Wanawake wenzangu wenye vitanzi (IUD), mnaendeleaje?

Wanawake wenzangu wenye vitanzi (IUD), mnaendeleaje?

Naona wamama mmeichangamkia hii mada ya jinsi ya kuliwa mbususu bila kushika mimba 😊...
Mada ya uzazi wa mpango kwenye dunia ya sasa haikwepeki. Ndio maana hadi watoto wa shule ya msingi wanafundishwa. Maredioni wanatangaza na mabango barabarani tunawekewa. Ni sehemu ya maisha na haimuhusu mwanamke peke yake,inawahusu wote wawili mwanamke na mwanaume maana mwanamke hajipi ujauzito, anapewa na mwanaume.
 
Kwa sisi waafrika mwanamke bado anachukuliwa kama " chombo cha starehe" na kazi yake ni kutimiza matamanio ya mwanaume bila kujali hisia au afya ya mwanamke huyo. Ni hivi punda afe mzigo ufike. Wanaume wanakuzwa na fikra hizo na wanawake wanakuzwa na fikra kwamba wao ni vyombo vya starehe na wanapaswa kutimiza haja za wanaume wao hata kama wao wataathirika. Ndio maana inatakiwa watu wazungumzie masuala haya kabla hata ya kufunga ndoa,matarajio yajulikane. Mimi binafsi pamoja na baba mjengo tuliongea hili suala kwa undani kabla ya kuoana,mimi nilikuwa nafahamu kwahiyo nilianzisha mada . Halafu tukajifunza wote kwa pamoja ( tulipata mwalimu online) alikuwa mwanamke na tuliomba nafasi ya kusikia kutoka kwa mume wa huyo mwalimu jinsi gani yeye kama mwanaume analichukulia hilo swala na anakabiliana na changamoto zinazojitokeza. Pia wao binafsi walipata fursa ya kuongea kivyao( man to man). Ilisaidia kwa kweli. So tulifunga ndoa tushajua what to expect.
Hongereni sana, i wish kipindi naolewa ningefanya hivi,ingeepusha mengi.
Ila sasa mihemko ilikua juu mno acha tudeal na consequences zakr 😄
 
Watu sikuhizi mnaogopa mimba kuliko ukimwi😅

Hapo dawa ni kuolewa na mwanaume mkae mbalimbali! Tofauti na hapo atakubaka kwa lazima😆
Haswaa sisi ambao tushazaa tunaogopa sana mimba 🤣🤣🤣 maana cha moto tumekiona!
Hamna mama anatamani kuleta mtoto halafu asipate mahitaji ya msingi, kwahiyo ukiona mmoja au wawili kichwa kinapata moto lazima uogope kuongeza!
 
Kurudia kosa ni kosa! tuweni makini sana kama tunaona kifo mbele yetu🤣💔
 
Hongereni sana, i wish kipindi naolewa ningefanya hivi,ingeepusha mengi.
Ila sasa mihemko ilikua juu mno acha tudeal na consequences zakr 😄
Hujachelewa dear. Unaweza anza hata sasa,halafu hiyo mihemko uliyoipata si ajabu, penzi likinoga unakuwa unatamani mchumba wako akuoe hata kesho. Ukiambiwa usubiri hata siku moja unaona mwaka. Kwahiyo nakuelewa.
 
Kitanzi hakisababishi UTI moja kwa moja bila kinaongeza hatari kwa sababu bacteria wanaweza kuweka makazi pale ya kudumu kisha bakteria hao wakawa wanahama mara kwa mara na kusogea kwenye njia

Kitanzi hakisababishi UTI moja kwa moja bila kinaongeza hatari kwa sababu bacteria wanaweza kuweka makazi pale ya kudumu kisha bakteria hao wakawa wanahama mara kwa mara na kusogea kwenye njia ya mkojo na kuleta maambukizi. Katika hili kitanzi kinakuwa kama makazi ya bacteria kitaalamu wanaita " biofilm".
Kwa hyo bacteria wa UTI wakiingia mfumo wa uzazi bado inaitwa UTI
 
Pole
Mie nachangia km mwanaume. Hayo ni mambo ya kuzungumzika, mfano mie siku za hatari zote nikitaka nipige mi BAM BAM namwagia nje na tunajitahidi kucheza na kalenda, sana, sababu tayari ana operation 2, na kondom ni kitu ambacho sikiwezi kabisaaa.. hivyo ni mwendo wa tarehe na kumwagia nje ikishindikana kuvumilia.
Hivi condoms ziliwafanya nini wanaume??
 
