Naonaga hainisaidiii huwa hakuna unafuu jamaniKwa uchungu ulivyo naupitaga huu uzi km ukoma
Hii ni laana kwa hakika
Hapo kwenye ukali huyo mkeo kama mimi tu nakuwaga kama simba au chui jike hadi kuunguruma huku nikiuma vyuma vya kitanda
Kuna stage manesi wanasema lalia ubavu na pumulia mdomoni wakati huo ukinywa chai ya moto......ebwana ndio
Naonaga hainisaidiii huwa hakuna unafuu jamani
Kwa uchungu ulivyo naupitaga huu uzi km ukoma
Hii ni laana kwa hakika
Hapo kwenye ukali huyo mkeo kama mimi tu nakuwaga kama simba au chui jike hadi kuunguruma huku nikiuma vyuma vya kitanda
Kuna stage manesi wanasema lalia ubavu na pumulia mdomoni wakati huo ukinywa chai ya moto......ebwana ndio
Usiogope mkuu.Uzi nauogopaga huu hapa nilicomment km mkimbizi as if ni rahisi vile!!
Nini zetu walikua wanarudiil mara 12 mama zetu mara nne hadi sita
Wa siku hizi mara moja yenyewe wanaogopaaaa
Pia nimewahi kusikia Maongezi ya watu wazima wamama Maana wako hapa wanaongelea dawa ya kupunguzaa uchungu kuchomwaa mgongoni au kisu
Je kuna tofauti yeyote ya mapenzi kwa mtooto kati ya mama ambaye kajifungua mtoto Ndani ya nusu kaputi yaani hakusikia lolote au kisu na mama Huyu aliyesukuma kwa jasho la damu?
Wamama hawa walikua wakisema ni muhimu Sana kuzaaa Kwa uchungu kama maandiko ilivyosema , kisu kiwe option ya mwisho baada ya kutapatapa
Yale maumivu ndio sadaka na gharama ya kumpata mtoto iweje wamama wa leo wengine wanayakimbia tena makusudiii ??!
Wanasema mama aliyepata uchungu Ana connection Kubwa na mwanaye kama “mungu” na anaweza hata kuhisi jambo haya Kwa mwanaye akiwa mbali Kwa tumbo kuuma , mwanamke aliyepata uchungu akimuona mwanaye anaumia au pengine bahati Mbaya kafariki annapata hisia za uchungu tumboni na ndio maaana anafungwa tumboooo ni kama a nakumbuka uzazi....
Mama aliyepata uchungu hawezi muacha mwanaye akiwa na mwezi na housegal akaenda disco au akalataaa kumnyonyesha
Hata kama Alikuwa kashindikana hatulii Nyumbani hiyo Tabia hupungua kwa kiasi kikubwa
Mama aliyejifungua kwa kisu hataweza kuchangia lolote kwenye Ushujaa wa kinamama hawa japo naye ni mama
Inahimizwa kuwatia Moyo wamama wajawazito wakifungue kwa njia Mungu aliyoagiza kama hawana tatizo la kitabibu linalotishia uhai wake na mtoto
Wengi ni videko na wabishi hawataki kuwasikiliza maelekezo ya wakunga!
Ukishaangia leba kanuni ni moja tu fanya kila atakachokwambia mkunga huku ukimuomba Mungu wako kimoyomoyo !
Ukifanya hivyo hutachelewa nakwambia Mungu anakufanyia wepesi ajabu!
Unapopiga Makelele hayakusaidii na unajichelewesha mwenyewe!
Mama Sabrina Nasikia ni kawaida tu ila mnakuza mambo, wengine uoga tu. Hiyo njia ya mtoto inapimwaje ebu tuelezee
NI KWELI KABISA KABISA KABISA mwanamke aliezaa na uchungu hata malezi ya mwanae ni tofauti na ya mama aliezaa kwa kisu..Nimelishuhudia hilo kwa macho yangu mawili ya nyama.Hili ndo jibu lililosababisha niufufue uzi huu
Mtu anabisha eti uchungu hauleti bond kati ya mama na mtoto
nyie nashangaa mnalalamika uchungu mtoto mwenyewe wa kwanza,mi wife kajifungua watoto wa3 kwa mpigo yuko kawaida tu,hongera sana msambaa wangu
Pole sanaMorogoro Hosp nikienda kujifungua pale, ukilia unapigwa kama mtoto, wale waupe mpaka wa napata wekundu kwa makofi. Mi hawakunipiga ila waliniulia mtoto.
Unanyanyaswa mpaka unaona hiki nini,,,sitasahau pale uchungu umekolea naambiwa nenda kafate dawa nje( sikujua kumbe wanataka rushwa) nikaanza kutambaa kwenda( kumbuka sakafu ya leba na serikalini uchafu wake) nilipofika mlangoni nikaskia we vipi wewe rudi,,utaendaje sasa
Aiseee I have a tale to tell
Kuna watu wanapenda kesi balaa, hata ukimtazama anaweza kukushtaki. Manesi hutoa maneno ya kebehi ili uwahi kujifungua.
Sasa hiyo trela,,,kuna kubwa mbili ndo nikikumbuka naliaga tuu
Ntakusimulia moja.
