Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Marahabaa
Kwa hili la kuzaa nawapa hongera wanawake wote duniani has a waliozaa kwa njia ya kawaida,, walio zaa kwa operation wasubiri tu,
Kisa,,,
Mwaka juzi nikiwa katika mishe zangu maeneo ya temeke hospital kwa nyuma ya majengo ya hospital ile kuna branch ya Bank ya NMB,sasa nikiwa naelekea huko nikasikia sukuma!sukuma!sukuma!mala nikasikia kilio na kauri sifanyi tena,sifanyi tena nakufaa,,,dah gafla jamaa akatokea akaniambia hapo ni ward ya wazazi,,Shikamoo wanawake
 
nakumbuka niliingia leba na mme wangu asa uchungu ulipokolea nikawa kama nataka kuwa chizi
yani namwambia mme wangu nasikia kama nataka kuwehuka basi akaanza maombi yani ile anaaza tu nikambinya mkono adi akatoa sauti nusu anikabe
yani niliona kama ananipigia kelele kisa maombi!
jamani uchungu unauma aisee
baadae nikamwambia kwa nguvu kibofu kinapasukaaaa dk 5 mtoto huyu
sijui kwanini eva alimshawishi adamu wale tunda jamani !popote alipo eva adhabu aongezewe yani moto ukolezwe zaidi
Hahahahaha huyo Eva si ni wewe au umesahau
 
Hahahaha imebidi niangalie tarehe ile kwa makini

Uchungu unauma ila kinachosababisha uchungu ni kitamu yawezekana nilinogewa na utamu(mood) mpaka nikaona km ni rahisi vile

Nimesoma nikaona majibu mengine ya siku mbili mbele yalikuwa kinyume
Usiogope mkuu.
 
Sina cha kuongeza tena mkuu,, kumbukumbu za uchungu zinamsisimua sana mzazi na hapo ndipo penye usemi wa uchungu wa mwana aujuae mzazi
NI KWELI KABISA KABISA KABISA mwanamke aliezaa na uchungu hata malezi ya mwanae ni tofauti na ya mama aliezaa kwa kisu..Nimelishuhudia hilo kwa macho yangu mawili ya nyama.

Mke wangu mtoto wa kwanza alijifungua kwa kisu...ki ukweli mwanangu yule nilikua namhangaikia mimi kiasi kwamba hadi nikawa nahisi huyu mke wangu WALINIBADILISHIA HOSPITALI NINI mbona hamjali mtoto kabisa? Basi nikapuuzia kwakua muda mwingi waifu anakaa na mtoto nkajua anakua anachoka na yeye so haikunipa shda kumuhudumia mwanangu.

Afya ya mwanangu wa kwanza haiku vile nitakavyo,mtoto akikataaa kula mke wangu hamlazimishi kula yani anaishi na mtoto the way mtoto anavyotaka...bhas miaka ikaenda kwa shda ivyo ivyo had mtoto amekua na sasa ana afya nzuri maana anakula mwenyewe nk.

MTOTO WA PILI WAIFU KAJIFUNGUA KWA UCHUNGU

Jamani Jamani Jamani sijawahi kuona upendo na caring ile ya uzazi aliyokua nayo mke wangu kwa mtoto,ki ukweli mtoto wangu wa pili anapendwa na mke wangu hadi mi namwambiaga ukweli BABE HUYU MTOTO UNAMPENDA BWANA basi ananijibu simple "HUJUI MAUMIVU YA UCHUNGU WEWE" natamanigi nimrudishie jibu moja hilooooo Sema namstahi namwachaga.

so kusema ukweli mwanamke zaaa kwa UCHUNGU tu...najua ina uma lakini kama unataka mtoto wako umpende 100+100+100% zaa kwa uchungu...Kuzaa kwa opareshen tusidanganyane MAMA atakua na upendo lakini nasema hiviiiii upendo wa MAMA kwa mtoto wake aliemzaa kwa oparesheni Unapitwa na upendo wa BABA kwa mtoto.

nina uhakika asilimia 100000 mimi nampenda first born wangu kuliko mke wangu anavyompenda...na hii ni sababu first born alikuja kwa kisu...ila nina uhakika 100000 pia mke wangu anampenda sec born wangu kunipita hata mimi hilo nakiri kwakweli.
 
