Sasa hiyo trela,,,kuna kubwa mbili ndo nikikumbuka naliaga tuu
Ntakusimulia moja.
Unajua uzazi wa kwanza unakua hujui vitu ,,sasa ikafika muda nimeshikwa haja ndogo lakini haitoki,( naskia mtoto anaweza gandamiza pale kwenye kibofu)kila nikienda haja haitoki,,nikaanza kuhisi maumivu makali sana,,nikaita nesi,,akaja kwa ukali,, nini?? Nikamwambia nesi tangia Jana usiku sijakojoa mkojo hautoki ( tangia SAA mbili usiku mpaka saa mbili asbh) akanambia pumbavu wewe kwa hiyo Mimi Nije kukukojolesha Nina kazi zangu usiniite ,,akaondoka. Kufika saa NNE nikaona kama sasa nakufa,, kama nataka kupasuka,,nikaita kwa yowe kubwa kwa uchungu sana,,,nilikua na mwenzangu mmoja( tuliweka chumba chetu Tulikua na pressure) akaita nesi njoo naye akawa anaogopa akajua nakufa,nesi akaja nikamwambia tena akafyonza akaondoka, ,Bahati muda ule kuna kijana wa field akapita ( Mungu ambariki aliko) nikamwambia akasema nipe hela nikanunulie mpira nje,,akaja akaniwekea ,,yani pale pale kifuko kikajaaa,,akasema Dada ulikua unapasuka kibofu,,SITASAHAU ,,,