Mimi nayotumia inaitwa Billings Ovulation Method au BOM kwa kifupi,kwa njia hii unachunguza ule ute unaotoka kwenye via vya uzazi kwa kuhisi tu " unajiskiaje" mfano unyevu, ukavu,utelezii, etc. Pia unaweza kuuchunguza kwa macho au hata kuushika kama bado hujawa mzoefu wa kuchunguza unajiskiaje. Ukishajichunguza na kujua kama uko kwenye siku za kushika mimba au siku salama then unaepuka tendo la ndoa kama hautaki kushika ujauzito kwa wakati huo. Njia nyingine zinahusisha teknolojia kama vile kupima homoni kwenye mkojo kwa vipimo unavyoweza kuwa navyo nyumbani au kupima joto la mwili kwa themometa maalum inawekwa mdomoni. Teknolojia hizi hurahisisha mwanamke kujua kama yuko kwenye siku za kushika ujauzito au lah kisha yeye mwenyewe atafanya maamuzi kulingana na anataka kushika ujauzito au kuzuia ujauzito.
Hii njia nzuri.. ila upatikanaji wa hivo vipimo itakua changamoto
 
Kwa hyo bacteria wa UTI wakiingia mfumo wa uzazi bado inaitwa UTI
Bakteria wakiwa kwenye mfumo wa mkojo ndio inaitwa UTI yaani Urinary Tract Infection haijalishi hao bakteria wametokea wapi. Hii ni kwa sababu,kwa kawaida mfumo wa mkojo haupaswi kuna na mdudu yoyote tofauti na mifumo mingine kama ya uzazi au mfumo wa chakula ambao huwa na bakteria wa asili ( normal flora)kwa ajili ya ulinzi. Kwenye hii issue ya kitanzi ni kuwa bakteria wanahama kutoka kwenye kitanzi kilichopo kwenye mfumo wa uzazi na kwenda kwenye mfumo wa mkojo ( hii mifumo ipo karibu sana ). Kwa kawaida uhamaji huu wa bakteria ni wa nadra lakini kitanzi kikikaa muda mrefu huweza kutumiwa na bakteria kama " biofilm" au makazi yasiyo ya asili ya vijidudu kwenye mwili wa binadamu. Bakteria wanaokaa hapo kwenye biofilm huwa wengi na baadhi yao huweza kuhama kwenda maeneo ya jirani. Kutokana na uwepo wa kitanzi ina maana muda wote kuna bakteria wanaohama na kusogea kwenye mfumo wa mkojo hivyo kuleta maambukizi ya UTI yasiyokwisha. Kuna tafiti zimefanyika kuhusu hili,naweza kutuma link ujisomee coz zimeelezea kiundani zaidi
 
Hii njia nzuri.. ila upatikanaji wa hivo vipimo itakua changamoto
BOM haihitaji kipimo chochote, ni wewe mwenyewe na mwili wako basi ,hakuna gharama ya vifaa vya kununua . Lakini kama unataka vipimo unaweza kuagiza online sasahivi tupo enzi za kidijitali.
 
Bakteria wakiwa kwenye mfumo wa mkojo ndio inaitwa UTI yaani Urinary Tract Infection haijalishi hao bakteria wametokea wapi. Hii ni kwa sababu,kwa kawaida mfumo wa mkojo haupaswi kuna na mdudu yoyote tofauti na mifumo mingine kama ya uzazi au mfumo wa chakula ambao huwa na bakteria wa asili ( normal flora)kwa ajili ya ulinzi. Kwenye hii issue ya kitanzi ni kuwa bakteria wanahama kutoka kwenye kitanzi kilichopo kwenye mfumo wa uzazi na kwenda kwenye mfumo wa mkojo ( hii mifumo ipo karibu sana ). Kwa kawaida uhamaji huu wa bakteria ni wa nadra lakini kitanzi kikikaa muda mrefu huweza kutumiwa na bakteria kama " biofilm" au makazi yasiyo ya asili ya vijidudu kwenye mwili wa binadamu. Bakteria wanaokaa hapo kwenye biofilm huwa wengi na baadhi yao huweza kuhama kwenda maeneo ya jirani. Kutokana na uwepo wa kitanzi ina maana muda wote kuna bakteria wanaohama na kusogea kwenye mfumo wa mkojo hivyo kuleta maambukizi ya UTI yasiyokwisha. Kuna tafiti zimefanyika kuhusu hili,naweza kutuma link ujisomee coz zimeelezea kiundani zaidi
Tuma link kiongozi
 
Back
Top Bottom