Here are nine reasons why pregnancy sex is not only healthy, but why it might be even better than before.
  • An easier labor and recovery. ...
  • Less bathroom breaks. ...
  • Complication prevention. ...
  • Lowered blood pressure. ...
  • Better orgasms. ...
  • Improved self-esteem. ...
  • Stress reduction. ...
  • Improved connections.


Story tu hizo
 
Labor Induction
If a woman is overdue, some experts say that having sex could possibly bring on labor, says Jimmy Belotte, an Ob-Gyn in the Department of Obstetrics & Gynecology and Women's Health at Montefiore Health System, and an associate professor in the Department of Obstetrics & Gynecology and Women's Health and the Albert Einstein College of Medicine. Part of the reason is that orgasms mimic uterine contractions, and sex releases a hormone that’s associated with labor (oxytocin).
But sperm might play a role, too. Semen contains a hormone-like substance called prostaglandins, which is capable of ripening the cervix, says Dr. Belotte. In fact, a synthetic form of prostaglandins are also used in labor inductionmedications like misoprostol.

Story tu hizo
 
Mi niliwekewa kidonge cha uchungu siku moja kabla ya due date. Nikawaaga rafiki zangu wale wa karibu kuwa naenda labor. Basi kila mara namuuliza nurse saa ngapi dawa itareact maana nilikua nishachoka nataka tu nimuone mtoto.

Niliwekewa saa saba mchana. Nikala mchana kama kawaida yangu nikawa busy nachat mwenyewe kwenye groups. Mama angu alikuwepo akakaa mpaka saa moja na nusu akasema ngoja arudi nyumbani akaniandalie chakula cha kesho asubuhi kama itakua sijajifungua.

Mama alivyotoka tu kule wodini nikaanza kusikia kama tumbo la period. Nakumbuka nilikua nimevaa wig nimepaka na lipstick mwenyewe. Mara nikawa sielewi elewi. Akaja nurse nikamwambia naumwa tumbo halafu kama najisikia kwenda kujisaidia haja kubwa. Akaniambia vua nguo zako jifunge tenge. Ile kujifunga tenge ndo kama nilimzindua huyu mkurya tumboni. Kutoka ward kwenda labor ni kama hatua kumi tu. Kufika nikakuta mama mtu mzima nae anasubiri kujifungua. Sasa nikaanza kutapika. Nikaanza kulia. Nikatupa wig kule maana niliona linanibana. Nilisali baba yetu mara kumi kumi. Nilikua nashikilia kitanda siachii. Nilijuta majuto yote. Nilijuta kwanini sikutoa mimba tu kuliko shida ninazopata. Nilijuta kuumwa mwanamke. Nilifikia hatua naomba Mungu anichukue tu kuliko maumivu ninayopitia.

Manurse walikoma na mimi mpaka wananiuliza mzigua gani muoga hivyo. Nilikua kiuno kikikaza sana nawaita wakija wanasema njia bado. Yule mama niliemkuta leba nikamuuliza mtoto wake wa ngapi yule anasema eti wa nne. Nikawa namuuliza unawezaje kuzaa watoto wote hao na maumivu yote haya. Ikafikia point wakanihamishia kitanda cha kujifungulia sasa.

Kitendo cha kutoka kitanda nilicholala mwanzo mpaka kitanda cha kujifungulia niliona ni kama natoka Dar Moro kwa miguu japo ilikua ni kitanda cha tatu toka nilipokua. Nikaishiwa nguvu. Nikawekewa dripu. Sasa mkono niliokua nautumia kujisugua kiuno ukawa umewekwa dripu. Nikaambiwa nikae pozi moja tu. Pale ndo nikazidisha sala za Mungu kunichukua duniani.

Hapo nishajaribu kupush kama mara nne hamna kitu. Nurses wakatoka nje wakaniambia nikijisikia haja nijisaidie tu. Sijui nilijuaje muda umefika ila niliita kwa sauti manesi kuja wakasema sasa tayari anza kupush. Hapo nimeshakata tamaa ya kuishi mmoja akawa amekaa anasubiri mtoto atoke mwingine akawa anamsukuma tumboni anamleta chini.
Mungu wa ajabu sana the moment mtoto ametoka maumivu yote yalikata.

Hata wakati wa kushonwa nyuzi wala sikuogopa sana na uoga wangu wote. Huyu mtoto mzuri nilie nae hapa nikimuangalia naona yale maumivu ya leba ni sawa tu kama nilipitia kumpata malaika mzuri hivi. Wanaume wangejua tunachokipitia leba wangetuheshimu sana.
Nawaheshimu mnoo.
 