Unajua uzazi wa kwanza unakua hujui vitu ,,sasa ikafika muda nimeshikwa haja ndogo lakini haitoki,( naskia mtoto anaweza gandamiza pale kwenye kibofu)kila nikienda haja haitoki,,nikaanza kuhisi maumivu makali sana,,nikaita nesi,,akaja kwa ukali,, nini?? Nikamwambia nesi tangia Jana usiku sijakojoa mkojo hautoki ( tangia SAA mbili usiku mpaka saa mbili asbh) akanambia pumbavu wewe kwa hiyo Mimi Nije kukukojolesha Nina kazi zangu usiniite ,,akaondoka. Kufika saa NNE nikaona kama sasa nakufa,, kama nataka kupasuka,,nikaita kwa yowe kubwa kwa uchungu sana,,,nilikua na mwenzangu mmoja( tuliweka chumba chetu Tulikua na pressure) akaita nesi njoo naye akawa anaogopa akajua nakufa,nesi akaja nikamwambia tena akafyonza akaondoka, ,Bahati muda ule kuna kijana wa field akapita ( Mungu ambariki aliko) nikamwambia akasema nipe hela nikanunulie mpira nje,,akaja akaniwekea ,,yani pale pale kifuko kikajaaa,,akasema Dada ulikua unapasuka kibofu,,SITASAHAU ,,,
Ni jukumu lao mbona wakunga wa kiume au wa kike ambae hajazaa huwa na huruma na wanatimiza majukumu yao pasipo tatizo lolote?Samahani ila wengi huumia tu kwa kutojua matumizi sahihi ya midomo yao,ukijua nesi ana frastresheni zake wala hupati taabu.!utajua namna gani useme naye na kauli nzuri hulainisha moyo mgumu.
Badae nilikuja kuanza kuhisi labda ni mawakala wa mashetani, ,sio kawaida,, ingawa Morogoro Hosp hayo mambo ni kawaida sana
Nimecheka huku nakuona huruma sana aise, nimepara pic wife alivyoteseka kunizalia vidume vyangu viwili! Pole na hongera,Mimi nilivyofika Leba ,nikapelekwa sehemu ya mapumziko walikuwepo wajawazito wengii,sasa uchungu ulikuwa haujanishika kivile nilikuwa natokwa na maji tu, daktari akanipima akasema bado,,sasa mle kwenye ukumbi kulikuwa na wamama wengi mwingine anaruka, mwingine anajivuta vuta chini, si nikaanza kuwacheka nikasema mbona mimi siumwii.
kKumbe bana uchungu unakuja taratibu, nikawa nashangaa kila muda unavyozidi kwenda maumivu yananizidia wale niliokuwa nawacheka wao wanajifungua wananiacha tu, kukakucha asubuhi niliona ni mwaka na nikasema sirudiii ,kama nilikuwa natembea uchungua ukaja ghafla naganda kama sanamu kama kuna mti ntaung'ang'ania kweli, ilifikia muda sitaki kuja kusalimiwa wala kuonwa na mtu yeyote maana watu wanavyozidi kuja kuniona ndivyo uchungu unazidi kuwa mkali nikawazuia.
Niliita majina yote ya Mungu nikawa namshika mama yangu namuambia aniombee haraka uchungu upoe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kiuno changu kilikuwa cha moto nauchukua mkono wa mama nauweka kiunoni kwangu namwambia aniombee[emoji23][emoji23][emoji23] mama yangu mpaka alilia nilivyokuwa nahangaika nyie acheni jamani.
Usiku ulipofika saa 2 nikasikia kusukuma nikapelekwa chumbani nimefika kule kila nikisukuma hola,,wakaniwekea maji ya uchungu wapiii wakasema huyu anatakiwa kisu tu nikajitahidi kusukuma wakaja madaktari na manesi wamenizunguka mwingine kanishika kichwa ,mwingine tumbo anabinya,mwingine anaangalia njia ya mtoto (sitasahau)mtoto alitoka saa 8 nanusu kuamkia tarehe 8 na mwaka ....8 loo kazi niliipata
Sasa najiuliza wanaozaa watoto 7 au 8 wanawezaje?maana mim toka nizae sina hamu tena halaf sijawah pata maumivu kama yale toka nizaliwe sema na ukweli
Mama Aheshimiwe ,maana wanaume wangepewa huu uchungu hata dakika wangeukataa na wangetuheshimu sana
Yawezekana maombi ndiyo yalimleta huyo kijana aliyetoa msaada acha watu waabudu kwa imani zao kuzaa ni kujitoa uhai maana yake kifo kinakuwa karibu,,, acheni waombehuu ndo ujinga wenyewe!
manesi wanahitajika kubadilika we unaleta maombi!!.. ni mara ngapi watu wameshaliombea taifa lakini hayo maombi hayafui dafu..?
inatakiwa tuishi maisha ya kweli si kuimagine!,unatenda hivi unadhibitiwa ili usitende si hizi lomolomo.. kuna mwanamke kakomenti kuwa ilikuwa amebakiza kidogo tu kibofu kipasuke,asingekuja huyo kijana akamtibia hicho kibofu kingelipona?
hayo mambo ya maombi watz tufute kichwani huo si uhalisia,we need to change our way,we will get changes.