seli za retina ambazo zinajulikana kwa kupokea homoni hizo.

  “Kuwepo kwa homoni za estrogen kunazisaidia seli hizo kuwa hai kwa hiyo wanawake wanapotumia vidonge vya uzazi, homoni hizo huharibiwa na kurahisisha uharibifu wa macho,” anasema Dk Pasquale.

  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk Cyriel Masawe wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MNH) anasema ni hatari kwa wasichana wadogo ambao hawajaolewa kutumia dawa hizo ovyo.

  “Kwa mfano mikoa ya Lindi na Mtwara, tumegundua wasichana wadogo ambao hawajaolewa wanatumia zaidi sindano za uzazi wa mpango na vidonge,” anasema

  chanzo.
  http://www.mwananchi.co.tz/Vidonge-vya-Uzazi-wa-Mpango-vyadaiwa-kusababisha-upofu/-/1596774/2092992/-/item/2/-/wp9iiv/-/index.html
   
 9. MKOBA2011

  MKOBA2011 Senior Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii njia ya kalenda ilikuwa nzuri enzi za wazee wetu sababu tarehe zilikuwa costant sasa hivi na mamisosi haya watu wanayokula,pilikapilika za maisha mara frustuation,mara unawaza kuibiwa ,mara sijui nini tarehe zinabadilika badilikan utashangaa unaanza kumhisi mkeo vibaya kuwa mimba siyo yako kumbe mambo hayako kama unavyofikiri hormone za watu sasa very disturbed ndiyo maana sasa mwanamke makini anatakiwa kuwa tayari kwenda ile safari ya kila mwezim uda wote bila kujali kalenda yake.Nadahani mshasikia mtu anasema jamani mbona siku ilikuwa haijafika.Thats how things is nowdays
   
 10. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kalenda ndiyo the best kwa usalama; lakini ni vizuri ikatumiwa pamoja na mbinu ya kuangalia mabadiliko ya joto la mwili na hali ya ute unaotoka katika sehemu ya siri ya mwanamke.
  Tatizo kubwa la njia hii ni kwamba katika kipindi cha kupata mimba mwanamke anakuwa na joto na hamu sana kuliko wakati mwingine. Lile ongezeko la joto huwavutia sana pia wanaume; hivyo inabidi wote wawili wawe na tahadhali.
  Inapotokea kuwa wanaona dalili zote hizo - yaani kalenda hairuhusu na ute na joto vinaonyesha hali ya hatari, lakini wote wanaona hawawezi kujizuia then watumie condom hasa za kiume!
   
 11. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  njia nzuri ya uzazi wa mpango ni kunyonyesha...ukiwa unanyonyesha miaka 2 au mitatu bleed hakuna, mpango mzuri tu huo
   
 12. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Njia nzuri na salama ni IUD sababu imeleta suluhisho kwa mapungufu ya njia zingine
  1. Condom: ukishindwa kuitumia vizuri haisaidii, na kuna wakati huna condom ndani.
  2. Diaphragm and cervical ring: it is not hygienic, tuseme tu ukweli.
  3. pills: they affect the mood, na unaweza kusahau au kushindwa kuzinya wakati fulani (umelala msibani, hujanywa, ukirudi home unakaribishwa na baba...
  4. sindano: ikiwa unataka kuzaa kati kati ya process, utashindwa kui-reverse, hadi dawa idisolve yote mwilini

  Kweli na IUD ina matatizo yake kama heavy bleeding (coper T) au less bleeding (hizi za plastic) ila unakua more in control. pia ikikutana na mwanamke mwenye hygiene pungufu au wanawake wenye kusafiri sana kama mimi, inaweza kusababisha au ku-worsen infections.
  Ila uzuri wake unaweza kuitoa saa yoyote au kubaki nayo for 3, 5 to 10 year, huna pressure ya kukumbuka iko wapi, next check ni lini etc. Na last but not least, you are in control, your partner plays a little role (if at all) in the whole process.
   
 13. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,435
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Asikwambie mtu.........ni kondomu pekee
   
 14. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Russian nimependa maelezo yako. Hapo kwenye IUD za plastic,hiyo less bleeding inaambatana na kuskip kabisa au inapungua tu uwingi? Please elimisha.
   
 15. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kijiti cha mkononi nimesikia wanawake 3 tofauti kimefanya mapigo yao ya moyo
  kwenda mbio sana. mmoja kati yao amepata tatizo la presha kupanda.
   
 16. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Jamani mie sielewi hata moja..msaada zaidi yaq hapo kabla sijaingia kunako ndoa..
   
 17. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kuna ambao inapoteza kabisa japo sio kawaida. normally inapunguza sana kiwango cha damu ingawa inaweza kuongeza siku za kubleed (ex: few dark spots the first and last 2 days with 2 light bleedings kati kati). Na hata kwa wale wanao skip, wanaweza kuskip mwezi huu, mwezi ujao ikatoka kidogo etc.
  Uzuri ni kwamba hata kama huoni damu huna stress sababu rate of failure ni 1/10 000 which is namna ya kusema "virtually impossible".
   
 18. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .....Kalenda njia salama, lakini inabidi mumeo awe muelewa na mshirikiane kwa pamoja. Kama una mume anayependa sex mara nyingi na bila schedule maalum hii haifai. Vile vile kuna hii njia, unaweza kuzaa hata mfululizo idadi ya watoto unaohitaji and then funga mirija.

  Madawa hayo siyo mazuri hata kidogo, hao wenyewe madaktari wa kike hata hawatumii.
   
 19. fxb

  fxb Senior Member

  #19
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ok hasa tunafikia bilioni 7......
  Kwa TZ wanasayansi jamii wanasema asilimia 96 ya wakinamama wenye umri wa miaka 15 mpaka 49 ambapo wengi wao wanaweza kupata ujauzito bila kipingamizi wameshawahi kusikia kwamba kuna njia za kupanga uzazi. ambao hawajaolewa ni asilimia arobaini na ushehe hizi ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango na wale walio kwenye ndoa watumiaji ni asilimia 27.
  Hebu niendelee kuona wapi wanajamvi wataangukia na kutujuza wadhaniavyo wao.
  Good staff MM
   
 20. Yerusalem

  Yerusalem Member

  #20
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Mimi nadhani njia salama ni kalenda tu....,Mimi nina mfano wa rafiki yangu ambaye alikuwa mtumiaji mzuri sana wa sindano
  mwanzoni hazikumpa shida lakini baada ya mwaka 1 ndipo alipoanza kuona joto ya jiwe yaani amebleed kwa muda kama wa miezi 8 mfululizo
  mpaka akahisi ataishiwa damu,ametumia dawa kwa muda mrefu mpaka akahisi amelogwa lakini Mungu ni mwema sasa hivi amepata nafuu, amesema amekoma hatarudia tena kutumia hizo njia za uzazi wa mpango.
   
Loading...