Hapa naona mm ndo sijaonja huu uchungu.😂
Ila kuna Dada aliniomba nimpeleke hospital kujifingua, nilikutana nae njiani, kazidiwa kaniomba msaada nikampeleka.
Jamani yule Dada alisababisha nakosana na manesi, uchungu ukimshika Analia kama mtoto, akinishika Mimi naenda kwa manesi kuwaomba waje wamuone, hata hawajali ninachowambia. Nikirudi wodi nakuta wema analia.

Nilivyomuita nesi kwa Mara ya pili akagoma, nikapiga magoti pale kitandani wema alipo kaa, nikaombaa nakuomba mama bikra maria anisaidie wema ajifunguwe maana sio kwa maumivu Yale.
Alikuwa Analia anamuita mama yake marehemu , nywele anazivuta, ananishika mm, ananiambia nimsaidie😂😂😂😂
Baadae sana Dr akaja kumpima akasema huyu bado, nenda umletee chai ya rangi, hapo kumbuka mtu simjui, kadi ya clinic hana, nikimuuliza anajibu analia eti yeye kama vile hana kwao, nimsaidie atanieleza baadae.
Nikaona hii sasa Kali kesho yake nilikuwa na pepa, ntawezaje kukaa hospital? Hapo nilikutana nae saa 4 asubuhi, town, zikivyofika saa mbili usiku, nikamwambia nesi huyu mtu simjui namsaidia tu, mm narudi nikasome, kesho baada ya pepa nakuja, akaniagiza ninunue vitu Fulani niviache hapo. Nikarudi kusoma nikamwacha na nesi,hata kusoma sikusoma mawazo yapo kule leba, nilishika lozari nilisalii, saa 8 usiku nes kanipigia kajifungua, nilifurahi pepa nilifanya within 1hr, nkasepa hospital, ahaaa nilikuta anacheka balaaa.

Shikamoo leba.
 
Siku nyingine nikampeleka Shoga yangu wa ukweli kujifungua ahaaaa, ile hospital ukishamfikisha leba, huruhusiwi kumuona tena, na vile tulimpeleka usiku, wakatwambia tumwache tuje asubuhi.

Huyo Shoga yangu yeye alikuwa atowi machozi ila uchungu ulipokuwa ukimshika ananinambia anakufa nimshike kiuno.

Nesi alivyokuja akaniambia ondoka mama kijacho, utamuona kesho. Maskini Shoga yangu aliniita kwa kwa huzuni sana akaniambia, " luckyline umeniacha nakufa, ila kama nitakufa mtoto mtakaenzaa umuite ANGELO😂😂😂😂asubuhi narudi kajifungua kasichana.dah😂😂
 
Siku nyingine nikampeleka Shoga yangu wa ukweli kujifungua ahaaaa, ile hospital ukishamfikisha leba, huruhusiwi kumuona tena, na vile tulimpeleka usiku, wakatwambia tumwache tuje asubuhi.

Huyo Shoga yangu yeye alikuwa atowi machozi ila uchungu ulipokuwa ukimshika ananinambia anakufa nimshike kiuno.

Nesi alivyokuja akaniambia ondoka mama kijacho, utamuona kesho. Maskini Shoga yangu aliniita kwa kwa huzuni sana akaniambia, " luckyline umeniacha nakufa, ila kama nitakufa mtoto mtakaenzaa umuite ANGELOasubuhi narudi kajifungua kasichana.dah
Unaitwa Angelo?/Angel
 
Kuna moja baba mtu alijipitisha nikamuona nikiwa stage hiyo ya ukali yaani nilivyomfukuza, toka usoni kwangu nisikuone kabisa.....hahahaha alikimbia balaa
Jamani mpaka nimeogopa.... Uwiiii sijui itakuwaje mwaka wa mimi kuingia huko nadhani manesi watanipiga makofi
 
Wengine wanazaa kama panya tu, sekunde mbili kapush katoka kama hakuna kilichotokea vile.
 
Wanawake huwa mnatutesa sana yaani unamwelekeza mama uchungu ukija fanya hivi lkn badala yake anafanya kivingine tu yaani utamu wako hafu ulete shida nyingine

Hicho nikilele cha kutanua mapaja mama

Tena sukuma kama ulivyokuwa unasikia ule utamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom